Thursday, June 12, 2014

HATA BARABARA HII PIA BASI TUNASUBIRI MAMLAKA KAMILI CUF.....????


Hii ni barabara ya Mtendeni mjini magharibi kabisa, inayopitwa na wananchi na viongozi wengi, hususan Makamo wa Kwanza wa Rais wa nchi ya Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.
Mtendeni, kabla, ilikuwa ndani ya Jimbo la Mlandege lililokuwa chini ya uongozi wa Mh Kamal Basha Pandu na Bi Fatma Said Ali. Ambao kwa miaka mingi walikuwa mawaziri waandamizi wa serikali zote mbili.
Mwaka 2005, Mtendeni ilijumuishwa ndani ya Jimbo la Mji mkongwe, chini ya uongozi Mh Ibrahim Sanya na Mh Fatma Ferej na Mh Ismail Jussa.
Lakini barabara hii ni maarufu kwa kuwa ndio inayoelekea Makao makuu ya Chama cha Wananchi – CUF. Leo barabara hii inapitwa angalau kila wiki mara moja na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Sio jambo la kushangaza kusikia ving’ora vikilia pale Makamo anapokwenda ofisini kwake.
Lakini kuna tofauti gani ya ubora wa barabara hii baina ya kipindi kile cha uongozi wa CCM na sasa chini ya uongozi wa CUF...??

NCHI YA ZANZIBAR NA MAURITIUS NCHI MBILI KATIKA BAHARI MOJA ILA NCHI MOJA ITABANI HATA KUTWITA HATWITI TENA


Zanzibar na Mauritius — kisa cha nchi mbili katika bahari moja.
Habu tujaribu kuvilinganisha visiwa vya Mauritius na vya kwetu Zanzibar na kuonyesha jinsi Mauritius ilivyotupita kwa maendeleo na kwa sababu gani.
Kwa hakika kilichonihamasisha kufanya hivyo ni mtazamo wa sahibu yangu mmoja wa Sweden mwenye mahusiano makubwa na visiwa vya Bahari Kuu ya Hindi — Comoro, Mauritius, RĂ©union, Bukini (Madagascar), Shelisheli (Seychelles) na Zanzibar. Kila mwaka huikimbia baridi ya Ulaya na huvizuru baadhi ya visiwa hivyo.
Ana mazoea mengine pia: haimpiti wiki moja au mbili bila kuniletea baruapepe anayoiambatanisha na makala yaliyochapishwa na moja ya magazeti ya visiwa hivyo.
Siku zote makala ayaletayo yanakuwa yanasifu maendeleo fulani katika moja ya nchi hizo au mambo yenye kumfurahisha katika jamii za nchi hizo. Jambo lenye kumkuna kuhusu Comoro, kwa mfano, ni jinsi wananchi wa huko wanavyoishi kwa amani bila ya kubaguana ingawa ni watu wa asili tofauti.
Mara nyingi lakini huwa ananiletea makala yanayohusu maendeleo ya kiuchumi ya visiwa hivyo vya Bahari Kuu ya Hindi isipokuwa Zanzibar. Kwa mfano, mapema mwezi Aprili aliniletea makala yaliyoarifu kwamba uwanja wa ndege wa Roland Garros ulio kisiwani Réunion umeorodheshwa kuwa wanne kwa ubora miongoni mwa viwanja vya ndege vya kimataifa vilivyo katika eneo la Bahari Kuu ya Hindi. Wa tatu ni uwanja wa ndege wa Shelisheli. Uwanja wa ndege wa Mauritius ni wa pili na wa kwanza ni wa Male Ibrahim Nasir ulio kwenye visiwa vya Maldive.
Viwanja bora vya ndege vilitajwa katika sherehe ya Tuzo za Viwanja vya Ndege vya Dunia iliyofanywa Barcelona, Hispania.
Aliponiletea makala hayo huyo sahib yangu alinikumbusha kwamba wakati wa kilele cha msimu wa watalii mashini ya kukagua mizigo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Karume huko Unguja ilikuwa imeharibika kwa muda wa miezi mitatu. Kwa hivyo, mizigo ilibidi ikaguliwe na wafanyakazi wa uwanja wa ndege jambo lililosababisha misururu mirefu ya wasafiri na kucheleweshwa kupanda ndege zao.
Mei 10 aliniletea makala yenye picha ya kituo kimoja cha mabasi huko Victoria, mji mkuu wa Shelisheli. Makala ya gazeti yalisema kwamba Shirika la Usafiri wa Umma la Shelisheli (SPTC) linawaarifu wananchi kuhusu kubadilika kwa mahala pa kuondokea mabasi kulikosababishwa na kazi ya kuezeka mapaa ya kituo hicho hichi ni kimoja cha vituwo walivyojengewa rai ili wasipingwe na mvuwa au juwaa.
seysheli kituo cha basi
Sahibu yangu alinieleza kwamba visiwa vya Shelisheli vilipopata uhuru 1976 taifa hilo lenye wakaazi 90, 000 lilikuwa na magari ya usafiri kama ya Zanzibar yaliyotengenezwa kwa mbao. Mfano wake ni kama yale tuyaitayo magari ya “matwana” au ya “mbavu za mbwa”. Miaka 15 tu baadaye kikajengwa hicho kituo cha kisasa cha mabasi ambacho hufanyiwa ukarabati mara baada ya mara.
Siku hizi badala ya mbavu za mbwa nchi hiyo ina mabasi 300 ya kisasa ikiwa na vyombo vya GPS. Huduma yote hiyo inatolewa na shirika la umma la SPTC. Huko si kama kwetu; hakuna matwana, hakuna mbavu za mbwa, hakuna matatu, hakuna daladala, hakuna bodaboda, hakuna bajaji.
Alichokuwa akinambia hasa ni kwamba wenzetu, majirani zetu katika Bahari Kuu ya Hindi, wanakwenda mbio na sisi hatuna letu jambo ila balaa na bla bla bla nyingi.
Kabla ya kuingia zama za siasa katika miaka ya 1950 Zanzibar ikijivunia kwa mengi licha ya kutawaliwa na Waingereza. Ubora wa maisha na jinsi watu walivyokuwa wakiishi mitaani ni miongoni mwa mengi yaliyowavutia Watanganyika na wengineo waje kuishi nchi kwetu Zanzibar.
Wengi wakiikimbia kodi ya kichwa ambayo wakoloni wakiwatoza Waafrika katika baadhi ya nchi ikiwemo nchi ya  Tanganyika. Kodi ya kichwa ilikuwa haitozwi katika nchi yetu ya Zanzibar. Wengine wakija kuchuma karafuu au kijitafutia riziki kwa njia nyingine kama walivyo wafrika wa bara zima wanavyo kwenda nchi za marekani,canada,ulaya na hata uwarabuni kutafuta maisha basi ndivyo ulivyokuwa kwa Watanganyika kukimbilia nchini kwetu Zanzibar kutafuta maisha na mpaka leo bado wanakuja halikuwa sisi wenyewe tumaji hahe hohe.
Jambo moja ambalo watu hulisahau ni kwamba katika siku hizo za neema nchi ya Zanzibar ilikuwa ikifuata sera mahsusi ya kiuchumi. Ilikuwa sera ya bandari huru. Dhana ya bandari huru ni kwamba bidhaa zinazoingizwa nchini huwa hazitozwi ushuru wa forodha.
Bandari Huru ni bandari, eneo la bandari au eneo lolote lile jengine ambalo sheria zake za utozaji kodi wa forodha hulegezwa na serikali inayohusika. Maeneo huru ya kiuchumi nayo pia huitwa bandari huru.
Kuna nchi nyingi zilizojitangaza kuwa ni bandari huru au zilizoyafanya maeneo yao fulani yawe na sifa za bandari huru. Miongoni mwao ni
hii ndio singapore leo iko hivi Zanzibar inanuka
Bahrain,Singapori, China, Misri, Liberia, Uturuki, Urusi, Hispania,  Mauritius,Libya, Eritrea, Morocco,  Nigeria na Muungano wa Tawala za Kifalme za Kiarabu (UAE).
Aghalabu bandari huru ni eneo mahsusi la forodha ambalo sheria zake za utozaji kodi za forodha hulegezwa sana au kodi za forodha huwa zinafutwa kabisa.
Sera hiyo iliifaa sana nchi yetu ya Zanzibar kwa vile Zanzibar ni visiwa vya wafanyabiashara wenye kusafirisha bidhaa zao nchi za nje na wenye kuingiza bidhaa nyingi kutoka ng’ambo. Visiwa hivi havikubarikiwa madini wala maeneo makubwa ya ardhi kwa kilimo au ufugaji wa wanyama kama walivyobarikiwa ndugu zetu wa Tanganyika wakoloni weusi.
Watanganyika nchi lote hili haliwatoshi tu....??
Kuyadhukuru haya kunanikumbusha Rasimu ya Katiba kwamba ingawa imewatetea wakulima, wafugaji na wavuvi lakini haikuwatetea ipasavyo wafanyabiashara ambao ni kiungo muhimu katika uti wa mgongo wa shughuli za kiuchumi za nchi yetu ya Zanzibar.
Nadhani wajumbe wa Zanzibar iwapo watarudi katika Bunge la Katiba litapokutana tena Agosti, wanapaswa wahakikishe kwamba vifungu maalumu vinaingizwa katika Rasimu ya Katiba vitavyovifanya visiwa vya Unguja na Pemba viwe ni bandari huru na bandari zisizotoza ushuru ili nasi tuwe na maendeleo.
Vikiwa na sifa hizo Visiwa hivyo vitaweza kuvutia uwekezaji na rasilimali kutoka nje, vitaanzisha ajira mpya na vitawapa wananchi fursa za ajira. Lengo ni kuvifanya visiwa vya Unguja na Pemba ving’are, viwe mfano wa kuigwa katika kanda hii ya Afrika kwa maendeleo yao.
pemba hiyoo
Zanzibar haitotendewa haki endapo Rasimu ya Katiba haitokuwa na vifungu hivyo. Kwa kutokuwa na vifungu hivyo kunaweza kumaanisha kuwa Rasimu ya Katiba itayazingatia maslahi ya wakulima, wafugaji na wavuvi wa Tanganyika peke yao. Kufanya hivyo itakuwa ni kuziendeleza sera za Muungano ambazo zimezoea kuyapuuza maslahi ya nchi ya Zanzibar na kudidimiza nchi yetu isipige hatuwa.
Kuna swali moja ambalo sahibu wangu wa Sweden heshi kuniuliza: kwa nini Zanzibar si mwanachama wa ile jumuiya ya Mataifa ya Visiwa Vidogo Vyenye Kuendelea (Sids)? Mwaka huu alichagiza kuniuliza swali hilo kwa sababu huu ni Mwaka wa Kimataifa wa Sids. Jibu la swali lake bila ya shaka ni kuwa Zanzibar haiwezi kuwa miongoni mwa Sids kwa sababu Serikali ya Muungano haitoiruhusu wakolini weusi Tanganyika.
Mataifa haya ya Sids yalitambuliwa na Mkutano Mkuu wa Ardhi uliofanywa Rio 1992 kuwa ni kundi tofauti la nchi zenye kukabiliwa na vitisho vinavyofanana vya kijamii, kimazingira na vya kiuchumi. Kwa sababu hizo za kimazingira na kimaendeleo nchi hizo zinaonekana kuwa ni zenye kustahili kupewa umuhimu maalumu.
Tangu 1992 nchi za Sids zimekuwa zikishirikiana kuhakikisha kwamba kunapatikana maendeleo endelevu duniani ili mahitaji ya vizazi vijavyo nayo yakidhiwe. Zanzibar ni nchi pekee iliyo katika Bahari Kuu ya Hindi ambayo si mwanachama wa jumuiya hiyo na inayokosa faida zake.
Hii leo nchi ya Zanzibar inahitaji kila msaada inaoweza kuupata ili kuunyanyua uchumi wake. Lakini kubwa linalohitajika ni mageuzi ya kimsingi katika uendeshaji wa serikali na namna viongozi wetu wanavyofikiri na wanavyozipanga na kuzitekeleza sera zao.
Wazanzibari wanatamani nchi yao izipate tena sifa zake za zamani za kuwa kituo cha ubora na bandari huru. Yote hayo mawili yanawezekana lakini lazima kwanza pawepo mageuzi makubwa.
Kweli nchi ya Zanzibar imeanza kupiga hatua katika miaka ya karibuni ukilinganisha na awamu za mwanzo tangu Mapinduzi ya 1964. Siku hizi, kwa mfano, watu wana uhuru wa kusema na wa kukusanyika (ingawa kuna nyakati ambapo wanabanwa banwa).
Hata hivyo, haionyeshi kama Serikali inakisikiliza kilio chao cha kutaka pawepo mageuzi makubwa. Kinachotia moyo ni ile imani waliyo nayo wananchi kwamba siku za nchi ya Zanzibar kuwa na mamlaka yake kamili haziko mbali.

BI ASHA BAKARI MAKAME NA WIMBO WAKE KUWA KAPINDUWA




BI ASHA HAWA NDIO WENZAKO MULIO PINDUWA PAMOJA SIO MWAKA 1964...?????

JE BUNGE LA KATIBA KATETEA NINI KWA WAZANZIBARI KUHUSU MAJI SAFI....??

JE BUNGE LA KATIBA KATETEA NINI KUHUSU WAZANZIBARI KUWA NA UMEME WAO WENYEWE...? SIO UMEME WAKUGAIWA NA WAKOLONI WEUSI TANGANYIKA MPAKA LINI..?

LINI ATATUHISABIA KUWA SASA BEI ZA VYAKULA ZITAPUNGU..??

LINI ATAWAMBIA WAKINA MAMA SASA MUSIWE NA WASIWASI TUMEJENGA HOSPITALI MPYA YANYE VIFAA VYA KISASA KWA WAJA WAZITO...??

JE NILINI ATAITETEA ZANZIBAR KUWA NI NCHI NA SIO WILAYA KATIKA WILAYA ZA TANGANYIKA..??

LINI ATAWAMBIYA WATOTO WA KIZANZIBARI KUHUSU ELIMU NA KUWAPA MOYO KUWA SASA TUNAJENGA SKULI MPYA ZA KISASA NA KOMPUTA KUANZIA DARASA LA KWANZA...???

LINI ATAWAMBIYA WAZANZIBARI SASA KILA NYUMBA ITAKUWA NA MIFEREJI NA MAJI SAFI MASAA 24 YATATOKA....??  HAKUNA HAJA TENA YA VISIMA WALA MFERI MOJA JIMBO ZIMA LINATEKA MAJI HAPO SASA BASI

LINI ATAWAMBIA WAZANZIBARI KUWA NA NYINYI MTAISHI MAISHA MAZURI KAMA ANAYO ISHII YEYE NA WATOTO WAKE NA FAMILIA YAKE..??

CHONDE CHONDE KIDOLE NA MACHO

NJAA IKIWA TUMBONI SIO TATIZO ILA NJAA IKIJAA AKILINI BASI UTAKUWA KULIKOMWENDAWAZIMU MAMA ZIMA OVYOO

HAYA BI ASHA TUDAGANYE ULIVYO SHIKA PANGA NA MTAIMBO SIKU YA MWAKA 1964 NA KUPINDUWA WEWE UMEPINDUWA SIO BI ASHA....??

HAYA HAYA HAYA TENA BI ASHA ATAKA PINDUWA TENA KAMA ALIVYO PINDUWA MWAKA 1964 HAYA HAYA TENA

PUNGUZA HATHABU BI ASHA HEBU KULA KEKI KWANZA UPUNGUZE MUNKARI

USIJALI BI ASHA TUTAKUPIGIA KURA ZETU ZOTE ILI USHINDE TENA UCHANGUZI UJAO NA WANACHAMA WAPYA WANAZIDI KUJITOKEZA NA KUJIUNGA CCM OYEEEE BI ASHA

HONGERA ASHA BAKARI,BALOZI MDOGO WA TANGANYIKA NA SALMIN AWADHI SALMINI KWA KUWAONYESHA WAZANZIBARI MULIVYO MAHASIDI WA SUK NA WAZANZIBARI KWA UJUMLA



WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamesisitiza msimamo wao wa kuwasilisha hoja binafsi ambayo itaamua kama muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) uendelee kutumika au ufutwe kabla ya Uchaguzi Mkuu 2015.
Shinikizo la kusudio hilo, limeendelea kusisitizwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja, uliohudhuriwa na wawakilishi wa CCM.
Miongoni mwa wawakilishi ambao walihutubia mkutano huo ni pamoja na Mnadhimu wa Baraza la Wawakilishi, Salmin Awadhi Salmini na Mtendaji Mkuu wa shughuli za Serikali, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.
Katika maelezo yake, Salmini alisema baada ya kuwasilishwa hoja hiyo katika Baraza la Wawakilishi, baadaye ataipeleka kwa wananchi ili waulizwe kama wanataka kuendelea na mfumo huo au la.
Alisema tayari hoja hiyo imeandaliwa na wakati wowote wataipeleka katika Baraza kwani Serikali ya umoja huo ambayo inajumuisha chama tawala cha CCM na Chama cha Wananchi (CUF) ambayo haijaleta manufaa yoyote kwa Zanzibar, tangu kuanzishwa.
“Tangu kuanzishwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa…hakuna linalofanyika badala yake tunashuhudia matukio ya ajabu ajabu yakiwemo ya vurugu…vifo na watu kuhujumiwa kwa kumwagiwa tindikali,” alisema Salmin.
Salmini ambaye ni mwakilishi wa CCM Magomeni alisema hivi sasa, CUF hawana amani tena baada ya kusikia CCM inataka kupeleka hoja hiyo kwenye Baraza kwani kuidhinishwa kwa Serikali hiyo kulitokana na hoja binafsi na wao watapeleka hoja binafsi.
Aliwataka viongozi wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUWAMAZA) kuacha kuchanganya dini na siasa kwani kufanya hivyo ni kutaka kuanzisha vurugu na kuhatarisha amani na utulivu ndani ya nchi.
Aliongeza, viongozi hao wanastaajabisha sana kwa kupeleka barua kwa Rais, wakimtaka asikubali kusaini hoja hiyo wakidai Serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyopo, ina amani na utulivu.
“Leo kwa kuwa tunataka kupeleka hoja binafsi ya kutaka kuvunjwa Serikali hii…JUWAMAZA wana wasilisha barua kwa Rais…haya matukio yote ambayo yametokea ya kujeruhiwa na kuuliwa viongozi wa dini ya Kikristo pamoja kumwagiwa tindikali viongozi mbalimbali wa dini hawakuyaona…sasa walikuwa wapi…mbona hawakutuma barua,” alihoji Salmini.
Naye Mwakilishi wa Viti Maalumu, Asha Bakari Makame alisema wameamua kupeleka hoja hiyo kwa sababu Serikali ya Umoja wa kitaifa haina maana na uwezo wa kuiondoa wanao .
Kwa upande wake, Balozi Seif Ali Iddi aliwataka wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) waliotoka nje ya Bunge Maalumu la Katiba warudi bungeni, ili wajumuike na wenzao kujadili na kutetea muundo wa Muungano wanaoutaka kwa kujenga hoja.
Alisema CCM hawabadiliki na hawatarudi nyuma bali wataendelea kutetea muundo wa Muungano wa Serikali mbili kama katiba ya CCM inavyoeleza. Hivyo ni vyema warudi bungeni kutetea muundo wanaoutaka na wao watetee muundo wao badala ya kutafuta visingizio.
“Kitendo walichokifanya UKAWA kutoka nje ya Bunge na kuanza kupita mitaani hakiwasaidii kwani Katiba ya nchi haitungwi mitaani wala katika mikutano ya hadhara inatungwa katika Bunge ambalo ni chombo kilichowekwa maalumu kufanya kazi hiyo,” alisema na kuongeza:
“Nawaomba vijana msikubali kushawishiwa na kuingia katika mambo ambayo hayataleta manufaa kwenu bali yatawaingiza katika vurugu na kuvunja amani na utulivu uliopo ndani ya nchi,” alisema Balozi Seif.
Alisisitiza kuwa lazima vijana wawe macho na watu wa aina hiyo kwa sababu wanataka kuwaletea vurugu ndani ya nchi sambamba na kuwataka wanawake kuwaunga mkono katika Uchaguzi Mkuu 2015 kwani wanawake ndio nguzo kuu wanayoitegemea kukiletea ushindi chama hicho.

Wednesday, June 11, 2014

VIDEO-WAZANZIBARI HATUTAISAHAU SIKU HII KISHA RAISI WA KISONGE ANASEMA NCHI INAKILA KITU MBONA HATA COASTI GADI WAKUOKO WATU BAHARINI HATUNA TUNAOKOLEWA NA WAVUVI...???

M,MUNGU AWALAZE PEMA PEPONI DUGU ZETU WALIO TANGULI NA SISI TULIOBAKI M,MUNGU ATUSALIM SALAMA

SH 150,000 KWA SIKU MBALI MSHAHARA SH 4.5 MILLIONI KWA MWEZI KWA KILA MJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI NA WALA HAWAHUTHURI VIKAO NA NCHI INANUKA




Nchini Zanzibar. Kikao cha Baraza la Wawakilishi nchini Zanzibar (BLW), kimeahirishwa kwa mara ya pili kutokana na idadi ya wajumbe kutokuhudhuria vikao na kushughulikia miradi yao kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa chombo hicho cha kutunga sheria,nchini Zanzibar.
Kikao hicho kiliahirishwa na Naibu Spika, Ali Abdallah Ali jana saa kumi na moja jioni baada ya Mwakilishi wa Mji Mkongwe (CUF), Ismail Jussa Ladhu kutoa hoja kutokana na mahudhurio ya wajumbe kutokamilika.
Jussa alisema BLW Zanzibar linaendeshwa kwa kuzingatia kanuni na suala la kukamilika kwa idadi ya wajumbe wanaotakiwa limepewa uzito na chombo hicho na kumtaka Naibu Spika kutoa hoja kutokana na hali iliyojitokeza.
“Mheshimiwa Naibu Spika, chombo chetu kinaongozwa na kanuni, idadi ya wajumbe iliyopo ni ndogo kimuonekano na hesabu yake, naomba kutoa hoja na kupendekeza kikao kiahirishwe kutokana na upungufu huo,” alisema Jussa.
Baada ya kuwasilisha hoja hiyo, Naibu Spika aliungana na Jussa na kuahirisha kikao hicho hadi leo asubuhi.
Baraza hilo lilikuwa liketi jana jioni kama kamati ya matumizi kupitia na kupitisha vifungu vya matumizi ya Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto ya Sh7.5 bilioni ambayo yaliwasilishwa na Waziri wake, Zaynab Omar Mohamed.
Mara ya kwanza kuahirishwa kwa kikao hicho kutokana na akidi ya wajumbe wake 82 kutokuhudhuria katika vikao  ilikuwa Mei 26, mwaka huu. Hadi kikao hicho kinaahirishwa kulikuwa na wajumbe 26 na wengine hawajulkani waliko wala wamefikwa na nini wala hawajaeleza ni kwa nini hawakuhudhuria vikao.
Baadhi ya wajumbe wa BLW nchini Zanzibar wamekuwa wakitumia usafiri wa daladala kwenda na kurudi kutoka kwenye kikao hicho na wengine kutofika kwa muda mwafaka tangu kufanyika kwa mabadiliko ya vituo vya usafiri huo katika Manispaa ya Mji wa nchi ya  Zanzibar ati hicho ndio kisingizio.
Wajumbe wa Baraza hilo kila mmoja hulipwa posho ya kikao ya Sh150,000 kwa siku mbali na mshahara wa Sh4.5 milioni kwa mwezi.
sibora basi hiyo mishahara yao ikatwe na pesa zinunuliwe vitanda vya hospitali au tuanzishe umeme wetu wenyewe au maji safi lakini wapi nchi hii kama iliyo laniwa astahafiri allah.