NCHINI ZANZIBAR: Vijana wawili wanasaidikiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha kwa muda wa miezi minne sasa tokea kutoweka nyumbani kwako huku wazee wao wakihangaika kuwatafuta.
Wakizungumza na waandishi wa habari kwenye ofsi ya Jumuiya ya Waaandishi wa habari za Maendeleo nchini Zanzibar (WAHAMAZA) Wazee wa watoto hao, Zubeir Ame Khalid na Masoud Salum wamesema watoto wao wametoweka nyumbani tokea msako wa vijana wanaotuhumiwa kujihusisha na ugaidi ulipoanza zaidi ya miezi minne iliyopita.
Vijana hao ambao wametajwa kwa majina ya Khalid Zubeir Ame na Said Omar Said, wazee wao wamesema tokea kutoweka wa vijana wao wamekuwa wakifuatilia katika vituo vya polisi, magerezani ya nchi ya Zanzibar na ya nchi ya Tanganyika bara bila ya mafanikio na wanashindwa kujua waliopo watoto wao kama bado ni wahai au wameshafariki.
“ Mimi mwanangu Khalid alikwenda kusali sala ya Ishaa tokea tarehe 17 mwezi wa nane na tokea hapo nimekuwa nikifuatilia kila pahala na kuwafuata baadhi ya wazee wenzangu ambao wamepotelewa na watoto wao lakini bahati mbaya sijafanikiwa kumuona mwanangu hadi leo hii” amesema Mzee Ame.
Siku chache baada ya kukamatwa kwa Kassim Mkadam Khamis ambaye mtoto wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi na kuunganishwa na watuhumiwa wa ugaidi waliopo gerezani Dar es Salaam nchini Tanganyika, ndipo alipopotea Khalid na kuanza kutafutwa.
“Mwanangu Khalid na mtoto wa Kamanda ni marafiki sana na wamekuwa wakisali pamoja msikitini na tulipata taarifa mtaani kwamba mwanawe anasakwa na polisi baadae tukasikia amekamatwa na amefikishwa mahakamani lakini mwangu hadi leo kimya” alsema Mzee huyo huku akionesha hali ya huzuni.
Mzee Ame amesema baada ya kuchelewa kurudi msikitini mtoto wake mwenye umri wa miaka 23 akaanza kupatwa na wasiwasi na kuanza kufuatilia lakini baada ya mwezi, Khalid akapiga simu na kumueleza baba yake kuwa yupo salama na ametoka kwa ajili ya kujitolea kutangaza dini kwa ajili ya Allah (Tabligh).
“Mimi nilikuwa na wasiwasi sana na nikajua sio kweli maana hana kawaida na kundoka bila ya kutuaga wazee wake itakuwa alikuwa katika mikono ya vyombo vya usalama na ndio maana akawa anakhofu kubwa wakati alipokuwa akiongea na sisi wazazi wake” alisema Mzee Ame.
Aliongeza kwamba “Tulikwenda kwenye taasisi ya Fiisbilillah ambayo inaratibu watu wenye kutangaza dini lakini tulipofika tukaambiwa hayumo jina lake halimo katika orodha ya walioondoka, nikenda jumuiya ya Uamsho ili nijue jee mwanangu yumo kwenye watu waliokamatwa? kwa sababu watu waliokamatwa wengi ni wa Uamsho labda na mwanangu atakuwa ameingizwa katika gurupu hilo lakini bahati mbaya jina lake halikuwemo”
Aidha aliwaeleza waandishi wa habari kwamba kutoweka kwa mtoto wake kumempa wakati mgumu na kulazimika kumtuma kijana wake mkubwa kufuatilia kwenye magereza yote Zanzibar pamoja na Tanzania bara lakini hawakufanikiwa kumuona katika magereza hayo wala hayupo katika orodha ya watu waliofikishwa mahakamani.
DSC06205
Naye kwa upande wake Mzee Masoud Salim alisema mtoto mkaazi wa Mbuyuni alisema mtoto wake hakuonekana nyumbani na hajulikani alipo tokea Agosti 30 mwaka huu.
Naye kwa upande wake Mzee Masoud Salim alisema mtoto mkaazi wa Mbuyuni alisema mtoto wake hakuonekana nyumbani na hajulikani alipo tokea Agosti 30 mwaka huu.
Alisema kutoweka kwa kijana wake kumewapa mashaka na kuanza kufuatilia kwenye vyombo vya ulinzilakini bila ya mafanikio ambapo wametoa ripoti kwenye vituo vya polisi tofauti.
“Tuna wasiwasi mkubwa na kijana wetu kwa sababu hatujui kitu gani kimemsibu haonekani wala habari zake hatuzisikii, tumekuwa na matumaini kwamba labda tutasikia jina lake akipandishwa mahakamani au atatangazwa na vyombo vya habari lakini tunasikia majina mengine lake yeye hatulisikii” alisema Mzee Masoud kwa huzuni.
Wazee hao kwa pamoja wameiomba serikali na jeshi la polisi kutoa taarifa za watoto wao na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria iwapo wamefanya makosa badala ya kuwashikilia kwa kuwaficha na kusababisha khofu kubwa ndani ya familia zao.
“Tunaomba vyombo vinavyohusika kama watoto wetu wamefanya makosa basi wawafikishe mahakamani kuliko kutusababishia sisi huzuni hatuna raha tuna huzuni hatujui kama watoto wetu wahai au wamekufa na khofu inazidi tunaposikia vijana wengine wamelawitiwa au kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji wakiwa mikononi mwa vyombo vya sheria” wamesema wazee hao.
Akizungumza malalmiko hayo, Naibu Mkurugenzi wa Upepelelezi wa Makosa ya Jinai DCI, Salum Msangi amesema hana taarifa za kupotea kwa vijana hao na wala kukamatwa kwao na kuwaomba wazee wa vijana hao waliopotelewa kufika ofisini kwake kutoa maelezo. Jumla ya wazanzibari 31 wakiwemo viongozi wa Uamsho, Sheikh Farid Hadi Ahmed na Sheikh Msellem Ali Msellem walikamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kujihusisha na ugaidi na wapo rumande hadi leo wakisubiri kusikilizwa kesi yao.
HAYA NDIO WALIO KUWA WAKIYAFANYA BAADA YA MAPINDUZI YA 1964 WAZANZIBARI WENGI WENGI SANA WALIPOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA NA WENGI WAO HAWAKUPATIKANA MPAKA LEO HII WALA MAKABURI YAO HAYAJULIKANI YALIPO KWA HIYO MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA NA VITUMWA AU NDIO TUSEME VIBARAKA WAKE KINA SHEIN,BALOZI MKAZI A.K.A.BALATOLI,NAHODHA,ALI VUAI,SAMIA N.K. WASHAJUWA KUWA MWAKA HUU NDIO MWISHO WAO KWA HIYO WANAFANYA HAYA ILI WATU WAINGIYE HOFU NA WAWACHE KUPIGANIA ZANZIBAR YENYE MAMLAKA KAMILI LAKINI NAONA MUMECHELEWA MAJI YASHAMWAGIKA PIA WAZANZIBARI MUKUMBUKE KUWA SHEIN ALISEMA ATAWAFANYIA MAMBO WAZANZIBARI HAWATA MSAHAU NA KWA ALIYO YAFANYA MPAKA SASA NAAM HATUTA MSAHAU.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
No comments:
Post a Comment