VUGURU kubwa zilizosababisha kuharibiwa kwa magari na watu kadhaa kujeruhiwa vibaya zilizuka jana kati ya makundi mawili ya wafuasi wa viongozi waandamizi wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad na Mbunge wa Jimbo la Wawi, Hamad Rashid Mohamed.Mapigano hayo makali yalizuka baada ya kundi kubwa la vijana walinzi maarufu ‘Bluu Gurds’ waliokuwa wamebeba mapanga, visu na nondo kutoka makao makuu ya CUF kuvamia ziara ya mbunge huyo eneo la Mabibo, Dar es Salaam wakiwa na nia ya kuzuia mikutano yake.Tanzania Daima lililokuwa katika eneo hilo, lilishuhudia kundi hilo la vijana lililowasili katika eneo la Mabibo kwenye Tawi la Chechnya ambako Hamad Rashid alikuwa akitangaza nia ya kuwania Ukatibu Mkuu, na kuanza kumshusha kwa nguvu kutoka katika jukwaa alikokuwa akihutubia.Hata hivyo, kitendo hicho kiliwaudhi wanachama na wananchi wengine waliokuwa wamefurika katika mkutano huo, ndipo mapigano yalipoanza kwa kurushiana mawe, mapanga na kila aina ya silaha iliyoonekana kuwa karibu kutumika.Katika vurugu hizo ambazo hakukuwa na ulinzi wowote wa askari polisi kinyume cha ilivyotarajiwa na wengi, vijana wa Bluu Guards walizidiwa nguvu na gari lao likaharibiwa vibaya kwa kupigwa mawe.Aidha, mwanachama mmoja wa chama hicho aliyejulikana kwa jina la Adam Edo, alikatwa mkono na kuachwa ukiwa unaning’inia na kukimbizwa katika Kituo cha Afya cha Muna kwa huduma ya kwanza, kabla ya kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu zaidi.Mara baada ya kutulia kwa mapigano hayo, mbunge huyo alilaani kitendo cha kuvamiwa na kundi la wafuasi wa Maalim Seif Sharif Hamad, akisema kuwa ataendelea na dhamira yake ya kugombea nafasi ya Ukatibu Mkuu wa CUF, ikiwa ni pamoja na kukifufua chama hicho ambacho alidai kuwa kimedodora.
Alisema endapo atagombea na kupata nafasi hiyo atahakikisha anafanya mabadiliko ya katiba ambapo mwenyekiti atakuwa ni miongoni mwa wajumbe wa kamati ya utendaji ya taifa na kiongozi mkuu wa chama tofauti na ilivyo katika katibaya sasa.“Mimi nitahakikisha kuwa chama kinakuwa kama taasisi na sitofanya maamuzi yangu mwenyewe kama ilivyo sasa ambapo viongozi wanaamua lolote bila kufanya mikutano wala kuwashirikisha viongozi wengine,” alisema Hamad.Mapigano hayo yamethibitisha mgogoro wa siku nyingi uliopo, ambao umefanya chama hicho kuanza kumeguka vipande vipande.Habari za uhakika zimebainisha kuwa viongozi hao sasa wameamua kuanza mapambano rasmi ya kuwania uongozi, ambapo wakati Hamad Rashid anaanza ziara za kampeni katika mji wa Urambo, mkoani Tabora Desemba 15, kabla ya kwenda Mkoa wa Singida Desemba 17, Maalim Seif atakuwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Na wakati huo huo Ismail Jussa, Naibu Katibu Mkuu (CUF) Zanzibar, amesema kinachojitokeza katika mzozo uliopo sasa ndani ya Chama hicho ni Mhe Hamad Rashid, kutumikia utashi na tamaa binafsi na maslahi ya baadhi ya watu ambao wanamsukuma kuleta mkorogano ndani ya Chama. ‘Lakini wanachama wamemuelewa, hawakubaliani nae kabisa katika mtazamo wake’, alisisitiza Jussa.
Akihojiwa na Sauti ya Ujerumani katika matangazo yake ya jana (Jumatatu Disemba 12,) Ismail Jussa alisema kinachoshangaza ni kuwa Mhe Hamad Rashid, mtu anaekifahamu vizuri Chama tokeo kilipoanzishwa, kuamua kutaka kuleta mkorogano. Jambo ambalo linaonekana linalengo la kutaka kuvuruga Maridhiano yaliyofikiwa baina ya Maalim Seif na Rais wa Zanzibar msataafu Dr Aman Karume.
Naibu Katibu Mkuu huyo wa CUF, alikwenda mbali na kudai kuwa wanazo habari kuwa Hamad Rashid katika siku za hivi karibuni, amekuwa na usuhuba mkubwa na kiongozi wa juu wa Serikali ya Muungano (bila kumtaja jina) na kuongeza kusema kuwa Chama (CUF) wanapata habari.Kuhusu madai ya Hamad Rashid, kutaka kuwa Katibu Mkuu wa CUF, Mhe Jussa ambae pia ni Muwakilishi wa Mji Mkongwe, alifafanua katika KATIBA ya CUF kila mwanachama anayo haki kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya Chama kwa kufuata utaratibu.Aidha alisema CUF, itaingia katika mchakato wa uchaguzi kwa ngazi mbali mbali kuanzia mwaka 2013 kwa ngazi za matawini na kufikia mwaka 2014 kwa ngazi ya Taifa. “Kama Mhe Hamad Rashid, ana nia njema na hoja yake ilikuwa asubiri Chama kitakapofanya uchaguzi wa viongozi wake na si hivi sasa kuibua suwala hilo”; alibainisha Jussa.Hamad Rashid na Maalim Seif, wote ni miongoni mwa wanachama wa CUF waliopata misukosuko na mateso mengi, ikiwamo kukaa Gerezani kwa muda mrefu, kuhusiana na harakati za siasa kwa lengo la kuwatetea Wazanzibari
WANANCHI WA ZANZIBAR NAFIKIRI NILISHAWAMBIYA HAPA MARA NYINGI SANA KUWA TUKISUBIRI VIONGOZI WATUKOMBOWE TUTA SUBIRI SANA SANA. MAANA MAMBO NDIO KAMA HIVI WAZANZIBAR WAMEUNGANA NA SASA WANATAKA KUJIKOMBOWA HUYU HAMAD RASHID ASHAZUKA NA YAKE. SASA WATU WATATENGANA TENA KISHA TUNARUDI KULE KULE TULIKOTOKA KWENYE SIASA ZA CHUKI NA KUBAGUWANA. KISHA MKOLONI MWEUSI ANACHEKA SANA ANASEMA WANGALIYE WENYEWE KWA WENYEWE WANATAFUNANA KWELI WATAWEZA KUJITAWALA..? NA HAYA SIO YA LEO WALA JANA HABU NIWAKUMBUSHE KIDOGO MIAKA YA NYUMA YA WAKATI WA CHAMA CHA HIZBU PIA KULIKUWA NA MKORONGANO MWISHO BABU AKAFUKUZWA NA AKANZISHA CHAMA CHAKE NYERERE AKAONA MWANYA AKAMLETA OKELLO NA VIKAPTURA WAKATUUWAA VIZURI SANA KISHA WAKATUTAWALA MPAKA LEO SASA HAMAD RASHID NAE ANA ANZA KISHA KUTAZUKA LA KUZUKA MWISHO KUTATOKEYA MAPINDUZI YASIYOJULIKANA MIGUU WALA KICHWA MWISHO WAKE TUTAJIKUTA TUNATAWALIWA TENA NA WATU HATA SIO WAZANZIBAR KWA MIAKA MENGINE 47 KWA HIYO WAZENJI FUNGUWENI MACHO NA FINIKENI KOMBE MWANAHARAMU APITE ASIJAKUTULETEA BALA ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment