Sunday, February 22, 2015

CCM MLIO BAKI CHUKUWENI KAULI HII.......MSEMO WA ‘DUNIA HADAA, YAGHILIBU SHUJAA!’

NYUMBA MPYA YA SALMIN AWADHI SALMIN ALIYO HAMIA ALIZO JENGA HAPA DUNIANI KAZI WACHA HAPA HAPA DUNIANI CCM WASAKA TONGE NA MADALALI MESOMA NINI KATIKA KIFO CHA SALMIN..?
Katika ndege waliotajwa kwenye kitabu kitukufu cha Qurani, kunguru yasemekana yumo. Kwa kawaida vitu au viumbe vilivyotajwa humo vina umaizi mkubwa na mafunzo makubwa tunayopaswa sisi wanadamu tujifunze kupitia kwao.
Utafiti mdogo tu uliofanywa na wanazuoni walioko hapa nchini Zanzibar na nchi ya Tanganyika wamegundua kuwa kunguru amepewa uwezo mkubwa wa macho. Inasadikiwa kuwa jicho la Kunguru lina uwezo wa kuona mara nne zaidi ya jicho la mwanadamu. Lakini je hiyo tu ndiyo hekima aliyonayo kunguru hadi kufikia kutajwa kwenye Qur-ani...? La siyo hiyo na wala sababu hasa hatuijui sisi waja wa kawaida. Tubakie tu kusema ‘allwahu a-alam!’
Sisi watu wa kawaida, tusiosoma, tunamkumbuka kunguru sana kwa ule mlio wake ambao kwa wafasiri wa milio ya ndege – iwe kiutani au kiudhati basi anapolia kunguru husema maneno yanayokaririka – ‘Dunia Hadaa, yaghilibu shujaa!’ Na ni maneno hayo hasa ndiyo yanayonipa kifungu na uwezo mwembamba wa kuandika ukurasa huu leo, kwa watakaobahatika kuusoma!!! in shaa allah.
Lengo, nia na madhumuni yangu ni kuonyesha jinsi gani cheo au uluwa, pesa, nguvu na punzi alizo tupa allah ambazo hatujuwi zinakwisha lini,wapi,wakati gani zinavyoweza kumpoteza njia mwanadamu aliye dhaifu mbele ya Allah hadi akafikia hatua ya kukufuru na kutakabari kulikopitiliza ada. Na basi bila kujua mwanadamu huyo dhaifu kuwa kuna nguvu kubwa zaidi inayomwendesha yeye, huendelea kutakabari hadi akafikia kupatilizwa na mola wake akaishia kupata hasara ya milele!!! huko tuendeko.
Tuna mifano mingi ya viongozi waliokubuhu na kufurutu ada. Wakatakabari kiasi ya kuvaa joho la Mungu. Matokeo yake wakafikia pabaya. Mfano mzuri wa hayo ni firauni wa Misri ambaye kwa jinsi alivyotaraghani ujeuri wake alifikia kusema; ‘Mimi ndiye Mungu wenu wa haki!’ aha!!! Basi alipofikia kipeo hiki, mumba wa haki akajitokeza akamdaka kwa kumgharikisha hata asipate kauli ya kwi! Seuze kupiga shahada!!!
Kwetu sisi watu mfano wa Fira-uni pia wapo. Wengi wao ni wanasiasa kwa bahati mbaya. Mfano wa karibu tutauanza kwa baba wa taifa wa nchi ya Tanganyika Julius Nyerere ambaye kwa jinsi ya nchi yake ya Tanganyika ilivyomtukuza, alifikia hadhi ya utume na kwa wengine hata Uungu haukuwa mbali naye –Astaghfiruh Allah! Naye kwa kupata kichwa, akabweteka, akawa jimbi anayewika.
Siku moja kama sikosei mwaka 1998 au mwanzoni mwa mwaka 1999, katika moja ya vikao vyake Nyerere alisema kuwa anashangaa sana kwanini mtoto mchanga hufa, Astahafiruh Allah. Hilo lisitoshe. Akasema yeye ana tamaa ya kuishi hadi miaka themanini.
Wakati huo alikuwepo Mzee Ruksa, Mwinyi ambaye ama kwa dhihaka au kwa hivyo kumutukuza Nyerere na kumpa bichwaa alimwambia ‘ Nakuongeza miaka mengine mitano, mwalimu!’ Jumla ikawa wamepeana miaka 85 ya kuishi kama kwamba wao ndio Miungu. Mwaka uliofuata Mwalimu Nyerere akafa! Paaa! Ikawa ndio mwisho wake huo na hakuna aliyeweza kumwombea asife!
Aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Rashid Abdalla Mamba, aliwahi kuunyayua mkono akasema kama kuna Mungu nauonyoosha huu mkono wangu, naaukunje huyo Mungu! Astahafiruh Allah Mwenyezi Mungu hana haraka hakuukunja siku ile Rashid Abdalla Mamba alipouliza ukuunjwe lakini kwa vile M.Mungu ana uwezo mkubwa, akaukunja mkono wa Mamba Kivengine. Akazikwa vipande vipande hadi akamalizika. Hassan Mandera aliyekuwa kinara wa uharamia kule gereza la Bamke kiinua miguu naye alioza kipande kipande hadi akamalizika.
Bi Safia Kawawa, siku aliyotaka kuleta hoja ya kuwa wanawake waruhusiwe kuolewa na mume zaidi ya mmoja baada ya shibe ya uluwa kumkaa kisawa sawa, Mungu alimpatiliza. Kifo chake kitabaki siri kubwa lakini hakitosahaulika kamwe katika Historia! Mpango wake wa kuwafanya wanawake wadai kuolewa na waume wengi, akaenda nao kaburini akiwa nyama pakachani!
Salmini Amour, Komandoo wa Udongo naye yumo anamomonyoka Komandoo wakati huo, ambaye kwa sasa ni kipofu kuzuizui, alipisha mipaka ya kejeli, jeuri na dharau dhidi ya damu y Kizanzibari wenye asili ya kisiwa cha pemba. Akawa anajiona kama yeye na Mungu wana mkataba wa pamoja wa kufanya atakavyo. Hajafa lakini pia hayu hai tena yumaji. Yameshamkuta ya kila aina. Ya aibu na fedheha. Ya udunifu na udhalilifu. Kuanzia kukatiwa umeme wakati wa Karume mtoto hadi kukataliwa ni mke hadharani. Hatima yake hatujaijua kama tulivyokuwa hatujazijua hatima zetu. Aliyekuwa Waziri Kiongozi Zanzibar Ramadhani Haji, naye yumo katika kundi hili.
Mwanadamu ni mnyama aliyetukuzwa lakini mjinga hata kuliko baadhi ya wanyama kwa sababu hajifunzi kwa waliomtangulia. Muda si mrefu wiki hii, Salmin Awadh tulikuwa naye akiwa hai na nguvu tele. Hafla tunapata habari kuwa ameshaaga dunia wakati siku tatu tu zilizopita alikuwa akijinadi na kujilabu kwa madebusi kuwa nchi hii CCM hawatoi kwa kura. Lazima damu imwagike ndio nchi hii itapatwa au watatumia vifaru lakini ushindi kwa CUF hata wakishinda kaisi gani nchi hawatoi!
Hayo, ukitoa maneno aliyoyasema kule Kisiwa ndui muda mchache kabla hajafa, ambayo mimi siyajui hadi sasa, ndiyo maneno yake ya mwisho kabla hajakabiliana na muumba wake uso kwa uso akhera. Maneno ya Salmin Awadh ni maneno ya kila kiongozi wa CCM Zanzibar hivi sasa. Kaanza Asha Bakari na wengineo wote wanasema kinaganaga kuwa nchi hawatoi! Lakini kwani nani hajui kuwa CCM nchi hawatoi......???
Ukweli kila mtu anajua kuwa nchi CCM hawatoi lakini hapakuwa na haja ya kuropoka na kupisha mipaka hadi kufika kutishia kuuwa watu kwa sababu ya vyeo na uluwa. Kwa hakika kauli aliyoagia dunia Salmin Awadh haikuwa nzuri wala ya kheri na ndio labda, allwahu aalamu, Mungu kwa kujua ubaya wa nia yake aliyokuwa nayo akaona amchukuwe ili kupishia mbali majanga yatakayotokana na shari za ulimi wa kiongozi huyo!basi yeye na wenzake CCM wamesema kuwa hawatowe naona Mwenyezi Mungu anawatowa wao kwa SAANDA
Hakika Zanzibar haihitaji vifaru kuiwezesha CCM kutawala. Inahitaji ‘wembe ule ule’ tu wa kuinyolea CUF ambayo haina ubavu wa kugoma kutia maji nywele zake zisinyolewe na CCM. CUF ni kichwa kama cha mwendawazimu. CCM wakiwa na wembe tu hujinyolea tu kila siku na hakuna liwalo. Hapakuwa na haja kwa Salmin Awadh Marehemu kupayuka na kumpa nafasi malaika wa dhambi kuharibu wino bure katika kitabu chake.
Salmin Awadh alikuwa anyamaze kimya asubiri uchaguzi ukifika CUF wanapiga kura kwa wingi wakisha wanaenda makwao kulala. Huku CCM wanaiba kura, wanabadilisha kura na kuchakachua kura ikifika usiku wanamtangaza mgombea wao. Asubuhi wakiamka, CUF kama kawaida yao watalia siku mbili kisha wataunda uongo mwengine wa kuwaambia wanachama wao kwanini hawakushinda uchaguzi. Hili halina shaka. Ndio mazoea yao wala sio geni tena hapa nchini Zanzibar! ila mara hii CUF wanasema sio hivyo tutaona ihio oktoba kwa tutakao jaliwa kuwa hai.
Lakini, masikini labda kwa kuchanganyikiwa Salmin Awadh,Umma wa Kizanzibari ulivyo chachama na kuchoshwa na ukiritibwa wa watu wachache wasaka tonge CCM wanao jaza matumbo yao na kuwawacha wengi wa Wazanzibari wakiteseka na maisha,huku CCM ikiendelea kuwandanganya kuwa wanaleta maendeleo wakati hata maji hayatoki ndio labda Salmin Awadhi akaona bora atumeye kiburi na cheo na woga wa kukosa ushindi katika uchaguzi ukamfanya afike mbali. Akasema ya kusema hadi akafikiakukufuru na kuitakia nchi hii na watu wake balaa la maangamizi kwa jambo dogo tu – uluwa!
Leo hii hata ile nia yake ya kuirudisha nchi ya Zanzibar kwenye fujo za kisiasa kwa kuivunja Serikali ya umoja wa kitaifa haikufanikiwa. Mwenye pupa, hadiriki kula tamu! Na hapo ndipo tukasema, tujihadhari na dunia. Kwani Dunia hadaa, yaghilibu shujaa! Mungu atustiri waja wake, na atuongoze katika njia ya kheri na wala tusihadaike na uluwa mfupi wa Shaitan wa hapa duniani usio kuwa na faida yoyote.
Amen Amen Amen!
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment