Thursday, November 13, 2014

MH KHATIB SAID HAJJ MBUNGE WA KONDE PEMBA AIPA DOZII BAKWATA NALO LAAZA KUPANDA MAPEPOBAKWATA YACHAGAWA
BARAZA KUU ATII LA WAISLAMU NCHINI TANGANYIKA (BAKWATA)
Limekuwa Likimtumia MESSEGE na simu za VITISHO Mbunge wa Konde Pemba, Mh Said Hajj, Kufuatia shutma alioitowa Mbunge huyo Bungeni 11/10/2014, kwa BAKWATA na serikali kutokana na ukimya juu ya malalamiko ya udhalilishwaji wa vyombo vya dola kwa Masheikh waliotolewa nchini Zanzibar na kupelekwa nchini Tanganyika.

Atii kwa tuhuma za ugaidi

Moja ya ujumbe aliyotumiwa Mheshimiwa huyo ni huu

Tunasikitishwa Sana kwa kitendo chako ulichokifanya jana katika bunge la jamhuri ya muungano ya Tanzania
Wewe ukiwa mbunge muislam haikuwa sahihi kukisema chombo cha waislamu Bakwata kuwa ni chombo cha kinafiki na baya zaidi kuisema jumuiya hii kuwa ni moja kati ya taasisi ya za CCM kama ilivyo jumuiya ya vijana ya CCM.
Na baya zaidi wewe ukiwa ni muislam kuliomba baraza kuu la maaskofu kuwatetea masheikh eti wanaothalilishwa katika magereza ya Tanzania bara. Jambo ambalo Halina uthibitisho wowote Bali ni maneno ya mitaani uliyokubali kulishwa nawe ukayameza bila kujitambua. Sisi kama taasisi ya kiislam inayotambuliwa kisheria na serikali yetu tukufutunakulaani sana kwa kuikashifu Bakwata na tunaanda Taratibu za kisheria kupitia wanasheria wetu kuona hatua za kuchukua dhidi yako ili iwe fundisho kwako na wale wote wenye tabia za kuidhakilisha jumuiya hii ya waislamu Tanzania
Wabillahi tawfiq
Sisi vijana wa Bakwata
Kny sheikh wa mkoa wa Dsm shk Alhad Mussa Salim;
BAKWATA HAMNA INTERNETE KWENYE OFISI ZENU..??


Na Mh Khatib kwa ujasiri mkubwa akawajibu kwa kuwatumia ujumbe huu
Mukienda mahkamani mutanikuta nimeshafika nawasubiri
Nilisema bungeni kila mtu ameona na nyinyi kama taasisi inayojiamini semeni au jibuni hadharani waislamu watapima wataamua Nani mkweli au muongo Hii ya kunitumia sms kwangu nahisi ni ishara ya woga mumewatawala! Niwahakikishie tu mimi najiamini na Allah pekee Ndio tegemeo langu
Allah aalam!
DUA NA USHIRIKIANO WA WAISLAMU UNAHITAJIKA KATIKA HILI KWA NDUGU KHATIB SAID HAJJ
TAFADHALI SAMBAZA UJUMBE HUU KWA WAISLAMU WOTE

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment