Monday, August 1, 2016

VIDEO-NCHINI ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI YUTAABANI

13895403_1052973924797767_177140258603422483_n
Wakati wafuasi wa chama cha wananchi CUF na Wazanzibari kwa ujumla wakisubiri kwa hamu mafanikio ya ziara za Maalim Seif Shariff Hamad Nchi za Nje kwa awamu ya pili,, hali ni tete kwa upande wa CCM na makada wao. Hii ni baada ya kufahamika kua hali ya afya ya Balozi Sefu Ali Iddi inazidi kua mbaya kadri siku zinavyokwenda jambo linalomfanya kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kichama na kiserikali yanayomkabili kila siku. Balozi Sefu hivi karibuni aliondoka nchini na kuelekea nchini Cuba kwa safari ya kimatibabu ambapo taarifa za ndani zinaeleza kua ugonjwa unaomsumbua Balozi umeshindikana nchini humo na kulazimika kukaa Lugalo kwa ajili ya matibabu lakini hata hivyo Lugalo nako waligonga mwamba na kulazimika kurudi nchini Zanzibar.


Taarifa kutoka kwa baadhi ya wanachama wa CCM zinaeleza kua kwa sasa hali ya afya ya Shein na Balozi zimekosa muarubaini na inaseleleya kuwa mbaya zaidi, na ndani ya wiki hii hali hiyo imezidi kua tete kwa Balozi na anashindwa kutekeleza kabisa majukumu yake ya serikali yao ya kulazimisha kama makamo wa pili wa raisi. Kutokana na hali hiyo baadhi ya wana CCM wanaeleza kua Makada kadhaa wakiwemo Dr. Mwinyi Haji Makame, Dr. Khalid na Haji Omar Kheir tayari njaa ishawashika na kuwaja wanataka kurithi nafasi ya Makamo wa Pili bandia ya Rais wa Zanzibar kama hali ya Balozi Sefu itashindwa kutengemaa. Pia ipo hofu kubwa kwamba Balozi Sefu amelazimishwa kuhudhuria katika Mkutano Mkuu utakaofanyika tarehe 23/7/2016 huku mdomo ukiwa bado umekaa upande. Mkutano huo ulikua na lengo la kumkabidhi Rais Magufuli kijiti cha Uenyekiti wa Chama. Balozi anasumbuliwa na presha ya macho na maradhi ya ngozi ambayo yamempelekea kufanya mabalanga mwili mzima yanayotoa uchafu na harufu mbaya na maji maji.

No comments:

Post a Comment