ABIRIA zaidi 400 wamekwama baada ya meli ya Mv. Maendeleo iliyokuwa inasafiri kutoka Unguja kwenda Pemba kushindwa kushusha abiria kwa kutoka na kuchaka kwa meli hiyo na ubovu limekwama baharini na dungu zetu wamo ndani ikielekea, Kisiwani Pemba hapo jana. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa watu waliokuwa ndani ya meli hiyo waliozungumza na gazeti hili kwa njia ya simu walisema meli hiyo ilipoteza muelekeo na kuingia sehemu ambayo ilipelekea kukwama na mashine kuzima kabisa.
Meli hiyo inayomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ilipoteza mwelekeo wakati inajiandaa kuikaribia pemba na kusimama kwenye kina kifupi cha maji ambapo palikuwa na mchanga na mashine kunyamaza kabisa.Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar (ZMA), Abdallah Hussein Kombo alithibitisha kukwama kwa meli hiyo kwenye eneo lenye kina kifupi cha maji ambapo alisema tukio hilo halikuweza na hakujasababisha madhara yoyote kwa abiria waliokuwemo ndani ya meli hiyo wala hakuna athari kwa meli yenyewe.“Taarifa zilizopo ni kuwa abiria wote zaidi ya 400 wako salama, na hakuna athari zilizopatikana katika tukio hilo ” alisema Kaimu Mkurugenzi huyo.Kaimu huyo alisema meli hiyo iliingia kwenye kina kifupi cha maji wakati inageuza mwelekeo kuelekea baharini baada ya kukaribia bandari ya Mkoani ikiwa ni hatua ya awali ya kujiandaa kushusha nanga na hivyo kuingia sehemu ambayo baadae ilikwama.“Meli inapokaribia bandarini inaogozwa na boya, lakini inavyoelekea boya lilisukumwa na maji likahamia kwenye kina kifupi na kusababisha meli kwenda huko na kukwama,alisema Kombo.
Kepteni wa meli hiyo alikuwa ni Hamad Suleiman Kombo na kwamba mbali na kubeba zaidi ya abiria 400 pia ilikuwa na wafanyakazi 19 wanaifanya kazi ndani ya meli hiyo.Wakizungumza kwa njia ya simu baadhi ya abiria waliokwama ndani ya meli hiyo walisema walikuwa na khofu kubwa kutokana na kuwa wahusika wa meli hiyo hawajasema lolote kwa abiria wao jambo amablo lilizusha khofu kubwa kwa miongoni mwa abiria.
Walisema tatizo lililokuwemo ndani ya meli hiyo kulikuwa na joto kali, ukosefu wa maji huku chakula kikikosekana jambo ambalo lilizusha zogo kubwa kutokana na wanawake wengi kushitushwa na hali hiyo huku watoto wakilia ovyo kutokana na hali ya joto kali lililokuwemo ndani ya meli na hakuna maji wala vyakula.“Sijui tumo abiria wangapi lakini kwa kweli naona meli imejaa sana lakini hilo joto na kuwa hakuan chakula wala maji ya kunywa ndani ya meli hii ati meli ya serekali na sisi tuliondoka Unguja saa 3 usiku basi tumechoka sana na mabaharia hawatuambi kitu tumekaa tu ndani ya meli hatujui chochote kianchoendelea khofu ndio inazidi maana mtu akitafunwa na nyoka hata ukuti ukikugusa huwa anauogopa…. Na sisi wazanzibari tushatafunwa na hatujasahau bado” alisema Asha Mkaazi wa Machomanne Kisiwani Pemba aliyekuwemo ndani ya meli hiyo akizungumza nasi kwa njia ya simu.Aidha wananchi waliokuwepo ndani ya meli hiyo wamelalamikia mamlaka zinazohusika kushindwa kuchukua hatua za dharura wakati inapotokea tatizo katika meli hizo na pia kulalamikia hali mbaya iliyokuwa ndani ya meli hiyo hivi sasa.“Kwa kweli ni shida kubwa sana uiyotupata maana tumetoka huko usiku tunasubiri tushushwe hatushushwi kila mmoja tafrani na humu kuna watoto wadogo wanalia tu, kuna watu wazima ambao wengine ni wagonjwa wa presha basi ni balaa tu” alisema Sabri mfanyabiashara moja aliyekuwa akenda Pemba kwa njia ya simu.
Meli ya Mv. Maendeleo iliondoka juzi usiku majira ya saa 3 na ilitarajiwa kufika saa 11:30 asubuhi na kushusha abiria lakini abiria hao waliokuwemo ndani ya meli hiyo wamekaa tuuu na hawajuwi msaada utatokeya wapi.Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo mbali mbali zinasema kwamba meli hiyo aidha ilipoteza muelekeo kutokana na upepo mkali uliovuma jana na kusababisha maboya kusogea mbele na kuchukuliwa na upepo huo au kempteni huyo kuchukuliwa na usingizi na kuipelekea meli hiyo pasipo pahala pake ambapo ilipanda juu ya mchanga.“Sisi ni wazoefu wa pahala hapa, amma ni upepo mkali uliochukua yale maboya na kuyapoteza na kusabaisha kapteni kushindwa kuona njia au kapteni kauchapa usingizi na ndio maana akaipeleka meli kwenye fungu la mchanga…maana hapa kukiwa na maji huwezi kuona unaweza ukaona ni sehemu ya kawaida kwa kuwa kuna maji lakini bwana eeeeh ni fungua la mchanga” alisema mzee mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake kazetini ambaye ni mzoefu wa masuala ya usafiri akizungumza nasi kwa njia ya simu.Mv Maendeleo ni miongoni mwa meli mbili kubwa zilizonunuliwa toka wakati wa awamu ya kwanza ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.pamoja na Mv Mapinduzi na hii ya mv mapinduzi imeuzwa na pesa hazijajulikana ziliko pelekwa na hakuja nunuliwa meli mpya tunaendeleya kujazwa kwenye mameli mabovu yaliyo chaka ambayo hata panya hawataki kuishi humo maana wanajuwa kuwa haina usalama kama wazanzibar hatuja amkaa wala hatuamki tena hata mwaka haujesha toka janga la meli ya mv spice kuzama na kuwa watoto na wazee na vijana na wanawake na waume kibao wamekufa na hakuna lolote lililo fanywa la msingi zaidi kuambia m/mungu kapanga mbona wao hawazipandi basi hizi meli tukasafiri nao..?.
No comments:
Post a Comment