Friday, June 7, 2013

UPUUZI WA RASIMU YA KATIBA MPYA NA UWANDIKIWAJI WAKE WA KILEVI

                                                                                                                                                                                                 

Rasimu ya katiba mpya na upuuzi wake inaanza kwa kunichefua kwenye SURA YA KWANZA, SEHEMU YA KWANZA inayo zungumzia MIPAKA, ALAMA, LUGHA, UTAMADUNI NA TUNU ZA TAIFA  insema:
 
1.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenyemamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla ya Hati za Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi
huru.”
Ukiisoma vizuri ibara hii utaona kwamba, katiba mpya inatangaza kwamba Tanganyika na Zanzibar si nchi huru tena, kwani uhuru wao ulikoma mara baada ya hati za makubaliano ya Muungano ya Mwaka 1964!!! Hii ndo kusema kwamba, uhuru wa Zanzibar ulikoma April 26, 1964! Huu ni upuuuzi!  Zanzibar bado ni nchi huru, muungano, haukuondoa uhuru wa mataifa haya! Kama kanuni ya kushirikiana ni kuondoa uhuru wako basi hakuna nchi ambayo ingekubali kushirikiana na nchi nyengine!
 
Upuuzi mwengine nausoma SURA YA NNE inayo zunguzumzia HAKI ZA BINADAMU, WAJIBU WA RAIA NA MAMLAKA ZA NCHI, kwenye kipengele cha
Uhuru wa imani ya dini, kinasema:

 31.-(5) Ni marufuku kwa mtu, kikundi au taasisi ya dini kutumia uhuru wa kutangaza dini kwa kukashifu imani na dini nyingine, kujenga chuki au kuchochea vurugu na ghasia kwa madai ya kutetea imani au dini.”

Sijui hawa waloandika rasimu hii walikuwa wapo katika hali gani!! walikuwa washakunywa chibuku kwanza au tusker sijuwi. Kimsingi dini zote asili yake ni kupingana!! Mafundisho ya dini moja hayawezi kuwa sawa 100% na ya dini nyengine, kama ingekuwa hivyo kusingekuwa na dini mbali mbali! Na kwa kuwa msingi ni kutofautina (kupingana), ni wazi kabisa mafundisho ya dini mbili katika ”ishu” flani yanapotofautina huwa ni kashfa kwa kila upande  dhidi  ya mafundisho ya mwenzake.
Mathalani; Wakristo katika kutumia  katika Biblia yao wanafundishwa kwamba Yesu ni mwana wa Mungu, na wengine katika Biblia hiyo hiyo wanafudishwa  Yesu ni Mungu, LAKINI waislam katika Quraani wanafundishwa Nabii Issa  (Yesu) ni mtume tu kama alivyokuwa Ibrahim, si Mungu wala si mwana wa Mungu! Katika muktasar huu, ni wazi kwamba dini hizi mbili zina kashifiana!! na hata hao wa kristo kwa wakiristo pia wanakashifiana maana hawa wanasema mwana wa mungu na hawa wengine wanasema ni mtume Iweje Mungu wa wengine wewe useme ni mtume kama alivyokuwa Ibrahim tu, ni kashfa hii au sio kashfa..??  Vile vile upande mwengine  iweje mtume wa wengine wewe useme ni Mungu, wakati wao wanaamini Mungu ni mmoja tu, hii ni kashfa!!!

Warioba na wenzake walitakiwa watupe “maelezo ya kifungu hiki, waeleze kinaga ubaga nini maana ya neno ”kukashifu” kama lilivyotumika katika sentensi hii! Jee waislam na wakristo wakigombea kumchinjia M/Mungu (Ng’ombe) wa wahindi ni kashfa kwa wahindi au sio kashfa..?? maana wahindi Ngo;mbe kwa ni mungu na waislamu na wakiristo Ngombe ni mnyama tu je si kashfa hiyo..?? Jee dini moja inasema Yesu kasulubiwa (kwa mujibu wa vitabu vyao) na wa dini nyengine   kwa mujibu wa vitabu vyao pia wanasema Yesu hakusulubiwa… Jee hapo yupi kamkashifu yupi.?? Mmoja akisema nguruwe haramu, mwengine anasema halali, yupi anamkashifu mwenziwe.??  Warioba na wenzake wanajaribu kujenga msingi wa matatizo….wangetafuta njia nyengine ya kuu address hii ishu, lakini si katika namna hii!
Mimi naogopa kifungu hiki kuja kutumika ndivyo sivyo na dini moja dhidi ya nyengine. Kwa mfano endapo kama watawala watakaokuja watakuwa wanawapendelea waislam, basi mafundisho yoote ya wakristo yatatafsiriwa ni kashafa kwa waislam kwa mujibu wa ibara hii! Hivyo wakristo watakosa uhuru wao wa kutangaza dini yao na kuhubiri, maana watakuwa wanakiuka katiba! Vile vile, ikiwa utawala ujao utawapendelea wakristo, basi waislam itabidi quraani yao waifungia kwenye makabati maana wakisoma na kueleza mafundisho itakuwa ina wakashifu wakiristo maana kila aya inayopingana na mafundisho ya ukristo itakuwa ni kashfa…ni wazi hawatakuwa na uhuru wakutangaza wala kuendesha dini yao!!
au warioba na hao walevi wengine walio andika hili gazeti mumeona hii ndio njia ya kuhalalisha kuwa serekali yenu haina dini..?
 
Nikaendelea kusoma SURA YA SITA,  inayohusu MUUNDO WA JAMHURI YA MUUNGANO.  Sehemu hii ya Muundo wa Muungano inasema:
57.-(1) Jamhuri ya Muungano itakuwa na muundo wa shirikisho lenye serikali tatu ambazo ni:
(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
(b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na
(c) Serikali ya Tanzania Bara.”
 
Huu ni upuuzi ulovuka mipaka, maana kwenye  sura ya kwanza Warioba amekiri kwamba JMT ni muungano wa mataifa mawili huru, Tanganyika na Zanzibar! Lakini cha ajabu anapopendekeza uwepo wa serkali tatu anaogopa kuirudisha Tanganyika! Eti serkali ya Tanzania Bara!!! Jee visiwa vyengine vilivyoko kwenye bahari ya hindi kama vile mafia ambavyo si sehemu ya  Zanzibar vitakuwa viko chini ya serkali ipi katika hizi mbili! Maana serkali ni za TZ bara na ZNZ tu! Kwanini Warioba aone tabu kuitaja Tanganyika..??

Katika ibara ya (5)  anasema Washirika wa Muungano watakuwa na hadhi na haki sawa ndani ya Jamhuri ya Muungano na watatekeleza majukumu yao kwa masuala yote yasiyo ya Muungano katika mamlaka ya Washirika wa Muungano kwa mujibu wa masharti yatakayowekwa na Katiba za Washirika wa Muungano”

Lakini cha ajabu baadae anasema wabunge wa Bunge la Muungano kutoka Zanzibar wawe 20, na kutoka bara wawe 50! Sasa hiyo hadhi na haki sawa ipo wapi hapo..??? ndio nikasema ni upuuzi mtupu.
 
Zaidi ni upuuzi kujifanya unaiachia Zanzibar iendeshe uchumi wake na ichangie gharama katika kuendesha serkali ya JMT, wakati umeibana kifursa katika njia za kuendesha uchumi wake!!! Zanzibar ni visiwa, uchumi wake unategemea bahari, biashara, na utalii! Hivyo sera zake katika kuendesha uchumi wake hazihitaji zitegemee fadhila au huruma kutoka Serkali ya Muungano!!
Unapoweka mambo ya nje kuwa ni ya Muungano, ni kuinyima fursa Zanzibar kutumia nafasi za uwakilishi wa mabalozi wake kwenye kuitangaza Zanzibar katika nyanja ya utalii na uwekezaji!! Kuweka ushuru kuwa ni sehemu ya Muungano, ni kuifanya Serkali ya Mapinduzi Zanzibar ishindwe kuifanya Zanzibar kuwa bandari huru, inafanya SMZ ifuate sera za uchumi wa nchi ya Tanganyika, ambazo kamwe haziwezi kuivusha Zanzibar, kwa sababu ki jiografia, kimali ghafi na kimazingira, Zanzibar na Tanganyika ziko tofauti sana, hivyo hata sera zao kiuchumi lazima ziwe tofauti ili ziiwezeshe nchi hizo kufaidi rasilimali zao na fursa za kichumi walizonazo!!!
Zanzibar ili iendelee inahitaji Benki kuu na sarafu yake, ni upuuzi ulovuka kiwango cha uhayawani kufanya Benki kuu ni jambo la Muungano!! Zanzibar imebanwa kwa muda mrefu katika kuendesha uchumi wake, sasa inahitaji kujijenga, unapo ilazimisha Zanzibar eti vijisenti vyake iviweke kwenye mfuko wa pamoja na Tangayika ambayo kwa muda wa miaka 50 imetumia jina la Tanzania kijanja katika kujijenga na kujiimarisha kiuchumi ni uhayawani uliokubuhu!!! naikiwa hivyo ndivyo itakavyo kuwa basi hakuna haja ya kuandika rasimu wala mavi ya rasimu maana bado munaisulubu Zanzibar katika njia za kiujanjanjanja munao kama watu wa Zanzibar wamelala sio..? labda hao wahafidhina wenu ndio bado wamelala ila Wazanzibari washamka.

 
Warioba anasema hati ya Muungano ndio msingi wa serkali ya Muungano, lakini halafu anasema vyama vya siasa iwe sehemu ya Muungano!!! Huu ni upuuzi pia, maana vyama vya siasa (TANU na ASP) vimeunganishwa 1977, wakati Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulikuwa 1964! Ni wazi kwamba muungano haukuhusisha vyama vya siasa…sasa yeye Warioba kasoma hati ipi ya muungano ilosema vyama vya siasa ni sehemu ya Muungano..??

Hii SURA YA TISA, SEHEMU YA KWANZA inayuhusu KUUNDWA KWA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO ndo imeniacha mdomo wazi eti inasema:

4) Katika kila Jimbo la Uchaguzi kutakuwa na nafasi mbili za ubunge, moja kwa ajili ya mwanamke na moja kwa ajili ya mwanamme.”
 
Hivi hiki kioja Ndugu Warioba kakitoa wapi.?? Kwani ameambiwa waTanzania wanahitaji Bibi na Bwana bungeni..?? Nani alimwambia bungeni kunapigwa ”bluz”, kwa hiyo kunahitajika ”pea” (Bibi na Bwana..??) Kwani nani alimwambia Bi Halima Mdee anawakilisha wanawake wa Kawe tu  au  Mama Anna Kilango anawakilisha wanawake wa  Same tu,  au nani alimwambia Warioba kwamba Zitto Kabwe anawakilisha wanaume wa Kigoma tu..??
 
Hayo mataifa yanayoongoza kwa kupiga chapuo ya uwakilishi sawa wa kijinsia kwenye vyombo vya sheria na maamuzi basi hawajafikia hatua hii! Tumeiga kutoka wapi yaa ilahii toba!!! Khaa imeshakuwa bunge la BIBI NA BWANA…mi simo! na Wazanzibari pia hawamo ndio maana tunata nchi yetu kisha nyinyi mtabaki na Tanganyika yenu mufanya Bibi na Bwana ndani ya bunge lenu munywe chibuku na kucheza Bluzz mpaka asubuhi.
 
Kuna haja gani yakuwa na makamo wa raisi, kwanini marais wa pande zote mbili wasiwe makamo wa rais wakiwa na hadhi sawa! Yanini kuwa na bunge la watu 70 wakati hata wabunge 20 wangetosha kujadili wizara nne za muungano?

TUNA TAKA NCHI YETU YA ZANZIBAR HATUTAKI RASIMU YA WALEVI NA WAPUMBAVU WALA KATIBA YA WALEVI NA WAPUMBAVU ZANZIBAR KWANZA

Wednesday, June 5, 2013

JINA LA TANGANYIKA HAWALITAKI WABAKIA KUPOTOSHA NA KUJIITA TANZANIA BARA HAHAHAHAH



JINA TANZANIA BARA MUMELITOWA WAPI  NA NYINYI NCHI YENU ILIPOFANYA MUUNGANO FEKI  ILIKUWA IKITWA TANGANYIKA KWA NINI MUNALIKATA JINA LA TANGANYIKA..? HAHAHAHAHAHAHAHAHAHA
Dar es Salaam. Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chakawe amesema upo uwezekazo wa Katiba Mpya ya (Tanzania Bara..?) ikapatikana kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Chikawe alizungumza Dar es Salaam jana kuwa, ikiwa mchakato wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano utakamilika kama inavyokusudiwa na rasimu hiyo kupitishwa na wananchi katika ngazi zote bila mabadiliko, muda utakaobaki utatosha kuandaa Katiba ya (Tanzania Bara..?).

“Watu wasiwe na hofu. Sioni tatizo endapo rasimu itapita bila mabadiliko na kupata Katiba Mpya. Aprili mwakani mpaka Desemba inatosha kabisa kuandaa Katiba ya (Tanzania Bara..?) na tukaenda katika Uchaguzi Mkuu tukiwa na Katiba Mpya,” alisema na kuongeza:

“Tunaweza kuwatumia wajumbe walewale wa Tume ya Katiba, lakini safari hii tukawachukua wale wa (Tanzania Bara..?) pekee wakashiriki katika kuandaa Katiba hiyo.”
Hata hivyo, Waziri Chikawe alisema kutokana na muda kuwa mfupi, Tume hiyo inaweza isifanye kazi ya kukusanya maoni kutoka kwa wananchi kama ilivyofanya sasa na badala yake ikaandaa rasimu na kujadiliwa na wadau kisha kupelekwa katika mabaraza ya Katiba kabla ya kupata Katiba Mpya.

Kwa mujibu wa ratiba ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajiwa kukamilika Aprili mwakani.

Chikawe anasema kuanzia hapo Serikali inaweza kuitumia tume ya sasa kutangaza rasimu ya kwanza ya Katiba ya (Tanzania Bara..?) kwa kurejea maoni iliyokusanya hivyo hatua ya kwanza ikawa ni kujadiliwa kwa rasimu hiyo kwenye mabaraza ya Katiba kwa miezi miwili na baadaye kupelekwa katika Bunge la Katiba jambo litakaloifanya ipatikane mapema.

Waziri Chikawe alisema kinachotakiwa sasa ni kujiandaa kwa (Tanzania Bara..?) kuwa na Katiba yake ambayo itatumika kwa ajili ya mambo mbalimbali, ukiwamo Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Waziri huyo aliwatoa hofu Watanzania kwamba hakuna mpango wa kumwongezea muda wa uongozi, Rais Jakaya Kikwete kama ambavyo imekuwa ikielezwa kwani Serikali ina uhakika kwamba kila kitu kitafanyika katika muda uliopangwa.

Siku chache zilizopita Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba alikaririwa akisema kuwa Serikali ina mpango wa kumwongezea Rais Kikwete muda wa kuongoza.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu

Wakati Chikawe akitoa kauli hiyo, habari kutoka ndani ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), zinasema kutokana na mapendekezo ya kuwapo kwa Serikali tatu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema anaandaa “kitu muhimu” ambacho atakiwasilisha bungeni siku chache zijazo.

“Kuna kitu AG anafanya na ndani ya wiki hii atakiwasilisha ndani ya Bunge kuhusu (Tanzania Bara..?),” kilisema chanzo hicho bila kufafanua ni kitu gani hasa.

Kwa upande wake, Waziri wa Katiba na Sheria wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Abubakar Hamisi Bakari alisema, suala la nchi ya Zanzibar kuwa na Katiba Mpya au la, lipo mikononi mwa wananchi wa Zanzibar… “Hayo watasema wananchi wa Zanzibar kupitia wawakilishi wao kama wanataka kufanya mabadiliko watafanya.”

Wasomi wanena

Mapema jana, baadhi ya wasomi walieleza wasiwasi wao kuhusu hatima ya (Tanzania Bara..?) ikiwa mapendekezo ya Serikali tatu yatakubaliwa na kupitishwa.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally alisema mabadiliko yaliyopendezwa mengi yameachwa kwa sababu ya pendekezo la kuwapo kwa Serikali tatu

“Katiba hii haiwezi kufanya kazi bila kuwa na Katiba mbili za washirika ambazo, lazima ziundwe na haijulikani itakuwa lini. Katiba ya Zanzibar lazima ifanyiwe marekebisho na (Tanzania Bara..?) kuandikwa,” alisema Ally na kuongeza: “Wananchi walihitaji demokrasia siyo Serikali tatu, jambo hili lina mchanganyiko mkubwa na litapita tu kwa sababu muda wa kujadiii haupo.”

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Gaudence Mpangala: alisema “Kwa muda mrefu wananchi na wanaharakati wamekuwa wakililia Serikali tatu hatimaye limefanikiwa.”

Hata hivyo, alisema jambo linalotakiwa kufanyiwa kazi ili kwenda sambamba na utendaji wa Serikali tatu ni (Tanzania Bara..?) kuwa na Katiba yake kama ilivyo nchi ya  Zanzibar.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Profesa Tolly Mbwete mbali na kutoa pongezi alisema: “Kitu ambacho naona hakikufanyiwa kazi ipasavyo ni suala la madaraka ya Rais kutopunguzwa pamoja na kutoelezwa mchakato wa (Tanzania Bara..?) kuwa na Katiba yake.”

LIME WAKA JIBA LA ROHO MPAKA SASA NDIO MUNAJUWA KUWA NCHI YENU YA TANGANYIKA PIA INAHITAJI KATIBA SIMULITUMIYE TU HILO KATIBA LENU LENYE VIRAKA MULILOLIGEUZA NA KUWA KATIBA LA MUUNGANO FEKI SI LINA MASLAHI NA NYINYI YANINI KUTAFUTA KATIBA MPYA KAENI NALO TU.
                               

SIO SAMIA SULUHU TU KUMBE KUNA NA DAFTARI MAMA TUBIA ULICHO IBA USHAIBA KAMA HUJAIBA HUTAIBA TENA

 
MWENYEZI MUNGU AKUOKOWE NA URUDI KWAKE KABLA HUJAFA KWA TAMAA
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Maua Daftari
Mapendekezo yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, kuhusu muundo wa serikali tatu, umeibua kauli za kukinzana miongoni mwa wabunge.
Kundi moja linatoa kauli zinazobainisha kuwa sasa kila upande ubabe mzigo wake.
Hata hivyo, wananchi na makundi mengine ya jamii yameunga mkono mapendekezo mengi yaliyomo katika rasimu hiyo na kukosoa machache.

Miongoni mwa wabunge wanaotoka nchini Zanzibar, wameelezea wasiwasi kuhusu hatima ya kiuchumi na kiusalama kwa eneo hilo la Muungano, ikiwa litaachwa kuwa katika mamlaka yake kamili.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Maua Daftari moja katika hao walionufaika na muungano na wako tayari nchi ya Zanzibar imezwe lakini yao yanawaendea, alisema Zanzibar haijaimarika kiasi cha kuwa na uwezo wa kuhudumiwa serikali yake na kuchangia katika serikali ya Muungano.(si vichekesho hivi)akiendelea kusema.
“Ni lazima tuwe wakweli, Zanzibar inasaidiwa kwa kiasi kikubwa na Muungano kwa kutegemea rasilimali za Bara!!!, sasa tukisema tujitenge, si rahisi (Wazanzibari) tukamudu kuiendesha serikali yetu na kuichangia ile ya Muungano,” alisema jana wakati wa kutoa maoni yake kuhusiana na tume kupendekeza kuwapo kwa serikali ya Zanzibar, Tanganyika na Shirikisho.
“Ingefaa zaidi kabla ya kuwasilisha mapendekezo hayo, Tume ingezitafakari faida na hasara za serikali tatu, na mimi binafsi naona hasara zake ni nyingi kuliko faida,” alisema Daftari ambaye kwa asili wanadai anatokea nchini Zanzibar inawezakuwa hivyo ila chembe chembe zake ni zakitanganyika ndio maana bado ananganganiya serekali mbili na muungano.
Daftari aliyewahi kushika nyadhifa tofauti serikalini ukiwamo naibu waziri, alisema ni vizuri kwa Zanzibar kujitafakari upya kuhusu kuingia katika mfumo wa serikali tatu, huku akikielekezea kidole Chama Cha Wananchi (CUF) kuwa watetezi wa mfumo huo.(kasahau kuwa sasa sio CUF tu hata hao CCM pia wanataka hayo isipokuwa wahafidhina kama yeye mwenyewe mama Daftari alivyo.
“CUF walihamasishwa sana kuhusu kuwapo kwa serikali tatu, kwa maana tangu awali Muungano unaonekana si sehemu ya hitaji lao,” alisema Daftari huyo.
Daftari alisema miongoni mwa hofu inayomkabili ni kuhusu hatima ya wafanyabiashara Wazanzibar waliowekeza na kuweka makazi ya kudumu upande wa Bara, ikiwa zitaundwa serikali za Zanzibar na Tanganyika (Bara).
“Wazanzibar wanafanya biashara sana Bara, wamejazana kila sehemu ya nchi, sasa tukifikia kila upande kuwa na serikali yake, maana yake itabidi warudi Zanzibar ili serikali ya Bara iwatambue na kuwahudumiwa raia wake,” alisema.(tunamulizwa swali huyu mama je wahindi wameungana na Tanganyika..? Wachina wameungana na Tanganyika..? wacha sera zenu bovu na kutapia mlo mama zere usioka ukatubia mamilioni uliyo iba bado.
Akiendelea kusema hali ilivyo sasa, wafanyabiashara hao wanaendesha shughuli zao pasipo kubughudhiwa, hali ambayo bila shaka itawaathiri ikiwa Bara itaunda serikali yake.
Daftari alisema jambo la msingi lililopaswa kufanyika ni kushughulikia kero za Muungano pasipo kuathiri muundo wa Muungano

Tuesday, June 4, 2013

HATUTAKI RASIMU WALA KATIBA TUNATAKA ZANZIBAR YETU KWANZA



shirts
Male wearing blank red hoodie
KAMA RASIMU YENYEWE NDIO ILE BORA TUKACHUME KARAFU KULIKO UPUMBAVU ULE WARIOBA KAKA NA TIMU YAKE WANAJIDAI ATI WANANDIKA RASIMU KUMBE JIRASIMU LIMEANDIKWA TOKA WAKATI WA JUMBE LIKAFUNGIWA NDANI YA KABATI SASA WAMEONA WAZANZIBARI WAMECHACHAMAA KUDAI NCHI YAO NDIO WAMEONA BORA WAIFUFUWE WAZANZIBARI TUNASEMA TUNATAKA NCHI YETU HATUNA HAJA YA RASIMU WALA KUNDE ZA RASIMU SISI ZANZIBAR TUNA KATIBA YETU NCHI YATANGANYIKA NAIJIFUFUWE HUKO ILIKO JIFICHA NA ITUNGE KATIBA YAKE KISHA KAMA WAZANZIBARI WATATAKA MUUNGANO WATAULIZWA KISHA NDIO KUWE NA MUUNGANO NARUDIA TENA WAULIZWE WANANCHI KWANZA.
 
 
 

 
 
 

 








 




Saturday, June 1, 2013

MPAKA LINI MTOTO WA KITANGANYIKA ATALALIA PESA NA WAKIZANZIBARI ATALALIA NJAA..???


HAKUNA CHA KATIBA WA LA MUUNGANO TUNATAKA NCHI YETU YA ZANZIBAR KWANZA,GASI YAO WANAYO MTWARA NAWACHIMBE,THAHABU WANAZO,ALMASI WANAZO,MAKA YA MAWE WANAYO,TANZA NIGHT WANAZO,BUGAA ZA WANYAMA WANAZO ARDHI ILIYO KUBWA KWA KILIMO NA KUISHI WANAYO.WATUACHIYE ZANZIBAR YETU MZANZIBARI SINDUKA ZANZIBAR KWANZA ZANZIBAR KWANZA.

WALOZOWEA KUFANYA UCHAFU WAO NCHINI ZANZIBAR SASA BASI MIAKA 30 AU MAISHA JELA CHAGUWA KUSUKA AU KUNYOWA


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (GNU), imetunga sheria ya kupiga marufuku 

ndoa za  watu wa jinsia moja.Waziri wa Katiba na Sheria wa nchi ya Zanzibar, 

Bwana Abubakar Khamis Bakar, aliyasema hayo kwenye Kikao cha Baraza la 

Wawakilishi Zanzibar. 

wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi, Saleh Nassor Juma kutoka 

Chama cha Wananchi (CUF).Katika swali lake, Bw. Saleh Nassor Juma alitaka kujua ni lini Serikali ya Zanzibar 

itatunga sheria ya kukataza ndoa hizo na kuweka adhabu kali kwa watu ambao 

watabainika kufanya vitendo hivyo vichafu. 

Waziri Abubakar amesema, ndoa za watu wa jinsia moja ni kinyume na 

utamaduni wa Zanzibar na kwamba sheria hiyo imeweka adhabu ya kifungo cha 

miaka saba kwa wale wote watakaopatikana na hatia hiyo.

Pia alisema kama ninavyomnukuu: "Sheria hii inahusu makosa mengi 


yakiwemo ya ubakaji, zinaa, usagaji na umalaya ambayo yote yana 

adhabu ya kifungo cha maisha au miaka isiyopungua 30 gerezani," 

mwisho wa kunukuu.

BALOZI MDOGO WA NCHI YA TANGANYIKA AENDELEA KUMWAGA FITINA NA CHUKI KATIKA KAMPENI ZA JIMBO LA CHAMBANI PEMBA

HEBU WAZANZIBARI MULIZENI YEYE NYUMBA ZAKE ZOTE ANACHOTA MAJI NJE WAKE ZAKE NA WANAWE WANACHOTA MAJI KAMA HIVI AU NI NYINYI TU NDIO MUCHOTE MAJI KAMA HIVI..?? KISHA ATI ANASEMA MUUNGANO UMELETA MAENDELEO NDIO HAYA KUCHOTA MAJI NJE KIJIJI KIZIMA MFEREJI MOJA NA NYINYI WAZANZIBARI MUNAZIDI KUFANYWA WAPUMBAVU NA HILI TWANA!! LA KITANGANYIKA.
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd amewataka Wazanzibari kutafakari kwa kina na kutokubali kushabikia kuvunjika kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar bila ya kuangalia hasara na tija za kiuchumi na kimaendeleo.Balozi Seif alitoa tamko hilo kufuatia kampeni zilizoibuka Zanzibar za kutaka kuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuratibiwa na baadhi ya wanasiasa, wafanyabiashara na jumuiya za kidini kupitia mjadala wa mabadiliko ya katiba unaoendelea nchini.
Akihutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo Chambani huko Pemba, Balozi Seif alisema wako wanasiasa wanaopigania maslahi binafsi wakiwa na lengo na kuisambaratisha misingi ya Mapinduzi na Muungano.
Alisema Tume ya mabadiliko ya Katiba haikuundwa kwa malengo ya kuvunja muungano na kuwataka wananchi kujiepusha pia wakitafakari kwa umakini na utulivu kwa vile athari za kuvunjika kwa muungano ni kubwa kuliko inavyotazamiwa.
“Tume ya mabadiliko ya katiba haina hadidu ya rejea ya kuvunja muungano, wanachotakiwa wazanzibari kuainisha kasoro zote zilizopo na kuzipatia ufumbuzi bila ya kuongozwa na jazba ya kuvunja muungano uliopo,”alisema Balozi Seif.
Akionekana kushagazwa na matamshi ya baadhi ya wanasiasa wanaotaka muungano wa mkataba bila ya kuonyesha mfumo wa uendeshaji wake, alisema iwe ni mwiko kwa watu hao kutumia jina la wazanzibari wote kwamba hawataki muungano uliopo.
Alisema kuna kikundi cha watu ambao mawazo yao kwa miaka mingi ni kuukataa muungano na si Wazanzibari wote huku akisema kwamba muungano huo umeleta tija na faida zaidi kwa Wazanzibari kuliko Watanganyika.
“Wenye maduka makubwa, wafanyabiashara, wakulima na majumba ya kifakhari huko Tanzania Bara ni Wazanzibari tena wenye asili ya Pemba, kuvunjika kwa muungano kutawapa athari na hasara badala ya faida zinazopatikana sasa,”aliasa Balozi Seif.
Alisema maneno hayo ya kishabiki ni sawa na kuwakaangia mbuyu watu waliojijenga kiuchumi, kimiradi na kimaendeleo kwasababu alisema anaamini nje ya muungano lolote lenye hasara na mtikisiko linaweza kutokea.
“Amani na umoja wa kitaifa ukivurugika, kina mama na watoto ndiyo waathirika wakubwa, amani ni mfano wa mke ukimpa talaka ni taabu kumpata tena, tumezishudia  nchi za Sudan Kusini na Kaskazini, Ethiopia na Eritrea, zimeyumba na kukosa utulivu wa ndani,”alisema.
Aidha  alisema inashangaza kusikia baadhi ya watu hasa wanasiasa wakisema Wazanzibari wote hawataki muungano bila ya kutoa takwimu na ushahidi wa maneno hayo, walikutana wapi, waliazimia mambo gani kuhusu jambo hilo hadi kujumuishwa na kudaiwa hawataki muungano.
Msimamo huo wa Serikali umekuja kufuatia kongomano lililokuwa likijadili mwelekeo wa Muungano wakati huu wa mjadala wa katiba mpya ambalo lilifunguliwa na Makamo wa kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad katika ukumbi wa Bwawani mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki.