Friday, July 22, 2016

PART 8 MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD ANAENDELEA NA ZIARA YAKE HUKO NCHINI UHOLANZI NA KUBISHA HODI (ICC) INTERNATIONAL CRIMINAL COURT

Saa 3:30 hadi saa 5:00 asubuhi leo Ijumaa, tarehe 22 Julai, 2016, ujumbe wa CUF ukiongozwa na Maalim Seif Shariff Hamad ulifika Mahkama ya Kimataifa ya Uhalifu (International Criminal Court - ICC) mjini The Hague ambapo ulipokelewa na kukutana na mmoja wa wanasheria mahiri wa ICC.
Kabla ya kufika ICC leo asubuhi, hapo jana, saa 9:30 mchana Maalim Seif na timu yake walikutana na Wakili mmoja mashuhuri wa kimataifa wa hapa Uholanzi ambaye kupitia kampuni yake ana rekodi kubwa ya kusimamia kesi za ICC.
CUF imeipa kampuni hiyo jukumu la kuandaa na kuwasilisha ICC maelezo na vielelezo vinavyohusiana na uhalifu dhidi ya ubinadamu vilivyotendwa na vinavyoendelea kutendwa na vyombo vya dola Zanzibar kwa maelekezo ya wakuu wa mamlaka mbali mbali.
Taarifa kuhusu hatua nyengine na taratibu zitakazofuata baada ya hatua ya jana na ya leo zitatolewa kila hatua moja itakapokamilika.

No comments:

Post a Comment