Tuesday, May 31, 2016

MCHANGO WA KUWAFUTARISHA NA KUWAPA IDI WATOTO MAYATIMA NCHINI ZANZIBAR!

watoto wafutari
Baadhi ya watoto mayatima wakifutarishwa katika Ramadhani ya mwaka jana huko Zanzibar!
Ndugu Wapendwa,
Sote tunaifahamu hali ya maisha duni wanayopambana nayo baadhi ya watoto mayatima nchini kwetu Zanzibar. Hatuwezi kuibadilisha hali yao hio, lakini tunaweza angalau siku moja kuwafutarisha vizuri katika hii Ramadhani ijayo na kuwapa mkono wa Eid siku ya Sikukuu.
Kwahivyo, ZANZIBAR-CANADIAN DIASPORA ASSOCIATION (ZACADIA) ya Toronto, Canada, inatoa wito kwa Wazanzibari wote wanaoishi nje kuungana pamoja ili kuwafutarisha watoto hao mayatima na kuwapa mkono wa Eid siku ya Sikukuu.
Kama unaguswa na hali ya mayatima kule Zanzibar basi changia chochote unachokiweza ili watoto hao mayatima wafutari vizuri angalau hio siku moja katika Ramadhani ijayo na siku ya Sikukuu wapate mkono wa Idi.
Tafadhali changia and Allah will reward you, Inshaa Allah!
Hii kampeni itamalizika Ramadhani ya 10, ili kabla Ramadhani haijesha tupate muda wa matayarisho ya shughuli ya kufutarisha hao mayatima kule Zanzibar na pia kupata muda wa kuwanunulia nguo za Sikukuu, kwani hali zao kama mnavyoona pichani hapa juu ni taabani
Tuma mchango wako kwa muwakilishi aliekuwepo karibu na wewe:
CANADA:
Hassan Othman @+1.647.404.8618 (Toronto)
Bi Shahida Hamad @+1.289.696.3089 (Toronto)
U. S. A
Mohammed Masoud @1.330.880.9524 (Ohio)
UNITED KINGDOM:
Miss Fauzia Karama @+44.7847.024.456 (Manchester)
Abdalla Juma (Dulla Ndende) @ +44.7909.225.287 (Milton Keynes)
CONTINENTAL EUROPE:
Dr. Muhammed Mwinyi Khami @ +46.70.426.9707 (Scandinavia / Sweden)
Nabil Salum (Nasser) / NASMO @ +32.487.28.39.96 (Belgium)
MIDDLE EAST:
Mohamed Omar @ +971.50.424.6878 (Dubai, U.A.E)
Ali Said Ali @+968.9.509.7454 (Muscat, Oman)
FAR EAST:
Suleiman Ali Al Rawahy @+81.80.4027.3510 (Japan)
Source: zacadia.com

No comments:

Post a Comment