Thursday, November 3, 2016

VIDEO-RAIS WA NCHI YA ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARRIF HAMAD MSIKITI WA BIZRED


ALICHOKISEMA RAIS WA NCHI YA ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARRIF HAMAD
KWENYE MSIKITI WA BIZRED BAADA YA KUKAMILIKA KWA SALA YA IJUMAA
ALICHOKISEMA MAALIM SEIF LEO TAREHE 21/10/2016 KATIKA MSKITI WA KWA BIZIREDI BAADA YA SWALA YA IJUMAA.
CCM WAPANGA KUMUUA.
MWENYEWE ASEMA NJAMA HIZO HAZIJAANZA LEO.
MIPANGO YA KUKAMATWA NA KUPELEKWA BARA KAMA WALIVYOFANYWA MASHEKHE YAANDALIWA.
MWENYEWE ASEMA YUKO TAYARI KUKAMATWA LAKINI KATU HATORUDI NYUMA.
ASISTIZA KUA KISIWA CHA FUNGU MBARAKA NI MALI YA ZANZIBAR.
ASEMA CCM KUTWA WAKO KWA WAGANGA WAKIOMBA MAALIM SEIF ASIPEWE NCHI KWASABABU SURA ZAO WATAKUA HAWANA PA KUZIWEKA.
Ndugu Waislamu kwanza nachukua fursa hii kumshukuru M/Mungu kwa kutujaalia siku hii ya leo kuwa wazima na kuisali sala hii.
Pia nimshukuru Khatib kwa khutba aliyoitoa ambayo imeeleza kila kitu. Bila ya shaka sote hapa hakuna anaejua kama atafika kesho lakini M/Mungu atujaalie kheri na atulinde na kila shari.
Tatu niushukuru uongozi wa Mskiti kwa kunipatia fursa hii ya kuwasalim Waislam wenzangu na Wazanzibari kwa ujumla.
Mimi leo sitaki kutoa khutba bali nataka nitoe salamu tu.
Tarehe 7/10/2016 nilisali katika msikiti wa Hurumzi lakini inaonekana watawala hawapendi hivi nikizungumza na Wazanzibari baada ya sala.
Tarehe 14/10/2016 nikasema nisali katika mskiti wa Kihinani lakini alienda mtu na kujitambulisha kua yeye ni Afisa wa Usalama na akawambia Viongozi wa Msikiti kua baada ya Sala hakuna ruksa ya kupewa Maalim muda wa kuongea watu wote wanatakiwa wachawanyike mara tu baada ya Sala.
Basi Viongozi wa Msikiti wakaniambia na mimi nikawambia mimi hao wananijua ni nani na kama wanataka kunizuia mimi basi kwa nini hawakuniambia mimi mwenyewe?
Kwa hiyo nikawambia hilo tena ni juu yenu mimi ni ndugu yenu sasa mukiamua kunipa fursa ni sawa na kama mukiona si vyema kuniruhusu na ni vyema kumskiliza huyo aliejitambulisha kua ni Afisa wa Usalama japo kua hakuwaonyesha kitambulisho chake basi pia ni sawa.
Uongozi wa Mskiti ukakaa shura na wakaamua kunipa fursa ya kuwasalimia Wazanzibari sasa sijui nyinyi hapa kama mulifuatwa na nyinyi au laa.
Na humu leo wamo hao Maafisa wa Usalama wingi wametumwa waje waniskilize halafu waende wakaseme nimesema nini lakini mimi hua najiuliza kwani mimi nimesema nini katika msikiti wa Hurumzi na Mskiti wa Kilimani?
Hurumzi nilisema vitu viwili tu ambapo kimoja ni swala la Katiba ambayo CCM baada ya tume kukusanya maoni ya Wananchi wao waliamua kuyatupilia mbali maoni yale na kuja na Katiba yao wao wenyewe na nikasema kua tunazo habari kwamba CCM wanapanga kuimaliza Zanzibar kwasababu wanataka kubadilisha sheria ya kura ya maoni ya Muungano ili watu wote ambao ni Wazanzibari na wasiokua Wazanzibari (Watanganyika) wapige kura Zanzibar na sasa hivi wanaleta watu wao kwa wingi ili waje wapige kura na ionekane kua Zanzibar imekubali.
Pili nikazungumzia swala la Kisiwa cha Fungu Mbaraka ambacho enzi na enzi kisiwa hicho ni milki ya Zanzibar na kila mwaka Viongozi wa Zanzibar walikua wakienda kupachika bendera ya Zanzibar katika kisiwa hicho. Mimi nilipokua Waziri Kiongozi pia nilienda kupachika bendera na Katiba ya Zanzibar inatamka wazi kua mipaka ya Zanzibar ni ile ile iliyokua kabla ya Ukoloni lakini Watanganyika hili hawalitaki na sasa hivi wanasema Kisiwa cha Fungu Mbaraka ni chao.
Kwa nini wanasema hivi? Wanasema hivi kwasababu kile Kisiwa ndicho Kisiwa chenye mafuta mingi ndio maana wanasema ni chao na ziko meli za kijeshi sasa hivi zinazotembea katika kisiwa hicho.
