Tuesday, April 12, 2016

VIDEO-KAULI YA RAIS POMBE MAGUFULI KWA CCM WA TANGANYIKA KUHUSU UMEYA WA JIJI LA DAR RAIS KAULI YAKO KWA CCM ZANZIBAR KUHUSU URAISI LINI UTAWAMBIYA....???

NAKUMBUKA ULESEMA KUWA CCM KUNA WANAFIKI NA UTAWASHUGHULIKIA WANAFIKI HAO JE NIKULIZE RAIS UNAFIKI NI KITU GANI
RAIS MAGUFULI AHUTUBIA WAZEE WA DAR ES SALAAM
KATIKA HUTUBA HII UMESEMA MSEMA KWELI KIPENZI CHA MUNGU
MBONA HUJASEMA UKWELI KUMUAMBIA SHEIN UMESHINDWA WACHIA MADARAKA,
MBONA HUJASEMA UKWELI KUHUSU UCHAGUZI HARAMU WA MARUDIO WA SHEIN NA
KUNDI LAKE LA MAHARAMIA,MBONA HUJASEMA UKWELI KUHUSE SERIKALI HARAMU
ANAYO IUNDO SHEIN,MBONA HUWALINDI WAZANZIBARI NA PEMBA KWA MAZOMBI YA SHEIN,MBONA HUJASEMA UKWELI KWA JESHI ALILO LIMIMINA KIKWETE NCHINI ZANZIBAR KWENDA KUKAMILISHA HARAMU YA KUFUTWA UCHAGUZI NA KULINDA UCHAGUZI HARAMU AU KWA HAYA POMBE MAGUFULI HUTAKI KUWA KIPENZI CHA MUNGU.....???
Unasema tume ya Zanzibar haingiliwi na mtu yoyote, mbona mumepeleka majeshi kituo cha matangazo ya kura ( Bwawani Hotel ILI JECHA AFUTE MATOKEO YA UCHAGUZI HALALI...?? KWA NINI MKAPELEKA MAJESHI TENA ILI WALINDE UCHAGUZI WA HARAMU AMBAO HAUKUPIGIWA KURA NA WANANCHI WA ZANZIBAR LAKINI UKAFANYIKA NA KUMTANGAZA SHEIN KUWA NI MSHINDI NA KURA ZAKE ZIMEKUWA NYINGI KULIKO HATA ZAKO WEWE WAKATI VITUO VYA KUPIGIA KURA VILIKUWA VITUPU..??? ) sisi WAZANZIBAR HATUJAKOSEMEHE DUNIANI NA KESHO 'AKHERA'
CCM WANAPENDA NAMBA LAKINI HAWAJUI HESABU
Jambo moja ambalo CCM wamejifedhehesha wenyewe ni lile la kutangaza kile walichokiita matokeo ya uchafuzi wao bila ya kuzingatia kwamba takwimu zina sifa moja, huwa hazisemi uongo.Vijana wana msemo wao siku hizi; wanasema CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu. Matokeo ya tarehe 20 Machi, 2016 waliyoyatangaza ni kwamba eti jumla ya watu waliopiga kura walikuwa 341,865 na kwamba Dk. Ali Mohamed Shein eti alipata kura 299,982 sawa na asilimia 91.4. Takwimu za uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 zilionesha kwamba jumla ya wananchi waliojitokeza kupiga kura walikuwa ni 402,354 na Dk. Ali Mohamed Shein alipata kura 182,011 sawa na asilimia 46.28.Wakati huo huo kwa uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia, wapiga kura kwa upande wa Zanzibar walikuwa 417,882 ambapo mgombea wa CCM, Dk. John Pombe Magufuli alipata kura 194,317 sawa na asilimia 46.5.Kwa hivyo, kwa kutumia takwimu hizi, mtu anapochukua takwimu hizi na kulinganisha wapiga kura 402,354 waliojitokeza tarehe 25 Oktoba, 2015 na wale wanaodai eti walijitokeza tarehe 20 Machi kwamba ni 341,865 watawala wa CCM walichotaka kutuaminisha ni kwamba tofauti ya waliokuwa hawakujitokeza kupiga kura ilikuwa ni 60,489 tu. Suala la kujiuliza ni kwamba iwapo hilo ni kweli kwa nini vituo vionekane vitupu kabisa tarehe 20 Machi, 2016..??Lakini kwa upande mwengine, mtu anapokosa hata tahayuri na kudai Dk. Ali Mohamed Shein amepata kura 299,982 anachotaka kutwambia ni kwamba ndani ya miezi mitano ya idhilali na mateso aliyowapatisha Wazanzibari ameweza kuongeza kura 117,971.
Kufedheheka kwa CCM kunakuja zaidi kwamba walisahau kwamba waliyakubali matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tarehe 25 Oktoba 2015 kwa upande wa Zanzibar ambapo kama tulivyokwisha onesha waliopiga kura walikuwa wengi zaidi wakiwa ni 417,882 (na hilo ungetegemea lingeinufaisha CCM) na bado mgombea wa CCM akapata kura 194,317 sawa na asilimia 46.5. Kwa kutumia idadi waliyotangaza ya kura 299,982 walizompa Dk. Shein wanataka kutwambia kwamba yeye amepata kura 105,665 zaidi kuliko Dr. Magufuli kwa Zanzibar.Kama takwimu zao zingekuwa sahihi ina maana pia wapiga kura waliomuunga mkono mgombea wa CUF ambao hawakwenda kupiga kura ni 60,489 tu (sawa na asilimia 15 tu). Hivi nani utamdanganya kwamba Maalim Seif Sharif Hamad anaungwa mkono na asilimia 15 tu ya wapiga kura wa Zanzibar..?? Nani utamdanganya kwamba ndani ya miezi mitano, CCM imeongeza kura 105,665 zaidi ya alizopata mgombea wake Dk. Magufuli kwa upande wa Zanzibar..??Kutokana na ubabe na kiburi cha utawala walicho nacho CCM, wameishia kujifedhehesha kwa takwimu zao za kupika wenyewe. Ndiyo vijana wakasema, CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu.


KISHA NYINYI MUNAYAITA MAPINDUZI MATUKUFU HIVI KWELI NYINYI MUNAJUWA UTUKUFU NI NINI AU DUNIA IMEWAVA KISAWA SAWA MPAKA MNAKUFURU


KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment