Sunday, May 22, 2016

VIDEO-YA ALIYEKUWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI NCHINI TANGANYIKA AKIJIBU SWALI BUNGENI HUKO AMELEWA


Video ya dakika 7 ikimuonyesha Waziri Kitwanga akijibu swali huku amelewaaa...
NCHI INAOMGOZWA NA WALEVI, WAZI, MATAPELI, WAZINZI, WAUWAJI, MABAHILI, WANGO, WAZUSHI, MAKATILI, WAVIVU, WASIO PENDA HAKI, MNAFIKIRI NCHI ITAKUWA VIPI......??

TAARIFA ZIMEVUJA KWAMBA WANASIASA WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM WALIO FILISIKA KISIASA WANATAJWA KUSHINIKIZA JESHI LA POLISI KUMKAMATA MAALIM SEIF SHARIFF HAMADUNGUJA NGANGARI

PEMBA NGANGARI
TAARIFA zimevuja kwamba, wanasiasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanatajwa kushinikiza Jeshi la Polisi kumkamata Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF),
Jumapili, Mei 22, 2016
Si Maalim Seif pekee, viongozi wengine wa chama hicho wanaoundiwa mkakati wa kukamatwa ni pamoja na Mansour Yussuf Himid na Mohamed Ahmed Sultan (Eddy Riyami), kwa sababu za kisiasa. Taarifa hizi zinathibitishwa na Nassor Ahmed Mazrui, Naibu Katibu Mkuu wa CUF-Zanzibar ambaye amesema: “Tunazo taarifa kwamba kuna wanasiasa wameliagiza Jeshi la Polisi kuandaa mashtaka kwa ajili ya kumshitaki Maalim Seif kwamba alipokuwa Pemba alifanya maandamano bila ya kibali wakati hakukuwa na maandamano yoyote.” Mazrui amesema hayo leo wakati wa Uzinduzi wa Taarifa ya Uvunjwaji wa Haki za Binadamu Zanzibar kwa mwaka 2015/2016. Hafla hiyo ilifanyika mjini Dar es Salaam. Mazrui amesema: “Viongozi hao wamepangiwa kukamatwa na kuletwa katika magereza ya Tanzania Bara kwa lengo la kuwanyamazisha Wazanzibar ili wasipaze sauti zao kupinga utawala wa kidikteta uliowekwa madarakani kwa nguvu za dola kinyume na matakwa ya kidemokrasia ya wananchi wa Zanzibar.”
Akizungumzia uzinduzi wa Taarifa ya Uvunjwaji wa Haki za Binadamu Zanzibar 2015/2016 amesema, CUF inajiandaa kuchukua hatua kutokana na uharibifu uliofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar/CCM visiwani humo. Mazrui akimwakilisha Maalim Seif kwenye uzinduzi wa ripoti hiyo amesema, nakala ya ripoti hiyo pia watamkabidhi Rais John Magufuli kwa lengo la kujua kilichofanyika na kinachofanyika Zanzibar: “Baada ya hatua ya leo ya uzinduzi wa taarifa hii, CUF kimejiandaa kuchukua hatua ikiwemo ya kumuandikia rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli na kumkabidhi nakala ya taarifa hii ili ajue kinachofanyika nchini na hasa akiwa Amiri Jeshi Mkuu,” amesema Mazrui. Hatua nyingine zitakazochukuliwa na CUF ni pamoja na kuiwasilisha taarifa hiyo pamoja na vielelezo vyote katika Jumuiya, Taasisi na Mashirika ya Kimataifa yanayotetea haki za binadamu ulimwenguni ili kuchukua hatua zao. “Pia tutaiwasilisha taarifa pamoja na vielelezo vyote katika Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora hapa nchini ambayo hata katika mkutano wa Geneva, ilitambuliwa uwepo wake,” amesema Mazrui na kuongeza.
“Na katika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) pamoja na taasisi nyingine zinazoshughulikia masuala ya haki za binadamu hapa nchini.” Mazrui amesema: “Hatua nyingine itakayofuata ni kufungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania dhidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) kuhusiana na matendo yanayohusisha Jeshi la Polisi visiwani Zanzibar. Hatua nyingine itakayochukuliwa na CUF ni kukamilisha taratibu zitakazoiwezesha Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kuanzisha uchunguzi dhidi ya watu wenye dhamana mbalimbali ambao wamehusika kuchochea, kutoa au kusimamia maagizo yaliyoepelekea makosa dhidi ya binadamu na makosa yaliyoilenga jamii ya watu fulani.
KISHA NYINYI MUNAYAITA MAPINDUZI MATUKUFU HIVI KWELI NYINYI MUNAJUWA UTUKUFU NI NINI AU DUNIA IMEWAVA KISAWA SAWA MPAKA MNAKUFURU MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA KATUPINDUWA TENA WAZANZIBARI NA KUWEKA VIONGOZI WAWATAKAO WAO WAKINA BT TUNAENDELEA TENA KUKA CHINI YA SERIKALI YA KIKOLONI YA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA MPAKA MIAKA MITANO IMALIZIKE KISHA TUTIWE TENA KATIKA SHENGESHA LA UCHAGUZI NA KUPIGA KURA KISHA WAZANZIBARI WAPIGE KURA NA KUCHAGUWA VIONGOZI WAWATAKAO MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA ATAKUJA NA STYLE MPYA YA KUZIPIGA KURA ZA WAZANZIBARI CHINI NA KUTUEKEA VIONGOZI WAWATAKAO KISHA TUTAKA TENA CHINI NA KUSUBIRI UCHAGUZI WA 2025 MAMBO YATAKUWA HIVYO HIVYO KISHA TUTAKA CHINA NA KUSUBIRI UCHAGU WA WA 2030 TUKIWA HAI KAMA HATUKO TENA WATAKAO BAKI WATAFANYIWA TENA HIVYO HIVYO NA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA KISHA WATAKA CHINI WASUBIRI......>>> MPAKA KIYAMA KISIMAME BASI NI BORA TU TUKUBALI KUWA NDIO TUMEKUBALI KUWA CHINI YA MKONI MWEUSI TANGANYIKA KULIKO UPUMBAVU HUU WA UCHAGUZI AMBAO KILA MOJA WETU HAPA ZANZIBAR KAMA UCHAGUZI WA MARA HII HAUJAWASOMESHA WALA HATUTA SOMA TENA MILELE. 

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

UTUMBUWAJI MAJIPU SASA YAMGEUKIA YEYE MWENYEWE RAIS POMBE MAGUFULI


DHANA ya utumbuaji majipu sasa imemgeukia Rais John Magufuli kutokana na kuongoza wizara iliyotawala na ubadhirifu wa fedha za umma, anaandika Regina Mkonde .
Katika Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, Dk. Magufili alikuwa Waziri wa Ujenzi – wizara ambayo inatajwa kujaa ubadhirifu wa pesa za umma na kwamba, rais huyo ameshindwa kuchukua hatua.
Kutokana na hali hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imemtaka Rais Magufuli kutumbua majipu yake wake wakati akiwa kwenye wizara hiyo.
James Mbatia, Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amesema, katika wizara hiyo kuna ubadhilifu wa fedha za umma.
Pia kumekuwepo na utendaji mbovu wa watumishi na kwamba, serikali haina mpango wa kuwachukulia hatua za kisheria wahusika kutokana na kutoonesha jitihada.
“Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inajiuliza kama  serikali ya awamu ya tano inafanya kazi yake kwa haki, uadilifu, uwazi na usawa kwa wote na hasa kwa kile kinachojulikana kama utumbuaji majipu, swali hapa ni nani amfunge paka kengele? au mkuki mtamu kwa nguruwe mchungu kwa binadamu?” amehoji Mbatia.
Wakati akitoa hotuba ya maoni ya kambi ya upinzani leo Bungeni mjini Dodoma kuhusu mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 Mbatia amefafanua baadhi ya dosari zilizofanywa na wizara hiyo.
Moja kati ya dosari hizo ni kitendo cha Wakala wa Barabara nchini TANROADS cha kuitia hasara zaidi ya Sh. 5 bilioni serikali.
“TANROADS imebainika kuwa na utendaji mbovu kama ambavyo mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) alivyobaini juu ya usimamizi mbovu katika mikataba ya ujenzi wa barabaa na madaraja ambapo ilikuwa chini ya iliyokuwa wizara ya ujenzi katika serikali ya awamu ya nne,” amesema.
Mbatia ameongeza kuwa “TANROADS wakati wa kipindi hicho, iliitia hasara serikali ya jumla ya Shilingi 5,616,652,051 kutoka kwenye riba (interest) inayoongezeka kila siku kutokana na TANROADS kuchelewa kuwalipa wakandarasi 11.”
Amesema kuwa, hasara hiyo iligundulika kati ya kipindi cha mwaka 2012 na mwaka 2015 kwa mujibu wa Ripoti ya CAG ya Hesabu za Serikali Kuu wakati wa ukaguzi wa taarifa za fedha kwa mwaka ulioishia tarehe 30 Juni 2015 iliyotolewa mwezi Machi 2016 (Ukurasa wa 134 na 135).
Dosari nyingine ni ile ya serikali kuruhusu matumizi ya matairi yanayofahamika kwa jina la Super single tires ambayo yanaharibu barabara.
“Utafiti unaonesha matairi haya (super single tyres) yanaharibu barabara. Matairi haya yameanza kutumika takribani miaka mitano iliyopita na mzigo uliokuwa unabebwa na matairi 24 sasa unabebwa na matairi 12,” amesema.
Mbatia amesema, uruhusiwaji wa matumizi ya matairi hayo haukuwa wa busara kutokana na kwamba matokeo yake ni uharibifu mkubwa wa barabara.
“Uamuzi wa kuruhusu matairi haya haukuwa na busara maana barabara zetu hazijabuniwa kuhimili shinikizo la uzito (excessive pressure) linalotokana na matairi hayo,” amesema.
Ameitaka serikali kuzuia mara moja matumizi ya matairi hayo ili kuzinusuru barabara lakini pia kuokoa fedha za walipa kodi zinazotumika kurekebisha mara kwa mara barabara hizo na kunyima fursa maeneo mengine kupata barabara za kiwango cha lami.
Akizungumzia uuzwaji wa nyumba za serikali Mbatia amesema, serikali iliuza nyumba zake kwa bei ya hasara hivyo kuigharimu nchi.
“Katika muktadha huo kambi Rasmi ya Upinzani  inalikumbusha Bunge kwamba, kati ya mwaka 2002 mpaka 2004  Serikali iliuza nyumba  zipatazo 7,921 na mpaka mwaka 2008 Serikali ilikuwa imejenga nyumba 650 tu,” amesema.
Amesema kuwa, katika biashara ya kuuza nyumba zilizokuwa mali ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), serikali ilipata Sh. 252,603,000/-
ambazo haziendani na thamani halisi ya nyumba hizo.
“Hivi sasa serikali inahitaji kusaka nyumba  zaidi ya mara dufu ya kiasi hicho kujenga nyumba za fidia.
Kwa mujibu wa taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge juu ya uuzaji wa nyumba za serikali kinyume cha taratibu, serikali itatumia Sh. 677,606,000/- kujenga nyumba mpya ili zirejeshwe kwa Tamisemi, Rejea taarifa ya Serikali Bungeni tarehe 25 April 2008,” amesema.
Mbatia amesema, waliouziwa nyumba hizo, kuna taarifa kuwa kati yao wapo walioziuza na kujipatia faida kubwa kinyume na mikataba ya mauzo hayo,na kwamba KRUB inapendekeza wanyang’anywe nyumba hizo kwa kukiuka mikataba na malengo ya mauzo.
“Kumbukumbu za taarifa rasmi za Bunge zinaonesha kwamba, serikali ilitoa taarifa ndani ya Bunge hili kuwa, kuna kamati iliundwa kuchunguza mchakato wa mauzo ya nyumba ya serikali.
“Kamati hiyo ilitegemewa kumaliza kazi mwezi Februari, 2007, lakini hadi Bunge la Tisa na Bunge la Kumi linamaliza uhai wake hakuna taarifa iliyotolewa na serikali. Kambi Rasmi ya Upinzani Buneni inaitaka serikali ya awamu ya tano irejeshe nyumba hizo,” amesema.
Mbatia amesema, kuna maadhimio kadhaa yaliyoadhimiwa na bunge ikiwemo kuitaka serikali kurejesha nyumba zilizouzwa kinyume cha taratibu na kwa watu ambao hawakuwa watumishi wa umma.
“Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeiitaka Serikali kutekeleza azimio hilo la Bunge, na kwa njia hiyo ile kauli mbiu ya hapa kazi tu, iweze kutafsiriwa kwa vitendo,” amesema na kongeza;
“Tunajua uuzwaji huo ulisimamiwa na Wizara aliyokuwa akiiongoza yeye na kuna uwezekano mkubwa kwamba alisimamia maamuzi ambayo hakuwa na uwezo wa kuyakiuka.”
Amesema, sasa ni muda sahihi Rais Magufuli kurekebisha kasoro alizozisimamia na katika mchakato huo ili kurejesha imani katika jamii.
“Tukumbuke kuwa Rais Kikwete alielekeza nyumba hizo zirudishwe serikalini lakini alikosa uthubutu wa kusimamia kauli yake,” amesema.

MAELEZO YA NAIBU KATIBU MKUU WA CHAMA CHA WANANCHI CUF MHE. NASSOR AHMED MAZRUI. TAARIFA YA UVUNJWAJI WA HAKI ZA BINADAMU ZANZIBAR 2015/2016
MAELEZO YA NAIBU KATIBU MKUU WA CHAMA CHA WANANCHI (CUF), MHE. NASSOR AHMED MAZRUI, KWENYE MKUTANO MAALUM NA WAANDISHI WA HABARI KWA AJILI YA UZINDUZI WA TAARIFA YA UVUNJWAJI WA HAKI ZA BINADAMU ZANZIBAR 2015/2016
LAMADA HOTEL, DAR ES SALAAM – 22 MEI, 2016
UTANGULIZI:
Kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 kilishuhudia kurudi upya kwa matukio ya uvunjwaji wa haki za binadamu na uhalifu dhidi ya binadamu na utu wao kwa kiwango kikubwa visiwani Zanzibar.
Matukio haya yalishika kasi wakati wa uandikishaji wa wapiga kura wapya katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika miezi ya Aprili hadi Juni 2015, yakaendelezwa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu na kuibuka tena kwa kiwango cha kutisha baada ya kile kilichoitwa tangazo la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salim Jecha, la kufuta uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na kuendelea hadi sasa.
Uvunjwaji huo wa haki za binadamu ulihusisha:
1. Kuibuka kwa makundi ya maharamia ambao wananchi wamekuwa wakiwaita MAZOMBI ambao hufunika nyuso zao na huku wakibeba silaha za moto na silaha za kienyeji na wakiwa ndani ya gari zenye namba za Vikosi Maalum vya SMZ wamekuwa wakipiga, kuwaibia mali zao, kuwajeruhi na hata kuwakata sehemu za miili yao wananchi wasio na hatia katika maeneo mbali mbali ya visiwa vya Unguja na Pemba.
2. Kuvamiwa kwa misafara ya wanachama na wafuasi wa CUF waliokuwa wakirudi kutoka kwenye mikutano ya kampeni na kupigwa na watu waliokuwa wamevalia sare za CCM na huku wengine wakiwa wamejifunika nyuso zao.
3. Kuwashambulia wananchi wasio na hatia kwa kutumia risasi za moto kulikofanywa na Polisi na Vikosi vya SMZ ambako kumepelekea watu kadhaa kujeruhiwa vibaya.
4. Matukio ya ubakaji dhidi ya wanawake.
5. Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya mahabusu wanawake waliokuwa katika mikono ya Polisi.
6. Kutekwa watu na kuwatesa wanapokuwa katika mikono ya watekaji.
7. Kukamatwa ovyo na kuwekwa ndani kwa watu wasipoungua 90 wakiwemo viongozi waandamizi wa CUF bila ya kuwafungulia mashtaka Mahkamani kinyume na Sheria za Mwenendo wa Makosa ya Jinai Zanzibar.
8. Kuwatesa na kuwaadhibu wanachama na wafuasi wa CUF waliokuwa chini ya mikono ya Polisi ambao hawakufikishwa Mahkamani huku wakilazimishwa kukiri kutenda makosa ambayo hawakuyatenda.
9. Kuchoma na kuvunja ofisi za matawi na majimbo ya CUF pamoja na baraza zinazotumiwa na wanachama na wafuasi wa CUF kwa kukutana na kubadilishana mawazo.
10. Kuchoma nyumba za wanachama na wafuasi wa CUF katika vijiji mbali mbali Unguja na Pemba.
11. Kuharibu miundombinu ya maji na huduma nyengine muhimu za jamii katika maeneo ambayo yana wafuasi wengi wa CUF.
12. Kuvamiwa kwa kituo cha redio binafsi na kuwatishia maisha waandishi wanaotangaza vipindi visivyowaridhisha watawala na kuchoma moto kituo kimoja cha redio binafsi.
13. Kutoa hotuba za kuchochea fujo, ubaguzi na vitisho kulikofanywa na wanasiasa waandamizi wa CCM ikiwemo kuruhusu mabango yanayochochea ubaguzi na chuki kwa jamii nzima ya watu walioitwa “MACHOTARA”.
14. Redio na Televisheni za Serikali kutayarisha na kurusha vipindi vinavyochochea shari, fujo na ubaguzi katika jamii.
15. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia ofisi zake za MASKANI YA KISONGE kuweka ubao maalum unaoitwa “SAUTI YA KISONGE” unaotumiwa kuandika na kusambaza ujumbe wenye kuchochea ubaguzi, fujo na ghasia dhidi ya watu wa jamii fulani hasa Wapemba na wanachama na wafuasi wa CUF.
16. Kuendesha kampeni za vitisho na kuleta hali ya taharuki na hofu kwa kupitisha askari wakiwa na silaha nzito nzito pamoja na magari ya kivita katika maeneo yenye makaazi ya raia visiwani Unguja na Pemba huku wakiimba nyimbo za ubaguzi kwa mfano kusema “HATUWATAKI MACHOTARA”.
UZINDUZI WA TAARIFA YA UVUNJWAJI WA ZA HAKI ZA BINADAMU:
Chama Cha Wananchi (CUF) kimeweka kumbukumbu za matukio yote haya na kimetayarisha Taarifa ya Uvunjwaji wa Haki za Binadamu ambayo leo hii tutaizindua hapa.
Nimuombe Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria, Mhe. Pavu Juma Abdalla, awasilishe kwenu muhtasari huo wa Taarifa hiyo. Mwisho wa mkutano huu tutawapatia nakala za Taarifa hiyo kila mmoja.
Baada ya kupokea Muhatasari huo, niwaeleze kwamba matukio haya na mengine yamechafua sana taswira na jina la Tanzania katika jumuiya ya kimataifa.
Katika mapitio ya kila mwaka ya haki za binadamu nchini Tanzania (Universal Periodic Review) yanayofanywa na Umoja wa Mataifa kupitia United Nations Human Rights Council ambayo yamefanyika mjini Geneva, Uswisi tarehe 2 – 13 Mei, 2016 yaani mwezi huu, mataifa kadhaa duniani yaliibana Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusiana na matukio haya na mengine.
Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katika mapitio hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome, alipata wakati mgumu kujibu hoja hizi.
Rekodi zote za mkutano huo zinapatikana katika mtandao. Miongoni mwa maazimio yaliyotolewa kwa Tanzania kutoka mataifa mbali mbali wanachama wa Umoja wa Mataifa ni pamoja na haya yafuatayo (na nayanukuu kwa Kiingereza kama yalivyoripotiwa kwenye mtandaohttp://www.upr-info.org/database/index):
* Ensure that police officers having committed acts of torture of illtreatment be prosecuted and punished appropriately
- Recommended by Belgium
- Response: Accepted
* Take adequate measures to protect its population from violence committed by the security forces and establish an independent mechanism for the investigation of complaints regarding abuses carried out by law enforcement officials
- Recommended by Denmark
- Response: Accepted
* Establish an independent body for investigating complaints about the actions of law enforcement officials
- Recommended by United Kingdom
- Response: Accepted
* Provide all victims of violence against women an unhindered access to justice and ensure that all perpetrators are brought to justice in accordance with international standards
- Recommended by Slovakia
- Response: Accepted
Improve the efficiency of the justice system by streamlining and simplifying judicial procedures including introducing a case management system that tracks individual cases from filing to disposition and limits the amount of time each case can be held at each stage
- Recommended by Canada
- Response: Accepted
* Vigorously prosecute security force personnel who violate the law
- Recommended by United States
Response: Accepted
* Ensure all security forces are subject to strict control of civilian authorities
- Recommended by United States
- Response: Accepted
* Guaranteeing the freedom of expression, association and assembly by allowing human rights defenders, political opponents and journalists to express freely their views in line with international human rights law
- Recommemded by Netherlands
- Response: Accepted
* Work with the media and other stakeholders to ensure that all organs of the State understand and appreciate the constitutional guarantees of freedoms of press and assembly
- Recommended by United States
- Response: Accepted
* Step up its efforts to protect women and girls from sexual violence
- Recommended by Norway
- Response: Accepted
* Work to abolish laws that restricts freedom of expression, information and freedom of media, and establish laws that will guarantee these rights in line with international human rights standards
Recommended by Sweden
Response: Accepted
* Respect the right to assembly throughout the process of reviewing the Constitution
- Recommeded by Norway
- Status: Accepted
Kama inavyoonekana maazimio yaliyoorodheshwa hapa ambayo pia yanaonyesha nchi gani iliyatoa yalikubaliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome. Yote tuliyoyanukuu hapa yameripotiwa kwamba ni “ACCEPTED” yaani yamekubaliwa.
Hata hivyo, wakati maazimio haya na kukubaliwa kwake kukiwa ndani ya mwezi huu huu, bado tumeshuhudia uvunjwaji wake ukiwa unaendelea.
Matukio ya watu kuvamiwa katika maeneo yao na kupigwa ovyo yameshamiri upya wiki hii hususan kisiwani Pemba hasa baada ya ziara ya Katibu Mkuu wa CUF na mshindi wa nafasi ya Urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015, Maalim Seif Sharif Hamad ambayo ilikuwa ya mafanikio makubwa.
Tunazo taarifa kwamba kuna wanasiasa wameliagiza Jeshi la Polisi kuandaa mashtaka kwa ajili ya kumshtaki Maalim Seif kwamba eti alipokuwa Pemba alifanya maandamano bila ya kibali wakati hakukuwa na maandamano yoyote.
Tunazo taarifa pia kwamba kuna njama za kuwakamata tena viongozi mashuhuri wa CUF na hasa Mhe. Mansoor Yussuf Himid na Mhe. Mohamed Ahmed Sultan (maarufu kwa jina la Eddy Riyami) na kuwaleta katika magereza ya Tanzania Bara kwa lengo la kuwanyamazisha Wazanzibari ili wasipaze sauti zao kupinga utawala wa kidikteta uliowekwa madarakani kwa nguvu za dola kinyume na matakwa ya kidemokrasia ya wananchi wa Zanzibar.
HATUA TUTAKAZOCHUKUA:
Baada ya hatua ya leo ya uzinduzi wa Taarifa hii, Chama Cha Wananchi (CUF) kimejiandaa kuchukua hatua zifuatazo:
1. Kumuandikia rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. John Pombe Magufuli, na kumkabidhi nakala ya Taarifa hii ili ajue kinachofanyika nchini na hasa akiwa Amiri Jeshi Mkuu.
2. Kuiwasilisha Taarifa hii pamoja na vielelezo vyote katika jumuiya, taasisi na mashirika ya kimataifa yanayotetea haki za binadamu ulimwenguni kwa hatua zao.
3. Kuiwasilisha Taarifa hii pamoja na vielelezo vyote katika Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora hapa nchini ambayo hata katika mkutano wa Geneva ilitambuliwa uwepo wake, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) pamoja na taasisi nyengine zinazoshughulikia masuala ya haki za binadamu hapa nchini.
4. Kufungua kesi katika Mahkama Kuu ya Tanzania dhidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) kuhusiana na matendo yanayohusisha Jeshi la Polisi visiwani Zanzibar. Tayari, tokea mwezi uliopita mwanasheria wetu ameshawasilisha taarifa rasmi kwa Waziri na IGP kuhusu nia hiyo kama sharia zetu zinavyotaka ikiwa ni hatua ya kwanza katika kufungua kesi hiyo.
5. Kuendelea na hatua ya kukamilisha taratibu zitakazoiwezesha Mahkama ya Kimataifa ya Uhalifu (International Criminal Court – ICC) kuanzisha uchunguzi dhidi ya watu wenye dhamana mbali mbali ambao wamehusika kuchochea, kutoa au kusimamia maagizo yaliyopelekea makosa dhidi ya ubinadamu na makosa yanayoilenga jamii fulani ya watu. Jopo la wanasheria wetu limeshaanza kazi hiyo wakiwemo wanasheria wa kimataifa waliobobea katika kesi za ICC. Tayari kampuni moja ya wanasheria tuliyoipa kazi hii imeshawaandikia rasmi ICC kuhusiana na suala hili.
MWISHO:
Tunawapongeza na kuwashukuru wananchi wote wa Zanzibar wanaokandamizwa na kuteswa kwa sababu tu ya kutetea utu wao na haki zao kwa moyo wao wa ujasiri, ushapavu na uvumilivu katika kukabiliana na ukandamizaji huu na mateso yanayowakuta.
Tunawahakikishia kwamba Chama Cha Wananchi (CUF) ambacho wamekiamini na kukipa ridhaa yao kitaendelea kuwa pamoja nao na kutetea haki zao ikiwemo haki yao ya kuheshimiwa chaguo lao la kiongozi yupi na chama gani kiwaongoze. Sisi kama viongozi wao hatuna wasiwasi kwamba kwa mashirikiano ya pamoja HAKI ITASIMAMA NA UTU UTASHINDA.
Ahsanteni kwa kunisikiliza.

Saturday, May 14, 2016

MSISTAJABU SIKU YOYOTE MKIMUONA SHEIN,JECHA NA SAID HASSAN SAID KWENYE MAHAKAMA HII YA KIMATAIFA YA UHALIFU (ICC)


Anayeitwa Rais wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein akimwampisha Mwanasheria Mkuu wa SMZ, Said Hassan Said. Tukio hili ni baada ya uchaguzi wa marudio wa Machi 20, 2016. Chama Kinachoaminika kuwa kilishinda Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa Oktoba 25, mwaka jana, Chama cha Wananchi (CUF) jana, kimetangaza rasmi kuwa kimefungua kesi dhidi ya anayejiita Rais wa Zanzibar, katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC ), The Hague. Kwa Mujibu wa Nassor Mazrui ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, amesema kwamba, CUF kimefungua kesi hiyo dhidi ya rais wa Zanzibar, pamoja na viongozi wengine kwa madai ya kudhoofisha haki za kidemokrasia visiwani Zanzibar. Mazrui amesema kwamba, kwa sasa CUF inasubiri maelekezo zaidi kutoka ICC juu ya kuanza na uendeshwaji wa kesi hiyo. Cuf inao ushahidi wa kutosha wa ushindi wa uchaguzi wa Oktoba, mwaka jana.
Endapo ICC, itaridhia madai ya kesi ya CUF, itakuwa ni kesi ya kwanza ya Zanzibar, kufunguliwa na chama cha siasa katika mahakama hiyo tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa Tanzania, mwaka 1992. Mwanyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jeche alifuta matokeo ya uchaguzi wote Oktoba 28, 2015 kwa madai kuwa taratibu, kanuni na sheria zilikiukwa. Hatua hiyo ya Jecha, kufuta uchaguzi huo ni baada ya Chama cha Wananchi (CUF), kuelekea kushinda katika uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka uliyopita. Aidha, Mazrui amesema katika kesi hiyo, mbali na Rais wa Zanzibar, watu wangine waliyoshitakiwa ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa SMZ, na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Tuesday, May 10, 2016

KIKWETE AOGOPA KUKABIDHI CHAMA KWA MAGUFULI AMEIKIMBIA DODOMA JE MNA MABUSHA NDANI YA CCM ANAOGOPA YATATUMBULIWA....???

Hali si shwari ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na mchakato unaoendelea wa kumkabidhi Rais Dk. Magufuli uenyekiti wa chama hicho, kukumbwa na sintofahamu.

Taarifa kutoka ndani kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC), kilichofanyika juzi Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma, zimethibitisha kutokea mgawanyiko wa vigogo ndani ya chama hicho.

Hali hiyo imekuja baada ya kutokea kwa mvutano juu ya tarehe rasmi ya kufanyika kwa mkutano mkuu maalumu uliopangwa Juni mwaka huu, ambao pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Rais mstaafu Jakaya Kikwete atakabidhi kijiti kwa Rais Magufuli.

Chanzo cha kuaminika ndani ya kikao hicho kilidokeza  kuwa, kabla kilifanyika kikao kidogo kilichokuwa na wajumbe wanne ambao pamoja na mambo mengine walijadili ajenda muhimu  ikiwamo ya kupanga tarehe kwa ajili ya mkutano huo.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, kikao hicho kidogo kilishirikisha viongozi wanne akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Jakaya Kikwete, Rais Dk. John Magufuli, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Habari hizo zinaeleza kuwa, katika kikao hicho kidogo viongozi hao walikubaliana wakatangaze tarehe rasmi, na Rais Magufuli alikubali kukabidhiwa uenyekiti wa chama kama ulivyo utaratibu wa CCM lakini baada ya kikao cha Kamati Kuu kuanza, Kikwete alikataa kuruhusu hoja hiyo ijadiliwe, hatua iliyozua mfarakano.

“Baada ya kumalizika kwa kikao kile viongozi hao wanne waliingia ndani ya kikao cha CC ambacho kilikuwa na ajenda kadhaa ikiwemo ya mkutano mkuu maalumu ambapo mwenyekiti alirusha na kutaka hoja ya tarehe isijadiliwe,” kilisema chanzo hicho.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, ilipofika ajenda ya tatu ambayo iliwasilishwa na Katibu Mkuu, Kinana kuhusu kutangazwa kwa tarehe ya mkutano mkuu maalumu,  Kikwete aligoma isijadiliwe na badala yake aliahirisha kikao na kutoka nje.

Chanzo hicho kilisema, uamuzi wa Mwenyekiti Kikwete wa kuahirisha kikao ulijikita katika suala la gharama za mkutano ambazo zinakadiriwa kuwa ni zaidi ya Sh bilioni mbili, hivyo aliwataka wajumbe waahirishe kikao ili kutoa fursa ya kutafuta fedha.

Taarifa hizo zilieleza kuwa, kutokana na hali hiyo yaliibuka makundi mawili, moja linalomuunga mkono Kikwete na jingine linalopingana na hoja hiyo, likidai kuwa fedha si tatizo kwa chama hicho kwa kwani kina miradi, ruzuku na marafiki wengi.

“Wanaompinga mwenyekiti walishangazwa na hoja hiyo wakisema kuwa, suala la fedha ni la watendaji wa chama na si la mwenyekiti, kitendo ambacho wamekitafsiri kwamba mwenyekiti hana dhamira ya dhati ya kukabidhi chama kwa sasa,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kiliendelea kutoa taarifa kuwa, baada ya Kikwete kugoma kujadili tarehe alisimama mjumbe Jenista Mhagama, ambaye alipinga uamuzi huo, huku akisema suala hilo ni lazima lijadiliwe kwa kina na tarehe ya mkutano mkuu itangazwe.

“Kauli ya mwenyekiti inaonekana iliwaudhi baadhi ya wajumbe, lakini Jenista alizungumza vizuri sana na kumhoji mwenyekiti inakuaje hataki kusema lini utafanyika mkutano mkuu maalumu ili akabidhi chama.

“Maana suala la makabidhiano ni la utamaduni wa ndani ya CCM, Jenista alisema aliyekaa muda mrefu alikuwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere pekee lakini na yeye alikabidhi kwa mzee Mwinyi (Ali Hassan) na pia ilipofika wakati kama huu mzee Mwinyi naye alikabidhi kwa mzee Mkapa.

“Si hilo tu hata mzee Mkapa naye alikabidhi chama kwake (Jakaya Kikwete), sasa inakuwaje yeye leo hataki kufuata utaratibu huo ambao ni wa kawaida ndani ya chama?,” kilihoji chanzo hicho.

Chanzo kingine cha habari kilisema kuwa baada ya mwenyekiti huyo wa CCM taifa kuahirisha kikao hicho juzi, aliondoka na kurejea jijini Dar es Salaam kwa gari tofauti na ratiba iliyokuwa imepangwa.

“Ratiba ya chama ilikuwa baada ya kikao cha jana (juzi) mwenyekiti angelala Dodoma na badala yake alipoahirisha kikao kwa utata alipanda kwenye gari na kuondoa hali ya kuwa alitakiwa kurejea Dar leo (jana).

“Baada ya kikao hicho alitoka mzee Kinana akiwa amekasirika sana, tena huku akiwa amekunja sura, unajua siku zote mzee Kinana anaamini kwamba kile kilichokuwa kinapiganiwa na chama hivi sasa ndicho kinachotekelezwa na Rais Magufuli tena kwa vitendo tofauti na huko nyuma,” kilisema chanzo chetu.

Baraza la Wazee kukutana
Taarifa nyingine zinaarifu   kwamba, kutokana na hali hiyo Baraza la Wazee la CCM linaloundwa na viongozi wastaafu, linatarajiwa kukutana kati ya leo na kesho kwa lengo la kujadili hali hiyo ili kuondoa mtanziko huo uliojitokeza.

“Ninachotaka kukuambia katika kipindi cha siku mbili baraza la ushauri la wazee litakutana na kujadili hali hii na baada ya hapo watakwenda kwa mwenyekiti kumshauri juu ya uamuzi wake na autafakari kwa kina.

“Tunajua tunakwenda vizuri katika hili na hakuna kitakachoharibika na wazee wetu watamshauri vema mwenyekiti ili kupata mwafaka wa kudumu na mkutano mkuu utafanyika mwezi uliopangwa,” chanzo hicho kilisema.

Baraza la Ushauri la Wazee wa CCM, linaongozwa na Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (Mwenyekiti), Pius Msekwa (Katibu) na wajumbe ni Rais mstaafu Benjamin Mkapa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM mstaafu (Bara), John Malecela.

BANIANI MBAYA KIATU CHAKE DAWA AU SIO MAHMOUD THABIT KOMBO...???

Serikali ya Kuwait imeahidi kutumia Sh 84 bilioni kwa ajili ya kuifanyia ukarabati Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja mjini hapa.
Akizungumza na Waziri wa Afya Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo katika ofisi za wizara hiyo mjini Unguja jana, Balozi wa Kuwait nchini, Jasim Al-Najim alisema Serikali yake imechukua hatua hiyo ili kudumisha umoja uliopo kati ya pande mbili hizo.
Balozi huyo alisema timu ya wataalamu kutoka Kuwait inatarajia kuwasili Zanzibar Agosti kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu juu ya utekelezaji wa msaada huo.
Alisema matengenezo yataanza baada ya wataalamu hao kumaliza kazi hiyo na kutoa maelekezo yakinifu juu ya utafiti wao katika majengo hayo.
Balozi Al-Najim alisema watakapokamilisha ujenzi huo mashirika mbalimbali yatajitokeza kwa ajili ya kusaidia miradi mingine.
“Mradi huu mkubwa utafungua milango kwa Serikali ya Kuwait kupitia mashirika ya misaada ya nchi hiyo kusaidia miradi mingine ya maendeleo ya uchumi na kijamii,” alisema.
Waziri Kombo aliishukuru Serikali ya Kuwait kwa kukubali kutekeleza mradi huo mkubwa utakaowasaidia wananchi wa Zanzibar.