Tuesday, August 16, 2016

VIDEO-BALOZI SEFU ALIUTUMIA VIBAYA MDOMO WAKE.Balozi Sefu yuko nchini India kwa ajili ya matibabu na safari hii ya India imekuja baada ya magonjwa yake kushindikana nchini CUBA ambako inasemekana alienda pia kwa ajili ya matibabu.

Sote tunakumbuka Balizi Sefu alivyoutumia mdomo wake kuwadhalilisha hadharani mashehe wa Uamsho huku akijisifia kwa kusema kua wananyea ndooni. Pia Balozi Sefu alisikika akimwita Maalim Seif bwege na kuahidi kua wao wataendelea kumpiga kwa vile kiongozi huyo ni bwege.

Haya yote Balozi Sefu aliyasema akitumia mdomo wake na kusistiza kwa mkono wake wa kulia huku akisahau kua dua za mwenye kudhulumiwa (Wazanzibari) M/Mungu hawezi kuzipuuza. Hatimae Balozi sasa yanayomfika anamtafta mchawi wakati mchawi ni yeye mwenyewe.

Balozi Sefu mdomo wake umepinda sasa na zipo taarifa kua anatumia zaidi mkono wa kushoto baada ya mkono wake wa kulia kupata stroke na kupungua nguvu. Pia Balozi Seif anatazamiwa kua huenda akapoteza nafasi yake ya umakamo wa pili kutokana na hali yake ya afya kuzidi kua mbaya.

Wako wanasema kua Balozi Sefu haumwi na chochote lakini bila ya shaka hawa ni wale wanaosubiri kuskia yuko mahututi au waskie taarifa kutoka katika Serikali yao haramu au chanzo chao cha habari cha CCM (ZBC)ndipo waamini jambo ambalo ni kugumu sana kutokea.

Sisi tunayasema haya na kuwathubitishia kwa picha sasa mwenye macho ataona na mwenye maskio bila ya shaka muda ukifika ataskia.

# ZANZIBAR NI NJEMA ATAKAE AJE #

2 comments:

  1. Nimepost comment Tangu asubuhi mpaka sasa hamjaiweka. Kwa nini? Hivyo ndio inavyo waonesha jinsi nyie watu mnavyotaka tugawa wa zanzibari. Kama kweli mnataka HAKI kila comment mngezipublish na sio za kumsifu seif tu. Kwani tuko wengi tunaotaka zanzibar huru kwa kupitia vyama vengine sio lazima tuwe ccm au cafu. Na pia tunahitaji tusikilizwe. After all sisi sote ni wazanzibar na tunahaki sawa.

    ReplyDelete
  2. kawaida tunajitahidi sana kuposti komment ikiwa haikutumwa basi hakutufikia sisi kwa bahati baya au kunamatusi huwa tunajitahi kuto kuruhusu matusi samahani ikiwa komment yako hukuiona hapa ila elewa itakuwa haijatufikia sisi au labda ilikuwa na matusi ndio maana haikuruhusiwa.ZANZIBAR KWANZA ZANZIBAR KWANZA ZANZIBAR KWANZA.

    ReplyDelete