Sunday, June 19, 2016

VIDEO-DUA MAALUMU KUWAOMBEA MADHALIMU WA ZANZIBAR


omar heri
Wazanzibari na waislamu wote Nchi nzima wanaombwa katika kumi hili la pili la “Maghfira” la Ramadhani kumuelekea
Mwenyezi Mungu (S.W) ili kumuomba awaangamize wote walioshiriki katika matendo ya udhalilishaji raia, Ya kupigwa na kukamatwa wananchi ovyo, kupigwa risasi, Utekwaji wa raia, ubakaji, udhalilishwaji wa wanawake na matendo mengineyo yaliyofanywa na makundi ya mazombi na vyombo vya ulinzi na usalama kwa amri za viongozi wa Nchi.
Kumshtakia Muumba wa mbingu 7 na ardhi 7 juu ya dhulma waliofanyiwa wazanzibari na kuporwa haki yao tarehe 25/10/2015.
Baadhi ya viongozi wa Serikali ambao ni wasimamizi wa dhulma wanayofanyiwa wazanzibari wamefanya kiburi hadi kutoa lugha za waziwazi juu ya mashekhe wa Zanzibar kwamba ‘wananyea ndooni’ na kwamba wao wapo nyuma ya dhulma wanayowafanyiwa mashekhe hao, ni mwaka wa tatu hadi wawekwe ndani bila ya kushtakiwa na kesi yao kutolewa hukumu.
Sote kwa pamoja tunyanyue mikono yetu juu kumuelekea Mwenyezi Mungu na kumuomba katika kumi hili la Maghfira:
“Ewe Mwenyezi Mungu Mtukufu mimi Mahuluku wako Mnyonge nisie na nguvu naungana na waumini wa misikiti zaidi ya 200 ya Unguja na Pemba inayokaliwa itikafu ndani ya kumi hili la Maghfira, Kukuomba usimpe Maghfira Dikteta Ali Mohammed Shein, Nduli Seif Ali Iddi, Jecha Salim Jecha, Haji Omar Kheri na wote waliohusika kwa njia yoyote katika kadhia hii na wale waliomo ndani ya BLM, BLW, wakuu wa Vikosi Vyote na wasakatonge wanaosambaza fitna na ubaguzi katika Nchi.
Tunakuomba Wadhalilishe, Wafedheheshe, hadi warejeshe haki ya Wazanzibari walioipora Oktoba 25, 2015.Siku ya Ijumaa tarehe 24/06/2015 saa 8:00 kamili usiku patasaliwa rakaa mbili halafu zitafuatiwa na kusomwa kwa SALATUN NARIA mara 4440 katika Misikiti 200 ya Unguja na Pemba itakayofaatiwa na dua mbali mbali kumuomba Mwenyezi Mungu awahukumu viongozi wa dhulma ya Oktoba 25, 2015.
Ewe Mzanzibari na Muislam usikose kushiriki katika dua hii muhimu ukiwa nyumbani kwako. Kila Muislam anatakiwa kusali rakaa mbili na kusoma SALATUN NARIA mara 4440 kama ilivyopekelewa katika hadithi mbali mbali za Mtume Muhammad (SAW):
“ALLAHUMMA SWALLI SWALATAN KAAMILA,
WASALLIM SALAAMAN TAAMMA, ALAA SAYYIDNAA MUHAMMAD,
ALLADHII TANHALLU BIHIL-ÙQAD, WATANFARIJU BIHIL KURAB,
WATUQDHAA BIHIL HAWAARIJ, WATUNAALU BIHI RRAGHAAIB,
WAHUSNUL KHAWAATIM, WAYASTASQAL GHAMAAMA BIWAJHIHIL KARIIM,
WAALAA AALIHI WASWAHBIHI FII KULLI LAMHATIN, WANAFASIN, BIADADI KULLI MAALUUMIN LAK”
Tafadhali wafikishie ujumbe huu wengine.
WABILLAHI TAUFIQ

No comments:

Post a Comment