HII NDIO BENDERA ILIYO PEPEA SIKU YA UHURU WA ZANZIBAR
NA NDIO ILIYO PEPEA KULE U.N.MJINI NEW YORK
IGAWA HISTORIA IMEPOTOSHWA NAKUSEMA KUWA NI BENDERA YA
SULTANI HUU NI UZUSHI NA MBINU YA KUTAKA KUTUTAWALA KAMA
ALIVYO FANYA GADDAFI NA WATANGANYIKA NDIVYO WALIVYO FANYA.
SIKILIZA HUTUBA YA WAZIRI MKUU WA KWANZA WA ZANZIBAR
AKIWAKILISHA ZANZIBAR NDANI YA U.N.1963 WAKATI HUO
TANGANYIKA HATA HAITAMBULIKI U.N.ZANZIBAR TAYARI
SIKILIZA HUTUBA YA WAZIRI MKUU WA KWANZA WA ZANZIBAR
AKIWAKILISHA ZANZIBAR NDANI YA U.N.1963 WAKATI HUO
TANGANYIKA HATA HAITAMBULIKI U.N.ZANZIBAR TAYARI
TAREHE 10-MWEZI 12-MWAKA 1963 ZANZIBAR ILIJULIKANA NI NCHI HURUKABISAA ssalam Alaikhum Wazanzibari mulioko nje na Wazanzibari muliko ndani ya Visiwa vyetu vya Unguja na Pemba.Ama sina budi ila kuwaomba nduguzangu wote wa kike na kiume kusimama pamoja na kuikumbuka siku ya tarehe 10.12.1963.
siku hii ndio siku azimu ya kukumbukwa milele, wakati Nchi yetu ya Zanzibar ilipata uhuru wa kujilinda wenyewe kutoka kwa British Government.Siku hii mdio siku tuliojiunga na UN na bendera ya taifa Dogola Zanzibar ikapandishwa juu ya Mlingoti kule Nchini New York.
Tukumbuke Nchi haiwezi kuwa Nchi kamili kama itatupa Historia yake. Tuna kila njia yakuadhimisha siku hii adhimu na kuwaelimisha watoto wetu wapi:
Tumetoka.
Tulipofika.
Na wapi Tunakoelekea.
Nduguzetu wa Denmark Copenhagen walifanya kumbukumbu hiyo mwaka jana 2010. Na mwaka huu maandalizi yapo njiani kuimarisha siku hii kwa kutayarisha Exhabition kubwa.
Mipango walionayo nduguzetu wa Copenhagen nikuchukua picha za Memories na matukio yote yaliopita na kuyafanyia Maonyesho.
Kila mtu mwenye Mkeka wa Chole, Mkoba wa ukili, picha za Zanzibar kabla ya Uhuru na Wakati wa Uhuru tunaomba atuletee hapa kwenye free-zanzibar people from mkoloni mweusi au awasiliane na Kiongozi wa Mzalendo.
Tunataka siku hii ikumbukwe na Wazanzibari wote Duniani na tunaomba michango yenu ya picha, ngoma za kibati, Msewe, Bomu, na ngoma nyengine zote zinazowakilisha mikoa mitano ya Ungbuja na Pemba.
Tukumbuke hatuwezi kuwa Wazanzibari wa kweli kama hatutoikumbuka siku hii. Shime tushikane bega kwa bega tuilinde Nchi yetu na Identity yetu.mpaka sasa tushajuwa kuwa 1964 sio siku ya uhuru bali ni siku ya msiba wa kuliwa dunguzetu na kunyanganywa nchi yetu na mkoloni tanganyika sasa lazima tushikane letu liwe moja nchi kwanza zanzibar kwanza natukishakana tutashinda.
Mungu Ibariki Zanzibar.
Wabariki Wazanzibari wa ndani na nje ya Visiwa vyetu.
Mungu ubariki Umoja Amani na Utulivu ulioko ndani ya Visiwa vyetu. Amin
No comments:
Post a Comment