Saturday, September 6, 2014

MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA HAKUNA GAIDI NCHINI KWETU ZANZIBAR KUNA WATAKA NCHI YAO YA ZANZIBAR. MAGAIDI,WAUWAJI,WALAWITI,MADHALIM,WAVUNJA SHERIA NI NYINYI TANGANYIKA



MMOJA wa watuhumiwa atii wa ugaidi lakini sote tunajuwa kuwa sio magaidi ni wakombozi wa nchi ya Zanzibar huru yenye mamlaka kamili ila wanapakwa mavi kuwa ni magaidi katika kesi inayomkabili Kiongozi wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI) nchi Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed (43), amevunja ukimya mahakamani baada ya kuonyesha suruali ilivyorowa kwenye makalio akisema ni madhara ya kulawitiwa na kuingizwa miti na polisi hao wa MKoloni Mweusi Tanganyika nchini huko Tanganyika.
Mshtakiwa huyo, Salum Ally Salum, aliamua kufanya hivyo jana ili kuithibitishia mahakama kile walichodai ni unyama waliotendewa na polisi hao Makaburu Weusi wa nchi hiyo ya Tanganyika wakati wakihojiwa.“Mheshimiwa hakimu, angalia (anageuka na kuinua suruali katika eneo la makalio), haya ndiyo madhara niliyopata kwa kuingiliwa nyuma na kuingizwa jiti,” alisema Mzanzibari akiwa katika Mahakama hiyo ya Mkoloni Mweusi Tanganyika.
Baada ya mshtakiwa huyo kuzungumza, Hakimu Hellen Riwa alimshauri kutoa taarifa kwa uongozi wa Magereza ili aweze kupata matibabu ya haraka kwani akiendelea kukaa hivyo anaweza kupata madhara makubwa.Kwa upande wake, Sheikh Farid, alimuomba Rais wa nchi ya Tanganyika JM Kikwete kuunda tume huru ya kuchunguza vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa.
Sheikh Farid aliieleza mahakama kuwa Tanganyika ((a.k.a.Tanzania)) hakuna ugaidi, na kwamba balaa hilo lisiombwe kutokea hapa nchini.Alisema kuwa yanayowakuta hivi sasa ni kutokana na kudai mamlaka ya nchi yao ya Zanzibar kwani kuna mgogoro mkubwa unaoendelea.
Sheikh Farid alisema hayo jana katika Mahakama ya Mkoloni Mweusi Tanganyika Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Hellen Riwa, wakati kesi yake na wenzake 19 ilipokuwa ikitajwa na kuunganishwa na washtakiwa wengine wawili, Sheikh Mselem Ali Mselem na Abdallah Said Ali.
“Mheshimiwa Hakimu, naomba mahakama ikunjue kifua itusikilize tunayotaka kusema, tunataka ufafanuzi kutoka kwako, kwanza nathibitisha kwamba madhila, unyanyasaji, ukatili tulifanyiwa na polisi wakati wa mahojiano.“Tatizo letu mheshimiwa ni matibabu, gerezani hakuna matibabu, kuna wenzetu tangu tulipoingia humo miezi miwili sasa, wanalala hospitali, dawa hakuna, inafikia hatua tunaagiza kutoka nje.
“Mheshimiwa hali ni mbaya, watu wanatokwa hadi na usaha, yote hayo ni kwa sababu ya ukatili waliotufanyia polisi, tutakapokwenda katika Mahakama Kuu ya Tanganyika iliyovaa koti la Tanzania tutazungumza mengi.
“Tunahitaji iundwe Tume Huru ya Uchunguzi, tunaomba Rais Kikwete aunde tume yenye haki, tume ndiyo itatoa ukweli, hiki ndicho kilio chetu.
“Niliuliza hapa mahakamani Zanzibar ni nchi.....???? Yule rais ni rais wa timu ya mpira.......???” alihoji Sheikh Farid.
Aliendelea kusema sheria ya ugaidi ni sheria ya dhuluma ambayo ipo kwa ajili ya kuwanyonga Waislamu na kwamba kuna mgogoro mkubwa wa Utanganyika.
“Tanzania hakuna ugaidi hapa, tusiombe balaa hilo, sisi kosa letu ni kudai mamlaka ya nchi yetu,” alisema Sheikh Farid.Hakimu Riwa akijibu hoja ya Sheikh Farid, alisema mahakama imewaruhusu kuandika barua kuomba kuundwa kwa tume huru kisha mahakama itajua pa kuipeleka.
Kabla ya kuwasilisha hoja hizo za malalamiko, washtakiwa walibadilishiwa mashtaka na kusomewa upya mashtaka manne na mawakili wa Serikali, Peter Njike na George Barasa.Inadaiwa katika shtaka la kwanza, washtakiwa wote kwa pamoja kati ya Januari 2013 na Juni 2014 maaeneo mbalimbali ndani ya Jamhuri ya Muungano feki ya a.k.a. Tanzania,Tanzania Bara,TZ,Bongo Land walikua njama na kuingiza watu nchini kushiriki vitendo atii vya kigaidi.
Katika shtaka la pili, washtakiwa wote wanadaiwa kuwaingiza watu nchini kushiriki vitendo vya ugaidi huku wakijua ni kosa.“Mheshimiwa, shtaka la tatu linamkabili mshtakiwa Farid na Mselem, mnadaiwa kati ya Januari 2013 na Juni 2014, maeneo ya Jamhuri ya Muungano feki wa Tanzania, mliwaajiri Sadick Absaloum na Farah Omary kushiriki kutenda vitendo vya kigaidi.
“Shtaka la nne linamkabili Farid, unadaiwa kuhifadhi watu waliotenda vitendo vya kigaidi, huku ukijua ni kosa. Ulimuhifadhi Sadick Absaloum na Farah Omary huku ukijua kwamba walitenda ugaidi,” alidai Balasa.Washtakiwa hawakutakiwa kujibu lolote, upelelezi wa kesi haujakamilika. Mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 17, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Jamal Swalehe, Nassoro Abdallah, Hassan Suleiman, Anthari Ahmed, Mohammed Yusuph, Abdallah Hassani, Hussein Ally, Juma Juma.Wengine ni Saidi Ally, Hamisi Salum, Saidi Amour Salum, Abubakar Mngodo, Salum Ali Salum, Salum Amour Salum, Alawi Amir, Rashid Nyange, Amir Hamis Juma, Kassim Nassoro, Said Sharifu, Sheikh Mselem Ali Mselem na Abdallah Said Ali.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment