Tuesday, May 10, 2016

SEHEMU YA 2) UKWELI NI HUU KUUSUTA UWONGO. MAVAMIZI YA NCHI YA ZANZIBAR KWA WAGENI KUUWAUWA WANYEJI KATIKA NCHI YAO NA KUSINGIZIA ((MAPINDUZI))



HALI ZA MAISHA

Matunda makubwa waliopata wananchi wa visiwani wa Unguja na Pemba kutokana na hayo yenyekuitwa, Mapinduzi ni shida za kimaisha katika kila upande. Vyakula havinunuliki,Nguo hazikamatiki,Mradi wananchi wamo katika kuhiliki kwa maisha yalivyo magumu. Vijana wamekuwa wazee kwa shida.Sokoni kunaitwa uwanja wa Mapambano Na kweli, Ukenda sokoni basi upanie kweli kweli kwani fungo la mihongo ikiwa huna shs 200 hulichukuwi. Mkungu wa ndizi ya Mtwike, shs 3000, nazi moja shs 50, pili pili za mchuzi fungu shs 30 mpaka 50,kicha cha mboga ya mchicha kuanzia shs 70 mpaka kuteremka shs 50,fungu la machungwa sita yaliyotukuka kidogo,shs 200 na yaliyokuwa madogo,shs 100.Takriban watu wote wamekuwa mabaniani,hawali nyama kwani kilo ya nyama ni shs 1200!! Mishahara ya wafanya kazi wa serikali ya kiwango cha chini ambao ndio wengi shs 7000!! Mtu, yeye na mkewe na watoto wawili,inabidi, tena kwa kujibana,atumie shs 1000 kwa siku kwa chakula cha asubuhi na cha mchana.Kwa hivyo inamlazimu apate shs 30,000 kwa mwezi. Ikisha kuwa mshahara wake ni shs 7000 kwa mwezi hizo 23,000,atazipata wapi..?? Kutokana na hali kama hizo za kimaisha,ndio utaona kuwa toka waongozi wa serikali mpaka wafanyajikazi wa chini wanaishi kwa magendo CURRUPTION (RUSHWA) katika nchi imefika katika kilele cha juu kabisa.Tunakubali kuwa Ulimwengu wote umeingiwa na shida za kimaisha likini huwepo sababu maalumu ambazo kwa Zanzibar-Alhamdulilahi hazijatokea na in shaa Allah zisitokee. Mara nyingi watu hukutwa na shida za kimaisha katika nchi zao kwa kutokana na hali za mabadiliko kama kutokupata mvua,kutokea mafuriko ya maji,kutokea moto wa misituni,kutokea mitetemeko ya ardhi au vita vya wenyewe kwa wenyewe,kama nilivyotangulia kusema shida kama hizo,Alhamdulilahi hazikufika katika nchi yetu.Sasa kipi kicho sababisha taabu na dhiki zote hizi za kimaisha...?? Hili ni swala ambalo kila mwananchi lazima ajiulize, Ikiwa tutajiuliza kwa insafu basi jawabu halitokuwa zito kulipata.

Mpaka Januari 11,1964 pishi moja ya mchele ilikuwa baina shs nne mpaka tano. (Pishi moja na sawa na kilo Tatu).Ina maana yakuwa kilo tatu za mchele zilikuwa shs nne mpaka tano. Na zilikuwa kabila mbali mbali za mchele ya namna kwa namna. Neema zote zilikuwepo visiwani Zanzibar, Mwenyezi Mungu ameziondosha kwa kutokana na maovu yaliyoletwa na hayo yenye kuitwa Mapinduzi. Ni kama wale watu walio mchinja bata aliyekuwa akitaga mayai ya dhahabu. Dulma zilizofanywa za kupoteza roho za viumbe wa Mwenyezi Mungu,bila ya kuwa na kosa lolote la kisheria,mali za watu zimechukuliwa kwa nguvu kutoka na wenye haki nazo. Natija ya hayo imekuwa leo sehemu kubwa sana ya vyakula vinavyouzwa masokoni vinatokana na ardhi zilizoporwa. Kwa hivyo wananchi wanalishwa vyakula vya HARAMU.nawale walio kuwa wamenunuwa majumba ambayo wanajua ni yenye kutokana na kuibiwa kutoka kwa wenye haki nayo,basi wajue Sala zao wanazo zisali katika majumba hayo,Mwenyezi Mungu hazikubali. Na ni hivyo hivyo kwa wale walionunuwa mashamba yaliyoporwa kutokana na wenye haki nayo,basi na wao wajue kuwa vyakula wanavyo vivuna katika mashamba hayo ni vyakula vya HARAMU. Kwa hivyo wao wanakula HARAMU na wakiviuza, wao ndio watakao chukuwa dhima ya kuwalisha wenziwao vyakula vya HARAMU. kutokana na hali kama hizo zilizokuwa zimefanyika katika nchi, ndio ikawa kila lifanywalo haliwi. Na ikiwa hapatafanywa TOBA ya kweli, basi na waje wowote wataokuja, ikiwa wataendelea na mwendo wa kurithi mwendo wa kidhalimu walioukuta, basi hapana litalo weza kutengenea ila itakuwa kuziba kiraka hapa na kupasuka pengine.kauli ya Mwenyezi Mungu Kattu haiwezi kwenda kombo. Mwenyezi Mungu anasema kuwa :HAZIDI MWENYE KUDHULUMU ILLA KHASARA:

NEEMA ZILIKUWEPO

Katika huo wakati unaoitwa wa kikoloni, Serikali ya Zanzibar ilikuwa ikiendesha mambo yake yote kama Kujenga Maskuli, Maspitali, Mabarabara, Kununuwa Meli za Usafiri, pamoja na kuyahudumia na kulipa mishahara ya wafanyajikazi toke wakigeni mpaka wananchi. Na hao wafanyakazi wa kigeni ambao wengi wao walikuwa Wazungu,basi juu ya mishahara yao walikuwa wakipewa posho maalumu (Inducement Allowances),pia walikuwa wakilipiwa nauli za kuwaleta na kuwarejesha na za wakati wa likizo zao,yote hayo na mengineyo yakifanywa na kutokana na mapato ya ushuru tu wa forodha.Serikali hii yenye kujita ya Mapinduzi ni wao peke yao ndio wenye kununu bidha muhimu zote za nchi kama vile, Karafuu, Bataa na pilipili hoho kutoka kwa wananchi kwa bei wazitakazo wao wenyewe na wakaziuza kwa bei  ziliopo katika masoko ya ulimwengu, Isitoshe, serikali hii haina gharama za kuwalipa hao wazungu kama ilivyokuwa hapo zamani, sasa ilikuwaje hata ifike serikali kuwa haina fedha hata za kuwalipa mishahara wafanyakzi wake wa kienyeji...?? Hapana shaka sababu kubwa ya hayo ni hii DHULMA iendeleayo hadi hii leo, uwendeshiji mpotofu, ukiongozwa na siasa za HUSDA na UROHO WA MADARAKA NA KIPATO, siasa ya Chukuwa Chako Mapema (CCM) siasa ambayo immefanya mwananchi kuwa hana uwezo wala itibari yoyote katika nchi yake. Kwa hali za kimaisha nchini mwananchi hawezi kukaa akatuan na kufikiria na kupanga juu ya maendeleao ya nchi yake, yeye anafikiri juu ya cha JIYO TU!! Siasa mbovu hii iliopangwa makusudi imemzuiliya na kumyima mwananchi uwezo na njia za kujiendeleza, Laa si katika kimaisha, walaa si katika kiutamaduni au kielimu. Inatilia nguvu mizizi ya siasa yake ile ile ilioanziwa, nayo ni MWENYE ILEMU NI ADUWI.

KUANZA HARAKATI ZA SIASA

Kabla Serikali ya Kiingereza kuiingiza Zanzibar chini ya Himaya yake, Zanzibar ilikuwa ni Dola kamili iliyokuwa na shughuli zake (ikimiliana) na ulimwengu wote. Mara tu Muingereza alipoitia Zanzibar katika makucha yake mnamo mwaka 1819, kila jambo kubwa na dogo lilikuwa lazima liamuliwe kutoka Uingereza. Mfalme wa nchi alifanywa kuwa ni alama tu ya Dola, hakuwa na uwezo kataika kukata shauri juu ya uendeshwaji wa nchi. Kama ilivyo kamaida ya wakoloni popote ulimwenguni wanapotawala, lazima watumie mbinu za kuwagawa wananchi (ili waendeleze utawala wao) kutokana na hali hii za namna fulani ziliopo katika nchi. Ikiwa kwa njia za Kidini, Ukabila, Urangi, Utajiri, uwezo wa kimaisha na hata umadhehebu. Katika Zanzibar Muingereza alitumia njia za kuwagawa wananchi kwa kutumia asili za makabila yao. Aliwafanya wenye asili za kiarabu wajione kuwa wao tu ndio wenye haki za utawala kwa vile ilivyokuwa mfalme wa nchi anatokana na asili zao. Aliwafanya Washirazi yaani, Wahadimu, Watumbatu na Wapemab wajione kuwa wao tu ndio wenye kila haki za nchi kwa vile ilivyokuwa wao ndio waliokwenda kuwaita waarabu (kutoka kwao Oman) kuja kuwasaidia kumuondowa mreno. Aliwafanya wafrika (weusi) wajione kuwa wao tu ndio wenye kusitahiki utawala wa Zanzibar kwa vile Zanzibar imo katika bara la Afrika. Na alichukuwa uchumi wote wa nchi na kuuweka katika mikono ya wenye asili za Kihindi kuwa wao ndio raia wa Kiingereza sahihi wa tangu asili, kwa uwezo wao wa kimaisha wakajiona kuwa wao ni wabora kuliko wengine katika nchi. Kutokana na hali kama hizo, wananchi walianza kujigawa mafungu kwa mafungu na walianza kufunguwa jumuiya zao za Kikabila. Waarabu walifunguwa yao, Washirazi walifunguwa yao, Waafrika walifunguwa yao na Wahindi walifunguwa yao na Wangazija wakafunguwa yao. Na ndani ya hizo hizo, zilijitokeza zengine na kila moja alikuwa ajitapa kwa upande wake. Kwa muada mkubwa jumuiya hizo zilikuwepo katika nchi na hazikuweza kupata wala kufanya lolote kwa maslahi ya nchi. kubwa walilokuwa wakilipata ni kualikwa chai ya alaasiri kwenye Bustani ya Jumba la Balozi wa Kiingereza, na kualikwa katika siku ya kuzaliwa Mfalme wa Kiingereza na Mfalme wa nchi na kualikwa kutembelea Manuwari za Kiingere zazinapofanya ziara kuitembelea Zanzibar. Katika miaka ya 1920 Muingereza katika jamaa zake za kuzidi kuwafarikisha wananchi ili aendelea kuwatumia katika kuendeleaza utawala wake, alianzisha kuwateuwa (appoint) wananchi kwa kuwatia katika Baraza la Kutunga Sheria (Legisltive Council) kwa njia za kikabila. Aliwateua hatimeya Waarabu Wane, Waafrika Wane, Waahindi watatu na Mzungu moja. Na upande wa Serikali walikuwemo wakurungezi wa idara wa Kiingereza kutoka idara mbali mbali za serikali walioteuliwa vile vile, hao walizidi kwa wingi katika baraza hilo kuliko raia. Mwendo huo uliendelezwa kwa muda wa miaka 28 na hapakuwezekana kupatikana lolote la maslaha ya nchi. Miaka nenda Miaka rudi, nchi haukuwa na maendeleo yoyote kukhusu mabadiliko ya katiba itayo wawezesha wananchi kuendesha wenyewe shughuli za nchi yao bila ya kuingiliwa na yoyote. Katika mwaka 1953 na 1954, Jumuiya ya Waarabu (Arab Association) Iliamuwa kupelekea Balozi wa Kiingereza madai ya kutaka yaletwe mabadiliko ya katiba yatayo wawezesha wananchi wa Zanzibar kuchaguwa wajumbe wao wa kuwapeleka katika baraza la kutunga sheria kwa njia ya uchaguzi wa Kura Moja Kwa Mtu Moja (One Men One Vote). Na miogoni mwa madai yao, walidai uondolowe mtindo wa kuwateua wananchi kwa njia za kikabila katika kila jambo la nchi. Pia walitaka baada ya kupatikana kwa matokeo ya uchaguzi huo, paanzishwe mazungumzo ya taratibu za kupatikana kwa uhuru kamili wa Zanzibar. Balozi wa Serikali ya Kiingereza aliyekuwepo Zanzibar wakti huo akiitwa Mr Renkin. Balozi huyo alikataa hata kuyatia maanani madai hayo. Jumuiya ya Waarabu walipoona hawakuweza kupata natija yoyote katika madai yao, bali hata hayakuzingatiwa, waliamua kuanzisha mgomo kwa kuwazui wajumbe wao kushiriki katika vikao vya Baraza la Kutunga Sheria na katika vikao vya Kamati za Mabaraza yote Walioteuliwa Kushiriki. Mgomo huo ulichukuwa muda wa miezi 18 bara bara.

Jambo la Kulizingatia katika suala hili ni kuwa, madi hayo kutokana na Jumuiya ya Waarabu hawakuyafanya kwa maslahi yao binafsi zao, bali kwa maslahi ya Zanzibar na Wazanzibari wote bila kujali asili za makabila yao.Haya yanajithibitisha zaidi kwa vile ukiangaliya idadi ya hao waliokuwa wakiitwa (au wanaitwa) Waarabu katika Zanzibar walikuwa ni kiasi cha 16 katika 100 (16%) Juu ya hivyo waliamua kuziachilia mbali nyadhifa walizopewa, sio hivyo tu , bali kutoa muhanga nafsi zao wakiweka mbele maslahi ya nchi. Bahati mbaya hawakupata kuungwa mkono na wanachi wenziwao wenye asili za makabila mengine juu yakuwa walizungumza nao na waliwataka washirikiane katika madai hayo. Mmoja kati yao (Aliteuliwa kushiriki katika Baraza la Kutunga Sheria-akiwa ni Mwenye Asili ya Kiarabu) alipinga uamuzi wa Jumuiya yake na alihudhuria katika kikao cha Baraza la Kutunga Sheria wakati wenzake walipokuwa wamesha amua kugomea. Matokeo yake, alitokea mwananchi mwenye uchungu na nchi yake na kumpiga bwana huyu kwa visu. Kwa bahati mbaya alikufa kutokana na pigo hilo.

SHEIKH ALI MUHSIN KWENDA NCHI ZA ULAYA IKIWEMO NA UINGEREZA KUPIGANIA UCHAGUZI WA COMMON ROLL (MTU MOJA KURA MOJA)

Wakati Jumuiya ya Waarabu ilipokuwa katika hekaheka za mgomo wao wa kuto kushiriki katika Mabaraza yote ya Serikali kwa madai ya kutaka papatikane mabadiliko ya katiba yatayo wawezesha wananchi kuchagua wawakilishi wao wa Baraza la Kutunga Sheria kwa njia ya uchaguzi wa One Men One Vote na kusita kuteuliwa kutokana na asili ya makabila yao, Mwananchi mwenzao mwenye uchungu na nchi alifunga safari (kwa gharama zake mwenyewe) kwenda kupingania maslahi ya nchi yake, akiendeleza madai ya wananchi wenziwe huko nyumbani. Wakati Sheikh Ali Muhsin Alipokuwa katika hekaheka hizo huko Uingereza alikutana na Seyyid Abdul-Rahman Mohammed (Babu) na waliweza kushirikiana katika juhudi hizo. Katika harakati hizo Sheikh Ali Muhsin alikutana na waongozi mbali mbali wa kisiasa na wengi wao walimshajiisha juu ya kuuendelea na juhudi za ukombozi wa nchi yake walimpa kila msaada (moral support) huko Uingereza alipata kuzungumza na wakuu wa Serikali ya Kiingereza, wakuu wa upande wa upinzani na wakuu wa vyama vya wafanyakazi. Pia alikutana na wakuu wa vyama na jumuiya mbali mabli zenye kupingania kuondoka kwa ukoloni katika Afrika na katika sehemu zengine za ulimwengu.


KUASISIWA HIZBUL-WATTAN
(ZANZIBAR NATIONALIST PART)

Wakati Sheikh Ali Muhsin akiwemo katika safari zake huko nchi za Ulaya huko nyumbani walichomoza wananchi wengine waliokuwa nao ghera na mapenzi ya nchi yao. (wote isipokuwa Abdalla Mahmoud-walikuwa si Waarabu) wananchi hao walikutana kuzingatia na kutafakari juu ya kupotea kwa nchi yao kutokana na mbinu za mkoloni za kuwagawa wananchi kwa kutumia asili zao makabila yao. Wananchi hao waliibuka amuo la kuanzisha umoja wa wananchi wa Unguja na Pemba. Umoja ambao kila raia wa Zanzibar atastahiki kuwemo bila kujali asili ya kabila yake wala Imani ya Dini yake, La Umuhimu ni URAIA WAKE.Hichi ndio kilukuwa chama cha kwanza na pekee katika nchi kuasisiwa kwa kufuatia Misingi ya UWANANCHI. Wananchi Waasisi hao walikuwa ni Sheikh Vuai Kiteweo, Sheikh Miraj Shaalab, Maalim zaid Mbarouk, Maalim Maksud Fikirini, Maalim Mwandoa Khamis, Maalim wazir Ali bin Maalim, Sheikh Haji Hussain Ahmed, Sheikh Othman Soud, Sheikh Abdulla Mahmoud Kombo, (wa makunduchi) Sheikh Ramadhan Tosir, (Ramadhan Madafu), Maalim Hija (wa Ndijani), Sheikh Ame, Sheikh Abdulla Mali, Sheikh Haji Kombo (wa Kiboje), Sheikh Abdalla Mahmoud na wenziwe wachache. Kwahivyo wale wenye kusema na kutangaza kuwa HIZBU (ZNP) iliasisiwa na Waarabu au kilikuwa chama cha Waarabu, hapana shaka wanakosea, amma kwa kutokujuwa ukweli ulivyo au wanasema hivyo kwa makusudio ya kutafuta maslaha yao. Ukweli na Hakika ilivyo ni kuwa Hizbu Haikuasisiwa na Waarabu Wala hakijapata kuwa chama cha Waarabu. Na kama Hizbu kigelikuwa ni chama cha Waarabu, basi kisingeweza kupata ushindi katika chaguzi zilizofanyika za (One Men One Vote) kwani idadi ya hao wenyekuitwa Waarabu nchini ilikuwa ndogo; kwahivyo idadi yao hiyo haingaliwesha kukipa (hicho kisemwacho ni chama chao) voti za ushindi. Madai hayo ni miongoni mwa maneno na mbinu za kufitinisha na kuwagawa wananchi kwa kuwaogopa umoja wao. Hapana shaka zimetungwa na wakoloni na kuimbwa na VIBARAKA VYAO, kwa maslahi yao. Mabwana hao tulio wataja hapo juu wakiwa ndio waasisi wa chama cha HIZBU-WATTAN, wao ndio waliomuendea Sheikh Ali Muhsin Nyumbani Kwake baada ya kurejea kutoka safarini na kumueleza kukhusu kuasisi kwa chama chao na nini dhamiri zilizo wapelekea kuasisi chama hicho. Baada ya kumueleza,walimtaka na yeye awaunge mkono kwa kujiunga katika chama. Sheikh Ali Muhsin alipoona kuwa hayo wayatakayo wananchi wenzake ndio hayo hayo ayatakayo na kuyapigia mbio daima basi, hapo hapo aliamuwa kujiunga na kushirikiana nao. Baada ya kujiunga, Waasisi hao walimtaka Sheikh Ali Muhsin aanze kuzungumza na nduguze wenye asili za Kiarabu-bali na kila anayefahamiana nae ili wajiunge na wananchi wenziwao. Sheikh Ali Muhsin Aliupokea na kuanzakutekeleza ujumbe huo. Miongoni mwa mwanzo (kati yao wenye kuitwa Waarabu) kujiunga na umoja huo ni, Sheikh Badr Muhammed Barwani, Sheikh Ahmed Seif Kharusi, Sheikh Amour Zahor Ismaily, Sheikh Ali Ahmed Riyamy, Sheikh Nassor Bin Isa Ismaily na Sheikh Ahmed Khalfan Naamini haukuchukuwa muda ila nao walijiunga. 

WAKOLONI DHIDI YA HIZBU,UHURU NA UMOJA WA ZANZIBAR

Serikali ya Kikoloni ilipoona umoja wa Hizbu Umesimama na kila siku Unazidi Kuungwa Mkono na Wananchi wakila pembe na kila aina, walizidi kuogopea maslahi yao. Kwa kuhifadhi maslahi yao walianza kuuandama umoja huo-Hizbu Wattan- nje ndani, usiku na mchana kwa kuwatumilia baadhi ya wananchi wafanyakazi wa idara ya utawala khasa Mamudiri na Masheha. Vitumishi hivyo vilifunga njuga na kuingia mitaani na viamboni katika juhudi za kuuvunja umoja huo wa Hizbu Wattan. Kwa kiasi fulani hapo mwanzoni waliweza kufanikiwa, Kwani walitumilia mbinu za kuwatisha Wananchi; Baadhi kwa kuwaambia kuwa, chama hich azma zake ni kuleta machafuko katika nchi na kwa baadhi ya wananchi wakiwaambia kuwa chama hichi kinataka kumuondowa Mfalme. Kila mmoja wakimpingia mdundo waliofikiria kuwa utaweza kumshitusha na kukiepuka chama hiki. Bali wananchi hawakuchukuwa muda illa waliweza kuzielewa mbinu zao hizo na kuwaepuka na badala yake kuzida kuungana na wananchi wenziwao.

MAKAO MAKUU YA HIZBU

Kabla ya uchaguzi wa Mwanzo wa Common Roll Election Yaani Mtu Mmoja Kura Moja, katika Zanzibar Mnamo mwaka 1957, Mwananchi Mzalendo Sheikh Mahmoud  wa Mtendeni aliyekuwa mwishoni akijishughulisha na utengezaji wa saa, alijitolea kwa kukipa chama jumba lake la ghorofa moja lililokuwepo Mtaa wa Mwembetanga kuwa ni Mkao Makuu ya Chama. Alitoa bila ya kupokea kodi hata senti moja. Baada ya kumalizaka kwa Uchaguzi wa mwanzo wa 1957, Hizbu iliondowa Makao Makuu yake kutoka Mwembetanga na kuhamia Mkunazini Karibu na Msikiti Gofu. Baada ya kuwepo hapo kwa muda, ndio iliweza kununuwa jumba lake wenyewe katika Mtaa wa Darajani na kulifanya ndio Makao Makuu ya Chama. Jumba Hilo, Baada ya MAVAMIZI YA JANUARI 12,1964 liliporwo na Serikali ya MAVAMIZI na kufanywa Makao Makuu ya Afro-Shirazi Youth League. kama ilivyo hali ya majengo mengi mengineo humo nchini, Jumba hilo limetupwa bila ya Matengenezo wala matumizi ya faida. na linachwa kubomka pole pole. Haya sio ajabu, bali haya yanazidi jinsi hao Viongozi wa Zanzibar walivyokuwa hawana uchungu na nchi bali na chochote cha nchi.

HIZBU KUMLETA ZANZIBAR SEYYID ABDUL-RAHMA (BABU)

Miezi michache kabla ya uchaguzi wa mwanzo wa 1957, Chama Cha Hizbu Wattan-kilimleta Babu Zanzibar ili ashirikiane na wananchi wenziwe katika harakati za kisiasa. Baada ya kufika Zanzibar, Hizbu ilimteuwa kuwa katibu mtendaji wa Chama (Excutive Secretary). Kutokana na maarifa aliyokuwa nayo katika mipango ya kuendesha Chama Cha Kisiasa, Babu baada ya muda mdogo alianzisha Umoja Wa Vijana (Youth Own Union) YOU kwa msaada na ushirikiano wa waongozi wenziwe na wananchi Babu alifanya kazi kubwa katika kukijenga Chama Cha Hizbu ndani na nje ya nchi. Lakini, kwa bahati mbaya, kama alivyokuwa hodari katika kukijenga, ndivyo alivyojaribu kwa uhodari - au ilivyo khasa - kwa kiujanja kutaka kukibomoa baada ya kushindwa kufikilia maslahi yake binafsi kwa kukitumilia Chama. (Baadae tutaeleza aliyoyatenda katika kukibomoa Chama na Kuifisidi Nchi). Alipojiunga Sheikh Ali Muhsin katika Chama Cha U wa Hizbul-Wattan - Zanzibar Nationalist Party (ZNP) aliwapa shauri wakuu wa Chama kumtaka Babu achukue mafunzo katika kuendesha Chama na baadae aje asaidie katika uendeshaji wa ZNP. Wakuu wakapendezewa na shauri hiyo, na Babu akawafik. Sheikh Ali Muhsin hapo tena aliiomba Labour Party ya huko Uingereza kwa kupitia kwa (wasta wa) Mr. John Hatch na Mrs. Eirene White M.P. na Labour Party ikakubali kumpokea Babu kwa Mafunzo. Mafunzo hayo yalikuwa ya muda wa miezi sita. ZNP (Hizbu) ililipia gharama zote za kimaisha kwa muda huo na za safari. Katika muda huo pia aliendelea kulipwa mshahara akiwa ni Excutive Secretary wa Chama ZNP. Utaona dhahiri kuwa imani ya Hizbu juu ya Elimu na Maarifa haikufungika sehemu mmoja tu, bali ilikuwa ni kwa kila upande. Hizbu iliamini kuwa uwongozi mwema wa chama na nchi utapatikana kutokana na watu wenye Ujunzi na Maarifa, Kwa hivyo iliona umuhimu wa kumpatia mafunzo na elimu ifaayo Katibu Mtendaji wake khasa, na wengine wafuatie.

NATIJA YA SAFARI YA SHEIKH ALI MUHSIN

Kama tulivyoeleza hapo mwanzoni kuwa Sheikh Ali Muhsin alizitembelea baadhi ya nchi za Ulaya pamoja na Uingereza kwa ajili ya kugombania kupatikana kwa mabadiliko ya Katiba ya kuanzishwa kwa Uchaguzi wa Common Roll yani One Men One Vote katika Zanzibar. Natija ya safari hiyo, Serikali ya Kiingereza, ilimleta Zanzibar Mr. Coutts akiwa ni Mchunguzi juu ya Maendeleo ya Katiba. Mchunguzi huyo alifika Zanzibar kati ya mwaka wa 1956. Chama Cha Hizbu kilifanya Maadamano Makubwa kwa kumpokea Mr. Coutts hapo kiwanja cha ndege cha Kiembe Samaki siku aliyofika Zanzibar. Waandamanaji walichukuwa mabango yaliyokuwa yameandikwa: Tunataka Uchaguzi wa One Men One Vote, Tunataka Uhuru Wa Nchi Yetu, Tumechoka Kutawaliwa, Tunapinga Ubaguzi Wa Rangi Na Wa Ukabila. Mjumbe huyo alipokuwa Nchini alikutana na wananchi pamoja na waakazi mbali mbali wa nchini. Alionana hata na watu binafsi. Na alipokea risala (za maandishi na za mdomo) kutoka vyama mbali mbali vyakikabila na vya kidini. Chama Cha Hizbu nao walionana na mjumbe huyo na walimkabidhi risala yao yenye kutilia nguvu matakwa yao, matakwa ambayo ndio msingi wa ujumbe wake wa kuja Zanzibar. Inafaa ifahamike kuwa tangu kufika kwa mchunguzi huyo na mpaka kuondoka hapakuwepo Chama Cha Siasa Nchini isipokuwa Kimoja Tu - Hizbu - Wattan. Vyama vyote vya kisiasa vyengine viliasisiwa baadae. Kwahivyo Hizbu -l- Wattan ndicho Chama Cha Mwanzo Cha Kisiasa Kuasisiwa Zanzibar. Mr. Coutts alipomaliza shughuli zake alirejea kwao. Baada ya muda alileta mapendekezo ya uchunguzi wake kwa Balozi wa Serikali ya Kiingereza aliyekuwepo Zanzibar. Katika mapendekezo hayo, Mr. Coutts alikubali kuwa Zanzibar inafaa kuanzishwa uchaguzi wa Common Roll yaani uchaguzi wa kwa pamoja, bila ya kujali khitilafu za kabila. Lakini alipendekeza kuwa uchaguzi uanzie kwa viti sita na vilivyobakia viendelee katika mpango ule ule wa kuteuliwa na Balozi wa Serikali ya Kiingereza kwa Kushauriana na Mfalme wa Nchi. Pia katika mapendekezo yake. Bwana Coutts alitaka Balozi wa Kiingereza aendelee kuwa Mwenye Kiti wa Baraza la Kutunga Sheria na watumishi wa Serikali ya Kiingereza waendelee kuwa waongozi wa upande wa Serikali. Hizbu haikuridhika hata kidogo na mapendekezo hayo, kwa vile asli ya madaai yao ni kuwa wawakilishi wote wa Baraza la Kutunga Sheria wawe ni wananchi walio changuliwa na wananchi kwa uchaguzi wa One Men One Vote, Juu ya hivyo, Hizbu ilikubali kushiriki katika uchaguzi huo kwa kuona kuwa msingi wa matakwa yao Ulipatikana, nao ni kuanzishwa kwa uchaguzi wa Common Roll kwa kukubaliwa minsingi hii Zanzibar, Ikawa ndio nchi ya mwanzo katika Afrika Mashariki, Afrika ya Kati na ya Kusini kuanzishwa uchaguzi kama huo. Baada ya Kupatikana haya Hizbu-Wanatta ilizindisha juhundi za kuwafahamisha wananchi misingi na faida ya kuchaguwa Wawakilishi wao kwakupitia uchaguzi huo.
Merehemu Sheikh Amani Thani Fairuz Mwenyezi Mungu Mlaze Pema Peponi Ameen.

KISHA NYINYI MUNAYAITA MAPINDUZI MATUKUFU HIVI KWELI NYINYI MUNAJUWA UTUKUFU NI NINI AU DUNIA IMEWAVA KISAWA SAWA MPAKA MNAKUFURU MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA KATUPINDUWA TENA WAZANZIBARI NA KUWEKA VIONGOZI WAWATAKAO WAO WAKINA BT TUNAENDELEA TENA KUKA CHINI YA SERIKALI YA KIKOLONI YA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA MPAKA MIAKA MITANO IMALIZIKE KISHA TUTIWE TENA KATIKA SHENGESHA LA UCHAGUZI NA KUPIGA KURA KISHA WAZANZIBARI WAPIGE KURA NA KUCHAGUWA VIONGOZI WAWATAKAO MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA ATAKUJA NA STYLE MPYA YA KUZIPIGA KURA ZA WAZANZIBARI CHINI NA KUTUEKEA VIONGOZI WAWATAKAO KISHA TUTAKA TENA CHINI NA KUSUBIRI UCHAGUZI WA 2025 MAMBO YATAKUWA HIVYO HIVYO KISHA TUTAKA CHINA NA KUSUBIRI UCHAGU WA WA 2030 TUKIWA HAI KAMA HATUKO TENA WATAKAO BAKI WATAFANYIWA TENA HIVYO HIVYO NA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA KISHA WATAKA CHINI WASUBIRI......>>> MPAKA KIYAMA KISIMAME BASI NI BORA TU TUKUBALI KUWA NDIO TUMEKUBALI KUWA CHINI YA MKONI MWEUSI TANGANYIKA KULIKO UPUMBAVU HUU WA UCHAGUZI AMBAO KILA MOJA WETU HAPA ZANZIBAR KAMA UCHAGUZI WA MARA HII HAUJAWASOMESHA WALA HATUTA SOMA TENA MILELE. 

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment