Thursday, March 24, 2016

SHEIN ASHAJIAPIZA LEO KWA KUSHIKA KURAAN
Shein anae jidanganya kuwa atii ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya nchi ya Zanzibar Shein leo amejiapiza kwa kushika kuraan kuwa atii yeye ni Rais kwa mujibu wa katiba katika kuongoza wananchi ambao hawataki hata kumuona uso wake wachilia mbali kuwaongoza katika nchi yao ya Zanzibar kwa muda wa miaka 5. Shein amejiapiza na huku akisaidiwa kujiapiza atii na Jaji Mkuu wa nchi ya Zanzibar Omary Othman Makungu mbele ya wahafidhina wa nchi pamoja na viongozi atii wa dini na kushuhudiwa na wananchi kutoka mrima walio letwa kuujaza uwanja wa Amani mjini Unguja hapa nchini Zanzibar.

Baada ya Shein kumaliza kujiapiza hao wanao jiti viongozi wa dini wanafiki wakubwa nao wakamaliza kabisa atii kwa kumuombea dua makubwa kiongozi thalimu aombewa duwa Duuuh!! wakiongozwa na Mnafiki wa Wanafiki Sheikh Khamis Haji Khamis na kufuatiwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini Zanzibar Augustino Shayo na Askofu wa Anglikana Dayosisi ya Zanzibar Padre Michael Henry Hafidh.

Viongozi mbalimbali wanao shiriki kuikandamiza nchi ya Zanzibar na kutaka kuendeleza Ukoloni wa Mkoloni Mweusi Tanganyika kuzidi kuimaliza nchi ya Zanzibar wamehudhuria Kiapo hicho alichokuwa Shein akijiapiza Mwenyewe walio shuhudia akijiapiza akiwemo Rais wa Jamhuri ya Tanganyika Mkoloni Mweusi Tanganyika Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu aliye pewa fupa anyonye na kuendeleza Ukoloni, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, viongozi wastaafu na jamaa wa mrima ambao sasa ndio wanahisabiwa kuwa ndio wananchi wa nchi ya Zanzibar. Aidha Shein amejiapiza na kuwa Rais Bandia wa awamu ya saba kwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na kukagua gwaride rasmi lililo jazwa nchini Zanzibar kuwadhibiti Wazanzibari wasidai haki yao na kuendelea kuwa chini ya Mkoloni Mweusi Tanganyika.

KISHA NYINYI MUNAYAITA MAPINDUZI MATUKUFU HIVI KWELI NYINYI MUNAJUWA UTUKUFU NI NINI AU DUNIA IMEWAVA KISAWA SAWA MPAKA MNAKUFURU

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment