Monday, February 22, 2016

VIDEO-TUNDU LISSU A.K.A. RONALDO ZANZIBAR KUKICHAFUKA MAGUFULI NA SHEIN HAWATOSALIMIKA KUSIMAMA ICC

TUNDU LISSU (01)

TUNDU LISSU (02)

TUNDU LISSU (03)

HUU NDIO MPAGO WAO NA DHAMIRA ZAO CCM MAGUFULI ANGALIA SANA AU UTAISHIA ICC WAKAKUTUMBUWE WEWE MAJIPU USIONE KUWA MKAPA ALIUWA PEMBA AKASALIMIKA KWENDA ICC NA WEWE UNADHANI UTASALIMIKA 

TUNDU LISSU ASEMA ZANZIBAR KUKICHAFUKA MAGUFULI (na Shein pia) HATOSALIMIKA KUSIMAMA ICC
HALI ya kisiasa nchini Zanzibar imezidi kuwa tete baada ya kurejea kwa kasi chuki za kisiasa, huku wanawake wakijikuta wakipewa talaka na waume zao pamoja na kushamiri kwa vitendo vya hujuma katika miradi ya maendeleo.
Suala hilo linaibuka wakati Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ikiwa imetangaza uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika Machi 20, huku vyama tisa vikitangaza kutoshiriki kikiwamo Chama cha Wananchi (CUF).
Chuki hizo za kisiasa ambazo ziliibuka kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, zinarejea kwa kasi ambapo kwa sasa baadhi ya familia zimeanza kutengana ikiwamo hata kutonunua bidhaa katika maduka ya watu ambao wanaamini hawana uhusiano nao wa kisiasa.
Kutokana na hali hiyo, juzi Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema hatua hiyo inaweza kuvirudisha visiwa hivyo katika chuki ambazo zilisahaulika baada ya kupatikana kwa mwafaka na hatimaye kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyovishirikisha vyama vya CCM na CUF.
Vuai alisema kwamba hivi sasa CCM inajiandaa kushiriki uchaguzi wa marudio licha ya baadhi ya vyama kuususia.
“Tunasikia baadhi ya vyama vikitangaza kutoshiriki ila ni lazima wananchi wajue kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa si ya CCM wala CUF, hivyo chama chochote kitakachoshiriki uchaguzi na kufikia matakwa ya kikatiba kitaunda Serikali ya umoja,” alisema Vuai.
Alisema ni lazima ZEC itangaze orodha ya vyama vitakavyoshiriki uchaguzi huo wa marudio kuliko kuendelea kukaa kimya.

KISHA NYINYI MUNAYAITA MAPINDUZI MATUKUFU HIVI KWELI NYINYI MUNAJUWA UTUKUFU NI NINI AU DUNIA IMEWAVA KISAWA SAWA MPAKA MNAKUFURU 

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment