Tuesday, October 6, 2015

VIDEO-NCHINI ZANZIBAR KAMATI YA MARIDHIANO SIX PART 1/3 LOWASSA UKAWA KIBANDA MAITI 17 AUG 2015

PART 1
PART 2
PART 3
KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

VIDEO-NCHINI ZANZIBAR KAMATI YA MARIDHIANO SIX: MKUTANO WA HADHARA, MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MALINDI, MFENESI MAZIZI

KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

Saturday, October 3, 2015

VIDEO-NCHINI ZANZIBAR KAMATI YA MARIDHIANO SIX: MKUTANO WA KAMPENI CUF MGOMBEA URAIS JIMBO LA MFENESINI, MWAKAJE

KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

VIDEO-NCHINI ZANZIBAR KAMATI YA MARIDHIANO SIX: MKUTANO WA KAMPENI CUF MGOMBEA URAIS JIMBO LA ZIWANI

KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

Friday, October 2, 2015

NCHINI ZANZIBAR CCM INAZIDI KUVURUGIKIWA MIAKA 50 NA USHAIYA UMEME BADO WA MGAO NA MAJI YA KUOMBA OMBA

Mwenyekiti wa wilaya ya Mjini, Borafya Silima moja kati ya mikutano ya CCM ya kuwanadi wagombea

 KADIRI siku zinavyo sogea kufikia 25 Oktoba, siku ya uamuzi wa kupata rais mpya au kubaki na yuleyule, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinazidi kuvurugikiwa. Shein anaimarisha ahadi ya kuendeleza anachoita “mafanikio” ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo ukweli, ipo ipo tu juu badala ya kushushwa ngazi ya chini hadi mitaani waliko Masheha. Anarudia rudia kusema, na Balozi mdogo wa nchi ya Tanganyika Baloteli Ali Iddi akimsaidia, serikali haitamvumilia mtu yeyote hata awe na pembe kiasi gani, anayechochea uvunjifu wa amani, na wasaidizi wake katika CCM wakizidisha kauli za matusi na kutisha wananchi. Mgombea mshindani mkuu, Maalim Seif Shariff Hamad ambaye ndiye Makamo wake wa kwanza, yeye anazidisha upole na kujenga watu matumaini kwa kutumia lugha nzuri. Ninavyofuatilia hutuba za viongozi hawa nathibitisha zaidi nilichopata kukieleza, wapo wagombea wawili wenye dhamira tofauti. Rais anajikaza kisabuni eti amesimama imara na anajaza imani wafuasi kuwa ushindi kwao ni lazima, ingawa katika vikao vyake vya ndani na makada, kikiwemo alichokifanya hivi karibuni kijijini Makunduchi, anakiri “mgonjwa yuhali mbaya na anatiwa maji.”
Tayari ameahidi mshahara wa Sh.300,000 kima cha chini, ambao haujawahi kufikiriwa serikalini ingawa kimekuwa kilio cha miaka mingi cha vyama vya wafanyakazi. Leo wanapo ahidiwa kiwango hiki, unajiuliza kwa uchumi upi....? Uchumi wa nchi ya Zanzibar wa kijungu mwiko usiomudu kulipa fedha hizo kila mtumishi wa chini, ikiwa na maana utaongezeka kwa wafanyakazi wa kada ya kati na juu. Rekodi zote za serikalini hazioneshi hilo litawezekana iwapo Shein atachaguliwa. Kiwango hicho kinawezekana tu iwapo kutakuja uongozi mpya wa serikali ambao utakuwa na utashi wa kukusanya kila senti inayopasa kukusanywa, itafuta misamaha ya kodi na kuziba mianya ya ufisadi. Serikali italazimu kuwa ndogo si kama ilivyo mawaziri wasio wizara, unaongeza wilaya na majimbo kwa sababu za kutafuta ushindi wa kutunga, na unazembea kukusanya kodi huku ukiachia watendaji kuiba watakavyo. Serikali itahitaji angalau mwaka kupata uwezo wa kulipa kiwango hicho, na hapo italazimu ikomeshe upotevu wa mamilioni ya shillingi kupitia wizi wa mishahara hewa na ununuzi wa huduma na vifaa serikalini usiofuata Sheria ya 2003. Pia iwe imezuia mtindo wa fedha za serikali kuchukuliwa katika mifuko ya rambo (badala ya kupelekwa benki) na zikalala majumbani kwa maofisa fisadi maswahiba wa viongozi.
Serikali ya viongozi walioamua hasa kuitumia Tume ya Kudhibiti Rushwa na Uhujumu wa Uchumi ambayo haijafanya la maana tangu ianzishwe kwa mbwembwe na 2013. Kama vile hakuna wala rushwa wala wahujumu wa uchumi hapa nchini Zanzibar; kama vile hakuna washenzi waingizaji wa ‘unga’ na kama vile hakuna wanaofisidi miradi ya maendeleo. Mabaya yote haya yameshamiri kutoka Novemba 2010 licha ya ahadi ya Shein kuahidi kuwa mlinzi mzuri wa raslimali za Wazanzibari kwa lengo, pamoja na mambo mengine, la kujenga uchumi. Sasa unapomsikia mtetea kiti akiahidi kupambana na mafisadi huku nchi ikiwa inazidi kutegemea chakula kutoka nje kwa sababu serikali haijasimamia ipasavyo mpango wa kukuza sekta ya kilimo hasa uzalishaji wa mpunga, ujue itabaki hivyo hivyo kwa mfumo uliopo chini ya CCM. Ukiambiwa changanya na zako, amesema Jayaka Kikwete, rais wa jamhuri ya Tanganyika anayestaafu baada ya Oktoba 25. Ahadi za Dk. Shein ni zilezile za uchaguzi wa 2010, nyingi kwelikweli na ukizisikia tamu kuliko; tatizo kubwa ni usimamiaji wa mipango ili kuleta tija. Juzi nikamsikia anaahidi vijana ajira za kutosha. Hivi kufikia tu Oktoba hii, vijana wangapi wameajiriwa....? Kwa kazi zipi na wapi wakati vijana wa nchi ya Zanzibar, kwa kukosa uwezo wa ada, wanashindwa kusoma Chuo cha Utalii Maruhubi ili watembeze watalii katika nchi iliyojaaliwa fukwe mwanana...? Hakuna vijana katika kilimo wala uvuvi ukiacha wa kuhisabu walioko vijijini wakirithi kazi walizofanya wazazi kwa kijembe kongoroka (kilimo) na uvuvi wa juya. Kipindi hiki nchi ya Zanzibar haina umeme wa kutosha. Wiki ya pili inaingia shirika la umeme – ZECO – linatoa umeme kwa mgao wa saa tano kwa siku.
Menejimenti imesema umeme umekuwa haba kwa sababu Shirika la Umeme kwa Masultani Weusi Tanganyika – Tanganyika Electric Supply Company (TANESCO) – linaingiza umeme kwa upungufu kwenye Gridi ya Taifa kutokana na hitilafu katika mitambo inayozoea kuendeshwa kwa kutumia gesi. Wala hili halina ukweli wa asilimia 100 maana taarifa za serikalini zinashawishi kuwa uzalishaji kwa nguvu ya maji unaofanywa Kidatu umezorota kutokana na mabwawa ya Mtera na Kihansi kupungua maji. Shein ameshindwa kuelekeza serikali kubuni mkakati wa nchi kupata umeme wake ili kuepusha gharika kama iliyotokea mwaka 2003 Tanesco waliposimama kuipatia umeme ili kushinikiza walipwe deni sugu la mabilioni. Nchi iliishi gizani kwa miezi mitatu mpaka suala hilo lilipotatuliwa kisiasa kwa maafikiano ya ratiba mahsusi ya nchi ya Zanzibar kulipa kwa awamu. Heko Wazungu wa Afrika Kusini kupitia Net Group Solution. Bila ya umeme wa kutosha na wa uhakika, huwezi kuahidi viwanda hata vidogo, achilia mbali kilimo cha kisasa na kukuza utalii, sekta ya pili kwa mchango bora katika Pato la Taifa (GDP). Hutazungumzia kamwe utafiti na uchimbaji wa gesi na mafuta pasipo umeme wa uhakika. Chini ya uongozi wa Shein, makada na askari wa SMZ wanaruhusiwa kuichezea amani kwa kaulimbiu ya “kutesa kwa zamu.” Askari wasio nidhamu wa vikosi maalum vya SMZ wanadhalilisha wananchi kwa vipigo na hawadhibitiwi; rushwa na ufisadi vinakua, ubaguzi serikalini ukishamiri.
Leo sitaji haja ya kuimarisha mfumo wa siasa ili ulete tija kwa maendeleo ya nchi. Eneo hilo ambalo nitalijadili wiki zijazo, lina maana kubwa katika kuilea demokrasia ya nchi ya Zanzibar, halkadhalika kuifanya siasa ichochee maendeleo makubwa ya kiuchumi. Nitagusa kwa undani ulazima wa kubadilishwa mfumo wa Muungano feki ambao ungali mfumo-dume usioisaidia hata kwa nukta nchi ya Zanzibar na watu wake, bali ukweli ukiendelea kuinyima fursa za kujijenga kiuchumi na kuacha kutegemea huruma ya Masulti Weusi wa Kitanganyika iliyovaa koti la Muungano feki. Kitu kibaya katika mfumo wa muungano wa serikali mbili, ni kuendelea kukandamiza mamlaka ya serikali yaliyopatikana kwa umwagaji wa damu ya wananchi wema kupitia mapinduzi ya 12 Januari 1964. Nitakapojadili hili, sitadharau umuhimu wa kuhusisha suala la Katiba mpya iliyotarajiwa iwe msingi wa kuivua nchi ya Zanzibar mnyororo unaoibana isifurukute mbele ya Masultani Weusi wa Tanganyika. Hili nalo ni eneo ambalo Shein pamoja na tambo zote na kauli laghai za viongozi wenzake wa CCM, amepotea kabisa njia. Kule kuamini kwa kutamka hasa kuwa kwake CCM hutangulia ndipo aifikirie nchi ya Zanzibar na Wazanzibari kwa ujumla, kumethibitishwa na kuridhia Katiba Inayopendekezwa inayodanganya Wazanzibari ila washachelewa Wazanzibari hawadanyiki tena.
KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

NCHINI TANGANYIKA LOWASSA ANGURUMA JIJINI DAR ASEMA SIKU 100 ATAFANYA MAMBO 13

Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema Edward Lowassa akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika viwanja vya TP Sinza Uzuri, jijini Dar es Salaam. Picha na Said Khamis
Mgombea urais wa Chadema na Ukawa, Edward Lowassa ametaja mambo 13 atakayoyafanya ndani ya siku 100 iwapo atachaguliwa kuwa Rais, huku akisema “atawakata kilimilimi” wanaombeza kuwa hawezi kuondoa umaskini wa wananchi. Lowassa alikuwa akihitimisha mikutano minne aliyofanya kwenye wilaya tatu za Jiji la Dar es Salaam jana kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers, Kawe. Wakati Lowassa akieleza hayo, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alitangaza azimio la Kawe lililobeba ajenda kuu tatu, ikiwamo ya kumtaka Rais Jakaya Kikwete kutoa mwongozo wa jinsi Serikali yake itakavyokabidhi madaraka kwa Ukawa kutokana na suala hilo kutokuwapo kikatiba. Wakati huo huo: Naye Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akitangaza mkesha kwa wananchi siku ya kuamkia tarehe ya kupigakura na kutaka wanaume wabakie kulinda kura zisiibiwe. Akizungumza kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya watu na viongozi wakuu wa Ukawa, Lowassa alisema mambo hayo atayatekeleza kwa kasi ya kilometa 120 kwa saa. Lowassa alitaja jambo la kwanza atakaloanza nalo kuwa ni uhakika wa dawa na vifaa vya uzazi wa akinamama. Alitaja mambo mengine kuwa ni umeme wa uhakika nchi nzima, kupunguza foleni jijini Dar es Salaam, kuondoa kero kwa wafanyabiashara wadogowadogo na waendesha bodaboda, kumaliza tatizo la maji nchi nzima, mfumo bora na rafiki wa wafanyabishara wakubwa na wadogo.
Kufuta ada na michango kwa wanafunzi, kupunguza kodi ya mshahara kwa wafanyakazi, kufuta kodi zote za mazao ya wakulima, mkakati wa kukuza michezo na sanaa, kuunda tume ya kutatua migogoro ya wafugaji na wakulima, kuanzisha kituo kila wilaya kwa ajili ya kutoa huduma za serikali na kuboresha maslahi ya polisi, wanajeshi na walimu. Mbali na mambo hayo 13, aliahidi kumaliza kilio cha wananchi cha kupata Katiba mpya inayotokana na maoni yao, akisema ni suala linalohitaji kutuliza kichwa kulipatia ufumbuzi. “Umaskini si mpango wa Mungu,” alisema Lowassa ambaye alikuwa akishangiliwa kwa nguvu. “Nina hasira ya kupambana nao na kuwaondoa Watanzania katika umaskini.” Waziri Mkuu huyo wa zamani aliyeihama CCM mwishoni mwa mwezi Julai, aligoma kushuka jukwaani akitaka awekewe muziki acheze na maelfu ya wananchi waliokuwa wakimsikiliza na kumkumbatia mkewe, Regina ambaye alifika uwanjani hapo wakati mkutano huo ukikaribia kumalizika, kisha akambusu. Awali, Lowassa alisema idadi ya kura anazohitaji ili ashinde urais ni milioni 14. Akiwa Mafinga mkoani Iringa, Lowassa aliomba wananchi wampigie kura milioni 10 ili awe Rais lakini jana alisema kuna haja ya kupata kura nyingi iwezekanavyo ili ushindi wake usiathiriwe. “Kilichonileta hapa ni kuomba kura,” alisema Lowassa. “Naomba mnipigie kura milioni 14 na ushee ili ziweze kutosha kuwa Rais. Baada ya kupiga kura, wananchi mnatakiwa kuzilinda ili zisiibwe.”
Lissu
Kabla ya Lowassa kupanda jukwaani, mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alitoa ufafanuzi wa alichoita “tamko la Kawe” ambalo ni kutaka ufafanuzi wa jinsi ya kukabidhiwa madaraka kwa upinzani, kitu ambacho alisema hakijaelezwa kwenye katiba. Alisema jambo jingine ni kumtaka Rais Kikwete ajibu kauli iliyotolewa na mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo kuwa CCM haitatoka Ikulu. “Kikwete atueleze kama hili ni tamko ni la chama au Bulembo,” alisema Lissu, ambaye pia anatetea kiti chake cha ubunge cha Jimbo la Singida Mashariki.
Mbowe
Akizungumza kabla ya kumkaribisha Lowassa, Mbowe aliwataka wafuasi na wanachama wa Chadema na Ukawa kuhakikisha wanakesha Oktoba 24, kujiandaa kupiga kura siku inayofuata: “Bado siku 24 tufanya uamuzi wa hatma ya maisha yetu na kuonyesha hasira kwa kutoichagua CCM,” alisema Mbowe. “Tunakwenda kuanza safari ya uhakika ya kutoa mwanga kwa taifa letu na kuonyesha heshima ya nchi na watu wake…“Oktoba 24 ni siku ya nini?…Ni siku ya kukesha kusubiri kupiga kura…Tunakubaliana tutakesha...?” Wananchi walimjibu kwa kelele kuwa watakesha na ndipo alipotoa maelekezo. “Akinamama mkishapiga kura rudini nyumbani mkaandae chakula, ila wanaume watabaki vituoni kulinda kura. Lakini hesabu hatua ya kwanza, ya pili… hadi zifike mia na hapo pigeni kambi kulinda kura,” alisema Mbowe. Kwenye mkutano wa Liwiti, Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye aliendeleza kampeni zake za kumnadi Lowassa huku akirusha tuhuma dhidi ya CCM na Serikali.
Sumaye alisema ni aibu kwa meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi kugombea ubunge wakati jiji analoongoza limekithiri kwa kipindupindu. “Ni lazima tuwe na aibu. Masaburi, jiji ni chafu limekushinda kipindupindu `kinatamba’ sasa unataka ubunge wa Ubungo, unadhani wananchi hawana akili za kupima,” alisema. Akiwa Kawe, Sumaye alimshangaa mgombea wa CCM, Dk John Magufuli akisema kuwa huwa ana maamuzi ya kukurupuka hadi ashikwe shati na kwamba akiwa Rais hakutakuwa na mtu wa kumzuia. Alisema alitaka kuvunja jengo la Tanesco la Ubungo ambalo limejengwa kwa kodi za wananchi, lakini akazuiwa. Pia aliamua kujenga barabara bila ya kuwa na fedha za kuwalipa makandarasi na kusababisha Serikali idaiwe Sh900 bilioni za riba, huku uamuzi wake wa kukamata meli ya uvuvi ukiigharimu Serikali mabilioni ya fedha.
Mbatia
Naye mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alikitaka Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kuitisha mkutano utakaovishirikisha vyama vya siasa ili Ukawa na CCM wakubaliane kuyakubali matokeo ya Uchaguzi Mkuu ikiwa tu utakuwa wa uhuru na haki. Mbatia, ambaye anagombea ubunge jimbo la Vunjo, alidai kuwa Serikali imeuza hisa zake katika kampuni ya bia ya TBL kwa Sh176 bilioni na kuzipeleka fedha hizo katika uchaguzi, huku akikitaka CCM kuibuka na kujibu jambo hilo akisema anao ushahidi.
Mnyika na Lubuva
Akizungumza kwenye mkutano huo wa Kawe, mgombea ubunge wa Jimbo la Kibamba, John Mnyika alimtaka mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva kuwapa jibu kabla ya Oktoba 4, mwaka huu kuhusu kupeleka wataalamu wao wa Tehama kwenda kuhakiki mfumo wa utakaotumika kupokea na kujumlisha kura za urais kwa lengo la kujua kama uko salama ili kuzuia uchakachuaji wa matokeo.
Awanadi Kubenea, Mdee, Mnyika
Akimnadi Saed Kubenea, ambaye anagombea ubunge wa Jimbo la Ubungo, Lowassa alisema sekta ya habari itapoteza mwandishi mahiri katika kazi yake, lakini wana Ubungo watakuwa wamepata mtetezi wa haki za wananchi. “Kubenea ni jembe mchagueni ili akafanye kazi bungeni na kusimamia maendeleo ya jimbo lenu,” alisema Lowassa. Pia alimnadi mgombea ubunge wa Kawe, Halima Mdee akimuelezea kuwa ni sururu badala ya jembe.
KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

Thursday, October 1, 2015

NCHINI TANGANYIKA POMBE MAGUFULI AKINYWA MAJI YA KIKOMBE CHA BABU

Leo Dodoma. Dkt @MagufuliJP amedai na kusisitiza kwamba katika uongozi wake dawa zitapatikana mahospitalini. Kwa babu wa loliondo alienda kufanya nini? Wanadai ana MSC + Phd ya kemia. Kuongea luha za taifa (Kiswahili, English) kwa ufasaha hajui. Akasafiri loliondo kunywa kikombe cha babu! Halafu ndio alete madawa hospitalini? Kituko cha karne.