Thursday, March 12, 2015

KURA YA MAONI YA HAIRISHWA KATIKA BARAZA LA WAWAKILISHI NCHINI ZANZIBAR BAADA YA WAWAKILISHI WA CUF KUPINGA VIKALI SHERIA ZA MKOLONI TANGANYIKA KUTUMIKA BARAZANI HUMO NA KUWAGEUZA KUWA MADALALI


SPIKA WA BARAZA LA WAWAKISHI AKITOKA NA RUNGU LAO LA KUIWA NCHI ZANZIBAR.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka Chama cha Wananchi (CUF) jana waliweza kuzuia kuuzwa nchi ya Zanzibar na madalali wa ki CCM katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi na kumlazimisha Spika wa Baraza hilo, Pandu Ameri Kificho, kuahirisha kikao hicho. Kuzuia huko ilitokea kabla ya kuwasilishwa kwa sheria ya kura ya maoni namba 11 ya mwaka 2013 ya Jamuhuri ya Muungano kwa mujibu wa kifungu 132(2) cha Katiba ya Zanzibar.
Wabunge wa CUF walikuwa wanapinga kuwasilishwa kwa sheria hiyo na CCM kutaka itumeke na ndio vurugu lilipoanza baada ya vurugu hizo kuendelea takribani kwa zaidi ya nusu saa huku Spika Kificho akihamasisha hali ya utulivu barazani, lakini ilishindikana na kuwataka wasaidizi wake kunyanyua siwa na kuanza kutoka huku wajumbe wengine wakicheza na kuendelea kushangilia. Wakati wajumbe hao wa CUF wakishangilia na kuimba kwamba CCM ni madalali wa Zanzibar, wajumbe wa CCM nao walisimama na kuimba CCM, CCM, CCM.
Kabla ya kuanza kwa vurugu hizo, mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu, alisema kuwa hawakubaliani na sheria hiyo kwani nchi ya Zanzibar ina sauti yake, hivyo hawezi kutumia kanuni ya Jamuhuri ya Muungano kwani kufanya hivyo ni sawa na kuwa dalali kwa Zanzibar. “Nasema sheria hii sisi hatuikubali kwani sisi hatutaki kuwa madalali wa nchi yetu ya Zanzibar, sheria hii tukiikubali tutakuwa ni madalali,” alisema Jussa. Baada ya kauli hiyo ya Jussa, moja wa madalali Waziri wa Nchi, Ofisi ya Raisi, Mwinyihaji Makame Mwadini, alilazimika kusimama na kumtaka Jussa atii kufuta kauli yake ya kuwahusisha Wajumbe wa Barala kuwa ni madalali wa nchi na kumtaka kuomba radhi. Kutokana na hali hiyo.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment