Saturday, August 6, 2016

TUNDU LISSU A.K.A. RONALDO AIBUWA MTIKISIKO WA AINA YAKE KATIKA MAHAKAMA ZA HAKIMU MKAZI KISUTU


Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria wa CHADEMA, Tundu Lissu, aliibua mtikisiko wa aina yake katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dsm jana wakati alipofikishwa kukabiliana na tuhuma atii za uchochezi. Baada ya kupandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka yake, ubishani mkali wa kisheria uliibuka na kudumu hadi giza lilipoingia mishale ya saa 2:25 usiku, ikiwa ni moja wapo ya kesi nadra za aina hiyo kunguruma hadi usiku. Lissu alikamilisha taratibu za kujidhamini mwenyewe saa 2:56 usiku baada ya kutimiza masharti kadhaa likiwamo la kusaini hati ya dhamana yenye thamani ya Sh. milioni 10.

No comments:

Post a Comment