Sunday, July 22, 2012

UAMSHO M/MUNGU WAO NI ALLAH NA HAWA WANAFIKI WANA MUNGU WAO.MBONA POLISI WA KIKURI HAWAKUWAPINGA MABOMU HAWA..?


SWALA YA WANAFI IKISWALIWA NA RIYAA YAO YAKUJIONYESHA

HITIMA YA KUFURAHIA PESA ZA RAMBE RAMBE

POLISI WA KIKURIA MUKO WAPI..? MUJE KUWAPIGA MABOMU NA HAWA

MAGARI YA VIONGOZI WOTE HAWA YANA MAFUTA ILA MAFUTA YA KUOKOWA WATU YALIKUWA HAKUNA.

WANAFIKI WAKUBWA WALIPO KUTANA

RAI WA ZANZIBAR KUFENI KWA MAMELI MABOVU VIONGOZI TUPATE PESA ZA RAMBE RAMBE ZAA MV SPICE HAZIJESHA NYENGINE ZAIGIA


PONDA MALI KUFA KWAJA

SERIKALI imesitisha rasmi zoezi la uokoaji wa miili ya watu waliozama katika ajali boti ya Mv Skagit Jumatano iliyopita kutokana na ugumu wa kazi hiyo, huku miili zaidi ya 76 ikipotea baharini. Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Idd alisema hayo wakati akipokea msaada kutoka Benki ya NMB kwa ajili ya waathirika wa ajali hiyo.
Alisema wataalamu waliokwenda kwenye eneo la ajali kwa ajili ya uokoaji wamethibitisha kutopata mwili hata mmoja kwa muda siku mbili, hivyo Serikali imeamua kusitisha zoezi hilo.
Kabla ya kauli hiyo ya Serikali, Jana ilikuwa siku ya nne kufanyika kwa zoezi la kutafuta maiti katika Bahari ya Hindi lakini waokoaji walirejea majira ya jioni bila ya maiti yoyote.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema waliokwenda katika uokozi huo walirejea bila kupata maiti hata moja.
Kati ya watu 290 waliokuwa wamepanda kwenye boti hiyo, ni 146 ndio waliookolewa wakiwa hai huku maiti 68 zikiopolewa baharini ambapo Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Vyombo vya Baharini, Abdalah Hussein Kombo alisema pia zoezi la uokoaji ni gumu.
Awali, mmoja wa wazimiaji ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema : “ Meli inaonekana lakini namna ya kuipindua ili kuziondoa maiti zilizopo tumeshindwa kwa sababu ya ukosefu wa vifaa.”Pia kijana moja alisema tumeambia kuwa kulikuwa hakuna mafuta kwenye boti za uwokowaji nashanga siku ya pili tu magari zaidi ya 6 ya (FFU)) pamoja la lori kubwa la kurusha maji ya muwasho yalikuwa na mafuta ya kuwadhibu rai wema wa zanzibar.na mtu mwengine ambaye pia alitaka jina lake lihifadhiwe alisema kama waokowaji wa meli wanaiyona meli ila tu kinahitajika kifaa cha kuigeuza meli ili maiti zipatikane kwanini serekali haifanyi hivyo.?alihoji bali inasitisha kisha huku inachekelea michango ya mamilioni ya fedha hii nikuonyesha wazi serekali inauwa watu ili ipewe michango na nchi za nje.
Katika hatua nyengine Chama cha NCCR-Mageuzi, kimetaka mfumo wa vyombo vya usafiri katika visiwa vya Zanzibar na Pemba kuangaliwa upya ili kuepusha maafa zaidi kutokana na ukweli kuwa hata ndege zinazofanya safari zake katika visiwa hivyo na Dar es Salaam zina walakini.
Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Samwel Ruhuza alisema, licha ya boti na meli ambazo hazipo katika viwango vya usalama lakini pia ndege zinazofanya safari kati ya Pemba na Dar es Salaam usalama wake ni wa mashaka.
Akizungumzia usafiri wa ndege alisema, mafuta hunuka katika sehemu ya abiria na kuongeza kuwa ni wazi kuwa ndege ya namna hiyo inaweza kulipuka wakati wowote na alienda mbali zaidi kwa kueleza kuwa ndege hizo ndogo nyingi milango yake mibovu.
“Niliwahi kupanda ndege kutoka Dar es Salaam kwenda Pemba, mlango unagonga gonga na nilipouliza niliambiwa na rubani kuwa kesho utatengenezwa ni kitasa ndio kimeharibika”, alisema Ruhuza na kuongea kuwa hana uhakika kama ndege hizo huwa zinakaguliwa na hilo ni jambo la hatari kuendelea kubaki kama ilivyo.
Mwenyekiti wa Chama cha Kijamii, Constantine Akitanda alisema, kilichotokea Zanzibar ni matokeo ya rushwa kwani chombo hicho kilipigwa marufuku kubeba abiria nchini Marekani lakini fedha zilitumika, ikachakachuliwa Mombasa kisha ikaletwa Zanzibar kufanyakazi jambo ambalo limegharibu roho za watu.
Alisema hali hiyo pia ni matokeo ya watendaji wa Serikali kutaka kufanyabiashara na kufanya siasa vitu ambavyo daima haviwezi kuchanganyika na ikitokea basi matokeo yake huwa kama ilivyotokea Zanzibar.
“Rushwa ndiyo matokeo ya ajali ile, kwani wasimamizi wa sheria na sera ndiyo wafanyabiashara hivyo wanashindwa kunyoosheana vidole na matokeo yake roho za watu zinapotea na ajali ambayo ni ya tatu kwa meli ambazo zinamilikiwa na kampuni hiyo.
Alisema ajali ya kwanza ilikuwa ya meli yao moja iitwayo Mv Fatah ambayo ilizama bandarini kabla haijaondoka na zingine ndio hizo mbili ambazo zimechukua roho za mamia ya watu na kuonya kuwa hatua za maana zisipochukuliwa Taifa kila mara litakuwa katika kazi ya kutafuta miili ya watu.
Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance for Democtaric Change (ADC), Dawi Kadawi Limbu alisema sera ya Serikali ya kujiondoa katika biashara zikiwamo za huduma muhimu ndiyo chanzo cha matatizo haya kwani sasa roho za watu zinashikwa mikononi mwa wafanyabiashara ambao wanaweza kuamua chochote wanachotaka wao.
“Kuna huduma Serikali haiwezi kukwepa kuzitoa ikiwa ni pamoja na za usafiri wa reli, majini na usafiri wa mabasi” alisema na kuongeza kuwa kuziacha huduma hizo muhimu mikononi mwa wafanyabiashara kwa kisizingizo kuwa serikali haifanyabiashara ni uvivu wa kufikiri.
Alisema dunia nzima suala la huduma za usafiri licha ya kuwapo watu binafsi pia Serikali inatoa ili kuwahakikishai usalama wananchi wake na ameshangaa kuiona Serikali ikishindwa kujifunza kutokana na ajali za majini.
“Mv Bukoba ilipoua mwaka 1999 tulidhani Serikali imejifunza kitu lakini cha ajabu hakuna kitu kama hicho na Ziwa Victoria ajali nyingine itarajiwa wakati wowote kwani meli ya Mv Victoria bado inafanyakazi kati ya Bukoba na Mwanza licha ya uchakavu wake”, alisema.

SIO TU HAMAD MASSOUD AJIUZULU LAA BALI SEREKALI NZIMA YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR WAJIUZULU


Ikiwa Waziri Mawasiliano na miundo mbinu atatakiwa ajiuzulu na mwenyewe binafsi akachukua uamuzi huo,itakuwa ni jambo la ajabu na hapana budi rekodi hio lazima iwekwe kwenye kitabu cha maajabu ya ulimwengu kwenye kumbukumbu ya Viongozi wa Afrika na utawala bora.Nasema hivi kwa sababu Waafrika hatuna utamaduni huo. Katika Nchi za Kiafrika na serikali zinazotawala kwa mabavu hili ni jambo la kawaida,mbona yanatokea mengi majanga ya aina hiyo. Hili sio suala geni,uzembe,rushwa na ubabe wa kutumia mabavu ndiyo mihimili ya serikali zetu.Nchi za aina hii fahari yake ni kupelekewa salam za rambi rambi na pesa za maafa kwa Viongozi wake baada ya tukio kutokea na sio kujikinga nalo.
Wazanzibar sifikirii kama wanapaswa kumshughulikia Hamad kama Hamadi,tukumbuke kwamba kidole kimoja hakivunji chawa. Tunapozungumzia suala hili, lazima lawama ziende kwa wote kuanzia sheha wa shehia mpaka kwa Rais Shein kwani yeye ndie mhusika na mhimili mkuu wa serikali. Sio vyema kumtupia Hamad massoud mpira pekee kama Hamadi wakati kosa hilo ni uzembe na utendaji mbaya wa Serikali mzima,kumlaumu Hamad pekee yake ni kutomtendea haki. Tatizo la kuzama kwa meli ni uzembe wa Serikali yote .Sifikirii kwamba hata boti za uokozi kukosa mafuta lazima waziri akasimamie hilo,sasa hivi huyu Waziri ana mikono mingapi na ajigawe vipande vingapi kama hata hilo lazima Waziri akalisimamie na kama hakwenda vyombo vitakosa mafuta,hivi ni vichekesho!
Tatizo letu sisi Wazanzibar nikuonesheana vidole kwa ubinafsi na chuki za kisiasa,lakini kile chanzo cha tatizo letu tunajaribu kulipuuza ,hatuna budi tuelewe kwamba Zanzibar hatuna Nchi wala utawala na wala kiongozi muadilifu, lakini hata hao Walioambiwa wamechaguliwa kwa magube basi haki haikutendeka katika uchaguzi na hili sote tunalijua,sasa kama ni hivyo unategemea vipi utendaji wao utakuwa,mpaka Nchi ipate maendeleo na tuepukane na majanga kama haya,ambayo ni tishio kwa Wazanzibar. Viongozi wa Zanzibar wanashughulikia mambo ya siasa zaidi ili wabaki madarakani lakini masuala yanayowagusa maendeleo na maslahi ya Wananchi hayo ni magumu kwao kufanyika.
Fikra zangu ni kwamba watu wengi wangekuja na hoja na mawazo ya kuishinikiza kujiuzulu kwa Rais wa Zanzibar na cabinet yake yote, matokeo yake wanamnyooshea kidole mtu mmoja tatizo jamani sio Hamad ,tatizo narudia tena kwamba ni Serikali mbovu inayoendeshwa na Dr Shein, ambayo inaongozwa na mtawala wetu Tanganyika.Si vyema kumtupia mtu mmoja lawama wakati tatizo letu tunalijua,ni uongozi mbovu.Katika serikali hii ambayo mambo yake yote yanaratibiwa kwa watawala wao,haya yanayo tokea ndio matunda yake,lililobaki tumshukuru Muumba lakini hili ni tatizo sugu kwa Wazanzibar na hatujui lini litamalizika, kwa sababu Wazanzibar wamegaiwa kivyama.
Mimi niulize suala moja Wazalendo,wale askari ambao wanawatesa na kuwanyanyasa Wazanzibar,waumini wa dini mpaka misikitini mwao,nao pia ni tatizo la Hamad na miundo mbinu yake? Jibu litakuja kwamba Serikali ndio mhusika wa yote yale. Tujaribuni kuwa wabunifu ili tuweze kuelewa chanzo cha matatizo yetu na sio kusema kwa jazba lakini ukweli tunauficha na kujitia pamba za masikio.Bado hatuna ndege zetu wenyewe lakini kama tungekuwa nazo basi hali ingelikuwa hivi hivi, ndege zingeanguka kila siku kwa mhusika kusahau kuweka mafuta ya kutosha tu,hivi ndivyo tulivyo.Umimi na uyakhe ndio unaotuongoza katika utendaji wetu. Sasa linapokuja suala la kwamba Waziri muhusika akakae chini ya tangi la mafuta kujua kwamba ndege imejaa mafuta au la, hilo haliwezekani lazima wahusika wawajibike,Waziri sio kila kitu akifanya yeye kuna watendaji na majukumu yao pia.
Dr. Shein amechaguliwa kwa mizengwe sio hivyo na hata hao Marais wengine waliopita ni hivyo hivyo,sasa katika hali kama hiyo tutegemee nini, isipokuwa uzembe kama huo ndio utendaji wa Serikali yetu tokea hapo awali.Hakuna mabadiliko ya watendaji yaliofanywa na Rais tokea kuchukua madaraka,isipokuwa alichokifanya ni kuzidisha watendaji wa zembe kwenye Mawizara na kuifanya Serikali yake kuwa kubwa kuliko Wananchi wake. Hata wale wakuu wa Mikoa na Wilaya Rais kashindwa kuwabadilisha sasa leo hii tunamlaumu mtu mmoja kwa kosa la Serikali mzima viereje,wote ni wahusika wanapaswa wajiuzulu kutokana na uzembe. Serikali kuonesha udhaifu wake ni kule kuendelea kukikodisha kisiwa cha chumbe kwa miaka mia,hivi hii ni Serikali au ni kampuni ya watu binafsi. Sehemu ile ni muhimu kuwekwa ”Police guard” kwa ajili ya uokozi,usalama wa nchi, matokeo yake mpaka msikiti pale umekabidhiwa wazungu wanakunywa pombe,wavuvi na raia wa Zanzibar wanashindwa kufika,watu wamefumba macho hilo halizungumzwi, hivi kweli tutafika ?.
Ukiwachilia hawa Mawaziri wachache wa C.U.F, Serikali na watendaji wake ni wale wale tuliowazoea wa chama tawala, kwa maana hiyo utendaji hapa haupo ndio maana nikasema kwamba Hamad Massoud hawashi wala hazimi ni kivuli tu katika Serikali hii Mapinduzi ya Zanzibar, ni sawa nakuchukua gunia la sukari na kulitupa nungwi ukafikiria kwamba maji yatageuka kuwa matamu hilo haliwezekani.Waswahili wanasema kamba hukatikia pabovu,ndio hili suala la kuzama kwa meli,lakini ukitaka ukweli ni kwamba Serikali yote haifai kuongoza imejaa madudu na haya Wazanzibar ndio tunayo yataka,wetu ni mdomo tu vitendo hamna. Matokeo kama haya yametokea mengi hapa visiwani,watu wengi wameuliwa hivi hivi na wala hakuna linalofanyika,uoga wetu ndio unaotuponza.Tunadanganywa kwa wimbo wa amani na utulivu huku tunamalizika mmoja baada ya mwengine. Hivi kama si uoga ni kitu gani ? Hawa askari wanaotesa ndugu zetu,mama zetu,dada zetu wanaishi mbinguni ?Kuna hatua yeyote tunayochukua kupinga dhulma hii,au ndio Mungu atatulipia ?
Kujiuzulu kwa Waziri sio suluhisho la Wazanzibar wala matatizo yetu,akiondoka leo kesho yake atakuja Hamad Massoud mwengine yatatokea yale yale kwani tatizo sio Waziri,tatizo ni Serikali kwamba haipo makini,Zanzibar ni mkoa wa Tanganyika kama vile Mtwara na kigoma.Tumeshindwa kijitawala leo tunatawaliwa lazima tukubali matokeo ya aina hii.Angalieni leo hii Zanzibar haina chake kila kitu unaambiwa hicho kinasimamiwa na Muungano lakini likitokea janga mpira unarushwa Zanzibar. Hivi ilipozama meli hii hawa watu wa hali ya hewa walikuwa wapi ? Jee kwa nini SUMTRA waliiruhusu meli kuondoka wakati wanajua kwamba bahari ni mbaya ? Baada ya kuzama kwa meli kwa nini waokozi wachukue masaa matatu kukifikia chombo ,Serikali na vikosi vyake vinafanya kazi gani? Kuna masuala mengi ya kujiuliza kabla kumuoneshea kidole mtu mmoja kisiasa.Ikiwa Zanzibar ni visiwa,serikali imejipanga vipi kukabiliana na hali za ajali kama hizi huku tukijuwa kwamba huu ndio usafiri wetu mkubwa ?
Serikali yetu ina udhaifu mkubwa kiasi ambacho hata ukihadithiwa kama wewe ni mgeni basi utashindwa kuelewa na hili ndio tatizo. Nchi yetu ni visiwa vidogo wananchi wake ni kidogo leo hii tunawatendaji kama vile Nchi kubwa zenye maendeleo makubwa,hili ni tatizo ndio maana kila moja anamtupia mpira mwenzake.Rais hakupaswa kuunda Serikali ya kizembe kama hii,hili ni tatizo kisaikolojia. Zanzibar kila kitu kinachofanyika lazima kiangaliwe kisiasa,nani kafanya, nani kasema,wapi anatokaka, jee rangi yake ni nyeupe buluu au nyeusi.Uongo,unafiki,fitna,majungu ndio unaotawala utendaji wa kila siku wa Serikali yetu ya Mapinduzi,anaepinduliwa siku zote ni Mzanzibar,wageni hapa ndio wanaokula nchi..
Ikiwa kweli Wazanzibar tunauchungu na Nchi yetu lazima tujitolee kwa hali na mali,maneno kwenye mtandao na hasira za mkizi hazitotusaidia kitu bado matatizo tunayo,matokeo yake yatakuwa ni faida ya Mvuvikupata kitoweo. Tuishinikize Serikali sio kwa maandamano tu bali kwa vitendo na mapambano ya mabavu kama yale wanayotumia askari wao. Wapemba na Waunguja tuungane kwa pamoja tupambane na adui yetu. Kwanza lazima taifa letu lipate heshima yake,lakini kubwa zaidi ni kutoa funzo kwa viongozi wetu ili mtawale mwengine yeyote atakae kuja ajue kwamba Wazanzibar wanataka heshima yao idumishwe na sio kuchezewa chezewa kizembe.

VIDEO-ZANZIBAR IS NOT A PEACE COUNTRY I PUT THIS VIDEO TO SHOW THE WORLD

KWELI NCHI HII INA AMANI...?
THIS VIDEO IT WAS RECORD 2 DAYS A GO
HAYA NDIO YALIYO TOKEA SIKU CHACHA TU
KISHA MUNADANGANYA WATU KUWA NCHI INA AMANI
WAKATI ASKARI NDIO WAVUNJIFU WA AMANI KATIKA NCHI
HII
YA ZANZIBAR

ASKARI NDIO WANAO CHOMA MAGARI YA WATU
NA KUPINGA MABOMU RAI WEMA JE NDIO AMANI
HIYOOO..?
ASKARI WANAPINGA MABOMU WATU KISHA WANAWAIBIA VITU
VYAO JE HII NDIO AMANI NDANI YA NCHI TUNAYO AMBIWA..?

VIDEO-UAMSHO-MARAISI WATATU WOTE WANA SIKIO LA KUFA HALISIKI DAWA-MUHADHARA-MSIKITI WA MBUYUNI

SHEIKH FARID 

VIDEO-UAMSHO-MUHADHARA-PAJE ZANZIBAR

SHEIKH FARID
PART 1


VIDEO-UAMSHO-MUHADHARA - PAJE ZANZIBAR

SHEIKH FARID
PART 2