Sunday, July 31, 2016

PICHANI ALIYEVAA SHATI LA DRAFTI NI SAYYID JAMSHID ALIYEKUWA MFALME WA NCHI YA ZANZIBAR
Pichani aliyevaa shati la drafti ni aliyekua mfalme wa nchi ya Zanzibar kabla ya Mapinduzi na Mauwaji ya Wazanzibari ya mwaka 1964 Sayyid Jamshid.
Hapo amehudhuria maziko ya marehemu Nassor Marjeb yaliyofanyika siku ya Ijumaa tarehe 29/07/2016 mijini Portsmouth Uingereza.
Marehemu alikua afisa mkuu wa upelelezi katika jeshi la polisi kabla na baada ya Mapinduzi,Na baadae akakamatwa kama walivyo kamatwa Wazanzibari wengine na kuwekwa kuzuizini katika gereza la Bamkwe baada ya kuachiwa alikimbilia Uingereza hadi kifo chake.Mungu amlaze mahali pema peponi-Ameen.Sasa yukumbushani jambo moja 
Kuna msemo unasemwa ukitaka kumtawala mtu fanya mambo matatu.mtie ujinga .mnyime elimu .mtie umaskini.na hilo ndilo walilofanya Wakoloni,Makaburu,Masultani Weusi Tanganyika juu ya Zanzibar na kwa Wazanzibari kwa ujumla wametiwa ujinga,wakanyimwa elima na wanaendelea kunyimwa elimu maana majuzi tu tumeona jinsi maskuli yalivyo feli vibaya vibaya na sasa tumetiwa umasikini mpaka Wazanzibari tunakula ugali asubuhi na chai kuna watu mpaka leo atii wanaambiwa na kuamini musimpe kura maalim seif atamrudisha JAMSHID zbar.huyo aliyevaa shati nyeupe ya drafti ni mfalme aliyetawala zanzibar anaitwa JAMSHID kabla ya hayo yanayoitwa mapinduzi.sasa watu wanaambia eti atarudi kuja kutawala tena zbar na atawafanya watumwa na ukoloni utarudi Zanzibar hebu muangaliene huyu kweli anahaja ya kuwa Sultani...?

Ukweli hausemwi hii ni nyimbo tu ili Wazanzibari tuzidi kulala na Mkoloni Mweusi Tanganyika azidi kutumaliza.Wazanzibar tubadilikeni hakuna muarabu atakaekuja zanzibar hebu angalieni nchi zao Oman,Qatar,Dubai, n.k. kama hamuwezi kufika huko hebu ingieni katika youtube muangalie video za nchi zao kisha mujiulize kweli mtu kama huyo iwache nchi yake aje kungangania kuishi kitope,mwera,bumbwini,tumbatu kwa lipi haswa....? hii ni bla bla bla tu ya Chama hichi cha Mkoloni Mweusi Tanganyika CCM kuendelea kuitawala nchi yetu ya Zanzibar na kuimaliza na sisi bado tu ati tumejipanga mwaka huu wataisoma nani anae isoma wao wanamaji ndani ya majumba yao sisi maji hayatoke nchi zao zina umeme sisi hatuna tulilo nalo,nchi zao wanakula wanavyotaka sisi ukipata mlo moja basi siku hii ni Eid Mubaraka hospitali zao madokta na manasi na madawa kila kona sisi mnazimoja mpaka glavis na pamba uje nazo mwenyewe hii sisi wazanzibari tuna nini kuwa hatuoni haya Mkoloni Mweusi Tanganyika anaitawala Zanzibar na kuwatawala Wazanzibari wanagaiwa mapande mapande kwa kutumiwa nano hizibu na hao vibaraka wao vijibwa koko vimo vinaendelea uhizbu na watamleta muarabu hatujaskia Tanganyika kuambiwa musimchaguwe mbowe au chadema atamrudisha Mjerumani au Muengereza aje atawale Tanganyika. Ila Zanzibar.mabalaa yote yanasukumizwa Zanzibar muarabu mara hizibu.mara huyu nani..wazanzibar wote ni wamoja na Zanzibar ndio pao hawana pakwenda achenu upumbavu na tumtimuwe Mkoloni Mweusi Tanganyika kisha tujenge nchi yetu ya Zanzibar au ashike adabu yake na adabu imshike kisha tutamuambia ni nini tunachotaka kushirikiana nae ili tuishi kwa salama na majirani zetu lakini huyu Mkoloni Mweusi Tanganyika lazima nchi hii aiteme akitaka asitake ataitema tu wareno walitema waingereza walitena masultani walitena na huyo Mkoloni Mweusi Tanganyika na vijibwa vyake hapa Zanzibar lazima waiteme.

No comments:

Post a Comment