WAKOLONI NA NYERERE NDIO WAASISI WA AFRO-SHIRAZI
Wakuu wa Sirekali wa Idara ya Utawala, Zanzibar baada ya kuona kuwa mpaka kuondoka kwa mchunguzi Coutts Zanzibar na mpaka kuleta mapendekezo ya uchaguzi wake, hapakuweza kuasisiwa chama chengine cha kisiasa nchini ili kipate kushindana Hizbu-Wattan (ZNP), waliamua kumtumilia Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Wakoloni Walimtumilia Mwalimu kwa kuja Zanzibar kujaribu kuwashawishi waongozi wa vyama viwili vya kikabila waweze kuungana na kuasisi chama kimoja cha kisiasa ili kiweze kushiriki katika uchaguzi na kiweze kuwa pingamizi kwa Chama Cha Hizbu. Katika ripoti ya Mr. Penny aliyekuwa Muangalizi wa Uchaguzi aliandika, Ofisi yangu na Idara ya Utawala zilisaidia kuundwa kwa Afro-Shirazi na kwahivyo ikaokolewa Zanzibar na kuwa na Utawala wa Chama Kimoja wa namna ya khatari;
Mwalimu Nyerere alikuja Zanzibar pamoja na Sheikh Zubeir Mtemvu mnamo mwisho wa mwaka 1956. Mwalimu pamoja na ujumbe wake alikutana na waongozi wa African Association, Sheikh Abeid Amani Karume,Bwana Mtumwa Borafia na Bwana Boniface. Waongozi wa Shirazi Association Alikutana nao Nyerere katika ujumbe wake huo ni,Sheikh Ameir Tajo, Sheikh Thabit Kombo Jecha na Sheikh Othman Shariff Musa. Mkutano huo ulifanyika katika nyumba ya Sheikh Abeid Amani Karume iliyokuwepo mtaa wa Kachorora, Mwembe Kisonge. Nyumba hio kwa wakati huo, ilikuwa ikikaliwa na Maalim Haji Ali Mnoga na Bwana Hija Saleh Hija. Njma hizo za Wakoloni na Mwalimu Nyerere zilifanikiwa. Taarikhi 2 Februari 1957 , miezi michache tu kabla ya kufikia Uchaguzi wa mwanzo wa Juni 1957 Chama Cha Afro-Shirazi kiliasisiwa rasmi. (kikiwa ni Muungano wa Jumuiya Mbili za kikabila yaani African Association na Shirazi Association) Karume akawa Rais wa Chama Sheikh Ameir Tajo Makamo wa Rais na Thabit Kombo Katibu Mkuu. Uwongozi wa Chama haukwenda kwa Mzalendo, haukwenda laa kwa Sheikh Ameir Tajo, wala kwa Sheikh Thabit Kombo, wala kwa Sheikh Othamani Shariff bali kwa Mzee Karume. Mbinu na njama za kuuwangamiza Uzanzibari zilianzwa zamani.
UCHAGUZI WA MWANZO JUNI 1957
Kutokana na mapendekezo ya Uchunguzi wa Bwana Coutts kukhusu uchaguzi, Uchaguzi wa mwanzo ulifanyika, juni, 1957. Na kwa uchaguzi huo ndio wananchi wa Unguja na Pemba kwa mara ya kwanza waliweza kushiriki katika kuwachagua wawakilishi wao wa Baraza la Kutunga Sheria la nchi yao. Uchaguzi huu ulikuwa wa viti sita. Majimbo Mane yalikuwa kwa Unguja na mawili Pemba. Majimbo sita hayo yaligaiwa kama hivi.
1) Unguja; Majumba ya Mawe
2) Unguja; N;gambo
3) Unguja; Kaskazini
4) Unguja; Kusini
1) Pemba Kaskazini
2) Pemba Kusini
Sheikh Ali Muhsin alisimama katika jimbo la N;gambo akiwa ni Muwakilishi wa Hizbu-Wattan, akishindania na Sheikh Abeid Karume akiwa Muwakilishi wa Afro-Shirazi, na Sheikh Ibuni Saleh alisimama katika jimbo hilo hilo akiwa ni Mgombea huru. (independent candidate) Bwana Rutti Bulsara alisimama katika jimbo la Majumba ya Mawe akiwa Mwakilishi wa Hizbu na washindani wake wakiwa, Bwana Choudhry, Mwakilishi wa Muslim Association, Bwana Anverali Hassan Virji, mgombea huru na Bwana AbdulQadir Mukri, akiwa naye pia ni mgombea huru. Sheikh Amour Zahor alisimama jimbo la kusini akiwa ni Mwakilishi wa Hizbu na Sheikh Ameir Tajo akiwa ni Mwakilishi wa Afro-Shirazi katika jimbo hilo hilo. Sheikh Haji Muhammad alisimama katika jimbo la Kaskazini akiwa ni mgombea huru akiungwa mkono a Hizbu, Sheikh Daud Mahmoud yeye alikuwa Mwakilishi wa Afro-Shirazi katika jimbo hilo. Hizbu ilimuunga mkono Sheikh Haji Muhammad kwa kuamini kuwa ana fikra za kizalendo, na kutarajia kuwa hayuko mbali bali naye atajiunga na wananchi wenziwe ndani ya Hizbu-Wattan; na hakika ikawa hivyo. Pemba kusini alisimama Sheikh Rashid bin Ali Khaify akiwa Mwakilishi wa Hizbu na Sheikh Muhammed Shamte Hamad alisimama jimbo hilo akiwa mgombea huru. Pia alisimama katika jimbo hilo Sheikh Abdallah bin Suleiman Busaidy, akiwa naye ni mgombea huru. Pemba Kaskazini alisimama Sheikh Rashid Hamad Othman akiwa Mwakilishi wa Hizbu,Sheikh Ali Shariff Musa akiwa mgombea Huru na Sheikh Shaaban Soud Mponda akiwa Mwakilishi wa Afro-Shirazi. Matokeo ya uchaguzi huo, Chama Cha Afro-Shirazi kilipata viti vitatu Unguja na hakikuweza kupata hata kiti kimoja Pemba. Hizbul-Wattan ilishindwa kupata hata kiti kimoja laa Unguja wala Pemba. Viti viwili vya Pemba vilichukuliwa na wagombea huru wake, yaani Sheikh Muhammed Shamte na Sheikh Ali Shariff, baadae waliviunga viti vyao kwenye Afro-Shirazi na kuwa na viti vitano katika Baraza Jipya la Kutunga Sheria. Kiti kimoja cha Nyumba za Mawe, kilichukuwa na Bwana Chodhry Mwakilishi wa Muslim Association. Natija hii ya Uchaguzi inathibitisha kuwa Hizbu ni chama kilicho asisiwa bila ya kutokana na asili ya chama au jumuiya ya kikabila iliyokuwepo nchini kwa muda, kama vile ilivyokuwa hali kwa Afro-Shirazi. Na kwa vile Hizbu-Wattan ilikuwa ndio kwanza chama kichanga haukustaajbu kwa kutopata hata kiti kimoja katika uchaguzi huu, kwani kilikuwa bado hakijawafikilia wananchi kwa wingi. Amma Afro-Shirazi ambayo ni muungano wa jumuiya mbili za kikabila, jumuiya ambazo kwa muda zilikuwa zishakuwepo nchini hakikupata taabu kupata ushindi wa uchaguzi huu, Kwani wanachama wake ndio walewale. Tafauti na Hizbu-Wattan ambayo ilibidi ikuwe kwa kupitia kwa wananchi polepole
1) Unguja; Majumba ya Mawe
2) Unguja; N;gambo
3) Unguja; Kaskazini
4) Unguja; Kusini
1) Pemba Kaskazini
2) Pemba Kusini
Sheikh Ali Muhsin alisimama katika jimbo la N;gambo akiwa ni Muwakilishi wa Hizbu-Wattan, akishindania na Sheikh Abeid Karume akiwa Muwakilishi wa Afro-Shirazi, na Sheikh Ibuni Saleh alisimama katika jimbo hilo hilo akiwa ni Mgombea huru. (independent candidate) Bwana Rutti Bulsara alisimama katika jimbo la Majumba ya Mawe akiwa Mwakilishi wa Hizbu na washindani wake wakiwa, Bwana Choudhry, Mwakilishi wa Muslim Association, Bwana Anverali Hassan Virji, mgombea huru na Bwana AbdulQadir Mukri, akiwa naye pia ni mgombea huru. Sheikh Amour Zahor alisimama jimbo la kusini akiwa ni Mwakilishi wa Hizbu na Sheikh Ameir Tajo akiwa ni Mwakilishi wa Afro-Shirazi katika jimbo hilo hilo. Sheikh Haji Muhammad alisimama katika jimbo la Kaskazini akiwa ni mgombea huru akiungwa mkono a Hizbu, Sheikh Daud Mahmoud yeye alikuwa Mwakilishi wa Afro-Shirazi katika jimbo hilo. Hizbu ilimuunga mkono Sheikh Haji Muhammad kwa kuamini kuwa ana fikra za kizalendo, na kutarajia kuwa hayuko mbali bali naye atajiunga na wananchi wenziwe ndani ya Hizbu-Wattan; na hakika ikawa hivyo. Pemba kusini alisimama Sheikh Rashid bin Ali Khaify akiwa Mwakilishi wa Hizbu na Sheikh Muhammed Shamte Hamad alisimama jimbo hilo akiwa mgombea huru. Pia alisimama katika jimbo hilo Sheikh Abdallah bin Suleiman Busaidy, akiwa naye ni mgombea huru. Pemba Kaskazini alisimama Sheikh Rashid Hamad Othman akiwa Mwakilishi wa Hizbu,Sheikh Ali Shariff Musa akiwa mgombea Huru na Sheikh Shaaban Soud Mponda akiwa Mwakilishi wa Afro-Shirazi. Matokeo ya uchaguzi huo, Chama Cha Afro-Shirazi kilipata viti vitatu Unguja na hakikuweza kupata hata kiti kimoja Pemba. Hizbul-Wattan ilishindwa kupata hata kiti kimoja laa Unguja wala Pemba. Viti viwili vya Pemba vilichukuliwa na wagombea huru wake, yaani Sheikh Muhammed Shamte na Sheikh Ali Shariff, baadae waliviunga viti vyao kwenye Afro-Shirazi na kuwa na viti vitano katika Baraza Jipya la Kutunga Sheria. Kiti kimoja cha Nyumba za Mawe, kilichukuwa na Bwana Chodhry Mwakilishi wa Muslim Association. Natija hii ya Uchaguzi inathibitisha kuwa Hizbu ni chama kilicho asisiwa bila ya kutokana na asili ya chama au jumuiya ya kikabila iliyokuwepo nchini kwa muda, kama vile ilivyokuwa hali kwa Afro-Shirazi. Na kwa vile Hizbu-Wattan ilikuwa ndio kwanza chama kichanga haukustaajbu kwa kutopata hata kiti kimoja katika uchaguzi huu, kwani kilikuwa bado hakijawafikilia wananchi kwa wingi. Amma Afro-Shirazi ambayo ni muungano wa jumuiya mbili za kikabila, jumuiya ambazo kwa muda zilikuwa zishakuwepo nchini hakikupata taabu kupata ushindi wa uchaguzi huu, Kwani wanachama wake ndio walewale. Tafauti na Hizbu-Wattan ambayo ilibidi ikuwe kwa kupitia kwa wananchi polepole
KWA NINI ALI MUHSIN ALIAMUWA KUSIMAMA NG;AMBO BADALA YA MAJUMBA YA MAWE
Sheikh Ali Muhsin alikuwa na hakika mia juu ya mia kuwa hatoweza kumshinda mpinzani wake katika sehemu hiyo kama alivyokuwa na hakika kuwa angeweza kupata ushindi ingekuwa amesimama katika Jimbo la Majumba ya Mawe. Lakini alitaka kuthibitisha kuwa kura chache za wananchi wenye asili mbali mbali zilikuwa pia nazo zina umuhimu katika kuendeleza siasa ya chama, si kasoro kuliko kura nyingi ambazo angeweza kuzipata katika Majumba ya Mawe. Lengo likuwa ni kuondowa ukabila na urangi. Kura 918 ndizo alizozipata, lakini zilikuwa na umuhimu mkubwa kwa chama na ziliongeza kumpa moyo zaidi katika kuendelea na juhudi za ugombozi wa nchi. Uchaguzi ulifanyika kwa salama na ulimalizika kwa salama ingawa wakoloni walijaribu kutaka zitoke fujo wakati wa uandikishaji wa uchaguzi. Kwani badala ya wao (wakiwa ndio serikali) kuchukua dhamana ya kuchunguwa na kuhakikisha ni nani mwenye kustahiki kuchagua na kuchaguliwa, kazi hiyo waliitupia vyama vya siasa. Kweli Sheria waliziweka za kuwa ni raia wa Zanzibar tu ndiye mwenye haki ya uandikishaji na upigaji wa kura, lakini sharia hizo hawakuzilinda na kuhakikisha kuwa zinatekelezwa. Matokeo yake kulitokea kupingana na kuzozana baina ya watu wenyewe kwa wenyewe na hayo ndiyo yaliyozidi kupalilia chuki na ukhasama. Katika uchaguzi huu, wageni wengi khasa kutoka Tanganyika ambao walikuwa wakiishi Zanzibar walipenya katika kujiandikisha na walipiga kura. Hata hivyo, si haba uchaguzi uliweza kufanyika kwa salama bila ya kutokea fujo la namna yoyote.
KWENYE SHARI HUZALIWA KHERI
Kushindwa Hizbu-Wattan katika uchaguzi wa mwanzo, ndiko kuliko zidi kuwazinduwa wananchi na kujitokeza paruwanja katika kusimama bega kwa bega na wanachi, wazalendo wenziwao katika juhudi za kuigombowa nchi yao kutokana na ukoloni wa Kiingereza. Baada ya kumalizika kwa machofu ya pirika pirika za uchaguzi, Chama cha Hizbu kilitayarisha mkutano maalumu wa hadhara katika Jumba la Seyyid Khalifa Hall (sasa ati linaitwa Karume House) Umma wa kike na wakiume uliomiminika siku hiyo ulikuwa wa aina ya peke yake. Haukupata kutokea tangu kuanza kwa harakati za kisiasa katika Zanzibar. Kwa jinsi mabibi walivyokuja kwa wingi kwenye mkutano huo, ililazimu wanaume wote waliyokuwemo katika ukumbi wa jumba hilo watoke nje kwa kuwapisha mabibi. Wanaume, wao walika katika uwanja wa Bustani ya jumba hilo. Siku hiyo ndipo wanawake walipodai wawe na sehemu yao katika Chama, na wapate kura sawa na wanaume. Waliopiga kifuwa mbele kati yao ni BiZuhura bt Saleh, BiSharifa Ahmed na BiZamzam Sultan. Kuanzia siku hiyo, kila usiku uchao, wananchi wake kwa waume walikuwa wakijitokeza kwa wingi katika kujiunga na Chama cha Wazalendo wenziwao. Waongozi wa chama kwa kulingana na umma unavyozidi kujiunga na chama kila siku ilibidi watengeneze mibango kukhusu kueneza mafunzo na siasa chama kila upande.
KUKUWA KWA HARAKATI ZA ZA SIASA
Baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa juni 1957, Hizbu ilianza kutayarisha mapango ya kuaneza fikra na siasa ya chama kwa Unguja na Pemba kwa mjini na mashamba. Natija ya juhudi hizo haikuchukuwa muda illa zilidhihiri. Matawi ya Hizbu yalikuwa yakifunguliwa kila siku Unguja na Pemba, mjini na mashamba. Kila Tawi ilikuwa na skuli yakusomeshea vijana na watu wazima (wa kike na wa kiume) waliokuwa hawakuwahi kuingia skuli wakati wa udogo wao. Vilevile kila Tawi lilikuwa na kituo cha kutoa; Huduma ya Kwanza (First Aid) kwa wenye kufikwa na maradhi madogo madogo. Vijana wa Youth Own Union ndio waliyokuwa walimu wa kusomesha na ndio waliyokuwa waganga wa kutibu maradhi madogo madogo. Sheikh Juma Aley, aliyekuwa Waziri wa Fedha katika Serikali ya ZNP / ZPPP, na yeye ndiye aliyekuwa akiwapa vijana hao mafunzo ya haraka juu ya namna ya kusomesha. Dr. Said Aboud Bin Tahir, yeye alikuwa akiwapa mafunzo juu ya matibabu madogo madogo. Sheikh Ali Makka na Sheikh Juma Ali (dogo dogo) wao wakitijitolea kwa kuwapa wogonjwa matibabu katika kituo cha matibabu cha Hizbu kilichokuwepo katika Jumba la Makao Makuu ya Chama, hapo Darajani. Katika kituo hicho vilikuwepo kila vifao vyenye kuhitajika kwa matibabu. Wagonjwa walikuwa wakiangaliwa na wakitibiwa bila ya malipo yoyote na bila ya kutizamwa msimamo wao wa kisiasa. Mu-Hizbu na Mu-Afro wote walikuwa wakipata matibabu sawa sawa. Pia katika Makao Makuu hayo ya chama kulikuwepo na sehemu ya Welfare ambayo ilikuwa ikijishughulisha na mambo ya kutoa misaada ya dharura kwa mwananchi yoyote (si kwa wananchama wa Hizbu tu). Sehemu hiyo ya Welfare ilikuwa na gari mbili za kuchukulia wagonjwa (ambulance) kutoka majumbani mwao kwa wale waliokuwa hawawezi kwenda kwa miguu yao au wanaishi katika sehemu zilizo mbali na Hospitali, kama mashamba na sehemu zengine. Pia sehemu hiyo ya Welfare ilikuwa ikishughulikia kuweka majina ya wananchi wanaojitolea kutoa damu kwa kusaidia wagonjwa. ilifika hadi Hospitali Kuu ya serikali wakihitaji damu kwa sababu ya wagonjwa, wakenda katika sehemu hiyo ya Welfare ya Hizbu kuomba watu wa kutoa damu. Vilevile ilifika wakati mmoja hospitali ya serikali kuazima dawa fulani kutoka katika kituo cha Hizbu cha matibabu. Sehemu hiyo ya Welfare ilikuwa chini ya uangalizi wa Seyyid Hashim Bin Abubakar Bin Salim, Bibi Aisha Salim (maarufu Bibi Aisha wa YOU au Aisha Mtumbatu) na Bibi Azza Mohammed Seif (mamawatoto wa Sheikh Ali Muhsin). Miongono mwa harakati za Hizbu katika kuwahudumia wananchi, wazee na vijana wa kiume na wa kike walijitolea bila ya malipo kwa ujenzi wa njia ya Nungwi. Mwishowe serikali ikaingia kusaidia katika ujenzi huo kwa kulete mepango ya siku moja kuwalipa na siku moja ya kujitolea. Yaani katika siku 30, wakilipwa siku 15. Mpango huo ukaitwa Jisaidie Nikusaidie. Vile vile Mahizbu kwa kuendeleza huduma kwa wananchi wenziwao walijiitolea kuijenga njia ya Uzi toka mwanzo mpaka mwisho, kwa kuunganisha kisiwa cha Uzi na kisiwa kikubwa cha Unguja hapo Unguja Ukuu. Pia walijitolea kuwapelekea maji ndugu zao wa Tumbatu. Wakati wananchi wa Tumbatu walipokuwa na shida kubwa ya maji Chama kilokodi matishali na kupakia mapipa ya maji kutoka mjini mpaka Tumbatu. Ikiwe nitaendelea kutaja ya kheri yaliokuwa yakifanywa na Chama Cha Hizbu katika kuwahudumia wananchi, basi itanifanya nisiendelee na hayo niliiyo yakusudia khasa kuzungumza na wananchi wenzangu. Kwahivyo, haya machache yanatosha kukupeni sura na fikra namna gani Chama cha Hizbu kilivyokuwa kikiendeshwa. Na kutokana na maedesho kama hayo, ndipo kila uchao wananchi walikuwa wakijiunga na Wazalendo wenziwao.
ATI HUSEMWA KUWA HIZBU IMEFELI!!!
Ikiwa Hizbu imefeli, iliyo fuzu ni ipi..? Yaliyofanywa na Hizbu kikiwa ni Chama tu cha siasa, basi serikali ya Zanzibar hii iliyokuwepo ya MAVAMIZI kwa muda wa miaka 30 (1964-1994) haijaweza kuyafanya. Hospitali za serikali kuwa hazina hata vidonge vya panadol licha ya Penicillin, ndio kufuzu huko...? Skuli za serikali kuwa hazina hata madeski ya kukalia, licha Walimu wajuzi wa kusomesha, ndio kufuzu huko..? Wanafunzi wa Chuo cha kujifunza Uwalimu hawana hata matandiko wala mashuka katika vitanda vyao. Chakula ni cha mipango mipango na wakati mwingi wanafunzi wanalala na njaa kwa ukosefu wa chakula cha kutosha. Huko, ndiko kuffuzu...? Barabara hazipitiki kwa uchafu wa maji ya makaro. Katika kila taa 10 za njiani, taa mbili tu ndizo zinazowaka na muwako wenyewe utadhani globu ya kurunzi (tochi) uchwara. huko ndio kufuzu...? Baada ya miaka 30 ya utawala wa serikali yenye kujiita ya MAPINDUZI kiwanja cha ndege cha Zanzibar hakina hata kiti kimoja cha kukalia wajao kuwashindikiza wasafiri wao. Ikiwa huko ndio kufuzu, basi hatujuwi kufeli kutakuwa na sura gani. Inaweza kuwa huko ndio kufuzu, yatengemea nia na azma za waongozi wa hizo serikali. Bali kwa nchi na wananchi huko hata kwa lugha gani hakuitwi kufuzu, bali ni Kudamirika. Kudamirika ambako ni sawa na kuteremkiwa na balaa, kwa iteremkapo balaa ya Mwenye Enzi Mungu (kwa maasi ya binaadamu) humfika mwema na mbaya. Maafa ya Zanzibar yamemteremkia kila mwananchi, mwema na mbaya, (In shaa Allah wako hao wema). Sababu kubwa ya hivyo ni kuwa juu ya maovu yaliyofanywa na yaendeleayo kufanywa hakuna tena kukatazana maovu na kufahamishana kutenda mema, na hapo ndipo Mwenye Enzi Mungu azidishapo nakama Zake. Mwenye Enzi Mungu tunakuwomba utunusuru.
KUGAWANYIKA KWA AFRO-SHIRAZI
Sheikh Ameir Tajo wa Kwanza Mwenye Kilemba Cheupe Alifukuzwa Afro-Shirazi na Abeid Karume
Mwanzoni mwa mwa 1959 kulitokea mgawanyiko wa wangozi wa Chama cha Afro-Shirazi. Sheikh Mohammed Shamte na Sheikh Ali Shariff waliamua kujitoa katika Chama na kwa kutoka kwao, kulifuatiwa na wananchama wenginyuma yao na khasa Pemba. Katika wakati huo huo, Chama cha Afro-Shirazi kilimfukuza katika Chama Sheikh Ameir Tajo kwa singizio la kuwa alikwenda kuwaombea msaada wa fedha vijana wa YASU (Young African Social Union) kwa Sir Tayebali Karemjee kwa ajili ya ujenzi wa klabu (club) yao iliyokuwepo Miembeni bila ya kuiarifukamati kuu ya Afro-Shirazi. Sababu Kubwa zilizompelekea Sheikh Mohammed Shamte na wenziwe kujitoa katika chama cha Afro-Shirazi ni zenye kutokana na hisia za uwanachama khalisi kwa nchi yake. Hisia zake za kisiasa na nyendo zake pamoja na matarajio yake juu ya nchi yake yalikuwa yakutaka kutumikia upatikanaji uhuru wa Zanzibar. Uhuru utaongozwa na Wazanzibari wenyewe bila ya kuchukua amri au shauri kutoka pahala pengine popote. Sheikh Karume yeye alikuwa hawezi kufanya lolote bila ya kuzungumza na Mwalimu Nyerere na kama
Karume alikuwa hawezi kufanya lolote bila ya amri ya Mwalimu
itavyoamuliwa na Mwalimu, ndivyo hivyo hivyo itavyofuata hata ikiwa si maslahi kwa Zanzibar. (mara nyingi hivyo ndivyo ilivyokuwa) Sheikh Mohammed Shamte, hayo yeye alikuwa hayakubali; kwahivyo daima walikuwa wakibuburushana mpaka mambo yalipofika hadi ya kufanywa mikutano ya Kamati Kuu ya Chama bila ya kuarifiwa Sheikh Mohammed kwa kukhofiwa kuwa akiwepo ataleta upingaji juu ya baadhi ya mambo. Ilipofika kiwango hichi, maji kuzidi unga, Sheikh Mohammed na Sheikh Ali Shariff walijitoa katika Afro-Shirazi.
KUASISIWA KWA ZANZIBAR AND PEMBA PEOPLE PARTY
(ZPPP)
Chama cha Z.P.P.P. kiliasisiwa November, 1959. Raisi wa Chama alikuwa Mohammed Shamte Hamad na Naibu Raisi alikuwa Sheikh Ameir Tajo. Makao Makuu ya Chama yalikuwa Malindi Zanzibar. Z.P.P.P. kilikuwa chama cha wananchi wa Unguja na Pemba. Kwa Unguja hakikuweza kupata wanachama wengi kwa wakati huo lakini kwa Pemba kiliweza kupata wananchi wengi kujiunga katika chama. Misingi na dhamira ya Z.P.P.P. ikilingana na ya Hizbul-Wattan. Nayo nikufanyakazi kwa pamoja Wazanzibari wote, kubali rangi, kabila au imani zao za kidini katika kugombania kupatikana uhuru wa Zanzibar kwa ajiili ya mslahi ya wananchi wote. Waongozi wa Hizbul-Wattan hawakuwa na shaka yoyote juu ya uzalendo wa Sheikh Muhammed Shamte na wenziwe, kwahivyo walikuwa wakiamini kuwa iko siku wataweza kufanyakazi pamoja.
Merehemu Sheikh Amani Thani Fairuz Mwenyezi Mungu Mlaze Pema Peponi Ameen.
KISHA NYINYI MUNAYAITA MAPINDUZI MATUKUFU HIVI KWELI NYINYI MUNAJUWA UTUKUFU NI NINI AU DUNIA IMEWAVA KISAWA SAWA MPAKA MNAKUFURU MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA KATUPINDUWA TENA WAZANZIBARI NA KUWEKA VIONGOZI WAWATAKAO WAO WAKINA BT TUNAENDELEA TENA KUKA CHINI YA SERIKALI YA KIKOLONI YA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA MPAKA MIAKA MITANO IMALIZIKE KISHA TUTIWE TENA KATIKA SHENGESHA LA UCHAGUZI NA KUPIGA KURA KISHA WAZANZIBARI WAPIGE KURA NA KUCHAGUWA VIONGOZI WAWATAKAO MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA ATAKUJA NA STYLE MPYA YA KUZIPIGA KURA ZA WAZANZIBARI CHINI NA KUTUEKEA VIONGOZI WAWATAKAO KISHA TUTAKA TENA CHINI NA KUSUBIRI UCHAGUZI WA 2025 MAMBO YATAKUWA HIVYO HIVYO KISHA TUTAKA CHINA NA KUSUBIRI UCHAGU WA WA 2030 TUKIWA HAI KAMA HATUKO TENA WATAKAO BAKI WATAFANYIWA TENA HIVYO HIVYO NA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA KISHA WATAKA CHINI WASUBIRI......>>> MPAKA KIYAMA KISIMAME BASI NI BORA TU TUKUBALI KUWA NDIO TUMEKUBALI KUWA CHINI YA MKONI MWEUSI TANGANYIKA KULIKO UPUMBAVU HUU WA UCHAGUZI AMBAO KILA MOJA WETU HAPA ZANZIBAR KAMA UCHAGUZI WA MARA HII HAUJAWASOMESHA WALA HATUTA SOMA TENA MILELE.
No comments:
Post a Comment