Wednesday, November 9, 2016

VIDEO-NASAHA KWA VIONNGOZI WOTE MAADHALIM NA WAENDELEZAJI WA DHULMAA NCHINI ZANZIBAR


Uchaguzi Zanzibar . 20~03~2016

Maalim Zuber Juma Khamis ni miongoni mwa walimu wa zamani wa Unguja, aliyesomesha skuli nyingi hasa skuli za mjini.
Maalim Zuber, kitaaluma ni mwalimu wa skuli, baadaye alibadilisha kazi na kuhamia katika kazi ya uhakimu katika mahakama za wilaya. Ni mwenyekiti wa pili tangu Tume ya Uchaguzi ya nchi ya Zanzibar (ZEC) kuanzishwa.
Maalim Zuber, aliteuliwa na Rais wa Zanzibar, Dk Salmin Amour (awamu ya 5) kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), mapema mwaka 1995 baada ya mwenyekiti wa kwanza wa tume hiyo, Maalim Mwinyiwesa Idarous, kujiuzulu kwa kashfa za kuropokwa.
Maalim Zuber kwa muda wa miaka mingi sana aliishi Hamamni, kwenye nyumba zilizopo Jaws Corner,nchini Zanzibar.
Alihama eneo hili la Jaws Corner baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 ambao uliibua utata na shangwe za migogoro kwa muda wote wa miaka mitano.
Maalim Zuber, alidorora sana katika kumtangaza mshindi wa u-rais wa nchi ya Zanzibar, ilhali ilijuilikana wazi kuwa CUF, ilishinda hadi kupelekea Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, kulalamika kwa kusema hawakubaliani na matokeo ya uchaguzi yalivyo.
Uchaguzi ulifanyika siku ya Jumapili, Jumatatu adhuhuri kura zote za urais zilikuwa zimeshahesabiwa, mshindi tayari alishajuilikana na kila mtu. Maalim Zuber, alimwendea Dk Salmin kumueleza kuwa ameshindwa.
Nakumbuka, Maalim Zuber ambaye BARAZA yake kubwa ya mazungumzo ilikuwa ni pale kwenye ukuta wa Skuli ya Mkunazini, kuelekea upande wa barabar ya Darajani.
Pamoja na kwamba alijitahidi kutunza siri lakini, kafa na siri nzito moyoni ya dhulma. Wapo wazungumzaji wake wanajuwa ukweli wa mambo.
Mbali ya Gazeti la Majira kutangaza matokeo siku ya Jumanne, kwamba CUF imeshinda lakini waandishi wengi wa ndani na nje walikuwa tayari na draft zao zinazoonesha kuwa CUF, imeshinda.
Maalim Zuber, alipotangaza mshindi wa u-rais Jumatano, na kumtanza Dk Salmin, mwandishi wa BBC World News, alibishana na Maalim Zuber: “No…No…Noooooo Salmin No…No…Noooo Salmin!. Alipiga mayowe na kwenzi akipinga kuwa Dk Salmin, hakushinda.
Waandishi wa habari wengi walishtushwa na matokeo kumtangaza Dk Salmin badala ya Maalim Seif, hali iliyoonesha wazi kuwa CUF ni mshindi wa u-rais.
Lakini, hata waangalizi la uchaguzi huo wa ndani na wa nje wote walijuwa kuwa CUF imeshinda na baada ya Maalim Zuber, kutangaza matokeo reports za waangalizi wa kimataifa zilieleza kuwa na shaka na utangazaji wa matokeo. Reports za waangalizi wa ndani hadi leo zimebakia kuwa embargo.
Kwa ufupi, Maalim Zuber Juma Khamis, Jecha Salim Jecha na wenyeviti ZEC wengine wote waliyopita na wajao kwa tume ya uchaguzi ya aina ya Maalim Zuber na Jecha, CUF isitarajie kabisa kutangazwa mshindi wa u-rais wa nchi ya Zanzibar. Hilo CUF, wanalijuwa 100 fil 100 isipokuwa ni ‘kuku lalalala kipanga yuwaja’.
Rais wa SMZ wa sasa Dk Ali Mohamed Shein, anajuwa kwa dhati kwamba si rais aliyechaguliwa kwa ridhaa ya wananchi wa nchi ya Zanzibar.
Ma-Rais wote wa nchi ya Zanzibar waliyopita tangu mfumo wa vyama vingi kuanza 1995, wanajuwa kwa dhati kuwa wanakaa madarakani kwa mabavu ya Mkoloni Mweusi Tanganyika lakini, si kwa ridhaa ya Wazanzibari.
Isipokuwa ma-Rais wa nchi ya Zanzibar, Dk Salmin Amour na waliyofuata wote baadaye wanapaswa kufahamu kuwa kuna siku ya hesabu na hukumu.
Kuiba au kudhulumu ni uamuzi wa mtu mwenyewe kutoka ndani ya nafsi yake. Huko hakuna Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Mkapa, Kikwete wala Magufuli wa kuweza kuwalinda na kuwatete.
Kama ana akili na uwezo wa kusema kwamba hakuna ICC wala UN ya kuweza kumuondoa madarakani basi, akumbuke kuna mauti, kuna siku ya hesabu na kuna siku ya hukumu.
Kwa ufupi, kuna siku ya mwisho ambayo hiyo haina utetezi lakini pia, kuna siku ya hesabu na hukumu. Siku hiyo hakuna king’ora wala Jeshi la Polisi wa FFU na gwaride la uwanja wa Amani.
Siku hiyo hakuna mlinzi wa kumlinda kwa mgangoni wala hakuna uombezi kutoka kwa Mkoloni Mweusi Tanganyika, kumlinda Rais wa Zanzibar, aliyedhulumu maamuzi ya watu.
Imeteremshwa Qur’an na haitoshi watu (waislamu) wametakiwa kuhudhuria misikitini kusikiliza darsa na mawadha ili kuzidi kujifunza na kujikumbusha kujuwa mazuri na mabaya, kujuwa dhulma na haki, kujuwa dunia na akhera na kujuwa pepo na moto. Viongozi wa Zanzibar, wajuwe hivyo..

No comments:

Post a Comment