MIAKA 50 YA UHURU WA NCHI YA TANGANYIKA NA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA NCHI YA ZANIBAR MAJI 20% UMEME 20% ELIMU 0% HOSPITALI 1% MADAWA 0% MLO MOJA KWA SIKU TAFAKARI SANA.CCM MNASHANGA LOWASSA KUPANDA DALADALA HAMSHANGAI TWIGA KUPANDA NDEGE.VIONGOZI WA CUF WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI 2015 WAKIONYESHA SHAHADA ZAO ZA USHINDI ZILIZO SAINIWA NA KUPIGWAMUHURI NA ZEC CCM HAYA HAMUNA,AIBU HAMUINI,FEDHEHA HAMUHISI,UBINADAMU UMEWATUKA,M.MUNGU HAMUMUOGOPI HEBU JIULIZENI NYINYI VIUMBE WA AINA GANI...?????
Friday, March 23, 2012
JE CUF NCHINI TANGANYIKA ITAINGIA IKULU AU ITABAKI TU KUISHI BADA LA UWANI...????
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba amesema inawezekana kabisa kwa kila mtanzania kulipwa sh. 450,000 kwa mwaka zinazotokana na rasilimali za asili.
Akizungumza na wanachama na wafuasi wa chama hicho kwenye viwanja vya Mwembeyanga Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema watanzania watalipwa fedha hizo kama watakiingiza kwenye katiba mpya kipengele hicho.
“Tanzania kuna rasilimali za asili nyingi, bahari, gesi, madini ya dhahabu, tanzanite, mbuga za wanyama na nyingine nyingi ambazo zinaweza kuingia sh. bil. 2 kwa mwaka ambazo zinatosha watanzania kukagawana sh. 450,000 kwa mwaka” alisema.
Alisema wafuasi wa CUF wasitishike na helkopta zinazoranda kwenye chaguzi kuwa vyama hivyo havina uwezo wa kuleta mabadiliko kwa watanzania ambao wamekata tamaa kutokana na kukosa ajira.
“CCM na vyama vingine vinavyoongozwa na wapiga disko haviwezi kuwakombioa watanzania akimaanisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambacho Mwenyekiti wake anamiliki ukumbi wa Billicanas.
Alisema uchumi wa Tanzania unazidi kuwa taabani kwa sababu gharama za kuyingia tani 100 kutoka China ni nafuu kuliko kusafirisha tani moja kupeleka mkoa wa Kigoma na kuongeza kuwa rasilimali ambazo Tanzania inazo zinakosa viongozi wa kuzisimamia na badala yake zibnaingia kwenye mikono ya mafisadi.
Profesa Lipumba hata hivyo alimsifu Rais Jakaya Kikwete kukubali kuruhusu uundaji mchakato wa kuanzisha Katiba Mpya na kuongeza kuwa napaswa kuungwa mkono.
Alisema ili mipango hiyo itimie watanzania wote wakubali kujiandikisha kupewa vitambulisho na kuchangia kuundwa kwa Katiba mpya ambayo itasema kila mtanzania alipwe rasilimali za nchi.
Awali Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad alisema wanaopiga kelele kuwa CUF imekufa wanajidanganya kwa sababu mapokezi wa Profesa Lipumba Machi 11 mwaka huu ni ushahidi tosha kuwa chama hicho hakitakufa kamwe.
“Mimi nilitoa machozi baada ya kuona umati mkubwa ulijitokeza kumpokea Mwenyekiti wetu, hiyo ni salamu kwamba tumeanza mikakati ya kuingia Ikulu, tumeingia mguu mmoja Zanzibar, mwaka 2015 tunaingia miguu yote je, Ikulu ya magogoni mnasemaje?aliuliza Maalim Seif na kuitikiwa na sauti kuwa CUF inachukua dola.
Katika mkutano huo CUF imetoa namba 15338 kwa njia ya mtandao wa zantel ambayo mwanachama wake atachangia kwa ajili ya kujiandaa na uchaguzi wa 2015 ambako pia aliywahi kuwa kiongozi wa chama hicho na baadaye kuhamia CCM, Bw. Hamisi Kituga amerejea katika chama hicho
Wakati huo aliyekuwa naibu mkurugenzi wa uchaguzi wa CUF taifa Bw. Khamis Katuga ambaye alikihama chama hicho na kuhamia CCM, amerejea tena CUF ambapo amerejesha kadi ya CCM na kukabidhiwa kadi ya CUF.na Mwenyekiti Profesa Lipumba.
Ametahadharisha kuwa tatizo kubwa linalorejesha nyuma maendeleo ya chama hicho ni kutokanyika kwa vikao katika ngazi ngazi mbali mbali, huku akieleza sababu zilizomrejesha tena CUF kuwa ni uimara na sera zinazotekelezeka za chama hicho, huku akifunga maelezo yake kwa usemi “asiyejua kufa achungulie kaburi”.
Pia Mjumbe wa baraza Kuu la Taifa la chama hicho kutoka mkoa wa Mbeya, Bw. Yassin Mrotwa ambaye alikuwa mmoja wa wanachama walioshtaki mahakamani amejitoa na kurudi CUF.
Wednesday, March 21, 2012
WABARA WALIOKUWEPO ZANZIBAR WAZIDISHA FITINA KTK MASKANI ZA CCM UNGUJA
HUU UBAO NIMEUPINGA PICHA KTK MASKANI MOJA YA CCM HAPA UNGUJA LAKUJIULIZI NI KUWA MUUNGANO NI WA UNGUJA NA TANAGANYIKA MBONA KURA YA MAONI TULIPINGA SISI UNGUJA NA PEMBA NA SIO TANGANYIKA NA UNGUJA..?PIA SASA NDIO WASHAJUWA KUWA WAZANZIBAR HAWATAKI TENA KUTANIWA WANATAKA NCHI YAO NDIO WANAJIAFANYA ATI WAO NA UNGUJA NI WAMOJA NA WAPEMBA WARUDI KWAO LAKUJIULIZA WAKURUDI KWAO NI NANI MPEMBA AU MTANGANYIKA ALIYE TUVAMIA 1964 NA KUTUUWA KWANZA HAPA UNGUJA KISHA WAKAMTUMA JOHN OKELLO MGANDA AENDE KUWAMALIZA DUNGU ZETU PEMBA VIBAYA VIBAYA JE NI YUPI WA KURUDI KWAO..?WAZANZIBAR TUWE MACHO TUWE MACHO KWELI KWELI TUSIMPE NAFASI MKOLONI MWEUSI KUTUGAWA TUSHIKAMANE MPAKA ATOKA WALA TUSICHOKE KUELIMISHANA KTK KILA HALI.UKIANGALI HUU UBAO UNAONA AHAA SIO NENO ILA HII NI SUMU TENA SIO DOGO KABISA KWA HIO TUWE MACHO WAZANZIBAR TUWE MACHO.
Thursday, March 8, 2012
DR MWINYE HAJI MAKAME AULIZWA SWALI LAKITOTO AJIBU UTUMBO NA KUSIMAMISHA UMAPINDUZI USIO NA MSINGI KWELI DR SHEIN ZANZIBAR NDIO ITAENDELEA.....?
Wachaa niazie hapa tokea mabadiliko makubwa ya kisiasa ya 1964 kufuatia Mapinduzi nimekuwa
nikisema mara nyingi Zanzibar kama nchi ilishindwa kuandaa mikakaati ambayo
ingesaidia kuondosha tatizo la chuki za kisiasa zilizojengeka kabla ya
Mapinduzi hayo.
Chuki za Zanzibar Nationalist Party ZNP, Zanzibar and Pemba Peoples Party
ZPPP kwa upande mmoja na upande mwengine ikiwa ni chama cha ASP, nja ambazo
zilifikia kilele pale vyama hivyo vilipouungana na kuchanganya kura zao na
kwa hivyo kuchukua Serikali ya kwanza ya Uhuru hapo 1963.ikiwa zanzibar ni nchi huru kabisa.
Ubaya ni kuwa chuki hizo zimeachwa zikuwe na zimee, pengine wengine
wamekuwa wakifaidika nazo na ndipo maana mpaka leo tuna serekali ya (SUK)LAKINI BADO MIJITU KAMA HII DR MWINYI HAJI MAKAME inataka kuirudisha chuki na hasama ili wao wale wananchi wateseke na pia zikajitokeza zaidi wakati siasa za vyama vingi 1992 ziliporudi na kuzagaa kwa hatari sana hata katika kizazi kipya ambacho hakikuwa kikijua ZNP, ZPPP wala Afro Shirazi zaidi ya ngano
walizokuwa wakisikia.Chuki hizo zilipelekea maovu mengi kutokea katika jamii na familia abayo hata hayasimuliki kabisa ni aibu haswa kwa kikwetu hapa zanzibar lakini yametokea. Mizizi yake iliingia katika uendeshaji wa Serikali ambapo mtu yoyote ambaye angedhaniwa asie wa chama kilicho madaraka imemuia vigumu kupata ajira au kupata cheo.Baada ya muda mrefu na jamii na nchi kutanabahi kuwa tumekuwa tukienda kusiko na hilo si jambo la tija kwetu, viongozi wawili wakuu wa vyama kinzani, Dk Amani Karume na Maalim Seif Shariff ambavyo kwa sababu zisizo za msingi vilikuwa vikiendelea kuhusisha na siasa za kabla Mapinduzi vilipoamua kuwa imechosha na imetosha.Wakasema chuki na ubaguzi iwe basi. Wakasema ni hatari kwa maslahi na mustakbali wa nchi ambapo athari yake ilionekana pia katika kila msimu wa
uchaguzi kwa kukosekana mshindi aliyepata imani ya nchi na kwa hivyo kuwa vigumu kushika hatamu za uongozi.Wakachoka kuonekana kila siku kuna magomvi katika nchi na kuona nchi inaendelea kugawika nusu kwa nusu na kuwa wanaofaidi fursa za nchi ni upande mmoja tu wa siasa na mwengine ukiula huu,chembilecho msemo maarufu wa Mombasa hapo zamani.Lakini wiki tatu nyuma nilibahatika kuwasilisha makala katika semina ya REDET ambapo nilitakiwa nitizame suala la ushirikishi tokea kuundwa kwa Serikaliya Umoja wa Kitaifa (SUK) , ambayo moja ya jukumu lake lilikuwa au
lingekuwa kujaribu kumaliza suala la ubaguzi ndani ya jamii kutokana na siasa.Ilikuwa ni fikra yangu kuwa hapana juhudi maalum iliyochokuliwa kuhakikisha chuki kama hizo zinazikwa na ndio maana hakuna kikubwa kilichobadilika kwa sababu ushiriki wa kujenga nchi bado una masharti na unalalia upande mmoja
na hilo linaiweka SUK njia panda.Katika mkutano huo ilitokana kauli ambayo mpaka leo inanitetemesha pale
nilipotoa hoja ya kukata mizizi ya ubaguzi kwa kuondosha kipingamizi cha Wazanzibari wasio na asili ya Kiafrika kuweza kujiunga na vikosi vya ulinzi kama watapenda, lakini kauliya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Mustafa Muhammd kusema, “ Haiwezekani kwa bunduki na risasi kupewa kwa mpinzani.”Ilibidi nifungue darasa kuelezea tofauti ya mpinzani na raia. Kwamba raia wote katika nchi wanatakiwa wawe na haki sawa bila ya kujali asili zao, na nikatoa mfano wa Marekani ambapo hata raia wenye asili Iran wana haki
kamili ya kuingia jeshini.Kumbe kauli ya kiongozi huyo bado inaashiria kuwa hali haijabadilika ndani
ya jamii na kuwa bado chuki za kisiasa zipo na mara hii zikijitokeza kupitia kiongozi ambaye ni Waziri tena katika Ofisi ya Rais, Dk. Mwinyihaji Makame.Katika sehemu kubwa mno ya maisha yangu nimekuwa nikibaguliwa hapa Zanzibar. Nimefukuzwa kazi, nimezuiliwa kuingia sehemu kadhaa, nimetishiwa
maisha hadharani hata mbele ya Rais Mkapa, nimebandikwa majina mengi,lakini hili alilonifanyia Waziri Dk Mwinyihaji nimeshindwa kulistahamilia kwa sababu nilikuwa najaribu kujenga imani kwamba ubaguzi unaondoka, ingawa najua bado upo.Nilisikitishwa kauli ya ubaguzi kutoka kwa Waziri ambaye ni msaidizi muhimu wa Rais na bila kisisi, aibu wala majuto yoyote akatoa kauli kama jambo la kawaida tu, kitendo ambacho kimedhihirisha labda pengine yeye si muumini mzuri wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo msingi wake mmoja ni kuondosha ubaguzi wa kisiasa.Tulikuwa katika mkutano wa waandishi wa habari ambapo Dk. Mwinyihaji alikuwa akikaimu nafasi ya Waziri wa Fedha na kuitishwa kueleza hali ya
nishati ndani ya nchi ambapo kulikuwa na uhaba mkubwa wa petroli.Nilimbana Waziri katika hoja mbili. Kwanza kitendo cha Serikali kukaa wiki mbili bila taarifa ya si uhaba bali ukosefu wa nishati hiyo na nikasema hilo haliwezi kukubalika. Pili nilijaribu kujenga hoja kuwa uchumi wa nchi ulisimama nikimtaka Waziri atoe takwimu Serikali imekosa mapato kiasi gani na uchumi umeathirika kiasi gani nikitaka takwimu.
Kwa kiasi kikubwa mkutano huo ulikuwa mkali na mimi na mwandishi Salma Said tukawa hatumpi Waziri nafasi ya kuvuta pumzi, na kwa kiasi aliona huo ni utovu wa nidhamu kwa kuwa pengine amezoea mikutano ya waandishi wa habari ambapo anasema mpaka anakwisha bila ya kukatishwa au kutupiwa suala la
kumkinza. Katika hili nafikiri anapaswa kupata mafunzo upya.Basi Waziri hakuweza kuchukua na usthamilivu ukamshinda na hapo akajivua gamba na kujionyesha rangi zake halisi, Ah…utanambia nini bwana…nyie
kama baba mmoja mama mmoja mna yenu mengine twambieni….sio haya bwana. Sote((anaposema sisi sote wazanzibar kuna mtu kamuliza kama wewe sio mzanzibar au anajishuku)) Wazanzibari bwana msitudanganye bwana…Wewe Buto (albarto yaani ally saleh) nakufahamu toka uko wapi mpaka leo…na huyu (mwandishi salma said)nakufahamu toka zamani mpaka leo”Sote Wazanzibari bwana msitudanganye. Wewe
Albarto nakufahamu toka uko wapi huko mpaka leo…na wewe Salma nakujua
uzuri…”Kwa hakika nilimuonea huruma sana Waziri Dk. Mwinyihaji kwa kuwa mpaka leo
ana fikra kuwatizama watu kwa kuamini anawatia kwenye dema la kisiasa.badala ya kujibu swali alilo ulizwa. Kwa wageni wa siasa za Zanzibar alichokusudia kusema Dk Mwinyihaji kuwa anatua
kwamba mimi na mwenzangu anatuhusisha na chama cha CUF na kwa hivyo ni wapinzani hata sasa ambapo CUF imo ndani ya Serikali.je upinzani ni haramu au ndio moja ya njia ya kujenga nchi...?Upande mwengine niliumia kuona kuwa bado kunaweza kuwa na mawazo kama hayo miongoni mwa watu ambao Dk. Ali Muhammed Shein amewapa vyeo vya uwaziri na unajiuliza kwa mtizamo huu nchi inakwenda wapi na kweli ubaguzi nchi hii utaondoka....???????????
Thursday, March 1, 2012
NJAMAA ZA KUTAKA KUWAUWA WAPEMBA KWA KUTUMIYA MELI ZAENDELEYA
ABIRIA zaidi 400 wamekwama baada ya meli ya Mv. Maendeleo iliyokuwa inasafiri kutoka Unguja kwenda Pemba kushindwa kushusha abiria kwa kutoka na kuchaka kwa meli hiyo na ubovu limekwama baharini na dungu zetu wamo ndani ikielekea, Kisiwani Pemba hapo jana. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa watu waliokuwa ndani ya meli hiyo waliozungumza na gazeti hili kwa njia ya simu walisema meli hiyo ilipoteza muelekeo na kuingia sehemu ambayo ilipelekea kukwama na mashine kuzima kabisa.
Meli hiyo inayomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ilipoteza mwelekeo wakati inajiandaa kuikaribia pemba na kusimama kwenye kina kifupi cha maji ambapo palikuwa na mchanga na mashine kunyamaza kabisa.Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar (ZMA), Abdallah Hussein Kombo alithibitisha kukwama kwa meli hiyo kwenye eneo lenye kina kifupi cha maji ambapo alisema tukio hilo halikuweza na hakujasababisha madhara yoyote kwa abiria waliokuwemo ndani ya meli hiyo wala hakuna athari kwa meli yenyewe.“Taarifa zilizopo ni kuwa abiria wote zaidi ya 400 wako salama, na hakuna athari zilizopatikana katika tukio hilo ” alisema Kaimu Mkurugenzi huyo.Kaimu huyo alisema meli hiyo iliingia kwenye kina kifupi cha maji wakati inageuza mwelekeo kuelekea baharini baada ya kukaribia bandari ya Mkoani ikiwa ni hatua ya awali ya kujiandaa kushusha nanga na hivyo kuingia sehemu ambayo baadae ilikwama.“Meli inapokaribia bandarini inaogozwa na boya, lakini inavyoelekea boya lilisukumwa na maji likahamia kwenye kina kifupi na kusababisha meli kwenda huko na kukwama,alisema Kombo.
Kepteni wa meli hiyo alikuwa ni Hamad Suleiman Kombo na kwamba mbali na kubeba zaidi ya abiria 400 pia ilikuwa na wafanyakazi 19 wanaifanya kazi ndani ya meli hiyo.Wakizungumza kwa njia ya simu baadhi ya abiria waliokwama ndani ya meli hiyo walisema walikuwa na khofu kubwa kutokana na kuwa wahusika wa meli hiyo hawajasema lolote kwa abiria wao jambo amablo lilizusha khofu kubwa kwa miongoni mwa abiria.
Walisema tatizo lililokuwemo ndani ya meli hiyo kulikuwa na joto kali, ukosefu wa maji huku chakula kikikosekana jambo ambalo lilizusha zogo kubwa kutokana na wanawake wengi kushitushwa na hali hiyo huku watoto wakilia ovyo kutokana na hali ya joto kali lililokuwemo ndani ya meli na hakuna maji wala vyakula.“Sijui tumo abiria wangapi lakini kwa kweli naona meli imejaa sana lakini hilo joto na kuwa hakuan chakula wala maji ya kunywa ndani ya meli hii ati meli ya serekali na sisi tuliondoka Unguja saa 3 usiku basi tumechoka sana na mabaharia hawatuambi kitu tumekaa tu ndani ya meli hatujui chochote kianchoendelea khofu ndio inazidi maana mtu akitafunwa na nyoka hata ukuti ukikugusa huwa anauogopa…. Na sisi wazanzibari tushatafunwa na hatujasahau bado” alisema Asha Mkaazi wa Machomanne Kisiwani Pemba aliyekuwemo ndani ya meli hiyo akizungumza nasi kwa njia ya simu.Aidha wananchi waliokuwepo ndani ya meli hiyo wamelalamikia mamlaka zinazohusika kushindwa kuchukua hatua za dharura wakati inapotokea tatizo katika meli hizo na pia kulalamikia hali mbaya iliyokuwa ndani ya meli hiyo hivi sasa.“Kwa kweli ni shida kubwa sana uiyotupata maana tumetoka huko usiku tunasubiri tushushwe hatushushwi kila mmoja tafrani na humu kuna watoto wadogo wanalia tu, kuna watu wazima ambao wengine ni wagonjwa wa presha basi ni balaa tu” alisema Sabri mfanyabiashara moja aliyekuwa akenda Pemba kwa njia ya simu.
Meli ya Mv. Maendeleo iliondoka juzi usiku majira ya saa 3 na ilitarajiwa kufika saa 11:30 asubuhi na kushusha abiria lakini abiria hao waliokuwemo ndani ya meli hiyo wamekaa tuuu na hawajuwi msaada utatokeya wapi.Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo mbali mbali zinasema kwamba meli hiyo aidha ilipoteza muelekeo kutokana na upepo mkali uliovuma jana na kusababisha maboya kusogea mbele na kuchukuliwa na upepo huo au kempteni huyo kuchukuliwa na usingizi na kuipelekea meli hiyo pasipo pahala pake ambapo ilipanda juu ya mchanga.“Sisi ni wazoefu wa pahala hapa, amma ni upepo mkali uliochukua yale maboya na kuyapoteza na kusabaisha kapteni kushindwa kuona njia au kapteni kauchapa usingizi na ndio maana akaipeleka meli kwenye fungu la mchanga…maana hapa kukiwa na maji huwezi kuona unaweza ukaona ni sehemu ya kawaida kwa kuwa kuna maji lakini bwana eeeeh ni fungua la mchanga” alisema mzee mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake kazetini ambaye ni mzoefu wa masuala ya usafiri akizungumza nasi kwa njia ya simu.Mv Maendeleo ni miongoni mwa meli mbili kubwa zilizonunuliwa toka wakati wa awamu ya kwanza ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.pamoja na Mv Mapinduzi na hii ya mv mapinduzi imeuzwa na pesa hazijajulikana ziliko pelekwa na hakuja nunuliwa meli mpya tunaendeleya kujazwa kwenye mameli mabovu yaliyo chaka ambayo hata panya hawataki kuishi humo maana wanajuwa kuwa haina usalama kama wazanzibar hatuja amkaa wala hatuamki tena hata mwaka haujesha toka janga la meli ya mv spice kuzama na kuwa watoto na wazee na vijana na wanawake na waume kibao wamekufa na hakuna lolote lililo fanywa la msingi zaidi kuambia m/mungu kapanga mbona wao hawazipandi basi hizi meli tukasafiri nao..?.
UDIKTETA UNAENDELEYA NCHINI ZANZIBAR.MBONA ALIYE UZAA MIPAKA YA BAHARI SHAMHUNA MPAKA LEO HAULIZWI KITU....?HAKUNA GNU WALA SUKARI UNAFIKI MTUPU
Akizungumza na waandishi wa habari jana Mjini Zanzibar, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo, Ali Saleh Mwinyikai alisema wahariri hao waliondolewa katika nyadhifa hizo kwa kukiuka taratibu na mwongozo wa shirika hilo ambapo walionekana watasababisha fitna kwa viongozi hao.
Wahariri walioondolewa ni pamoja na aliyekuwa Mhariri Mkuu, wa Televisheni, Juma Mohammed Salum na Msaidizi wake, Ramadhan Ali ambao wamehamishiwa Idara ya Habari(MAELEZO).
Mwinyikai aliyasema hayo kufuatia masuali ya waandishi wa habari waliotaka kujua nini chanzo cha wahariri hao kuondoshwa katika nyadhifa zao hizo na kuhamishiwa Idara ya Habari Maelezo.
Katika mkutano huo baadhi ya waandishi wa habari walilalamikia hatua zinazochukuliwa na wizara kwa kuwapa adabu wahariri na pia kuwasumbua waandishi wa habari ambao wanafanya kazi zao kwa kufuata maadili.
Aidha walisema dhana ya uhuru wa habari inaonekana haipo kwani serikali imekuwa ikiingiza mkono wake kwa vyombo vya habari na kutoa mfano wa wahariri wa ZBC kuondolewa katika nyadhifa zao kwa madai chombo hicho kinampa nafasi kubwa zaidi Maalim Seif kuliko Dk Shein.
Akifafanua Dk Mwinyikai alisema kuondolewa kwa Juma Mohamed katika wadhifa wa Mhariri Mkuu wa ZBC na Ramadhan Ali katika nafasi zao, Naibu Mhariri Mkuu wa chombo hicho kulisababishwa na utendaji wao kuwagonganisha viongozi hao ambapo Maalim Seif alipewa nafasi kubwa katika hafla kuliko Dk Shein.
“Walioondolewa sio kwa sababu ya kumtangaza zaidi Maalim Seif kuliko Rais Shein, walikwenda kinyume na taratibu na mwongozo wa shirika, zaidi ya habari tatu za Maalim Seif zinapewa dakika tano mfululizo huku za Rais Shein zikipewa dakika moja,” alisema Dk Mwinyikai.
Dk Mwinyikai alisema ZBC haliendeshwi kwa misingi ya itikadi za kisiasa kwa sababu ni mali ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoundwa na vyama viwili vikuu vya siasa vya CCM na CUF kwa mfumo wa kugawana madaraka.
Mkurugenzi Mkuu wa ZBC, Hassan Abdallah Mitawi kwa upande wake alisema kuondolewa kwa wahariri hao katika nafasi hizo ni utaratibu wa kawaida na sio jambo kubwa kwa kuwa wlaikuwa katika kipindi cha kuangaliwa utendaji wao wa kazi.
“Hilo sio jambo kubwa ni utaratibu wa kawaida kuwahamisha watendaji sehemu moja na kuwapeleka sehemu nyengine lakini walikuwa na makosa mengine sio hayo tu” alisema Mitawi.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba katika habari ambayo inalalamikiwa kwa siku hiyo, habari kuu katika ZBC Televisheni ilikuwa ni ya Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akimwapisha DPP na Naibu Mufti Mkuu na kuondoka nchini kwenda Uingereza iliyotumia muda wa dakika 3:56.
Habari ya pili kwa uzito ilikuwa ya Makamu wa kwanza wa Rais,Maalim Seif Shariff Hamad akizungumza katika kongamano la jumuiya ya wanawake ya CUF alitumia muda wa dakika 2:42. Habari nyengine ya Rais kwa siku hiyo ilikuwa ni ya upande wa michezo ambayo ndio iliyokuwa habari kuu alizungumza na kamati ya kombe la mapinduzi iliyotumia muda wa dakika 2:32 huku ya CUF ya michezo ikitumia dakika 1:30.
Habari zaidi zinaeleza kuwa taarifa ya habari ya shirika hilo la ZBC TV ni dakika 30 tu.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu Mhariri aliyeondoshwa, Juma Mohamed iwapo alipewa nafasi ya kujitetea kutokana na kadhia hiyo alijibu kwa ufupi kwamba hawajapewa nafasi ya kujitetea bali walihamishwa baada ya kutakiwa kutoa maelezo kwa nini walimpa muda mrefu Maalim Seif na sio Dk Shein.
Hadi sasa utendaji kazi wa serikali unaendelea ambapo vyombo vya vya habari vinatakiwa kuipa uzito taarifa au tukio lolote lililofanywa na Rais wa Zanzibar, akifuatiwa na Makamu wa kwanza na baadae kamamu wa pili na kisha mawaziri jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa sana na wadau wa habari nchini wakisema ifike wakati utaratibu huo uondoshwe kwani kuna mambo na matukio muhimu yanakosa kupewa uzito unaostahiki.
Katika mkutano huo, uliandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Waziri wa wizara hiyo Abdillahi Jihadi Hassan alisema wizara yake imepata mafanikio katika mambo mbali mbali ikiwemo michezo na utamaduni.
Subscribe to:
Posts (Atom)