Tuesday, May 13, 2014

WAASIA WA MAREHEMU SHEIKH ILUNGA HASSAN KAPUNGU KWA WAZANZIBARI WOTE


MAREHEMU SHEIKH ILLUNGA WAKATI WA UHAI WAKE AKITOWA DAWAA M.MUNGU AMSAMEHE MATHAMBI YAKE NA AMPE PEPO IN SHAA ALLAH

Asalamu alaikhum ndugu zangu Wazanzibari wa Ndani na Nje ya Visiwa Vyetu Adhimu.
Hutuba ya Shekh KISHKI
MAKAMO wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, MaalimSeif Sharif Hamad, alikuwamiongoni mwa maelfu ya Waislamu walioshiriki faradhi kifaya ya kumzika Sheikh Ilunga Hassan Kapungu siku ya Jumaa tatu wiki hii.
Kama alivyosema Sheikh‘Kishki’ katika nasaha zake pale msikitini TIC, Magomeni Kichangani, Maalim Seif kashiriki maziko yale kama Muislamu. Alishiriki kumzika Muislamu mwenzake kama Uislamu unavyo himiza.‘Kishki’ akatumia fursa hiyo kuwazindua viongozi wengine wa kiserikali na wanasiasa kwamba,kuwa kwao madarakani hakuwaondolei wajibu wao wa kidini. Akawataka,wasione fahari tu kujitokeza kushiriki maziko yawana muziki Bongo, ‘Bongo movies’, na mambo kama hayo, lakini vyema zaidi waone fahari kujumuika na Waislamu wenzao katika maziko kama yale ya Sheikh Ilunga.
Katika muktadha huu,pamoja na kuchukuliwa kwamba Maalim kaja kama Muislamu, na si kama kiongozi wa kisiasa au kama Mzanzibari, lakini pengine ingekuwa vyema kutumia fursa hii kusema yale ambayo Sheikh Ilunga aliyasema mwaka 2011 kama nasaha zake kwa Maalim Seif na viongozi wenzake wa nchi ya Zanzibar na Wazanzibari wote kwa ujumla. Katika muhadhara wake mmoja kule Pemba nchini Zanzibar, Sheikh Ilunga alisema kuwa kabari ya mfumo kristo imewakaba barabara Wazanzibari,hawafurukuti. Hata hivyo,pamoja na hali hiyo,Sheikh Ilunga aliwataka Wazanzibari kuto kukata tamaa, bali watumie fursa zilizopo kurejesha hadhi yao.
Fursa ya kwanza akasema ni wao kuwa Waislamu. Akawataka watizame kwanza hadhi ya Uislamu, ndio ifuatie nchi yao na dola yao. Alisema kuwa,Wazanzibari ni lazima watumie maridhiano ya kisiasa yaliyopo ili kuleta maridhiano ya Kiislamu. Kwamba amani iliyopo itumike kuimarisha udugu wa Kiislamu, watu wajitambue kwamba wao ni Waislamu kwanza kabla ya jambo jingine lolote. Ni Waislamu kabla ya CUF, Ni Waislamu kabla ya CCM na ni Waislamu kabla ya kuwepo Tanganyika (Tanzania) na Muungano wake. Akasema hilo linahitaji Da’wah ya kutosha na watu warejee katika Qur’an walonena kutafakari jinsi Mwenyezi Mungu anavyo waonya juu ya kuwafanya Mayahudi na Manasara kuwa marafiki na wasiri wao.
Akawakumbusha pia kuwa Qur’an imesema wazi kwamba chuki iliyofichwa na Manasara ndani ya vifua vyao ni kubwa mno kuliko wanayo idhihirisha na kwamba hawataridhia mpaka wawaritadishe Waislamu, japo wabakie Waislamu wa majina lakini makafiri kwa kauli, vitendo na maadili. Kufuatia kauli ya Bwana William Lukuvi Kanisani na Bungeni, bila shaka maneno haya ya Shekh Ilunga yanathibitika zaidi. Kwamba ipo chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu. Na hiyo namna pekee ya kukabiliana nayo, ni kujitizama kama Waislamu, kama Lukuvi na waliokuwa Kanisani pamoja naye walivyo jitizama kama Wakristo kutoa hofu yao dhidi ya Waislamu walio wengi nchini  Zanzibar.
Baada ya neema ya Uislamu, na fursa ya kuwepo maridhiano na serikali ya umoja wa kitaifa ( G.N.U), shekh Ilunga alitaja fursa nyingine kuwa ni mabadiliko ya katiba yanayokuja. Akasema, ni lazima fursa hiyo itumike vizuri kuhakikisha kuwa kichaka kinachoficha mfumo kristo kinapigwa moto. Na hiyo itafanyika kwa kuwa na muungano wahaki ambapo pande mbili za Muungano, Tanganyika na Zanzibar zitakuwa na haki sawa, sio huu wa serikali ya Tanganyika kujivika joho la Serikali ya (Tanzania.)
Shekh Ilunga alimalizia kwakuwapa changamoto viongozi wa serikali ya nchi ya Zanzibar, Shein,na Makamo wake wawili, Maalim Seif Sharif Hamad na ((Balozi Seif Ali Iddi Balozi ndogo wa nchi ya Tanganyika)) kwamba wao wametoka katika migongo ya wazee wa Kiislamu na hivyo, hawawezi kukwepa jukumu la kuona hadhi ya Uislamu inarudi kama ilivyokuwa wakati wakilelewa na wazee wao. Kabla ya kutoa nasaha hizo, Sheikh Ilunga alisema kuwa mfumo wa Muungano uliopo umekuwa kama
kichaka unakojificha mfumo kristo kuiburura nchi ya  Zanzibar katika idhilali kwa kuipora nguvu zake za kisiasa na kiuchumi na kubwa zaidi kuhujumu Uislamu na Waislamu.
Aliyabainisha hayo katika kongamano lililofanyika katika eneo la Markazi Tabligh, Ole Kianga, Pemba nchini Zanzibar Jumapili Oktoba 2011. Kongamano hilo lililohudhuriwa na maelfu ya Waislamu kutoka sehemu mbalimbali za Pemba, lilijadili hatari ya mfumo kristo kwa nchi ya Zanzibar na Tanganyika (Tanzania) kwa ujumla. Awali Sheikh Ilunga Hassan Kapungu alisema kuwa, inaweza kuwa jambo lisilo eleweka ukizungumzia mfumo kristo alisema japo kwa vile takriban viongozi wote waserikali na taasisi muhimu nchini  Zanzibar ni Waislamu, Wapemba na Waunguja. Hata hivyo akasema kuwa,ile kuwa inaitwa ni serikali ya Zanzibar haina maana kuwa Serikali hiyo ni serikali inayo ongoza dola kwani mamlaka yote ya kisiasa yapo katika serikali ya muungano.
Akifafanua alisema kuwa yapo mambo ambayo Wazanzibari wangetaka kufanya au kuamua kwa masilahi ya Nchi yao ya Zanzibar. Lakini hawawezi kuyafanya kwa vile Muungano umewapora nguvu za kisiasa. Na kwamba, yale mamlaka ya kidola na kisiasa ya nchi ya Zanzibar yalizikwa nakusomewa talakini siku ASP ilipoungana na TANU ambapo CCM ilishika hatamu na maamuzi yote muhimu kuwa yanafanyika Dodoma. Akitoa mfano alitaja uchaguzi mkuu ambapo jina linalopitishwa kugombea Urais laweza kuwa lile ambalo halikupata ridhaa ya Wazanzibari. Na hata kuondoka madarakani, kiongozi anaweza kuondolewa bila ya Wazanzibari wenyewe waliompigia kura au vyombo vyao vya uwakilishi kama Baraza la Wawakilishi kuhusishwa. Akataja mfano wa Mzee Aboud Jumbe aliye kwenda mkutanoni Dodoma akiwa Rais akarudi Urais akiwa ameuacha Dodoma. Sheikh Ilunga kwa kutoa mfano huo alisema kuwa Alhaj Aboud Jumbe, yalimfika kwa sababu alihoji Muungano nakuhoji kwenyewe si kutaka kuuvunja, bali kutaka uwe wa haki.
“Yalimfika.” “Kwa nini..?”
“Kwa nini imefanywa kuwa mwiko kuhoji Muungano..?” Alisema na kuhoji Shekh Ilunga. Kabla ya kutoa jawabu, Sheikh Ilunga alirejea pia hali ilivyokuwa wakati wa Mzee Abeid Aman Karume ambaye alishaonesha kuwa koti la Muungano linambana, lakini mauti yakamfika muda mfupi kabla ya kutimiza nia yake ya kulivua. Aligusia pia yaliyo mfika Maalim Seif Sharif Hamad, hata hivyo hakutaka kufafanua bali akawataka Wazanzibari wenyewe wamuulize Maalim nini kilimkuta na kwa nini...? Katika kukamilisha hoja yake akasema kuwa Muungano umefanywa jambo nyeti na mwiko kujadiliwa kwa sababu ndio uchochoro na kichaka mfumo kristo unakopitia kuiua nchi ya Zanzibar na kuuwa Uislamu.
Katika hali hiyo akasema kuwa, Wazanzibari watakuwa wakiwalaumu na pengine hata kuwachukia bure viongozi wao, lakini nao wanashindwa kufanya yanayotakiwa na Wazanzibari kwa sababu inabidi kwanza watizame Dodoma inasema nini. Kwa maana kuwa jambo kama halijapata ridhaa yamfumo Kristo, haliwezi kuwa kama ambavyo haikuweza nchi ya Zanzibar kujiunga na OIC na hivi sasa Tanganyika (Tanzania) haiwezi kujiunga na jumuiya hiyo kwa sababu Maaskofu hawataki, mfumo kristo hautaki. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernad Membe aliliambia rasmi Bunge kuwa serikali haioni tatizo Tanganyika (Tanzania) kujiunga na OIC, lakini ghafla msimamo ukabadilika baada ya kuitwa na Kardinali Pengo.
JE VIONGOZI WA CCM NCHINI ZANZIBAR DINI YENU SASA NI CCM NA SIO UISLAMU TENA....????

2 comments:

  1. Asalaam Alaykum, nimependa na kala zako ila karibu kufikiria nini Allah anataka siasa za Nyuma ndio zinazoturudisha wengi, Hasa wale ambao nyerere hivi au nyerere angekuwa hai ,NDIO hayupo ujinga Wa nyerere angekuwepo au babu zetu walivyokuwepo wametuhadithia hiki na lile Ni Ujinga Tutizame nini Mitume walifanya Tusikubali Zulma Ila siasa tu zibadilishwe muelekeo Mambo tunaongea kama Hao Mababu ndio Waliumba Zanzibar? Mpaka tunachukiana bure Tanganyika na Zanzibar Kumbuka TAnganyika pia kuna Waislamu pia. Muda Mwengine unaponda kama sie Bara wote makafiri, tupeane ushauri Mzuri maalim Seif na wengine tuwape ushirikiano zanzibar irudi kwenye Hali nzuri siasa za zamani alivyokuwa sijui Mzee gani au mzee gani alituambia hivi ndio Inaturudisha nyuma Vijana walichosoma cha maana Vinapotea wakirudi sababu Ya wao wakirudi tu ZNZ Au bara Wanatengeneza siasa za kale basi chuki tu Na Nchi za Nje ndio wanapenda hivi, na walio madarakani wanapenda iwe hivi sie tunaona hawapendi sababu ukweli wa zamani unaongelewa , wao basi wanapenda wanajuwa mvutano utaendelea Wao wale tushachoka hizi siasa za zamani,Dar es salaam neno Waswahili limeharibiwa ni muda kutenda Ya sasa Tu watoe Wezi kote kwa ustaarabu wa dini hata mtu awe Comoro Au burundi, Kama tunaipenda ZNZ sababu Ya Dini basi na Wenye dini yetu hata wawe wapi tuwape de Mungu ndio kaumba Dunia Kote kwetu. Sorry keypad kidogo inaharibu maandishi ila natumai tumeelewana.

    ReplyDelete
  2. waleikum salamu nimekuelewa na in shaa allah nitayafanyia kazi kwa sote mpaka tufanikiwe.

    ReplyDelete