Thursday, April 7, 2016

VIDEO-MARA HII TUNA MZAMBIA NDANI YA BARAZA LA WAWAKILISHI TANGANYIKA KWA WATANGANYIKA,KENYA KWA WAKENYA,ZAMBIA KWA WAZAMBIA CHA AJABU ZANZIBAR SI KWA WAZANZIBARI BALI NI KWA WAFRIKA WOTE

TUNA MZAMBIA KATIKA BARAZA LA WAWAKILISHI JE MAALIM UNALIJUWA HILO..?


Ukweli usiopingika ni kwamba Moudline Cyrus Castico ni Mzambia wa kuzaliwa na wa kukulia huko Zambia. Kuhamia kwake nchini Tanganyika ((Tanzania)) kumetokana na kumfuata mumewe Joseph Moses January Castico. Alijipenyeza kufikia cheo cha juu kwenye chama cha Mapinduzi, CCM, kupitia UWT na umaarufu wake kuzidi kuenea mpaka pale alipojikwaa kisiki na kuangukia pua pale alipo jinasibisha kwenye kundi la wanaodai haki ya Wazanzibari. Wakati huo Nyerere alikuwa bado yuko hai na kuonekana waziwazi kukerwa na kauli zake , alikiamuru chama kimvue madaraka na moja ya sababu zilizotolewa kuwa alikuwa si mwanachama halali wa CCM kwa vile alikuwa si raia wa nchi ya Tanganyika ((Tanzania.))  Yeye ni Mzambia.
Siku zote MaCCM hujivunia kufuata nyayo za hayati baba  au ndio babu yao wa Taifa Nyerere , hivi ni nani aliethubutu kufuta uamuzi wa Nyerere na kuuhalalisha tena uraia wake....?? Au kwa vile ni kada wa chama tawala CCM.....?? Juzi, Shein Nkurunziza kwa mamlaka aliyonayo amemteua miongoni mwa wateule wake kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, BLW. Hii ina maana kuwa anaweza pia kuteuliwa kushika nafasi nyingine adhimu kama vile uwaziri na baadae hata kugombea/kuteuliwa na Ufalme kama alivyo sasa Sultani Shein Nkurunziza. Inawezekana aliomba uraia wa Tanganyika ((Tanzania.))  Lakini tukumbuke kuwa kila Mzanzibari ni Mtanzania lakini sio kila Mtanzania anaweza kuwa Mzanzibari. Na kama kaomba uraia wa Tanganyika ((Tanzania))  (kwasababu uraia ni suala la Muungano) je Sheria zetu za nchi ya Zanzibar zinasemaje juu ya uraia wa kuomba kwenye ngazi za uongozi wa Kitaifa wa Zanzibar...??
Au ndio la muhimu kwa CCM Zanzibar ni uafrika wake tu kama ilivyo kwa hiyo MiCCM mengine iliyo jazwa hapa nchi, Zanzibar ni nchi ya waafrika, kwa hiyo Moudline anatosha wakati sifa ya uafrika anayo. Tujuwe tu kuwa Zanzibar ni nchi tofauti na nyingine, hata Tanganyika kama si huu muungano ingekuwa ndoto kwa mwenye asili ya Zanzibar kupewa nafasi ya uongozi, na hao wazanzibar unaosikia viongozi kule bara basi ni kwa ajili ya katiba ya muungano. Hakuna hata diwani mzanzibari licha ya mbunge. Hakuna mtu kama mapuri, sefu ali Idd, sepetu, jumbe, ali Hassan mwinyi na wengineo, kwamba wamekuja tu wakapata sauti kwenye nchi. Tanganyika kwa watanganyika, Zambia kwa wazambia, Kenya kwa Wakenya, lakini ajabu Zanzibar ni kwa waafrika wote na Mzanzibari bado kalala anakula urojo forodhani.
KISHA NYINYI MUNAYAITA MAPINDUZI MATUKUFU HIVI KWELI NYINYI MUNAJUWA UTUKUFU NI NINI AU DUNIA IMEWAVA KISAWA SAWA MPAKA MNAKUFURU

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

2 comments:

  1. ah inasikitisha jamaani tuandamaneni kaka zanzu mi kichwa kinaniuma huyu kenge kafikia haya munajua madhara yake makubwa kaeni tu mujifungie ndani duniani kote wanajua kama zanzibar kuna balaaa watanganyika watanganyika munafanya hivi lakini jueni kitawaharimu kama wanzanzibari ucharwa maslahi yanakuekeni kwawa bora tumbo iko siku tutakuwa pamoja na watanganyika wenye imani na sisi na wapo wengi hao ndio wenzetu na hususani watu wote wa chaadema nccr na vyama venginevo na wasokuwa na vyama hao ndio wetu na sisi ni watu wao tutashikamana wakristo wailam ilituishi vizur maisha matamu lakini mafupi tunawaomba watu wakanisani wamwambie sheni aondoke mana hasiikii msikiti wala kanisa bali twaomba mapadri na viongozi wakubwa wa dini zote imuondoe sheni kabla ya asar

    ReplyDelete
  2. huu mchezo kujidai kuwa kura pemba nimezulumiwa muongo m nyie munae hoji eti mwalim sefu kajitangaza sasa yeye kafanya nini kupora kataka atangazwe yeye lanatullah zulma ina mwisho shueni utaondoka tuu kwa nguvu za allah na wanzanzibar watananyika na mataifa yote na the hauge utaenda we na sefu iddi

    ReplyDelete