Wednesday, September 2, 2015

NCHINI TANGANYIKA-TUNDU LISSU KINACHO MSUMBUWA DR SLAA NI TAMAA YA URAIS TUNAMTAKA DR SLAA ARUDISHE MALI ZOTE ZA CHAMA.


USIFANYE MCHEZO NA CCM UKIWA NA NJAA UTALISHWA UKIWA NA TAMAA UTAPOZWA UKIJIFANYA MJANJA UTATULIZWA UKIJIFANYA MUAMINIFU WATAKUGEUZA MSAALITI HAYA TUELEZENI NDIO NINI SASA WATU WAZIMA KUMBE OVYOO TAMAA YA URAIS IMEISHIYA KWENYE MEZA YA JUICE NA VILEJA MKINUKA VYOTE MNAVIPELEKA CHOONI NDIO MAAPATA NINI...????? 

Katibu Mkuu wa  Chadema, Dk Wilbroad Slaa, jana  alitangaza rasmi kuachana na siasa  baada  ya  kutofautiana  na  chama  chake  katika  kumpokea  Edward  Lowassa  na  hatimaye  kumfanya  mgombea  urais  wa  chama  hicho  chini  ya  mwamvuli  wa  UKAWA.

Dr. Slaa  alitoa  uamuzi  huo  jana  mbele  ya  waandishi  wa  habari  ambapo  pia  mbali  na  kutangaza  kuachana  na  siasa  aliwatuhumu  Lowassa  na  Sumaye  kuwa  ni  MAFISADI  wa  kutupwa  na  kwamba  hawastahili  kupewa  nchi .

Akijibu tuhuma za Dk. Slaa mwansheria wa CHADEMA Tundu Lissu amesema anashangaa kwamba Dr. Slaa anadai hakubaliani na uteuzi wa Lowassa kwa ajili ya kiti cha rais wakati yeye ndiye aliyepanga na kumleta Lowassa katika chama hicho.

Lissu  amesema  kinachomsumbua  Slaa  ni  tamaa  ya  Urais  maana  CHADEMA  walikuwa  wamekwisha  mteua  kugombea  urais  tangu  mwezi  wa  kwanza.

"Kamati  kuu  ilimteua  kugombea  urais  kwa  tiketi  ya  chadema  tangu  mwezi  january  na  ilipofika  mwezi  April  kamati  ilimthibitisha  tena  kuwa  yeye  ndo  mgombea  wetu.

"Ilipofika  mwezi  wa  tano, Dr.  Slaa  mwenyewe  akaanzisha  mazungumzo  ya  kumleta  Lowassa  Chadema.

"Amesema  mshenga  ni  Gwajima,hajasema  mposaji  ni  nani.  Nani  aliyemfuata  Gwajima  kumwambia  tunamtaka  Lowassa, ni  Dr. Slaa mwenyewe.

"Yeye  ndiye  aliyemwambia  Gwajima halafu  ndo  akamwambia  Mwenyekiti  wa  chama  kuwa  Lowassa  akikatwa  tumchukue, na  tumchukue  kwa  sababu  ana  nguvu  kubwa  na  ataipasua  CCM  katikati.   

"Mbowe  alipoambiwa  hivyo  alikubali  na  Dr. Slaa  ndiye  aliyeunda  timu  ya  majadiliano  ya  Chadema  yenye  wajumbe  watatu  ambao  ni  Benson Kigaila, John Mrema, Reginald Munishi.

"Walikaaa  na  kufanya  mazungumzo  ya  kina  na  Dr. Slaa  alishiriki  kila  hatua.Majadiliano  hayo  yalikamilika  tarehe  22.7.2015  ambapo  Slaa  aliitisha  kikao  cha  kamati  kuu  cha  dharura  chenye  ajenda  moja  tu  ya  kumkaribisha  Lowassa  ili  awe  mgombea  urais  wa  Chadema."  Amesema  Lissu

Kwa nini  Dr. Slaa amewasaliti......????
Tundu  Lissu  amesema  kilichomfanya  Dr. Slaa  awageuke  ni  First  Lady, kwa  maana  ya  mke  wake  ambaye  hakukubaliana  na  kitendo  cha  Slaa  kumpisha  Lowassa

Lissu  amesema  kuwa wakati Lowassa anapokelewa tarehe 27 July kwenye Kamati Kuu, Dr.Slaa hakulala nyumbani,  aliporudi nyumbani mchumba wake alimtupia mabegi nje na DR. alilala kwenye gari.

"Aliporudi  nyumbani, Slaa  alitupiwa  mabegi  nje, akalala  kwenye  gari. Kesho  yake  akaja  na  kusema  anataka  kujiuzulu." Amesema  Lissu  na  kuongeza:

"Slaa  anasema  hana  chama  na  hajihusishi  na  chama  chochote, lakini  cha  ajabu  ni  kwamba  mwezi  huu  amepokea  mshahara  wa  katibu  mkuu  wa  chama, bado  anatembea  na  gari  ya  katibu  mkuu  wa  chama.

"Japokuwa  amekitukana  chama, lakini  bado  anatembea  na  magari  ya  chama, nyumba  anayokaa  alinunuliwa  na  chama  na  inalindwa  na  walinzi  wa  chama.

".....Ajitokeze  atuambie  ni  nani  aliyemwandalia  huu  mkutano  wa  serena  hoteli....???  hizo  gharama  zimelipwa  na  nani.....???  na  kwa  nini  ametamka  leo.....???

"....Kwa  kuwa  Slaa  amekitukana  chama,  litakuwa  ni  jambo  la  busara  sana  kama atarudisha  mali  zote  za  chama."

Akizungumzia  tuhuma  zilizotolewa  na  Dr.Slaa  dhidi  ya  Lowasaa, Lissu  amesema  CHADEMA  walimhoji  Lowassa  kuhusu  sakata  la  Richmond  na  aliwaambia  kuwa  aliyeruhusu  mkataba  wa  Richmond  uendelee  ni  Rais  Kikwete.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

MNARA WA MIAKA 50 WAZINDULIWA NCHINI ZANZIBAR


 Muonekano wa Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi ukionekana wakati wa mandhari ya usiku katika bustani ya michezani kisonge ukiwa katika maandalizi ya uzinduzi wake uliofanyiuka asubuhi hii na kuzinduliwa na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Shein.


Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Shein amewatahadharisha watu wanaoogopa mabadiliko ya Maendeleo kwamba waachane na tabia hiyo vyenginevyo Dunia  bila ya shaka na ajizi itawabadilisha. Alisema Wazanzibari wanapaswa kwenda na wakati katika  kuendesha  pamoja na kusimamia masuala yao ili waende sambamba na wananchi wa visiwa vyengine Duniani wanaoonekana kupiga hatua za haraka za Maendelei ya Kiuchuni na Ustawi wa Jamii. Shein alieleza hayo wakati akizungumza na Watu wa rika mbali mbali ambao wengi wao ni vijana na Watoto mara baada ya kuuzindua Mnara wa Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 uliojengwa katika Majumbe ya Maendeleo Michenzaji Kati Kati ya Mji nchini Zanzibar.

Alisema wapo watu wakiwemo baadhi ya watendaji wa Taasisi za Umma wenye madaraka ya kutoa maamuzi ambao wana tabia ya kuogopa Mabadiliko kwa kuchelewesha kuidhinisha miradi ya Kiuchumi inayokusudiwa kuwanzishwa na wawekezaji walioamua kuwekeza hapa nchini Zanzibar.Shein alikemea kwamba tabia hiyo mbaya isiyo na sababu za kimsingi imekuwa ikichelewesha na kuviza Maendeleo ya Wananchi na kupunguza Mapato ya Taifa kupitia uanzishwaji wa miradi hiyo wakati Serikali tayari imeshaweka milango wazi kwa wawekezaji wa ndani na nje ya Nchi. Aliupongeza Uongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar chini ya usimamizi wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko huo kwa juhudi iliyochukuwa ya kujenga mnara huo wenye urefu wa Mita 33.5 ambao utatoa fursda kwa wananchi na wageni kuona mamdhari nzuri ya Mji wa Zanzibar sambamba na kupata huduma za msingi.

Alisema chimbuko la Mnara huo lililoibuliwa na Baraza la Mapinduzi Zanzibar  wakati wa maadhimisho ya sherehe za Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar  lilikuwa na lengo la kuonyesha vugu vugu la Maendelei ya Zanzibar tokea kufanyika kwa Mapinduzi ya Zanzibar ya Tarehe 12 Januari Mwaka 1964. Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar {ZSSF } Nd. Abdulwakil Haji Hafidh alisema ujenzi wa Mnara huo mbali ya kutoa fursa kwa wananachi na wageni kuangalia mamdhari ya Mji wa Zanzibar lakini pia utatoa nafasi kwa wazazi kupata mapumziko  huku wakiwasubiri watoto wao wanaowapeleka katika Viwanja vya Kufurahishia Watoto Kariakoo. Alisema tahadhari hiyo imechukuliwa maalum kwa kuzingatia kwamba Mji wa Zanzibar bado haujawa na maeneo mengi ya kupumzikia kiasi cha kuongezwa maeneo hayo ili kukidhi mahitaji kwa siku zinazotokea kuwa na idadi kubwa ya watu  hasa siku za siku kuu ambazo watu wengi huamua kutembelea viwanja hivyo.

Mkurugenzi huyo wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar { ZSSF } alifahamisha kwamba mnara huo utakuwa na sehemu maalum zitakazowekwa kwa ajili ya watu na wageni kujifunza Historia ya Mapinduzi ya Zanzibar, sehemu za kujifunza wachezaji wa michezo mbali mbali maarufu duniani, kuangalia mandhari ya Mji wa Zanzibar pamoja na Mkahawa unaozunguuka. Alisema taasisi za Fedha kama Benki ya Wananachi wa Zanzibar PBZ, na Ile na NMB zitatoa huduma za fedha kwa kutumia mtandao wa ATM ili kuwaondoshea usumbufu wateja wao wakati wanapoishiwa na Matumizi. Nd. Abdulwakili alieleza kwamba  katika kulibadilisha eneo hilo la Michenzaji Mfuko huo umeshaandaa mpango wa kujenga majengo la Kimataifa ya Kibiashara  { SHOOPING  MALLS } upande wa Kaskazini kwa kutafuta washirika wa Maendeleo watakaoshirikiana katika kujenga majengo hayo. Mnara huo wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar  wenye ghorofa 9 uliojengwa kwa gharama ya Shilingi za Kitanzania Bilioni Nane unatarajiwa kurejesha thamani ya Fedha hizo katika kipindi cha miaka 12 ijayo.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

JE NI YUPI WA KUPELEKWA MAHAKAMANI TENA ((THE HAGUE)) WEZII WA MABILLIONI WA ESCROW, BENJAMENI MKAPA ALIYE FANYA MAUWAJI YA RAI WASIO NA HATIA YOYOTE AU MTUHUMIWA LOWASSA.....????



Tokea atangeze kujiondoa CCM na kujiunga chama cha democrasia na maendeleo( CHADEMA)Mh Edward Lowassa ,imekua kasakamwa na wanafiki wa chama tawala na kulikuza swala la richmond mama vile yeye ni mtuhumiwa pekee ndani ya CCM alokua sio msafi.....?? Tumesahau kuwa nijuzi juzi tu hapa Serekali nzima ya ccm chini ya raisi huyo huyo Kikwete kumetokea wizi wakutisha wa Tageta Escrow na hakuna alofikishwa kwenye vyombo vya sheria wala nini na baadae wezi hao hao wameteuliwa na CCM kuwania nafasi zao za uongozi.
Sasa iwaje leo tuhuma za swala la Mh Lowassa lionekane nikubwa kuliko Mapapa yalomo kwenye CCM.....?? ikiwa kulitokezea ubadhirifu wa kupotea pesa za Richmond jee kikwete atalikwepa vipi haliyakua yeye ndio alokua Raisi......?? na ubadhirifu wa kuibiwa mamillioni ya Tageta Escrow jee kikwete atalikwepa vipi na hili haliyakua yeye bado na ndio alokua Raisi.....??? au swala la Tageta Escrow vipi lisimuhusu Waziri mkuu Mizengo Pinda...... ?? Au kikwete atawaeleze nini waislamu kwa kuwafunga Masheikh na Wazanzibari wasio na hatia yoyote katika magereza ya nchi yake ya Tanganyika...??? Au tuchukulie swala la Benjameni Mkapa kuwaua raia wa nchi ya Zanzibar wasio na hatia yoyote ndio jepesi lakuweza kuonekana la Mh Edward Lowassa ni kubwa kuliko raho za Wazanzibar na Waislamu wa Muiembe chai.........???.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

Tuesday, September 1, 2015

NCHINI TANGANYIKA SHERIA YA MAKOSA ATII YA MTANDAO KUANZA KUTUMIKA LEO NCHINI TANGANYIKA


Nchini Tanganyika Serikali atii imewatoa hofu wananchi kuhusu Sheria ya Makosa ya Mtandao inayoanza kutumika rasmi leo kuwa haijatungwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu, bali kwa maslahi mapana ya taifa na kuleta maendeleo ya nchi, kujenga uchumi imara na kupambana na wahalifu.

Aidha,  serikali imewasisitizia wananchi kutumia vizuri mitandao kwa faida yao na taifa na kujiepusha na mambo ambayo yanakatazwa na sheria hiyo  ili kutoingia matatani.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika jana kuhusu kuanza rasmi kutumika kwa sheria hiyo na ya miamala ya kielektroniki.

“Serikali imejiridhisha baada ya kufanya maandalizi yote muhimu ikiwamo kutoa elimu kwa umma na kujenga uelewa kwa watekeleza wa sheria hizi. Sasa sheria hizi zitaanza kutumika rasmi Septemba 1 (leo),” alisema Prof. Mbarawa.

Alisema sheria hiyo itasaidia kupambana na uhalifu kwenye mtandao kutokana na watu wengi kutumia vibaya mtandao na kuwalaghai watu kutuma fedha ama kuiba katika mabenki.

Alisema kwa mujibu wa sheria hiyo, watu wanaosambaza meseji za uchochezi ama za uongo kwa watu wengine ni kosa la kisheria na kufanya hivyo watakumbana na adhabu kali.

Alisema mtumiwaji wa meseji za aina hiyo akifuta pasipo kusambaza kwa watu wengine sheria hiyo haitamwadhibu wala kumhusu.

“Sehemu ya kifungu cha sheria ya makosa ya mtandao, kifungu cha 16 kinaeleza: mtu   atakayechapisha   taarifa au data katika picha, maandishi, alama au katika namna nyingine yoyote katika mfumo wa kompyuta, huku akijua kwamba taarifa au data hizo ni za uongo, zinapotosha, zisizo sahihi, na kwa lengo la kudhalilisha, kutishia, kuudhi au kwa njia nyingine au kudanganya umma au kuchochea utendaji wa kosa, atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atalipa faini isiyopungua Sh. milioni tano au kutumika kifungo kisichopungua miaka mitatu au vyote kwa pamoja,” alisema.
Prof.   Mbarawa alitoa wito kwa wananchi wazingatie matumizi salama na sahihi ya huduma za mawasiliano na mitandao kwa manufaa ya kila mtu na kwa maendeleo ya taifa na kuepuka matumizi yasiyo sahihi.

Baadhi ya makosa ambayo yanaweza kukufanya ushtakiwe
  1. Kuweka mtandaoni picha za kingono za watoto
  2. Kuweka mtandaoni picha za ngono au za utupu
  3. Kuweka taarifa za uongo mtandaoni
  4. Kuweka taarifa za uchochezi mtandaoni
  5. Kutukana au kumdhalilisha mtu
  6. Kuweka mtandaoni tetesi zisizothibitishwa
  7. Kutukana au kumdhalilisha mtu kwa misingi ya udini/ukabila.
  8. KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

NCHINI TANGANYIKA DR SLAA AONGEA AKIWA SERENA HOTEL AKIWA NA HAYA YA KUSEMA JE NIKUIJENGA CHADEMA NA UKAWA AU KUIUWA UKAWA NA CHADEMA...????


1.Napenda  kumshukuru  mwenyezi  mungu  kwa  kutujalia  uzima.

2. Nimeamua  kujitokeza  leo  hii  ili  kukomesha  upotoshaji  na  kuuweka  wazi  ukweli.


3.Sina  tabia  ya  kuyumbishwa  na  ninasimamia  ninachokiamini.

4.Sina  ugomvi  na  kiongozi  yeyote  maana  siasa  sio  uadui.

5. Siasa  inapoongozwa  kwa  misingi  ya  upotoshaji, matokeo  yake  ni  vurugu.

6. Naweka  wazi  kuwa  mimi  sikuwa  likizo  na  hakuna  mtu  yoyote  aliyenipa  likizo.

7.Kilichotokea  ni  kuwa  niliamua  kuachana  na  siasa  tangu  tarehe  28.7.2015  saa  sita  usiku  baada  ya  kutoridhishwa  na  kilichokuwa  kinaendelea  ndani  ya  chama  changu.

8.Ni  kweli  nilishiriki  kumleta  Lowassa  CHADEMA  Lakini  nilikuwa  na  misimamo  yangu  ambayo  ilitufanya  tusielewane. 

9. Baada  ya  Lowassa  kukatwa  pale  Dodoma, Gwajima  ambaye  ni  mshenga  wa  Lowassa  alinipigia  simu  kutaka  kujua  ninii  cha  kufanya.

10. Nilimpigia   Mwenyekiti    Mbowe  kumjulisha  na  tukakubaliana  kupanga  muda  wa  kuwasikiliza.

11. Kabla  ya  kuanza  kuwasikiliza, msimamo  wangu  ulikuwa  ni  kumtaka  Lowassa  kwanza  atangaze  kuhama  chama, aweke  wazi  ni  chama  gani  anaenda  na  ajisafishe  juu  ya  tuhuma  zake

12.Tangu  akatwe  jina, Lowassa  hakutangaza  kujitoa  CCM  na  wala  hakujisafisha  na  tuhuma  zake, kitu  kilichonifanya  nitofautiane  naye.

13. Niliwauliza  wanachadema  wenzangu  kuwa  Lowassa  anakuja  kama  Mtaji  au  Mzigo?

14. Swala  sio  urais  kama  watu  wanavyozusha, mimi  nilikuwa  nataka  mgombea  mwenye  uwezo  na  sifa  ambaye  ataweza  kuitoa  CCM.  Sikuwa  na  tamaa  ya  urais  kama  watu  wanavyosema 

15. Tangu  Gwajima  atupe  taarifa  za  ujio  wa  Lowassa, Swali  langu  la  Lowassa  kuwa  Mtaji  au  mzigo  halikuwahi  kujibiwa.

16. Nilitaka  kujua  ni  mtaji  gani  lowassa  atakuja  nao  na  ni  viongozi  gan  atakuja  nao.

17. Nilijibiwa  kuwa  anakuja  na  wabunge  50  wa  CCM, wenyeviti  22  wa  mikoa  na  wenyeviti  80  wa  wilaya.

18.Baada  ya  ahadi  hiyo, nilitaka  sasa  nipewe  majina  ya  hawa  watu  lakini  mpaka  tarehe  25  july  sikupewa  hayo  majina 

19. Wenzangu  waliniambia  kuwa  tarehe  27  niitishe  kikao  cha  dharura  ila  niligoma  kwa  sababu  nilikuwa  sijapewa  haya  majina 

20. Ndani  ya  kikao  hicho,  tulianza  kwa  mabishano  makali  kati  yangu  na  Mbowe, Lissu  na  Gwajima, viongozi  wenzangu  ni  shahidi  na  mungu  anajua. Msimamo  wangu  ulikuwa  ni  uleule  kujua  mchango  wa  Lowassa 

21. Kikao  kile  kikavunjika, baadae  tukaingia  kamati  kuu  lakini  bado  msimamo  wangu  ulikuwa  ni  uleule. Baadae  nikaandika  barua  ya  kujiuzulu.

22.Profesa  Safari  aliichana  ile  barua. 

23.Cha  kusikitisha  ni  kuwa  Kesho  yake  picha  zikaanza  kusambaa  mtandaoni  zikimuonyesha  na  lowassa  japo  viongozi  wangu  walizikana  zile  picha.  Kibaya  ni  kuwa  viongozi  waliuficha  ukweli 

24.  Kesho  yake  niliandika  tena  barua  rasmi  ya  kujiuzulu. 

25. Baada  ya  pale  zikaanza  propaganda  za  uongo  zikimuhusisha  hadi  mke  wangu  eti  kanizuia.

26. Naomba  watanzania  wajue  kuwa  mke  wangu  hakuwahi  kunizuia  kwa  lolote, lkn  hata  angefanya  hivyo  sio  mbaya  maana  hata  yeye  ni  mwanaharakati  mwenye  uchungu  na  nchi  hii. 

27. Mke  wangu  aliwahi  hadi  kuumia  wakati  akipigania  ukombozi  wa  nchi  hii.....Lakini  sio  mbaya, familia  yangu  imezoea  propaganda. 

28. Kikubwa  katika  harakati  ni  credibility  ambayo  lazima  uilinde  na  mimi  sitaki  jina  langu  liharibiwe  na  ni  haki  yangu.

29. Maslah  mapana  ya  taifa  ndiyo  yaliyotufikisha  hapa  na  sio  maslahi  binafsi. 

30.Lowassa  na  wapambe  wake  ni  waongo  maana  hakuna  hata  kipengele  kimoja  walichokitekeleza.

31. Tulitaka  hao  wabunge  50  waje  kwanza  kabla  ya  mchakato  wa  uteuzi  ccm

32. Napinga  kuchukua  makapi  ya  CCM  na  kuyaita  MTAJI.

33.Mtu  kama  Sumaye  ni  FISADI  na  nilikuwa  siongei  naye 

34. Sumaye  aliwahi  kusema  CCM  wakimchagua  Lowassa  atahama  chama. Leo  Lowassa  kawaje  msafi?? 

35. Tulitaka  Mtaji  toka  kwa  Lowassa  na  sio  MAKAPI 

36. Wenyeviti  walioletwa  na  Lowassa  ni  MIZIGO  na  namjua  vizuri. Akithubutu  kunijibu  ntamwaga  UOZO  wake  wote 

37.Nani  asiyejua  Guninita  pia  ni  mzigo??

38:  Nawataka  viongozi  wangu  wanijibu  ni  mtaji  upi  walioupata  toka  kwa  Lowassa.

39. Mimi  ni  Padri  Mstaafu, sipendi  siasa  za  uongo. 

39. Ukisema  unataka  kuiondoa  CCM  ni  lazima  ujikumbushe  misingi  ya  CHADEMA  ambayo  ilikuwa  ni  uadilifu. Leo  chadema  hii  ina  Uadilifu  gani?? 

40.  Namshangaa  sana  Lowassa  eti  kusimama  mbele  ya  watu  akijinasibu  kuwa  ni  msafi.....kwamba  mwenye  ushahidi  aende  Mahakamani. Ni  dhambi  kupotosha  watu.

41. CCM    hawana  ujasiri, ni  waoga  na  ndiyo  maana  wamewalea  watu  kama  akina  Lowassa 

42. Ukitoa  kinyesi  chooni  na  kukipeleka  Chumbani  maana  yake  hata  chumba  chako  ni  CHOO  na  kitakuwa  kinanuka  zaidi  kuliko  choo  cha  kawaida 

43.Mimi  nilikuwepo  wakati  sakata  la  Richmond  likijadiliwa.Mimi  nina  ugomvi  wa  muda  mrefu  na  Lowassa.

44.  Mwaka  2010  mimi  nilimtaka  Lowassa  atangaze  Richmond  ni  ya  nani.

45. Leo  tena  namtaka  Lowassa   Lowassa  atoke  hadharani  atangaze  Richmond  ni  ya  nani.  Unaposema  ni  ya  mkubwa, atuambie  mkubwa  gani

46. Ukitaka  kuijua  Richmond  rejea  Ripoti  ya  Mwakyembe. Nampongeza  Mwakyembe  na  Sitta  kujitokeza  hadharan  kuusema  ukweli.

47. Siku  moja  kabla  ya  ripoti  kusomwa, nililetewa  Rushwa  ya  milioni  500  ili  tukaupindishe  ukweli  bungeni  lakini  nilikataa 

48. Ripoti  ya  mwakyembe  iliamua   mambo  mawili,  moja; Lowassa  ajipime  au  bunge  lijadili  na  lichukue  hatua.  Lowassa  kuona  hivyo  akaamua  kukimbilia  kujiuzulu  kukwepa  aibu  ya  kung'olewa  na  bunge 

49:  Lowassa  haaminiki, ni  muongo  na  hastahili  kuwa  Rais  wa  nchi....

50.  Lowassa  ni  FISADI  na  kama  mimi  ni  muongo  ajitokeze  hadharani  akanushe

51. Anasema  Lowassa  ataleta  maji, mbona  jimbo  lake  la  Monduli  halina  Maji???

52.  Mnasema  Lowassa  kaanzisha  shule  za  kata, iv  mjua  msingi  wa  shule  za  kata?  waandishi  rudini  shule  mkajifunze  upya.

53.Nilifanikiwa  kuijenga  Chadema  na  ikawa  tumaini  jipya  la  watanzania.....Vijana  wangu  wa  Chadema, naomba  niwe  mkweli  propaganda  imekivamia  chama.

54.  Inasikitisha  kuona  CHADEMA  inajazwa kwa mabasi  pale  jangwani .....alafu  mnawadanganya  watu  eti  ni   MAFURIKO

55.  CHADEMA  ya  kipindi  changu  ilikuwa  inakemea  Rushwa. Niambien  leo  chadema  watasema  nini  kwenye  majukwaa? 

56. Mnaomtetea  Lowassa  na  nyie  jitokezen  hadharani...mimi  nasema  kwa  sababu  nina  ushahidi  na  sio  lazima  ushahidi  huu  niupeleke  mahakamani.

57. Wenye  uwezo  wa  kumpeleka  Lowassa  Mahakamani  ni  Serikali, na  mwakyembe  alisema  juzi  kuwa  kesi  ya  jinai  haina  kikomo, mtu  anaweza  kushitakiwa  muda  wowote 

58. Sitaki  kuingila  swala  la  Babu  Seya, lakini  waliolawitiwa  ni  watoto  waliokuwa  chini  ya  umri. kwa  nini  haki  yao  ipotee?

59.  Rais  hana  mamlaka  ya  kumtoa  Babu  Seya. Lowassa  asiwadanganye.

60.  Kuhusu  swala  la  Masheikh, Sumaye  ndiye  aliyeamuru  mapolisi  wavamie  misikiti  wakiwa  na  mbwa......Watanzania  msikubali  kudanganywa. hizo  ni  propaganda  za  wasaka  urais 

61. Masikubali  Rais  Muongo  na  mimi  naapa  ntapiga  kelele  kila  kona  kumpinga  Lowassa.

62.Lowassa  alipokuwa  waziri  mkuu, matatizo  yanayotokea  leo  hayakuwepo?  mapigano  ya  wakulima  na  wafugaji  hayakuwepo?

63.  Lowassa  akiwa  waziri  mkuu  alisababisha  migogoro  mizito  sana  kati  ya  monduli  na  karatu.  Rais  wa  aina  hii  wa  nini?

64.  Naomba  nisiongee  mengi  kwa  sababu  ntakosa  ya  kusema  siku  nyingine.....Nawataka  Lowassa  na  Sumaye  wajitokeze  kunijibu.

65. Siku  nyingine  ntakuja  kuongelea  kuhusu  hisa  za  Lowassa  kwenye  makampuni 

66.  Nahitimisha  kwa  kusema  kuwa  Nimestaafu  siasa  na  sina  chama  lakini  nina  nchi, hivyo  ntaendelea  kuwatumikia  watanzania  kwa  jinsi  mungu  alivyonipa  vipawa 


67.  Narudia  tena, Sina  chama  na  sitajiunga  na  chama  chochote. 

Waandishi  wanauliza  Maswali: 
Mwandishi:  Umesema  hujiungi  na  chama  chochote, utawasaidiaje  watanzania?  Rais  gani  unamuunga  mkono?

Mwandishi  Guardian:  Ulisema  Lowassa  atakuwa  assert  kama  atakuja  na  wabunge  na  hao  wenyeviti.  Je  angekuja  kama  assert  ungeyasema  haya  yote?

Mwandishi  binafsi:  Umesema  waliohamia  Chadema  ni  makapi.  Mwaka  1995  Uliihama  CCM,   ukahamia  chadema. Je  na  wewe  ni  KAPI?

Mwandishi-Azam:  Umetangaza  kustaafu  siasa, lakini  bado  unakadi  ya  CCM  na  CHADEMA?  Je  utazirudisha?

Mwandishi  Blog:  Inaonekana  baada  ya  chedema  kukutosa  ndo  maana  unamshambulia  Lowassa, je  ni  kweli?

Majibu:
1. Kadi  ni  mali  zangu  na  siwezi  kuzirudisha. Ya  chadema  nimeilipia  miaka  20,ya  CCM  bado  haijaisha  muda  wake.

2. Kuhusu  urais, mimi  sijagombea  urais  na  sikuchukua  fomu.  sasa  kwa  nini  nikasirike  kisa  wamempa  Lowassa?
Sina  ugomvi  na  Mbowe  na  nakumbuka  alinisaidia  nyumba

3.  Mimi  sio  KAPI....Ili  kuujua  ukweli  unahitaji  kutumia  kigezo. KAPI  ni  yule  aliyekataliwa  na  chama  flani, mimi  sikuwahi  kukataliwa.  Sikuwa  na  uchafu  wowote  wakati  naingia  CCM.

4.  Lowassa  ni  mzigo  tu  hata  kama  angetuletea  hao  watu  wake.....Lowassa  ana  makandokando  mengi. Angetuletea  hao  watu  ndo  tungeamua  tumpokee  au  tusimpokee

5.Mimi  sina  chama  na  sitampigia  kampeni  mtu  yeyote. Mimi  nimefanya  utafiti  kwa Lowassa  pekee, kwamba  taifa  litapata  madhara  gan  Lowassa  akiwa  Rais.....Lowassa  ni  Fisadi.
  
 -Kazi  yangu  leo  ilikuwa  ni  kuwaambia  watanzania  waachanane  na  ushabiki.Ukihamishia  CHOO  chumbani, manake  harufu  itahamia  huko.
 -Chadema  ya  leo  kwa  sasa  imetekwa  na  Lowassa  na  hawawezi  tena  kuongelea  Ufisadi 

Maswali  ya  nyongeza

1.Umesema  waliohamia  chadema  kwa  sasa  ni  sawa  na  mfano  wa  Choo. Je, wewe  ulipohama  hukuwa  choo?  kwa  nini  wewe  uliweza  kukibadili  chama  halafu  akina  Lowassa  washindwe?

Jibu:  Wakati  mimi  nahama  sikuwa  mchafu  kama  hawa  akina  Lowassa  na  Sumaye.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

UFISADI WA ESCROW UMEPEWA BARAKA ZOTE NA IKULU YA NCHI YA TANGANYIKA


Mgombea Urais kupitia Chadema, Edward Lowassa akizungumza katika uzinduzi wa mkutano wa kampeni za Rais, wabunge na madiwani kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Jumapili, Agosti 30, 2015
Sumaye awa mbogo, amvaa Kikwete
Ajibu mapigo, aorodhesha ufisadi Serikali ya Kikwete
Umo Escrow…EPA…Mabehewa mabovu ya Mwakyembe
Hotuba kiduchu ya Lowassa yazua maswali
Mgombea Urais kupitia Chadema, Edward Lowassa akizungumza katika uzinduzi wa mkutano wa kampeni za Rais, wabunge na madiwani kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa). ‘Kama unaishi nyumba ya vioo basi ni vema usiwarushie wenzako mawe’ usemi huu ulidhihirika jana baada ya baadhi ya viongozi waandamizi wa upinzani wakiongozwa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye kujibu tuhuma za ufisadi huku akiorodhesha ulaji rushwa uliokithiri ndani ya serikali ya Rais Jakaya Kikwete. Akizungumza mbele ya umati wa kihistoria katika Viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika, Sumaye alisema Edward Lowassa, alijiuzulu February 2008, ili kunusuru serikali ya Kikwete, isianguke kutokana na kashfa ya kufua umeme ya Richmond. Hata hivyo, kitendo cha mgombe urais wa Ukawa kutumia chini ya robo saa kuhutubia mkutano huo jana, kiliacha maswali mengi hasa kwa wapinzani wake wa kisiasa ambao wamekuwa wakihoji afya yake katika kuhimili mikiki ya kampeni siku sitini nchi nzima. Huku akishangaliwa kwa nguvu Sumaye aliyekuwa waziri mkuu kwa miaka kumi katika serikali ya awamu ya tatu, alisema tangu Lowassa ajiuzulu, kumekuwepo na kashfa kubwa za ulaji rushwa ndani ya serikali ya rais Kikwete zikiwemo ununuzi wa mabehewa mabovu uliofanywa na Yusufu Manji kwa kushirikiana na waziri wa zamani wa uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe, iliyogharimu zaidi ya Sh. bilioni 200. Sumaye alitaja kashfa kubwa kuliko zote katika masuala ya umeme ya Escrow iliyobarikiwa na Ikulu na kusababisha mfanyabiashara kutoka Afrika Kusini, Harbinder Singh Sethi, kuchota kiasi cha shilingi bilioni 305 toka katika akaunti maalumu ya benki kuu ya Tanganyika ((Tanzania,)) Zanzibar mwaka 2013.
Sumaye aliorodhesha kashfa zingine chini ya utawala wa Rais Kikwete ikiwemo utoroshaji wa twiga katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, Wizi wa shilingi bilioni 133 toka katika akaunti ya madeni ya nje maarufu kama EPA, huku akisisitiza kwamba utawala wa Kikwete ulijaa ufisadi kupindukia lakini viongozi wa CCM wanamtuhumu Lowassa kama kinara wa rushwa. Alisema viongozi wa CCM wamekuwa wakimshambulia Lowassa kwamba ni fisadi lakini tangu ametoka madarakani mwaka 2008, ameendelea kuwapo nchini na hajachukuliwa hatua na kwamba kama angekuwa fisadi kweli wasingemuacha. “Tangu lini waziri mkuu anakuwa mkubwa wa serikali, waziri mkuu anabebeshwa mzigo ili kumuokoa Rais wake,”alisema. Alisema Lowassa aliamua kuwajibika ili kuinusuru serikali isiumbuke,” alisema Sumaye na kusisitiza kwamba Lowassa alijitishwa mzigo ili kumuokoa Rais Kikwete na serikali yake. Sumaye alikumbusha kwamba Mwalimu Nyerere alilia katika kikao kimoja cha Halmashauri Kuu akimsifia Kawawa kwamba anabeba mzigo asiostahili kwa ajili yake (Nyerere). “Hivi twiga waliopandishwa kwenye ndege, Lowassa alikuwapo madarakani mbona alikuwa ameondoka toka 2008, EPA waliochota mabilioni Lowassa alikuwapo?” “Hivi madawa ya kulevya yanapopita uwanja wa ndege hadi yanakamatwa Afrika Kusini, Lowassa alikuwapo?, Vichwa vya treni vilivyonunuliwa Lowassa alikuwapo?, Feri mbovu zilizonunuliwa na kuonekana mpya Lowassa alikuwapo? wamelamba Escrow Lowassa alikuwapo?” Alihoji Sumaye Sumaye aliweka bayana kwamba katika ufisadi wa Escrow, waliokula hela za James Rugemalira walitajwa lakini wale waliochota sehemu kubwa ya fedha hizo toka benki ya Stanbic kwa kutumia sandarusi mpaka leo hawatajwi.
Alisema serikali ni dhaifu na Katibu Mkuu wa CCM alishalithibitisha hilo kwani alishanukuliwa akisema kuna mawaziri mizigo na kwa kiongozi kama huyo akisema hayo inatakiwa chama chake kiondoke madarakani: “Wewe hiyo ni serikali yako unakuja kushitaki kwa wananchi ni ajabu,” alihoji Sumaye. “Wanamsema Lowassa kuhusu ugonjwa, kwani Magufuli ni mzima na kama wao wanajiona ni wazima wanakwendaga kufanya nini Ulaya,” alihoji Sumaye. “Rais Mkapa alipougua si alikwenda nje kufanyiwa operesheni kubwa, Rais Kikwete naye si alikwenda nje kufanyiwa upasuaji wa tezi dume,” alisema Sumaye. Alisema urais siyo kazi ya kwenda kubeba zege Ikulu hivyo wananchi wana kila sababu ya kumchagua Lowassa, ili kufanya mabadiliko ya nchi .MASHA
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, alisema yeye na wenzake ambao wamejitoa CCM na kujiunga na Chadema, siyo kwamba ni makapi bali ni haki yao ya kidemokrasia na hiari yao: “Kwa tuliojiunga Chadema sisi siyo makapi, tuna akili zetu sawa tumetumia hiari yetu,” alisema Masha. Masha alisema wananchi wasihofu kwa yaliyotokea, yeye pamoja na vijana 19 kuwekwa ndani na Jeshi la Polisi kwa hivyo ni vitisho vya kuwatisha wananchi, lakini mabadiliko yapo pale pale.MBOWE
Akizindua ilani ya Chadema, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe jana alisema kuwa imejaa maslahi mapana ya taifa, na kusisitiza kwamba lazima CCM iondolewe madarakani mwaka huu.“Tunawashukru walioamua kupata ujasiri kuondoka CCM na kujiunga na Ukawa wakiongozwa na Lowassa na Sumaye, kwani kuja kwenu Ukawa kumeleta chachu katika vyama vinavyounda umoja huu,” alisema Mbowe. Alisema wananchi wameitwa malofa lakini, waliowaita hivyo walisahau kwamba wao watakuwa chanzo cha ulofa huo kwa vile wametawala kwa miongo zaidi ya mitano. Mbowe alitaka rais mstaafu Benjamini Mkapa, asamehewe kutokana na kauli aliyoitoa hivi karibuni pale alipowaita Watanganyika na Wazanzibari walio vyama vya upinzani ni ‘wapumbavu…malofa’.Mwenyekiti huyo wa Chadema alisema Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba alinukuliwa akisema mgombea urais wa CCM hana urafiki na matajiri.
Alisema Jaji Warioba, lazima atambue kuwa umaskini siyo sifa na wala Ukawa hautamani umaskini, Watanganyika na Wazanzibari wote wanatamani kuwa matajiri, wakati wa kutamani umaskini uwe sifa ya uongozi umepitwa na wakati. “Tumeridhika na Lowassa anaweza kuwa chachu ya mabadiliko na tuwaahidi tutafanya kampeni za kistaarabu,” alisema Mbowe. Mbatia
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema hivi sasa wakuu wa wilaya na vyombo vya usalama wanakutana Ngurundoto mkoani Arusha, kupanga uhalifu na hujuma na kumtaka Lowassa atembee na tenzi za rohoni. “Mhe Lowassa, Maalim Seif na Duni, umma wa watanganyika na wazanzibari utawalinda…Rais Kikwete asilete uchochezi ndani ya taifa hili, Tanganyika ((Tanzania)) Zanzibar ni mali ya wote siyo ya kikundi cha watu wachache,” alisema Mbatia. Alisema wameitwa malofa na wapumbavu lakini heri ya kijana maskini mwenye hekima kuliko mzee mfalme mpambavu.LOWASSA
Alisema akiingia madarakani kipaumbele chake cha kwanza hadi cha tatu kitakula elimu kwa kutoa elimu bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu. Alisema jambo hilo linawezekana na hakuna mtu kwenye utawala wake atakayesema haiwezekani. “Nanukuu maneno ya aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza, Tony Blair aliulizwa atafanya nini akiingia madarakani na kujibu kipaumbele changu cha kwanza kitakuwa elimu, cha pili elimu cha tatu elimu na jambo hilo liliwezekana, kwa nini sisi tushindwe,” alisema Lowassa.
Kuhusu afya alisema ataiboresha kwa kujenga hospitali na Watanganyika na Wazanzibari watatibiwa nchini kwa sababu wengi hawana uwezo wa kwenda nje. “Tunapoteza fedha nyingi kuwapeleka watu nje lakini wengi hawana uwezo wanaoenda huko ni watu wakubwa,” alisema. Akizungumzia mawasiliano alisema serikali yake itajenga reli ya kati kwa kiwango cha kisasa kutoka Dar es Salaam, Mwanza mpaka Kigoma na kufufua Shirika la Ndege kwa kununua ndege mpya na kulifanya lijiendeshe kibiashara. “Hatuna sababu ya kushindwa na nchi ndogo kama Rwanda, Malawi na Kenya ambazo wana ndege nzuri na mashirika yanayotambulika,” alisema Lowassa.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

HIVI NDIO JESHI LA POLISI / ASKARI LILIVYO ANZISHWA KWALI LITAKUWA NA HURUMA NA RAI WAKE....?


mwaka 1858 ndipo lilipo undwa jeshi la polisi au askari na liliundwa kwajili tu ya kuwakamata watumwa wanajaribu kukimbia au walio kata kufanya kazi ya utumwa katika mashamba ya miwa,pamba,kulima, n.k. kisha baada ya miaka na kakaka kupita na utumwa ukawa sio halal tena ndio jeshi hilo hilo likaundwa kuwa ati lilinde rai na mali zake je kweli jeshi hilo litakuwa na huruma..??

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.