Friday, July 1, 2016

JESHI LA DIKTETA UCHWARA LIMESHIKA KASI KUWATESA NA KUWAFUNGA WATU JELA BILA YA KUSAHAU WANAO PINGWA RISASIDIKTETA UCHWARA MSAIDIZI ZANZIBAR!
Wenyeviti na makatibu wote wa CUF wa mkoa wa Kusini Pemba toka majuzi waliletewa barua za kwenda polisi Chake chake na Leo ni siku ya 5 wameshikiliwa kituoni hapo bila dhamana wala kupelekwa mahakamani. Ni pamoja na Mhe. Hija Hassan.Hija (mwakilishi jimbo la Kiwani), Mhe. SEIF mwakilishi wa jimbo la Mkoani na dereva wa Mhe Masoud (mbunge wa jimbo la Mtambile).
MY TAKE;
Mkuu alisema yeye anapeleka majeshi tu, mengine hayamhusu. Ni kweli sasa tunashuhudia nguvu na ubabe wa majeshi huko Zanzibar. Na hapo hatujaongelea watu wanaopigwa risasi kila kukicha, kwa bahati mbaya vyombo vyetu vya habari vimejiweka mbali na kuripoti yanayotokea Zanzibar. Pamoja na kuwa Bara tuna msiba wetu, huwenda msiba wa Zanzibar ni mkubwa zaidi. Yale aliyoyaona Tundu lissu Central Police ni ya kawaida kabisa Zanzibar, Zanzibar inajiendesha kama nchi isiyo na sheria wala katiba. Na dikteta uchwara msaidizi anafanya atakalo, hakumbuki historia. Shame on this current leadership.
Mtatiro J.

No comments:

Post a Comment