Katika Mskiti wa Kilimani nikasema pia mambo haya mawili na nikaongeza moja ambalo ni Sheria ya mafuta iliyopitishwa katika baraza la Wawakilishi na nikasema kua Wazanzibari tusidanganywe swala la Mafuta ni swala la Muungano kwasababu sheria ya Muungano iko vile vile haijabadilishwa na sheria imesema wazi kua swala la mafuta na swala la kukusanya kodi (mapato) ni swala la Muungano na Kikwete kabla ya kumaliza muda wake wa uraisi alipitisha sheria mbaya zaidi Bungeni tena haraka haraka ili kuibana zaidi Zanzibar na hii Serikali yao batil imeekwa kusudi ili kufanikisha hayo kwasababu wanajua kua hakuna kiongozi anaeweza kuyasemea haya katika Serikali hii. Asaivi wameambiwa huko kua wawe na Serikali moja (nchi moja) wengine wamekataa wengine wamekaa kimya kama kawaida yao.
Kwa hiyo nikasema tusidanywe kua Mafuta ni swala la Zanzibar na nikatoa tahadhari kwa Wazanzibari.
Sasa leo hapa nitaongeza na jengine na wale waliotumwa naomba waniskilize vizuri sana ili wakapeleke taarifa kama walivyotumwa.
Kwanza nakwambieni kawambieni hao waliowatuma kua Balozi Sefu ndie mbaya na ndio kikwazo cha Zanzibar.
Tunazo taarifa za uhakika kua CCM wanataka kuondosha nafasi mbili za wajumbe wa tume ili wabaki peke yao wafanye vile wanavyotaka.
Pia juzi alikuja
Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani na akasema katika vikao vyao kua wafanye haraka iwezekanavyo Serikali ya Umoja wa Kitaifa iondoshwe katika
Katiba ingawa hilo ni gumu kwasababu ili Serikali ya Umoja wa Kitaifa iondoke ni lazima iitishwe kura ya maoni na Wazanzibari washiriki katika kura hiyo kukataa mfumo huo, lakini wenyewao wakasema kua wajitahidi kufanye vyovyote ili waiondoshe.
Sasa mimi najiuliza kwa nini haya yote yanakuja muda huu haraka haraka hivi kuna nini huko ndani?
CCM wanajua kua Katiba ya Zanzibar inataka muda wote pawepo na Serikali ya Umoja wa Kitaifa na wao kupitia Serikali yao hii batil hawakukizi matakwa ya Katiba kwa hiyo na Serikali ya Umoja wa kitaifa haipo sasa wanafanya hivi wakiamini kua mipango hii itawasaidia lakini mimi najua wanahangaika tu.
Pia tunazo taarifa kua eti wamepanga wanikamate na wanipeleke Bara kama walivyowapeleka Mashekh wetu kwa kusingizia eti wanataka kunifanyia mahojiano.
Lengo lao kwanza eti ni kuniua na wanasema watanieka katika chumba maalum ambacho watapuliza madawa yao halafu wataniachia lakini huku afya yangu itakua inaathirika siku hadi siku mpaka mwisho wake nitaondoka duniani. Sasa Ikiwa Mungu kapanga iwe hivyo itakua lakini mimi ninavyoamini ni kwamba hakuna anaeweza kuniondosha duniani zaidi ya mwenyewe M/Mungu na kama wanadhani kua wakifanya hivyo ndio nitalegeza misimamo yangu basi kawambieni kua kurudi nyuma kwangu mimi ni mwiko. Sitorudi nyuma mpaka haki yetu ya tarehe 25 irudi mikononi mwetu.
Pia wanapanga hivi eti nisipate kusafiri kwenda nje wanasema nawachafua lakini ivi mtu asiekua na uchafu anachafuka? Ivi bila ya wao kufanya uchafu wao mimi ningeenda nikaileza dunia kua huu ndio uchafu ulioko Zanzibar na wakaniamini? Wamefanya uchafu na dunia nzima imeona sasa wasimsingizie Seif mimi sie niliewachafua wamejichafua wenyewe.
Lakini pia wanafanya hivi ili kuwarudisha nyuma Wazanzibari wasidai haki yao lakini mimi najua na wakubwa wao wanajua kila kitu na najua kua wanakwenda mbio sana na wengine wanaenda kwa waganga Muambe kule wanasema “tujaalie Maalim Seif asipewe nchi akipewa n chi sisi wengine tutakua vipi?” Sasa kama M/Mungu kapanga huyu awe raisi atakua rais na kama hakupanga hivyo basi hatokua.
Kwa hiyo ninachosema ni kwamba mimi niko tayari waje wanikamate lakini pamoja na yote hayn mimi nasema kwamba SI MTUTU SI BUNDUKI KUIDAI HAKI YETU HATUCHOKI.
Assalaam Alaykum!
MAALIM SEIF: NIA YA NYERERE 
ILIKUA NI KUIMEZA ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment