Saturday, May 4, 2013

MR SIMUOGOPI MTU ASEMA-ELIMISHENI WANANCHI JUU YA MAPINDUZI NA MUUNGANO.


MUUWE WATU MUTHULUMU WATU MUWABAGUWE WATU KISHA MUJIDAI KUOMBA DUWA YAGUJUUUUUUUUUUU.MR SIMUOGOPI MTU NA DUWA YA MKEKA

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein ametoa wito kwa viongozi wa chama hicho kuwa na mpango maalum wa kuelimisha jamii mara kwa mara kuhusu historia na malengo ya Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 pamoja na Muungano wa Tanzania wakati wote badala kulifanya jambo hilo kuwa la msimu.
Dk. Shein ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alitoa wito huo jana wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama hicho huko Kinduni Wilaya ya Kaskazini ‘B’ katika mkutano wa majumuisho ya ziara yake ya kichama ya siku mbili katika mkoa wa Kaskazini Unguja.
“Tuwe na mpango maalum kwenda kwa wananchi hasa vijana kuzungumzia Mapinduzi na Muungano wetu isiwe kwa msimu kwa sababu tunapokuwa kimya tunatoa fursa kwa wengine kusema wayatakayo na kupotosha umma”alisema Dk. Shein.
Sambamba na wito huo Dk. Shein aliwataka viongozi hao kuwaelimisha pia wanachama wa chama hicho na wananchi kwa jumla Katiba na Sheria ili kuwaepusha na kufanya vitendo vya uvunjaji sheria kutokana na kukosa ufahamu wake. “Tuwaelimishe wanachama wetu Katiba na Sheria ili kuwaepusha na kuingia katika matatizo ambayo yanatokana na kutojua sheria na Katiba ya nchi”alieleza Dk. Shein.
Alifafanua kuwa imedhihiri katika baadhi ya matukio ya uvunjifu wa amani baadhi ya vijana wameingia kwa kufuata mkumbo bila kufahamu kuwa wanavunja sheria za nchi na kutahamaki wako katika mikono ya vyombo vya dola.
Dk. Shein aliwataka viongozi wa CCM kwenda kwa wananchi kutangaza mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ili wasiwape nafasi watu wengine ambao wameamua kujipa sifa ambazo hawastahiki.
Aliongeza kuwa mafanikio hayo yameifanya Zanzibar kuwa kipenzi cha washirika wa maendeleo ambao wamekuwa bega kwa bega kusaidia jitihada za Serikali za kuimarisha maendeleo na ustawi wa wananchi wa Zanzibar. “Wahisani wetu wameridhika na jitihada zetu za kuwatumikia wananchi na ndio maana kila mara wamekuwa wakija nchini kwetu kuzungumza masuala mbalimbali ya ushirikiakiano kati ya nchi yetu na nchi zao”alisema.
Kwa hivyo aliwahimiza viongozi kuelimisha wanachama na wapenzi wa CCM juu ya Ilani ya Uchaguzi na Mwelekeo wa Sera ya Chama hicho kwa miaka 2010 hadi 2020 ili waweze kukieleza vyema chama hicho mbele ya umma.
Katika mkutano huo Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM Zanzibar alirejea tena wito wake wa kuwataka wananchi wasivunje sheria kwa makusudi kwa kujenga hisia kuwa Serikali inawaogopa. “Watu wanaofanya vitendo hivyo wasidhani wako juu ya sheria. Ninawakumbusha kuwa hakuna mwananchi aliye juu ya sheria nikiwemo mimi mwenyewe ninayeongoza Serikali”alisisitiza Dk. Shein.
Alibainisha kuwa yeye akiwa Rais anaendesha nchi kwa kufuata Katiba na Sheria ya nchi na kuongeza kuwa hamuogopi mtu katika kuongoza Serikali lakini anapaswa kumheshimu kila mwananchi na ndivyo anavyofanya kuwaheshimu wananchi wote. “Zanzibar kuna Serikali ya Mapinduzi na inaongozwa na Rais anayetoka CCM. Katika kuiongoza Zanzibar simuogopi mtu bali namheshimu kila mwananchi kwa kuwa ni wajibu wetu kuheshimiana” Dk. Shein alieleza.
Makamu Mwenyekiti wa CCM aliupongeza ushirikiano na mshikamano mzuri wa uongozi baina ya Chama cha Mapinduzi na Serikali mkoani humo na kutoa wito kuimarishwa zaidi ushirikiano huo kuongeza ufanisi wa utendaji.
Mapema akizungumza kumkaribisha Dk. Shein Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai alieleza kuwa katika ziara ya siku mbili mkoani humo Chama cha Mapinduzi na jumuiya zake kimeweza kuingiza wanachama wapya 4865 miongoni mwao 2996 ni wa CCM na 1869 ni wa jumuiya zake.
Vuai alimshukuru Dk. Shein kwa kueleza kwa uwazi na kutetea Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 na Muungano ambapo alitoa wito kwa viongozi wengine wa chama hicho wakiwemo mawaziri, wabunge, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pamoja na madiwani kuyazungumzia masuala hayo kama ambavyo Makamu Mwenyekiti amekuwa akifanya.
Katika ziara hiyo ya chama ambayo ni ya kwanza tangu achaguliwe kushika wadhifa wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Shein aliweka mawe ya msingi ya majengo ya ofisi za chama hicho ngazi ya matawi na jimbo pamoja na maskani.
Dk. Shein anatarajiwa kuwasili kisiwani Pemba Jumapili ambapo Jumatatu ijayo atazindua mbio za Mwenge wa Uhuru katika sherehe zitakazofanyika huko katika kijiji cha Chokocho Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba na baadae kuendelea na ziara ya kichama katika mikoa miwili ya Pemba kuanzia Jumanne ijayo.
FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI TUNAKULIZA WEWE MR SIMUOGOPI MTU NI SHERIA GANI HIYO UNAYOPITA UKINADI KILA MAHALI AU KATIKA KATIBA YA  NCHI YATU YA ZANZIBAR NI PAHALI GANI PANAMO SEMA UWAFUNGE JELA MASHEIKH NA KUWANYIMA THAMANA..???
FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI PIA TUNAKULIZA KAMA WEWE MR SIMUOGOPI MTU KWELI KWELI KWELI HUMUONGOPI MTU MBONA UMEWAFUNGA JELA MASHEIKH..???
HUONI KAMA HII NI DALILI KUWA UNAWAOGOPA NDIO UKAWAFUNGA JELA ILI UPATE USINGIZI MAANA WALIVYOKUWA NJE ULIKUWA HULALI AU NI UWONGO HIVI TUNAVYO KULIZA...???

No comments:

Post a Comment