Mawakili wa watuhumiwa waliopo kizuizini kutokana na tuhuma za makosa atii ya ugaidi kutoka nchini Zanzibar, wamedai kuwa kitendo cha Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwapeleka Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam nchi jirani ya Tanganyika ni kuidhalilisha nchi ya Zanzibar kisheria.
Mawakili hao wakiongozwa na Abdallah Juma walitoa madai hayo mbele ya Jaji Mkusa Isack Sepetu wa Mahakama Kuu ya nchi ya Zanzibar wakati wakiwasilisha hati ya maombi ya dharura kufuatia wateja wao waliokamatwa nchini Zanzibar na kupelekwa nchi ya jirani Tanganyika kushtakiwa.
Alisema watu hao wamenyimwa uhuru wao wa kikatiba kwa mujibu wa katiba ya nchi ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu cha 14 (1) (2) na kifungu cha 16 (1).
Alisema kuwa kitendo kilichofanywa na Jeshi la Polisi cha kuwaweka kizuizini wateja wao kwa mienzi miwili sasa tena nje ya nchi yao ya Zanzibar wakati Zanzibar ni nchi, ni kinyume cha sheria ya makosa ya jinai kifungu cha 28 sheria namba 7 ya mwaka 2004 ya nchi ya Zanzibar.
“Zanzibar ni nchi tena ina mahakama yake kwa nini wateja wetu wakamatwe nchini kwao hapa Zanzibar wakawekwe katika kizuizi kisicho halali nchini Tanganyika......? alihoji, hivyo jaji huoni kitendo hicho ni kuidhalilisha mahakama yako tukufu,” alimuliza Abdallah Juma Jaji huyo.
Aliongeza kusema kuwa wateja wao wanne walikamatwa na polisi nchini Zanzibar miezi miwili iliyopita kwa kuhusishwa na tukio la mlipuko wa bomu uliotokea eneo la Darajani Juni 13, mwaka huu na kuua mtu mmoja na majeruhi tisa.
Alisema kwa mujibu wa sheria za nchi yetu ya Zanzibar tukio limefanyika hapa hapa nchini kwetu Zanzibar, hivyo watu hao wangepaswa kuhukumiwa katika mahakama za hapa hapa nchini kwetu Zanzibar na siyo Dar es Salaam nchini Tanganyika.
Aliendelea kusema kuwa wateja wao hawajapewa fursa ya kusikilizwa na kuiomba mahakama hiyo kufuata sheria.
Hata hivyo, upande wa mashitaka uliiomba mahakama kutupilia mbali madai hayo na Jaji Sepetu aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 28, mwaka huu mahakama hiyo itakapotoa maamuzi kuhusiana na maombi hayo.
Watuhumiwa hao waliokamatwa miezi miwili iliyopita kutokana na kosa la ugaidi ni Nassor Hamad Abdallah, Mohammed Ishaq Yussuf, Said Kassim Ali, Hassan Bakari Suleiman, Rashid Ali Nyange, Antar Humoud, Khamis Salum Amour na Salum Ali Salum.
No comments:
Post a Comment