Monday, June 13, 2016

MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD AHUDHURIA NA KUHUTUMBIA MKUTANO ULIO ANDALIWA NA TAASISI YA CENTER FOR STRATEGIC NA INTERNATION STUDIES (CSIS) NCHINI MAREKANI


Maalim Seif aendelea na ziara yake nchini Marekani.
Ikiwa ni katika muendelezo wa ziara yake ya kichama nchini Marekani, jioni ya leo Maalim Seif Sharif Hamad ameshiriki katika mhadhara ulioandaliwa na taasisi ya Center for Strategic and International Studies (CSIS) ya nchini Marekani.
Kupitia Muhadhara huo Maalim Seif alipata muda wa kutosha kuzungumzia ubakwaji wa demokrasia ya nchi yetu ya Zanzibar uliofanywa tarehe 28 Oktoba 2015, ambao ulifuatiwa na kile kilichoitwa uchaguzi haramu wa marudio wa tarehe 20 Machi 2016.
Katika muhadhara huo Maalim Seif ameweka wazi mambo kadhaa yaliyotokea ikiwa ni pamoja na sababu za kwanini CUF haikushiriki kile kilichoitwa Uchaguzi wa marudio.
Pia alipata nafasi ya kujibu masuali kadhaa yaliyoulizwa na Waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa, moja katika suali ambalo amelijibu kwa ufasaha mkubwa ni propaganda zinazoenezwa kuwa CUF ni chama cha kidini; amejibu kwa kuweka wazi kuwa CUF ni chama cha kidemokrasia ambacho tangu kuanzishwa kwake kimekuwa kikipigania umoja na mshikamano wa Wananchi wa itikadi na dini tofauti Zanzibar na Tanganyika kwa ujumla (Tanzania).
Maalim Seif ametahadharisha kuwa kuendelea kupuuzwa kwa matakwa ya wananchi kunaweza kuwashawishi wananchi wa Zanzibar hasa vijana kutumia njia nyengine ili kuweza kuitafuta haki yao iliyoporwa na watawala.
Kiujumla mjadala wa leo umetoa taswira kuwa, Chama Cha Wananchi CUF ni chama kinachosimamia misingi ya demokrasia ya kweli kwani muda wote tangu kurudishwa kwa mfumo wa vyama vingi kimekuwa kikitumia njia za amani na kidemokrasia kutetea haki yake.
Na kubwa zaidi imetudhihrishia kuwa Wazanzibari hawako peke yao katika kuitafuta haki yao iliyoporwa na Watawala na kwamba dunia nzima inawaunga mkono katika kuipigania haki ya Wazanzibari.

No comments:

Post a Comment