Thursday, March 17, 2016

POLISI YA SHIKA KASI KUWASWEKE JELA VIONGOZI WA CHAMA CHA CUF NA KUINDELEA KUWAPIGA RAI WASIO NA HATIA YOYOTE NCHINI ZANZIBARWakati wananchi wa Tumbatu wakidai kuchoshwa na madhila wanayofanyiwa na vyombo vya ulinzi na kusababisha baadhi yao kuondoka kwenye nyumba zao kama alivyobainisha Bw. Chambu Ahmad Makame huku Mjini nako jioni hii Mshauri wa Maalim Seif, Mansoor Yussuf Himid anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mara nyengine tena, Mansoor aliitwa na polisi leo hii kwa ajili ya mahojiano akiambatana na Wakili Karume Haji Mrisho ambaye amesema Mansoor ameshutumiwa kwa mambo mbali mbali ikiwemo suala la kuripuliwa Kisonge hata hivyo wamekataa kumpa dhamana hivyo ataendelea kuwepo polisi. Mwenyeenzi Mungu atuvushe na balaa katika nchi yetu
Orodha ya viongozi wa CUF wanaoshikiliwa na polisi Zanzibar kwa mujibu wa Naibu katibu mkuu wa CUF Magdalena Sakaya, hadi sasa viongozi waliokamatwa ni pamoja na, Eddy Riamy mwanamikakati ya ushindi CUF; Nassoro Mazrui, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar; Mahomoud Mahinda, Katibu Mtendaji JUVICUF; Abeid Hamis Bakari, Mkuu wa Idara ya Habari na Uenezi na Hamad Masoud, Mkurugenzi wa Habari CUF.
KISHA NYINYI MUNAYAITA MAPINDUZI MATUKUFU HIVI KWELI NYINYI MUNAJUWA UTUKUFU NI NINI AU DUNIA IMEWAVA KISAWA SAWA MPAKA MNAKUFURU

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment