Saturday, July 2, 2016

MAALIM SEIF AGOMA KUKAA PAMOJA NA BALOZI SEFU.HATA INGELIKUWA MIMI PIA NINGELIGOMA KUKA NAE KWA JINSI YA VITIMBI ANAVYO WAFANYIA WAZANZIBARI KATIKA NCHI YAO YA ZANZIBAR

 
MAALIM SEIF AGOMA KUKAA PAMOJA NA BALOZI SEFU.
Katika muendelezo wa kuigomea serikali haramu na viongozi wake wote, Maalim Seif jana aligoma kukaa sehem moja na balozi Sefu Ali Iddi wakiwa safarini.

Wawili hao walikutana ndani ya boti wote wakielekea Dar es salaam ambapo Maalim Seif alienda kwa shughuli zake za kawaida na balozi Sefu alienda kupanda ndege kwa ajili ya safari yake ya Quba ambako anaenda kimatibabu.
Taarifa zinaeleza kua awali wawili hao walipata sifa tofauti kabla ya Maalim kuingia ndani ya boti na kuamua kugoma kukaa pamoja na balozi Sefu.
Maalim wakati yuko bandarini anataka kuingia botini alipata wakati mgumu kupokea mikono ya wananchi ambao walikua na hamu na shauku ya kutaka kusalimiana nae huku balozi Sefu akishindwa kupewa hata mkono mmoja wa pole jambo ambalo lilimuacha katika mfadhaiko mkubwa.
Maalim alipoingia botini aliendelea kuthibitisha kua hayuko pamoja na madhalim kwani alikataa kata kata kukaa First Class sehemu ambayo alikueko balozi Sefu pamoja na captain wa boti hiyo kumtaka na kumuomba Maalim akae huko.
Hali hii ilipelekea balozi Sefu kujikuta akifurukuta na kushindwa kujua nini afanye na wapi akae na hatimae kujikuta akikaa peke yake First Class huku Maalim Seif akikaa na wananchi wa kawaida katika sehemu ya abiria wa kawaida.
Pamoja na hayo taarifa za ndani zinaeleza kua hali ya afya ya balozi Sefu kwa sasa sio mzuri na inataka moyo kuweza kukaa nae pamoja kwa kile kinachodaiwa kua mwili wake unatoka maji yenye harufu mbaya yatokanayo na mabalanga alionayo mwilini.
Pia inasemekana kua Balozi anasumbuliwa na maradhi ya presha ya macho(eye hypertension) maradhi ambayo ni sugu sana duniani.
# Mungu ibariki Zanzibar#

Friday, July 1, 2016

VIDEO-TUNA ASHA BAKARI MPYA ZANZIBAR MUNIRA MUSTAFA KHATIB USIJALI AGIZO LAKO MSANGI ASHAANZA KULITEKELEZA

IMG-20160701-WA0057

JESHI LA DIKTETA UCHWARA LIMESHIKA KASI KUWATESA NA KUWAFUNGA WATU JELA BILA YA KUSAHAU WANAO PINGWA RISASI



DIKTETA UCHWARA MSAIDIZI ZANZIBAR!
Wenyeviti na makatibu wote wa CUF wa mkoa wa Kusini Pemba toka majuzi waliletewa barua za kwenda polisi Chake chake na Leo ni siku ya 5 wameshikiliwa kituoni hapo bila dhamana wala kupelekwa mahakamani. Ni pamoja na Mhe. Hija Hassan.Hija (mwakilishi jimbo la Kiwani), Mhe. SEIF mwakilishi wa jimbo la Mkoani na dereva wa Mhe Masoud (mbunge wa jimbo la Mtambile).
MY TAKE;
Mkuu alisema yeye anapeleka majeshi tu, mengine hayamhusu. Ni kweli sasa tunashuhudia nguvu na ubabe wa majeshi huko Zanzibar. Na hapo hatujaongelea watu wanaopigwa risasi kila kukicha, kwa bahati mbaya vyombo vyetu vya habari vimejiweka mbali na kuripoti yanayotokea Zanzibar. Pamoja na kuwa Bara tuna msiba wetu, huwenda msiba wa Zanzibar ni mkubwa zaidi. Yale aliyoyaona Tundu lissu Central Police ni ya kawaida kabisa Zanzibar, Zanzibar inajiendesha kama nchi isiyo na sheria wala katiba. Na dikteta uchwara msaidizi anafanya atakalo, hakumbuki historia. Shame on this current leadership.
Mtatiro J.

VIDEO-DIKTETA UCHWARA JE UTAKWENDA MAHAKAMANI KUSIBITISHA KUWA WEWE SIO DIKTETA UCHWARA....???

Alichokizungumza Tundu Lissu baada ya kupata dhamana

VIDEO-LEMA: HATUTAKUBALI NCHI HII IENDESHWE KIFALME, HATA KWA GHARAMA ZA DAMU ...

LEMA: HATUTAKUBALI NCHI HII IENDESHWE KIFALME, HATA KWA GHARAMA ZA DAMU YETU

VIDEO-DIKTETA UCHWARA AENDELEA KUWASWEKA JELA VIONGOZI WA UPINZANI NA UNGUJA NA PEMBA WANAWAFUNGA JELA RAI WASIO NA HATIA YOYOTE

Tundu Lissu ahojiwa na polisi kwa dakika 180

HUU NI UJUMBE KWA DIKTETA UCHWARA HII NCHI ILIKUWEPO,IPO NA ITAKUWEPO NA UTAIWACHA HAPA HAPA