Wednesday, July 20, 2016

PART 6 MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD ANAENDELEA NA ZIARA YAKE HUKO NCHINI UHOLANZI
Maalim Seif Sharif Hamad na ujumbe wake wamewasili mjini Amsterdam, nchini Uholanzi leo, Jumatano tarehe 20 Julai, 2016 saa 8 mchana tayari kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi nchini hapa.
Maalim Seif na ujumbe wake walitumia usafiri wa treni kutoka Brussels, nchini Belgium hadi Amsterdam ambapo safari yao ilichukua muda wa takriban saa tatu.
Kesho asubuhi, Maalim Seif na ujumbe wake watalelekea The Hague ambako watakuwa na mikutano minne.

No comments:

Post a Comment