Wednesday, August 3, 2016

TUNDU LISSU AKAMATWA NA ASKARI SINGIDA


TUNDU LISSU AKAMATWA NA ASKARI WA DIKTETA UCHWARA JOHN POMBE MAGUFULI.
Breaking News!!!!!!! Wakubwa sana salaam. Ninawaandikieni maneno haya nikiwa chini ya ulinzi wa polisi Singida. Nimemaliza kuhutubia mkutano wa hadhara mji mdogo wa Ikungi ambao ni makao makuu ya Jimbo langu la Singida Mashariki. Mara baada ya kushuka jukwaani nimefuatwa Regional Crimes Officer wa Mkoa wa Singida aliyejitambulisha kwa jina la Babu Mollel na kunitaarifu kuwa ameelekezwa na Regional Police Commander Singida nikamatwe. Apparently kuna amri ya kunikamata iliyotoka Dar es Salaam. Kwa hiyo niko nguvuni na ninasubiri maelekezo ya RPC juu ya wanakotakiwa kunipeleka. It's likely nitasafirishwa Dar usiku huu. In fact ni usiku huu kwa taarifa za sasa hivi. Kwa vyovyote itakavyokuwa, there's no turning back. There's no shutting up. Nitapambana kutetea haki yetu ya kuwasema watawala popote nitakapokuwa, whether in freedom or in jail, as long as I've a voice to speak with. Sitakubali kunyamazishwa na Dikteta Uchwara. Msikubali kunyamazishwa na Dikteta Uchwara. Aluta continua! !!!!!
Tundu A.Lissu

No comments:

Post a Comment