Sunday, May 1, 2016

MSAADA WA HARAKA UNAHITAJIKA KUOKOA MGUU WA KIJANA HUYU!

MSAADA WA HARAKA UNAHITAJIKA KUOKOA MGUU WA KIJANA HUYU!
Bwana Daudi ambaye anaonekana katika picha, anahitaji msaada wa HARAKA wa fedha kwa ajili kusafirishwa kupelekwa jijini Dar es Salaam ili kuokoa mguu wake wa kushoto.
Alipata ajali ambayo imesababisha kuharibika sehemu kubwa ya mguu wake na kuna uwezekano mkubwa wa kukatwa kwa mguu huo endapo atakosa matibabu ya haraka yanayohitajika.
Ili kusaidia kuokoa mguu wake usikatwe, msaada wa fedha wa haraka zaidi unahitajika kwa ajili ya kuuwahi mguu wake kwa ajili ya matibabu kabla haujaharibika zaidi na hatimae kupelekea kukatwa.
Bwana Daudi kwa sasa yupo Zanzibar, yeyote atayeguswa na kuwa na wasaa wa kuchangia katika hili anaombwa kutuma mchango wake kwa kutumia tiGO pesa.
Nambari ya kutuma ni +255 715 448 943, jina la akaunti ni Ismail Ali Abeid.
Mchango wako ni muhimu sana katika kusaidia kuokoa mguu wa kijana huyu.
Ahsante!


No comments:

Post a Comment