Thursday, August 4, 2016

RAIS WA NCHI YA TANGANYIKA POMBE MAGUFULI SIO MSEMA KWELI WALA SIMPENDA HAKI TANGULINI CCM KUPENDA HAKI NA KUSEMA KWELIAskari Polisi wakiwa katika mafunzo maalumu ya kupokea simu katika kituo kipya cha kupokelea simu za dharura (CallCentre) 
Rais Pombe Magufuli na IGP Enerst Mangu, wamekula njama dhidi ya wapinzani wa kisiasa na mkakati maalumu wa kukandamiza haki za binadamu na demokrasia na kuhakikisha upinzani unakufa na nchi nzima inafuata amri ya mtu moja kama mbuzi ninalo taka kumuambia Pombe Magufuli zama hizo zishapita funguwa macho. ISHARA zote za utawala wa nchi ya Tanganyika, chini ya uongozi wa Pombe Magufuli zimeshajidhihirisha wazi wazi kwamba kiongozi huyo amechanganyikiwa, hajui atokako wala endako. Kwa ufupi niseme, ameshapoteza dira. Rais huyu wa nchi ya Tanganyika, Pombe Magufuli…nasema ‘Rais wa Tanganyika’ kwa sababu kwa kauli yake mwenyewe aliikana nchi ya Zanzibar, akasema haimuhusu na wala hawezi kuingilia masuala ya nchi ya Zanzibar, kwa sababu Zanzibar ina serikali yake safi sana sisi Zanzibar tumefurahi sana sana sana kwa kauli hii ya Rais huyu wa nchi ya Tanganyika Wakoloni Weusi. Pombe Magufuli aliikana nchi ya Zanzibar, wakati ule yalipofutwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana matokeo halali ambayo yalionyesha wazi jinsi Chama Chao Cha CCM cha Wakoloni Weusi Tanganyika kimekataliwa na hakifai tena kuendeleza Ukoloni wa Kitanganyika nchini Zanzibar na jikoni yaani CCM, wakawa wanapika jungu lao la uchaguzi mwingine. Huu ulikuwa si uchaguzi bali ulikuwa ni uchafuzi na danganya toto wa Machi 20, mwaka huu.
Kauli ile ya Pombe Magufuli ya kudai kuwa hahusiki na nchi ya Zanzibar na hawezi kamwe kuingilia masuala ya nchi ya Zanzibar, ndiyo iliyopelekea kuwamsha Wazanzibari ambao bado walikuwa wamelala na sasa kujuwa kuwa alaa kumbe na kuamuwa  kumwita Rais wa nchi ya Tanganyika. Ingawa kauli yake ile ilikuwa imejaa unafiki, ufisadi na uharamia dhidi ya Wazanzibari waliyo wengi. Pombe Magufuli, baada ya kukataa kusaidia kuleta suluhu ya kile kilichoitwa ‘Mkwamo wa Kisiasa nchini Zanzibar’ alijibadilisha na kujivisha nguvu za ufisadi kwa kutumia cheo cha Amiri Jeshi Mkuu. Alimwaga Unguja na Pemba, utitiri wa jeshi na silaha nzitonzito, mpaka vifaru sasa bado tunamuliza ulisema mwenyewe mwenyewe kuwa mambo ya Zanzibar haimuhusu na wala hawezi kuingilia masuala ya nchi ya Zanzibar, kwa sababu Zanzibar ina serikali yake sasa vipi tena ukatumwagia majeshe wewe Pombe Magufuli Dikteta Uchwara Mkoloni Mweusi....??? Alisema hataingilia mambo ya Zanzibar, kwa kuwa hayamuhusu. Lakini kupeleka majeshi na silaha za kivita kwa lengo la kuuwa Wazanzibari, hilo linamuhusu. Alikataa utu na uungwana, akaamua kukumbatia ushenzi na utwana kwa hiyo unatuonyesha wazi kuwa huko tayari kuleta suluhu ili Wazanzibari waishi kwa salama na amani munayo jidai kuipigia debe kila munapokuwa majukwani ila uko tayari kuwauuwa wote ndio maana ya kuleta majeshi na vifaru. Tangu siku alipokataa kusimamia haki katika uchaguzi wa nchi ya Zanzibar, akawaiga akina Mkapa na Kikwete huku akijifanya ni mpenda haki (mtumbua majipu), moja kwa moja nilimuingiza kwenye kapu la watu wanafiki waliyozoea kudhulumu.
Anaposema ‘Msema Kweli Mpenzi wa Mungu’ anaisema kinywani tu bila kufahamu kwa undani tafsiri ya neno hilo. Msema kweli hasiti kusema ukweli hata kama nafsi yake itaathirika, muhimu ni kusema ukweli ili kumridhisha Mwenyezi Mungu. Pombe Magufuli si msema kweli wala si mpenda haki ni mnafiki wa shoka maana kama ni msema kweli na mpenda haki basi alikuwa awambiye tu CCM Zanzibar mumeshindwa uchaguzi kubalini na mujipange tena kwa 2020 hapo angelikuwa amesema ukweli na kama ni mpenda haki alikuwa asema jamaa huyu Maalim amedhulumiwa haki yaki tokea kuanzishwa kwa uchaguzi za vyama vingi anashinda hapewi haki yake mimi napenda haki kwenye utawala wangu mimi sitakubali adhulumiwe haki yake kwa hiyo apewe haki yake kashinda apewe haki yake hiyo ndio mpenda haki sio kumimina majeshi na vifaru na kushadidia kuapishwa Shein kwa lazima na kumlinda Shein kwa nguvu zote za Jeshi lako la Mkoloni Mweusi Tanganyika kisha unajidai unapenda kusema kweli na unapenda haki hakuna CCM hata moja anaependa haki na msema kweli wote wote CCM Chama Chenyewe kimeanzishwa kwa njia za uwongo na kuvunja haki vipi nyinyi mtatenda haki na kusema kweli wakati mumezaliwa ndani ya Chama kilicho undwa kwa kuvunja haki na kusema uwongo nyote mumekula na kushiba uwongo na kuvunja haki umejidai kujifanya ni Rais ambaye hajapata kutokea lakini sasa makucha ya CCM ya Chama kilicho undwa kwa kuvunja haki na kusema uwongo yanaanza kuchomoza huwezi kuyazui makucha CCM ni Chama kilichocho anzishwa kwa kusema uwongo na kimeanzishwa kwa kuvunja haki.
Pombe Magufuli, ishara zote za unafiki katika uongozi wake amezibainisha katika muda mchache aliyoshika madaraka. Kwa mfono: Anashirikiana na Madikteta, Yoweri Museveni na Poul Kagame ambao wamekubuhu katika kuwatesa raia na viongozi wa upinzani na kuuwa. Pombe Magufuli tangu siku aliyoingia Ikulu, amekuwa kiongozi wa ajabu na kushangaza katika masuala ya ‘human rights and democracy’ hoja ambayo imepoteza ile kauli mbiu yake ya ‘Hapa Kazi Tu’. Kwa ufupi amepoteza dira na mwelekeo. Ameanza kujiimarishia uadui mkubwa ndani ya nchi na makundi mbali mbali. (l) Ana uadui na upinzani wa vyama vya kisiasa (ll) Ana uadui ndani ya CCM anayoiongoza (lll) Ana uadui na nchi ya Zanzibar. Hao ndiyo maadui wakubwa wa Pombe Magufuli. Kwa sababu Wazanzibari kwa sasa hawasikii tena la muwadhini wala la mteka maji msikitini wanataka nchi yao. Na katika madai ya nchi Wazanzibari hawatafuni maneno. (lV) Halafu ana uaduia na taasisi za utumishi wa umma anaowatumbua. Kwa ufupi: Pombe Magufuli amekuwa kiongozi wa ajabu tangu uhuru wa nchi ya Tanganyika, hajawahi kutokea kiongozi wa ‘design’ hii, wakati mwingine anashangaza kuwa msomi wa PhD anaongoza nchi kama mwanafunzi wa shule ya ngumbaro. Ingawa kuna taarifa kuwa siku hizi anafanya ‘english course’. Vichekesho vitupu ati anafanya english course Vichekesho vitupu kweli kweli. Kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ imeanza kupotea haitoki tena vinywani mwa wanaCCM, mitaani na kwenye mitandao ya jamii na hii ni kwa sababu mwenye kauli mbiu hiyo amekuwa kama kinyonga. Na hali ya maisha ya Watanganyika, itazidi kuwa mbaya huko mbele twendako.
Tundu Lissu, amekamatwa na Jeshi la Polisi baada ya kumaliza kuhutubia wananchi katika mkutano wa hadhara, Singida. Soma ujumbe wake aliotuma:
——— Ujumbe alioandika Tundu Lissu——
Wakubwa salaam. Ninawaandikieni maneno haya nikiwa chini ya ulinzi wa polisi Singida.
Nimemaliza kuhutubia mkutano wa hadhara mji mdogo wa Ikungi ambao ni makao makuu ya Jimbo langu la Singida Mashariki.
Mara baada ya kushuka jukwaani nimefuatwa Regional Crimes Officer wa Mkoa wa Singida aliyejitambulisha kwa jina la Babu Mollel na kunitaarifu kuwa ameelekezwa na Regional Police Commander Singida nikamatwe.
Apparently kuna amri ya kunikamata iliyotoka Dar es Salaam. Kwa hiyo niko nguvuni na ninasubiri maelekezo ya RPC juu ya wanakotakiwa kunipeleka.
It’s likely nitasafirishwa Dar usiku huu. In fact ni usiku huu kwa taarifa za sasa hivi.
Kwa vyovyote itakavyokuwa, there’s no turning back. There’s no shutting up.
Nitapambana kutetea haki yetu ya kuwasema watawala popote nitakapokuwa, whether in freedom or in jail, as long as I’ve a voice to speak with.

No comments:

Post a Comment