Saturday, November 12, 2016

MWAKA 1964 WALENGWA WALIKUWA NI WAARABU TUKAWAPA JINA (MASULTANI) MWAKA 2017 WALENGWA NI WAFRIKA MAPINDUZI DAIMA KIDUMU CHAMA CHA KUPINDUWA WAZANZIBARI NA KUWAUWA WAZANZIBARI CCM

IMG_3726
Salama Aboud Talib
Waziri wa Dhulma na Madhalim,ardhi makazi maji na nishati na mazingira
Waziri wa ardhi Bibi Salama Aboud Talib ametangaza kiama kua ifikapo febuary 2017 yani miazi 4 tu kutoka sasa kua atazitaifisha viwanja vyote vilivyo kua vimezungumshiwa kuta au viwanja vyenye foundetion ya nyumba bila kulipwa fidia au mkopo wakukopeshwa wahusika kuendeleza majengo yao. Nikimnukuu anasema hio ni kwamujibu wa sheria ya Zanzibar ya 1984 kua ardhi ni mali ya Serekali. Sasa wana ukumbi tujiulize ok ardhi ni mali ya Serekali..? Jee hio Serekali ni akina nani....?? Sisi maskini wazalendo wa nchi yetu tulio hapa nchini Zanzibar ambao kila siku tunasema  tumepindua sasa sisi hatumo katika Serekali hio alio itaja Mh Bibi SALAMA ABOUD TALIB...??

Huwa tunasema kila siku Tumepindua 1964 kwa kuondosha zulma,ubagizi na unyanyasaji ili tuishi kama wananchi walio huru katika nchi yao na ardhi yao. Sasa sheria hii ya ukandamizaji ya wenyewe kwa wenyewe wafrika kwa wafrika wa Wazanzibar tunao jinasibu kua tuko huru ndani ya nchi yetu huyu Bibi kapewa na nani...? Kama ni sheria ya Serekali ya mapinduzi ilipindua kwa lengo hilo hapo juu...?? basi chama cha CCM kimefeli na Serekali yake kuenzi mapinduzi na mazumuni ya mapinduzi. Hii watakayo ifanya ita wa cost sana na litakua ni donda sugu jingine kubwa zaidi tukiachana na lile la 1964, hili litakua kushinda lile maana watatifua chuki baina ya Serekali ya CCM na wananchi wake ambao ni Wafrika sio Warabu kama walivyo sema 1964 mara hii ni Wafrika wenzao. Wako vigogo waliokua nyuma ya msukumo huu wa huyu Bibi Lakini wajuwe likipasuka hili litakua silammoja na CCM Zanzibar itakua haina manusura kwa kukatika vipande vipande’jaribuni tuone...??

Hata kama ni Sheria lakini hio sheria hapa kwa style hii haikuangalia huruma za maskini Wananchi wa zanzibar wa kipato cha chini ambao ndio wengi nchini Zanzibar. ikiwa leo Mzanzibar kajaaliwa angalau hajajipangaa vizuri kupiga foundation lakini kajaliwa tu kuzibia uaa (ukuta) kiwanja chake. unasema mutakitaifisha...? Kama SMZ sikuwatengenezea maradhi ya kichaa (wendawazimu) wananchi wake ni nini lengo...?? CCM kwa hili itafeli tena itafeli sana na wanaichimbia kaburi wenyewe kwa mikono yao vigogo na watu wataazidi kuichukia CCM na kulaniwa mbali ya kuichukia. Sheria gani hio kandamizi eti ardhi ni mali ya Serekali wakati wowote wanaweza kuichukua...?? Ok lakini mumesahau kua ndani ya hio ardhi kuna binadamu wanaishi kwa kipato duni na wenye uwezo tafauti ya kimaisha....?? Sasa na hao ndio muko tayari kuchukua maisha yao kwa kuwanyaganya....??

Hivi sasa tayari watu kwa tarifa yako Bibie BI SALAMA ABOUD TALIB wanakusukumizia Ma Dua makubwa makubwa kwa kukushtaki kwa M/mungu,sasa kama unao ubavu wa sheria na katiba kukulinda. basi muulize Kamandoo Dr Salmini Amour na Balozi Seif Iddo  Baloteli hali yake ilivyo sasa na usisahau kuwa wako walojifanya majabari na kufanya mambo katika nchi hii ya Zanzibar,hivi sasa kwa tarifa yako wanakula mavi yao,na wengine wameshatangulia mbele ya haki kujibu. In shallah Allah atujalie Wazanzibar lenye kheri na sisi na Yarabii Jalia uwalinde na madui masheikh zetu huko waliko na utulinde na wabaya na mabaya wazanzibar wote sisi na nchi yetu.

No comments:

Post a Comment