Friday, November 7, 2014

SHEIN KAMA WEWE KWELI NI MSEMAJI WA WANANCHI WA ZANZIBAR WOTE BASI WASEME WAZANZIBARI WALIO CHUKULIWA NA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA USIKU NA KUFUNGWA JELA YA NCHI YA TANGANYIKA WAREJESHWA HARA NCHINI ZANZIBAR UKIUFYATA BASI WEWE NI KIDAMPA TU WA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA.

tapatalk_1415268423908
Raisi wa Maskani ya Kisonge, Dk Ali Mohamed Shein amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuacha kutumia vibaya mchakato wa Katiba Inayopendekezwa kwa lengo ya kuwagawa wananchi na kutishia amani na utulivu uliopo nchini.Lakini pia ameelezea kukerwa na kuchoshwa na atii na matusi yanayojitokeza katika kipindi hiki kutoka kwa baadhi ya viongozi, huku akisema atawachukulia hatua za kisheria na za kinidhamu bila kujali wana nyadhifa gani. Aliyasema hayo jana katika ukumbi wa Grand Palace,nchini Zanzibar wakati akizungumza na wananchi na viongozi wa CCM katika maadhimisho ya miaka minne ya kuwepo madarakani tangu aliposhindwa Urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 na kupewa kwa mabavu ya guvu za Mkoloni Mweusi Tanganyika.


“Nitawachukulia hatua za kisheria na kinidhamu viongozi wanaotumia vibaya mchakato wa kupata Katiba mpya kwa kutoa kauli za chuki na kutukanana katika majukwaa… nitatumia Katiba na Sheria na sio ubabe kwa sababu sio kawaida yangu kufanya hivyo,”((ngoja tukulize Shein hivi ni katiba ipi inayo sema Wazanzibari washikwe usiku wa manane nakupelekwa jela za nchi ya Tanganyika kwa Mkoloni Mweusi Tanganyika..? ni katiba ipi inayosema kuwa wewe ndiye msamaji wa Wazanzibari na sio Maalim Seif Sharrif Hamad..? ni katiba ipi iliyo sema muwalazimishe wazanzibari kubaki katika utumwa,utwana na kuwa nchi yao ni Koloni la Mkoloni Mweusi Tanganyika..? ni katiba ipi iliyosema wananchi wa Zanzibar wasiwe na uwezo wakujisemea wenyewe na wakijesemea basi waishiye jela za nchi ya Tanganyika kwa Mkoloni Mweusi..? ni katiba ipi iliyosema kila jambo la nchi ya watu wa Zanzibar liamuliwe Giningi Dodoma..? ni katiba ipi ilosema kuwa raisi hata kama hakuchanguliwa na wananchi basi apige magoto kwa Mkoloni Mweusi Tanganyika ili apewa uraisi kwa nguvu za Kijeshi..? ni katiba ipi ilosema kuwa wazanzibari walazimishwe kuikubali katiba ya Mkoloni Mweusi Tanganyika na wakati huo huo katiba ya nchi yao imezwe na kubadilishwa na kufanyiwa ukiritibwa..? Shein ni katiba ipi ilosema wazanzibari washikwa na kupelekwa nchi ya Tanganyika wakalawitiwe na kupigwa mpaka wengine imebidi wakatwa miguu..? N.K.))   Alisema kumeanza kujitokeza viashiria vya kuanza kuvuruga amani na utulivu iliyopo sasa kwa kisingizio cha mchakato wa rasimu ya Katiba Inayopendekezwa hivi sasa.

Alisema Katiba Inayopendekezwa ni mkombozi kwa wananchi wa Zanzibar kwa sababu imejibu hoja za malalamiko na kero za Muungano ambazo awali zilikuwa zikilalamikiwa na wananchi ikiwemo wanasiasa.(hahahahahaahhaha bora nicheke maana huyu anaonyesha hata hajuwi Wazanzibari wanataka nini)
Akifafanua, alisema kwa muda mrefu wananchi wa Zanzibar walikuwa na malalamiko mengi katika Muungano ambayo kwa bahati nzuri katika Katiba Inayopendekezwa yamepatiwa jawabu sahihi.
Kwa mfano alisema si kweli kwamba Muungano uliopo sasa umeimeza Zanzibar na haitambuliwi katika jumuiya za kimataifa.((swali tunakuliza kama tunatabuliwa mbona hatuombi misaada wenyewe..?mbona bendera yetu haipepei U.N. mbona hatuna paspoti zetu zinazo onyesha kuwa sisi ni Wazanzibari,Mbona hatuna sarafu yetu N.K). Ameelezea kushangazwa na tabia ya vyama vya upinzani kususia mchakato wa Katiba wakati ndio waliokuwa mstari wa mbele kulilia uwepo wa Katiba mpya. Aidha, ameelezea kushangazwa na msimamo wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi ya  Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuikataa Katiba Inayopendekezwa, ilhali mambo anayoyalilia yamo katika katiba hiyo.((hebu shein tuambia ni mambo yapi anayo yalilia Maalim Seif Sharrif Hamad ambayo yapo katika katiba hii ya CCM..??))
Alisema Katiba Inayopendekezwa imetoa fursa kubwa kwa Zanzibar kufanya mambo yao kwa mapana zaidi ikiwa katika Jamhuri ya Muungano wa (Tanzania) au wa Mkoloni Mweusi Tanganyika...?? ((kama yapi mbona huyasema basi hayo mambo wananchi wakakusikia..?)) Alisema Katiba Inayopendekezwa ni kwa maslahi ya (Watanzania) au (wana CCM na Wake zao na Mahawara wao na Watoto wao..?) ambayo imezingatia mambo yote muhimu ikiwemo kwa upande wa Zanzibar. Alisema: “Nimesikitishwa sana mwenzangu, Makamu wangu wa Kwanza wa Rais amekuwa akisisitiza kutungwa kwa sera za nishati na mafuta kwa ajili ya kujitayarisha kuchimba mafuta, lakini yeye Katiba Inayopendekezwa haikubali.” Akifafanua zaidi alisema Baraza la Wawakilishi ndiyo lililopitisha azimio la kutaka nishati ya mafuta na gesi kuondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano. Aidha, alimtaka Maalim Seif kuacha kuwashawishi wananchi wa Zanzibar kuikataa Katiba Inayopendekezwa akisema yeye sio msemaji wa wananchi wa Zanzibar.
NAMNUKU SHEIN...alimtaka Maalim Seif kuacha kuwashawishi wananchi wa Zanzibar kuikataa Katiba Inayopendekezwa akisema yeye sio msemaji wa wananchi wa Zanzibar.NAENDELEA KUMNUKU SHEIN....“Msemaji wa wananchi wa Zanzibar wote ni mimi na sio yeye MWISHO WA KUMNUKU SHEIN.  JE SHEIN HAWA KWENYE HIZI PICH MBILI HAPA CHINI SIO WAZANZIBARI HAWA.....??? MBONA HUWASEMEI......???
Msemaji wa wananchi wa Zanzibar wote ni mimi na sio yeye…nawataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ya kuipitisha Katiba mpya Inayopendekezwa,” alisema. Alisema Katiba Inayopendekezwa imezingatia mambo yote ambayo wananchi wa Zanzibar wametaka kuzingatiwa na kusisitizwa ikiwemo mafuta na gesi. Alisisitiza na kusema Katiba Inayopendekezwa imezingatia na kuuenzi Muungano wa Tanganyika wa Zanzibar pamoja na Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ambayo yameasisiwa na viongozi wakuu wa nchi mbili hizo. Aidha, Dk Shein amesema amekubaliana na kuridhishwa na Katiba Inayopendekezwa ambayo imetoa kipaumbele kwa Zanzibar kupiga hatua kubwa ya maendeleo.Alisema mambo yaliyobakia katika Muungano ni muhimu sana ikiwemo ulinzi na mambo ya elimu ya juu ambayo yatasaidia kuwawezesha vijana kupata elimu ya juu kwa kutumia bodi mbili za elimu.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment