Wednesday, March 30, 2016

VIKWAZO ZAIDI KWA NCHI YA ZANZIBAR IKIWA PAMOJA NA TRAVEL BAN KWA VIONGOZI

MCC-Gold-Stars
MAREKANI INATARAJIWA KUTANGAZA VIKWAZO ZAIDI KWA ZANZIBAR IKIWA NI PAMOJA NA “TRAVEL BAN” KWA VIONGOZI WA SERIKALI YA ZANZIBAR NA KUZUILIWA NA MALI ZA ZANZIBAR ZILIZOPO MAREKANI (ACCOUNT ZA PBZ).
Taifa la Marekani linatarajia kushusha rungu la aina yake kwa serikali ya Tanganyika ((Tanzania)) kufuatia hali ya sintofahamu inayoendelea nchini kutokana na sakata la uchaguzi mkuu wa nchi ya Zanzibar. Habari zinadokeza kuwa taifa hilo kubwa duniani litaweka vikwazo vya kiuchumi kwa ya Tanganyika ((Tanzania)) hali itakayopelekea nchi ya Tanganyika ((Tanzania)) kuandika historia nyingine mbaya mbele ya uso wa dunia. 
Serikali ya Marekani tayari imezuia misaada mbalimbali kwa nchi ya Tanganyika ((Tanzania)) na pia ndiyo iliyoshinikiza Tanganyika ((Tanzania)) kunyimwa fedha za MCC. Hata hivyo serikali ya Tanganyika ((Tanzania)) bado haijatilia maanani jambo hilo huku ikioneknana kupuuza juhudi za kimataifa kuitaka kuumaliza kwa haraka mgogoro wa nchi ya Zanzibar unaofukuta kwa kuacha haki ichukue mkondo wake. Habari zinadokeza kuwa balozi wa Marekani nchini atatoa msimamo unaoelezwa kuwa ‘mkali’ ili kuishinikiza serikali ya Tanganyika ((Tanzania)) kuheshimu maamuzi ya wananchi kwenye uchaguzi mkuu wa nchi ya Zanzibar uliofanyika mwezi october mwaka jana ambao ulielezwa kuwa huru na wa haki.

No comments:

Post a Comment