Friday, April 29, 2016

SEHEMU YA 1) UKWELI NI HUU KUUSUTA UWONGO. MAVAMIZI YA NCHI YA ZANZIBAR KWA WAGENI KUUWAUWA WANYEJI KATIKA NCHI YAO NA KUSINGIZIA ((MAPINDUZI))


Nimechanguwa jina hili la UKWELI NI HUU KUUSUTA UWONGO, baada ya kuyasikia na kuyasoma mengi ya uwong na hata kufikia kusomeshwa watoto wetu katika Maskuli ya Zanzibar kuhusu hayo yenye kuitwa (MAPINDUZI) yaliyo fanyika katika visiwa vyetu vya Zanzibar mnamo Taarikh 12 januwaru 1964.

kabla ya kuingia katika hayo, nigependa kuwambia wasomaji wangu kuwa mimi si mjuzi hata kidogo wa fani hii uandishi; tena ni mbovu sana katika spellings na katika nahau za kiswahili cha kisasa. Pia nawaomba radha kwa kiswahili changu cha kizamani, Bali, kutokana na huo uzushi na kupotezwa kwa makusudi ukweli wa hayo yaliyofanyika kuhusu hayo yanayo itwa (MAPINDUZI) nimeona sina budiilla nijitole hivyo hivyo juu ya upungufu wangu wa katika fani hii juu ya uandishi. Lakini ukweli lazima niudhihirishe ili vichepukizi vyetu viweze kuyaelewa vilivyo yaliyo tendeka katika nchi yao. Kwani wengi walikuwa wadogo na wengi walikuwa hata hawajazaliwa wakati huo. Ilivyokuwa kiswahili ni lugha yangu ya kuzaliwa, basi ninaiandika kama ninavyo isema. Si shughuliki na kua au kuwa, aliniambia au aliniambiya, aliniambia au aliniambiya, ameuawa au ameuwawa, kenda au kaenda, amekwenda au ameenda; Hayo kwa watamu wa lugha ni mambo muhimu lakini kwa mimi nakutakeni msamaha juu ya hayo. Muhimu yakuyaangalia na kuyazingatia ni yale nikusudiayo kuyaeleza, kwani hayo ndio muhimu na ndio ya kweli tupu isiyukowa dosari hata chembe.

La Mwanzo nitakalo waombeni mlifahamu uzuri ni ile hakika kuwa hayo yaliyo fanyika katika visiwa vyetu Taarikh 12 januwari 1964 hayakuwa (MAPINDUZI) wala hayafai hata kidogo kuitwa mapinduzi kwa maan ya asili ya neno.Bali kwa maana zote yalikuwa khasa ni MAVAMIZI yani kwa kiengereza INVASION. Mapinduzi lazima yapangwe, yaongozwe na yatekelezwa na wananchi wenyewe kwa maslahi ya nchi na wananchi wake. Sasa tukiangalia yaliyotendeka Zanzibar, yalipangwa, yaliongozwa na yalitekelezwa na WAGENI kutoka nchi za nje za jirani zetu.(Ni wao wala si wananchi ndio waliochukuwa ngawira kubwa kubwa) Haya yathibitika zaidi kwa vile kuwa huyo jamadari aliyeyaongoza hayo mavamizi ni John Okello na wachini yake walikuwa Injini na Mfaranyaki. Nani kati ya hao aliyekuwa kitovu chake kimizikwa kisiwani...?? Okello amezaliwa na kukulia kwao Uganda, Injini amezaliwa na kukulia kwao Kenya na Mfaranyaki amezaliwa na kukulia kwao Tanganyika.Wote hao walikuja Zanzibar wakiwa watu wazima na shughuli zao,wamekuja kutafuta kibarua na kukimbia kodi za vichwa katika nchi zao.Liangalie ilo walilolita Baraza la Mapinduzi utaona sehemu kubwa ya wanachama wa baraza hilo walikuwa si Wazanzibari,Laa kuzaliwa wala kwa uchukuwa Tajnisi (kuandikisha uraia) John Okello, Khamis Darweshi, Seif Bakari, Said Natepe, Said Washoto, Muhammed Mfaume, Enditong Kisasi, Mohammed Abdallah Kaujore. Ukiwacha wengine nao vile vile walikuwa si wananchi wa Zanzibar kwa kuzaliwa, bali wao walikuja Zanzibar wakiwa katika migogo ya wazee wao na waliendelea kuishi humo visiwani kwa maisha yao yote.Na wakachukuliwa kama ni Wazanzibari japo kuwa sio Wazanzibari.


UTUKUFU NA NEEMA YA ZANZIBAR
Mwenyezi Mungu amevipa visiwa hivi viwili yani Unguja na Pemba bahati ya utukufu katika kila jambo lake.Hayo yaliendelea toke karne na karne mpaka pale ulipo tendwa ufisadi wa Taarikh 12 januari 1964,ndipo neem na utukufu wa Zanzibar ulipoanza kutoweka.Hapo tena badala ya zumari lakipulizwa Zanzibar,watu wa maziwani (Bara) walikuwa wakihemukwa,ikawa linapulizwa Bara,tuliopo visiwanitunahemukwa!!! 

ZANZIBAR NA UBAGUZI KABLA YA MAVAMIZI
Nathubutu kusema bila ya wasi wasi wowote kuwa Zanzibar hakukuwepo ubaguzi wa namna yoyote kwa maana khasa na ya wazi ya neno UBAGUZI. Kwanza Wazanzibari ni watu walio changanya sana damu hata sio rahisi kuweza kumtambuwa mtu kuwa ni mwenye kutokana na asili ya kabila fulani kwa kuangalia rangi yake au pua yake au masiki yake au kimo chake au kwa jina lake.Je watu hao watabaguwani namna gani...?? Malipo ya wafanyakazi Serikalini yalikuwa hayakupangwa ki-ukabila.Wale Serikali haikuwa na sehemu maalum katika Maskuli wala katika Mahospitali kuwa zimetengwa kwa ajili ya watu wa makabila fulani.Katika nchi za jirani zetu, Tanganyika, Kenya na Uganda kote huko kulikuwepo na ubaguzi uliokuwa ukiongozwa na serikali za nchi hizo.Malipo ya mishahara ya wafanyakazi yalikuwa yakilipwa kutokana na makabila yao wala si kutokana na ujuzi wao wa kazi kulikuwepo na African Scale Asia Scale na Europen Scale. Madaktari, Mainjinia, Waalimu na wowote nawawe wana elimu na ujuzi na maarifa ya namna moja, yani wote sawa sawa kwa elimu na ujuzi wa kazi zao,lakini mishahara yao ilikuwa tafauti kutokana na makabila yao.Waafrika ndio wenye kulipwa malipo ya chini kabisa kuliko wote.Wazungu walikuwa ndio wenye kulipwa mishahara minono (hata baadhi yao walikuwa hawana elimu yoyote isipokuwa huo uzungu wao) Waliofuatia ni Waasia. Vyoo vya njiani (Public Toilet) na sehemu za kungojelea usafiri wa reli navyo vile vile vilikuwa vikitumika kwa ubaguzi wa kikabila. Waafrika waliekewa vyoo vyao na sehemu zao za kungojelea usafiri, Wazungu walikuwa na sehemu zao, Waasia walikuwa na sehemu zao,wote mbali mbali.Lilikuwa ni kosa na kuvunja sheria ikiwa imetokea kwa yoyote kuingia katika sehemu asiyo kuwa amekhusika nayo.Khasa Muafrika awe ameingia au amekaa  sehemu za Waasia au za Wazungu.Katika Tanganyika, Kenya na Uganda kote huko kulikuwa na kodi ya Kichwa. kodi hiyo ilikuwa ikilipwa na kila mtu aliyekwisha fikia balegh katika umri wake. Nayo pia ikitekelezwa kwa njia za ubaguzi wa kikabila. Waasia na Wazungu hata ikiwa wao wamechelewa kulipa kodi zao basi walikuwa hawakamatwi majiani wala walikuwa hawaendewi majumbani mwao kukamatwa.Laikini Waafrika walikuwa wakisakwa majiani na wakiendewa majumbani mwao mnamo pinga pinga za usiku.Na wakikamatwa,basi walikuwa wakifungwa kamba za viunoni au hufungwa ncha ya shati la huyu na huyu kisha walikuwa wakiongozwa mmoja nyuma ya mmoja na huku wakipingwa mateke na kusukumwa mpaka wakifikishwa Bomani. Huko ikiwa hawatakuwa na cha kuwalipa basi walikuwa wakihukumiwa na wakifungwa.kutokana na hali kama hizo,ndipo wengi kati ya wananchi wa nchi hizo,khasa kutokaTanganyika walikimbia kutoka makwao na kuhamia Zanzibar kwa sababu ya kufuata hali njema za kimaisha.Zanzibar hakukuwepo kodi za kichwa wala ubaguzi wa vyooni wala malipo ya mishahara wala ya namna yo yote.ilikuwa ni njema na atakae naaje.

UBAGUZI UMEANZISHWA ZANZIBAR WAKATI WA SERIKALI YENYE KUJIITA YA MAPINDUZI
Mara tu baada ya kufika hiyo serikali ya mavamizi katika Zanzibar ubaguzi wa ukabila ulianzishwa kila mrangi rangi kama walivyo kuwa wakiwaita wenyewe, yaani wenye asili za kiarabu, za kihindi na za kingazija walianza kuolewa makazini bila ya kupewa hata haki zao za ufanyaji wa kazi.mashamba,majumba na hata mabiashara yao yalichukuliwa kwa nguvu na kupewa wageni ikiwa ni tunzo la ukatili na maovu waliyowafanyia wananchi katika nchi yao.Serikali ya mavamiza ya Zanzaibar ilitangaza rasmi kupitia vyombo vya khabari vya serikali kukhusu ubaguzi katika Taalimu.Waafrika wakipasi au wasipasi bali idadi yao yakuingia katika form one ya secondary school ilikuwa ni 77 katika mia (77%) Waarabu 16 katika asili mia (16%) wahindi 6 katika mia (6%) na wangazija MOJA katika mia (1%) Si hayo tu, bali serikali ya mavamizi imetumia pesa za umma kwa ajili ya kujijengea hospitali yao wao tu ya wananchama wa Baraza la Mapinduzi na Familia Zao na wameita (MAPINDUZI WING) vitanda,mabetishiti,foronya za mito,vyombo vya kulia kama sahani,vikombe,visu na nyuma (forks) vyote viliangizwa kutoka ulaya.Ilikuwa ikitokea Mheshimiwa kulazwa huko, basi na mkewe alikuwa akihamia huko huko na kulala kitanda kimoja kama kwamba wamo katika siku za fungati haya yakitendeka wakati wananchi wanyonge hawana hata dawa mahospitalini!!! huwo ulikuwa ndio usawa sio ubaguzi!!! 

ELIMU NA MATIBABU BURE
Tuunambiwa na Serikali yenye kuujita ya Mapinduzi kuwa elimu na matibabu yameanza kuwa bure kwa wananchi baada ya kupatikana serikali ya Mapinduzi huu ni uwongo uliyokuwa hauna hata kifuniko.Toka lini elimu na matibabu yalikuwa kwa malipo katika Zanzibar....?? Tangu kuanzishwa kwa skuli ya serikali ya Sayyid Ali bin Hamoud na toka kuanzishwa kwa matibabu katika mahospitali, kamwe hayapata kuwa ya malipo.Toka kwa kuangaliwa na madaktari mpaka kwa madawa,chakula,na mpaka kulala kwa kutibiwa katika mahospitali kulikuwa BURE

TAALIMU
Wananchi na wageni,kuanzia chumba cha kwanza (standard one) mpaka kufikia chumba cha nane (standard eight) masomo yalikuwa bure kwa wote. Sio hivyo tu kila mwanafunzi alikuwa akipewa madaftari ya kuandikia bure, vitabu vya kusomea bure, kalamu za kuandikia bure, vidawa vya wino na wino wake bure hata blotting paper (la kukaushia wino) pia wakipewa bure. Na kila ijumaa wanafunzi walikuwa wakipewa sabuni za kufulia bure. Skuli za mashamba, wanafunzi walikuwa wakipewa kifunguwa kinywa, kunde na uji - kabla ya kuingia katika vyumba vya masomo bure. Kuanzia chumba cha tisa mpaka cha 12, na baada ya muda katika miaka ya 1950 kuanzia chumba cha saba mpaka cha 12, wazee walitakiwa wasaidiye kitu kidogo katika masomo ya watoto wao.Malipo hayo yalikuwa ya kitu kidogo sana na si kila mzee alikuwa akilipa ada hizo. Wengi sana katika wazee walikuwa hawalipi hata senti moja. Na hao walikuwa wakilipa, wengi wao walikuwa wakilipa kuanzia kuanzia shs tano mpaka shs 20 kwa wingi kila baada ya miezi mitatu au mine. Kabla ya mzee alipe au asilipe, kulikuwepo utaratibu maalumu zilizokuwa zikifanywa.Mzee wa mtoto alikuwa akipelekewa (questionnaire) karatasi yenye masuala yaliyokhusu mapato yake, kazi yake na idadi ya watu wake wa nyumbani.kwa kutaka kuhakikisha uwezo wa mzee huyo,basi akipelekewa waraka huo kwanza sheha wa mtaa kuhakikisha yaleyaliandikwa na akisha sheha humpelekea mudiri wake humpelekea D.C. wake.Baada ya khatuwa hizo ndio tena hapo hutolewa uamuzi wa kulipa au wa kutokulipa, na kama kulipa alipe kiwango gani.Kutokana na mipango kama hiyo,zaid ya 70 katika mia (70%) ya wazee watoto wao walikuwa wakisoma bila ya kulipiwa kitu chochote na kiasi cha 20 katika mia (20%) walikuwa wakilipiwa kitu kidogo na kiasi cha 10 katika mia (10%) ndio waliokuwa wakilipiwa idadi kamili ambayo ilikuwa chini ya shillingi 200, kwa mwaka mzima.Wengi waliokuwa wakilipa kima hicho walikuwa ni wazee wenye asili za Kihindi.Wanaoitwa Waafrika na Wanaoitwa Waarabu hayo yalikuwa sio maji yao.Muhimu katika hayo si kulipa au kuto kulipa, muhimu ni thamani (quality) ya elimu iliyokuwa ikipatikana siku hizo. Je leo inapatikana....?? Hilo ndilo suala muhimu la kujiuliza na kulizingatia. Ikiwa hiyo isemwayo leo kuwa elimu bure, na imekuwa wanafunzi hawana madeski ya kukalia,hawana vitabu vya kusomea,wala chochote cha kusomea,bali zaidi hawana hata walimu wenye ujuzi wa kusomesha;basi bure kama hiyo ni bure ghali kwa hiyo bure,basi watoto wetu leo wametokwa na vibyongo kwa kuinama wakati wa kuandika.Wakirijea kutoka maskuli utadhania wanatoka kuchimba makaburi kwa mavumbi yalivyo watapaka kwa kusota chini.Elimu bure!!! Wanafunzi wapotezewa wakati wao wa masomo kwa kuchezeshwa ngoma za sindima na kuimbishwa majimbo ya kanisani ati huitwa Kwaya kuanzia Disemba Wanafunzi walikuwa wakianzishwa mazoezi ya kucheza ngoma na kuimba hizo Kwaya pamoja na magwaride kwa ajili ya kujiweka tayari kwa sherehe za hayo yenye kuitwa Mapinduzi katika mwezi wa januari. Wakimaliza tu, hawawahi hata kushusha pumzi wanangojewa kwa sherehe za kuasisiwa kwa Chama cha Afro Shirazi 2 - 2 (February 2) wakimaliza tu,hawawahi hata kunywa maji,wanazolewa tena kwa mazoezi ya sherehe za Muungano April 26. Hawawahi hata kuka kitako,wanabebwa tena kwa mazoezi ya sikukuu ya Wafanyakazi May Day hapo hupumua kidogo kisha huzolewa tena kwa mazoezi ya kusherehekea Saba Saba July 7. Hawawahi hata kwenda chafya hunyakuliwa tena kwa mazowezi ya sherehe Elimu bure!! Septemba. Wakimaliza hapo wanazolewa tena kwa mazowezi ya sherehe za Uhuru wa Tanganyika Desemba. ukiangalia utaona kuwa mwaka mzima badala ya watoto wetu kusomeshwa,walikuwa wakichezeshwa ngoma,kuchezeshwa magwaride na kuimbishwa manyimbo ya kanisani.Bado ati husema ELIMU BURE, kweli bure lakini BURE KWA MJINGA kwa kweli kiwango cha elimu Zanzibarkimeanguka kiasi kikubwa sana, kiasi cha kuitwa chini ya sufuri. Imefika hadi leo kuwa Mwanafunzi aliyemaliza hicho wanachokita kidato cha nne (Form IV) ukimuambia aandika barua ya kuomba kazi kwa lugha ya Kiingereza anashindwa hata kujaribu kuadika na ikiwa atajaribu,basi kichwa huwa miguu na miguu huwa kichwa.Hapo yalipokuwepo masomo ya kweli na walimu wa kweli wenye kufunzwa wakafunzika katika fani ya kusomesha, wanafunzi waliomaliza chumba cha nane ilikuwa wakiandika kiengereza utawavulia kofia.

MATIBABU
Tukija katika matibabu, ndiko tutakako kukuta kumeporomoka vibaya kabisa. Hospitali hazina madawa, hazina vifaa vya matibabu, hakuna hata vitanda na mabetishiti ya kutosha. Wagonjwa wanatakiwa wakenda kutaka matibabu,wachukuwe zana zao wenyewe tokea pamba,gauze,vijembe vya kunyolea na hata chupa za Drips pia wende nazo shuka za kutandika vitandani,mito na foronya zake na nguo za kujifunikia wakati wa kulala vyote hivyo lazima waendenavyo mwenyewe; kama si hivyo basi hatapata matibabu. ubavuni mwao wakitizama wanaiyona Mapinduzi Wing bwana na bibi wanaingia na kutoka. Tokea miaka yalipoanzishwa mahospitali ya serikali Zanzibar, matibabu yalikuwa BURE KW WOTE. kwa wananchi kwa wageni hata kwa wapita njia. Kuangaliwa na daktari ilikuwa bure, dawa bure, ukilazwa kwa jili ya matibabu, bure. Na Hospitali zilikuwa Hospitali kweli kwa kila kitu.Madawa ya kila maradhi yalikuwepo. Madaktari wenye ujuzi wa kazi zao, waliosomeshwa wakakhitimu walikuwepo wa kutosha.Sivyo kama ilivyo hivi sasa wauguzi (Staff Nurse) ndio madaktari tana wa kufika kuuchana na kuupasuwa mwili wa binadamu Kwenye nchi yenye sheria,pindi likitokea lolote, basi ushahidi wa watu kama hao, hauwezi kukubalika katika mahakama za sheria, kuwa ni ushahidi wa kidaktari. Lakini ndio kama ule masemo wa kiswahili, Likikosekana la mama hata la punda hufaa; Ni kweli kulikuwepo katika hospitali kuu ya serikali sehemu maalumu za kulala wagonjwa wa kulipa.Lakini hayo yalikuwa kwa kupenda kwake mwenyewe huyo mgonjwa.Malipo yenyewe yalikuwa kwa watu wenye kufanya kazi serikalini, walikuwa wakilipa shs sita kwa siku, na waliokuwa hawafanyi kazi serikali, walikuwa wakilipa shs 12. Kwa hakika hakukuepo tafauti kubwa baina ya huko kwa malipo na kwa bila ya malipo. Tafauti ziliyokuwepo baina ya sehemu za kulala wagonjwa kwa malipo na sehemu za bure za nyongeza tu, Sio ya kwa lazima. Kwa mahitajio ya kimatibabu kulikuwa hakuna tafauti hata kidogo. Tafauti zilikuwa kama hizi: katika upande wa malipo, wangonjwa walikuwa wakipewa panjama za kulalia, vyakula vyao wakiletewa katika sinia na sahani zao zilikuwa za kaure na walikuwa wakipewa chai ya kitandani (bed-tea) na pia walikuwa wakipewa chai ya alaasiri (afternoon-tea). pia walikuwa wakipewa taula ya kujifutia maji baada ya kukoga.Chakula kikubwa kilikuwa wali na mchuzi wa nyama na kibakuli cha punding. Upande wa wagonjwa wa bure,wao walikuwa wakiletewa vyakula vyao bila ya kutiliwa katika sinia na sahani zao zilikuwa senti (alimunium) chai walikuwa wakitiliwa katika makopo ya senti. Hapakuwa na tafauti kubwa ya chakula isipokuwa wao badala ya kupewa chai ya kitandani,wakipewa uji.Wagonjwa wote-wa kulipa na wa bure-walikuwa wakipewa matunda na mboga. Na ikiwa mgonjwa ameandikiwa na daktari chakula maalumu kutokana na maradhi yake,basi alikuwa akipewa chakula hicho (bila ya malipo) sawa sawa na mgonjwa aliyekuwa katika sehemu za malipo ikiwa maradhi yao ni ya namna moja.Madaktari na wauguziji walikuwa ndio hao hao kwa wote,wa kulipa na wa bure.Leo tuambiwayo kuwa matibabu bure mgonjwa akenda hospitali baada ya kuangaliwa na daktari (pengine na muuguzaji nurse tu) na akaandikiwa dawa, akifika kwa watoa dawa jawabu analolipata ni kuwa, dawa hizi hazipo, kanunuwe nje jawabu kama hizo ni za kila siku.Ukenda kuwaangalia wangonjwa waliolazwa, ukianza tu kupanda ngazi, unakaribishwa na harufu za mikojo na za mashonde kutoka vyooni.Hospitali haina maji ya kutosha.Ukiingia katika vyomba vya kulala wagonjwa,unawakuta mapaka wanacheza foliti kwa jinsi ya uchafu uliomo ndani. Makunguru wana ruka huku na huku humo vyombani, wanapita dirisha hili na kutokea jingine. Sakafu zinanata kwa uchafu. Sasa watizame hao wagonjwa namna walivyo lala humo vitandani.Vichekesho khasa.Wengine wamejifunika kanga za kisutu, wengine za mkeka,wengine za visima na za namna mbali mbali.Utadhani watoto wa kizamani walipokuwa wakitiwa kumbini (kutahiriwa) Mabetishiti yaliyotandikwa vitandani kwa ilivyokuwa kila moja kaja na lake,basi, huyu katandika jeupe la mfuto,huyu lililofumwa tausi na huku limeandikwa KARIBU MGENI,na kwa kipembani ya chumba utaona mengine yameandikwa FURAHA YA BIHARUSI, na jengine limeandikwa kwa mandishi naksi SINA MWENGINEWE,au MAPENZI YETU YA UTOTONI,au MIMI NA WEWE HATULISHANI YAMINI,mradi huwa rangi rangire.Hospitali zimepoteza jina na thamani yake kwa kila upande,haziwezi hata kidogo kutowa huduma zitarajiwazo.

Hiyo ndio hali ya hayo yanayoambiwa ni MATIBABU BURE !!! Lakini haya yote yanaowapata ni wananchi wa kawaida tu.Ama wenyewe wakina fulani na fulani pamoja na watoto wao,wao bukheri wa sururu hata hawana khabari nayo wala hawayasikii licha ya kuyaona. khalafu kwa kuundanganya umma ati husema, Tumeondoa serikali ya Kisultani na Kibwanyenye. Wakati wa huo Usultani, Mfalme wa nchi hajapata kuwa na hospitali yake peke yake.Yeye pamoja na ukoo wake wakenda katika hospitali hiyo hiyo wanayokwenda watu wa kawaida. Aliyekuwa Mfalme wa nchi, Seyyid Abdulla Bin Khalifa Bin Haroub,alipopata maradhi,alilala katika hospitali hiyo hiyo na alifanyiwa operesheni katika hospitali hiyo hiyo wanayotibiwa watu wa kawaida.Wakoloni wa Kiingereza waliweka sehemu yao ya kutibiwa waliita  European Wing kutokana na makelele ya wananchi,khasa kutokana na makala yaliyokuwa yakiandikwa katika gazeti la wananchi la mwongozi sehemu hiyo ilibadilishwa jina na bada yake kuitwa European Wing ikaitwa West Wing kutokea wakati huo ilikuwa wazi kwa yoyote mwenye kupenda kwenda sehemu hiyo ikiwa yutayari kulipa ada zilizowekwa.Leo baada ya Mapinduzi ya kuleta usawa na kuondowa Usultani na Ubwanyenye, Mheshimiwa akiumwa na mdudu upande basi mbio anachukuwa ndege anakwenda zake Uiingereza au Ujerumani kwa matibabu. Ikiwa matibabu yapo nchini BURE, mbona wao wanayakimbia na kuyafuatia ya malipo,tena katika nchi za ngambo na kwa kutumia pesa za wanyonge kwa matibubu yao...?? sasa ipi inayostahiki kuitwa serikali ya Kibwanyenye....?? Hii ya waheshimiwa waliyojitenga mbali na umma au ile ya waliyokuwa wakiishi pamoja na umma....?? Mwenye macho haambiwi tizama! Unaweza kuwandanganya baadhi ya watu baadhi ya siku, lakini huwezi kuwandanganya watu wote siku zote.
Merehemu Sheikh Amani Thani Fairuz Mwenyezi Mungu Mlaze Pema Peponi Ameen.

KISHA NYINYI MUNAYAITA MAPINDUZI MATUKUFU HIVI KWELI NYINYI MUNAJUWA UTUKUFU NI NINI AU DUNIA IMEWAVA KISAWA SAWA MPAKA MNAKUFURU MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA KATUPINDUWA TENA WAZANZIBARI NA KUWEKA VIONGOZI WAWATAKAO WAO WAKINA BT TUNAENDELEA TENA KUKA CHINI YA SERIKALI YA KIKOLONI YA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA MPAKA MIAKA MITANO IMALIZIKE KISHA TUTIWE TENA KATIKA SHENGESHA LA UCHAGUZI NA KUPIGA KURA KISHA WAZANZIBARI WAPIGE KURA NA KUCHAGUWA VIONGOZI WAWATAKAO MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA ATAKUJA NA STYLE MPYA YA KUZIPIGA KURA ZA WAZANZIBARI CHINI NA KUTUEKEA VIONGOZI WAWATAKAO KISHA TUTAKA TENA CHINI NA KUSUBIRI UCHAGUZI WA 2025 MAMBO YATAKUWA HIVYO HIVYO KISHA TUTAKA CHINA NA KUSUBIRI UCHAGU WA WA 2030 TUKIWA HAI KAMA HATUKO TENA WATAKAO BAKI WATAFANYIWA TENA HIVYO HIVYO NA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA KISHA WATAKA CHINI WASUBIRI......>>> MPAKA KIYAMA KISIMAME BASI NI BORA TU TUKUBALI KUWA NDIO TUMEKUBALI KUWA CHINI YA MKONI MWEUSI TANGANYIKA KULIKO UPUMBAVU HUU WA UCHAGUZI AMBAO KILA MOJA WETU HAPA ZANZIBAR KAMA UCHAGUZI WA MARA HII HAUJAWASOMESHA WALA HATUTA SOMA TENA MILELE. 

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment