Jumuiya za Chama cha Mapinduzi UVCCM, UWT na Wazazi zinakusudia kuwajengea uwezo Vijana ili kujinasua na hali ngumu ya kimaisha kwa kuwasomesha kupitia Skuli za Wazazi na Elimu ya Amali ili waweze kujiajiri wenyewe. Zimesema Vijana watakapopata Elimu hiyo itawasaidia kuweza kujiajiri na kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira linaloendelea hapa nchini.
Naibu Katibu mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanganyika (Tanzania) UWT Salma Abuod Talib ameyasema hayo huko Makao makuu ya CCM nchini Zanzibar Kisiwandui alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kupongeza mafanikio ya ziara ya kichama iliyofanywa na Dkt.Kumbi Shein au Mr Simuogopi mtu.
Amesema Mafunzo ya Amali yatawasaidia Vijana kuondokana na fikra za kutegemea ajira Serikalini na kuwawezesha kujiajiri wenyewe badala ya kutegemea Serikali.
Akizungumzia ziara hiyo Bi Salma amesema ziara ya Dkt.Kumbi Shein au Mr Simuogopi mtu imekuwa na mafanikio makubwa kwani imeweza kuongeza wanachama wapya jambo ambalo ni ishara ya wazi ya uhai na matumaini ya ushindi wa Chama hicho katika chaguzi za baadae .
Amesema katika hali hiyo kuna haja kubwa kumpongeza kiongozi hiyo kwani ametoa picha ya kufanikiwa kukiimarisha chama na kukiletea maendeleo hapa visiwani nchi Zanzibar kwa ujumla.
“Jumuiya za Chama cha Mapinduzi (UVCCM , UWT na Wazazi) tunampongeza kwa dhati kabisa kuwa mjasiri wa kutembea bila kuchoka na kuwa tayari kutumika kila ambapo alitakiwa ushiriki wake, inaonesha wazi kuwa Makamu Mwenyekiti wetu ni mtu wa watu na anapenda watu pamoja na maendeleo yao” amesema Bi Salma.
Aidha alisema katika ziara hiyo Dkt.Kumbi Shein au Mr Simuogopi mtu alikagua na kutembelea miradi ya CCM ambapo miradi 35 iliwekewa jiwe la msingi na kuziduliwa zikiwemo SACCOS mbali mbali na Vikundi vya Ushirika.
Akizungumzia sintofahamu iliyopo katika baadhi ya Majimbo Bi Salma alisema CCM imepanga kufanya vikao vitakavyojumuisha viongozi wa Majimbo wakiwemo Wabunge na Wawakilishi pamoja na wananchi wao ili kuimarisha utendaji wao.
Amesema vikao hivyo vitatoa mustakabali mzuri kwa viongozi hao na kuweza kuwatumikia wananchi walio wachagua katika hali inayofaa.
Jumla ya Wanachama wapya 5,448 kutoka vyama mbali mbali vya siasa wamejiunga na Chama cha Mapinduzi kufuatia ziara ya Makamo Mwenyekiti wa chama hicho Dkt.Kumbi Ali Mohammed Shein au Mr Simuogopi mtu aliyoifanya hivi karibuni kutembelea mikoa mitano ya Unguja na Pemba kwa lengo la kuangalia na kukipa uhai Chama cha Mapinduzi na Jumuiya zake.
No comments:
Post a Comment