ZANZIBAR TUITAKAYO AKIPENDA M.MUNGU
Baada ya kumaliza ziara ya Uingereza, leo hii Maalim Seif Shariff Hamad akiwa na ujumbe wake wameanza ziara ya kikazi ya siku mbili mjini Brussels, nchini Ubelgiji ambayo imelenga kukutana na viongozi wa Umoja wa Ulaya (European Union - EU) na wale wa Serikali ya Ubelgiji.
Saa 4 :00 hadi 5:30 asubuhi leo, tarehe 19 Julai, Maalim Seif na ujumbe wake walikuwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Ulaya (European Union - EU) ambako walikutana na Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Afrika (Managing Director of Africa Department) wa Umoja huo, Bw. Koen Vervaeke, Mkuu wa Divisheni ya Nchi za Pembe ya Afrika, Afrika Mashariki na Bahari ya Hindi, Bibi Claudia Wiedey, na Ofisa wa Mahusiano ya Kimataifa anayeshughulikia nchi za Uganda na Tanzania, Bibi Márta Szilágyi pamoja na mwakilishi wa Kitengo cha Utatuzi wa Migogoro.
Pichani ni Maalim Seif akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Afrika katika EU, Bw. Koen Vervaeke, baada ya kumaliza mkutano wao.
No comments:
Post a Comment