Friday, June 7, 2013

UPUUZI WA RASIMU YA KATIBA MPYA NA UWANDIKIWAJI WAKE WA KILEVI

                                                                                                                                                                                                 

Rasimu ya katiba mpya na upuuzi wake inaanza kwa kunichefua kwenye SURA YA KWANZA, SEHEMU YA KWANZA inayo zungumzia MIPAKA, ALAMA, LUGHA, UTAMADUNI NA TUNU ZA TAIFA  insema:
 
1.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenyemamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla ya Hati za Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi
huru.”
Ukiisoma vizuri ibara hii utaona kwamba, katiba mpya inatangaza kwamba Tanganyika na Zanzibar si nchi huru tena, kwani uhuru wao ulikoma mara baada ya hati za makubaliano ya Muungano ya Mwaka 1964!!! Hii ndo kusema kwamba, uhuru wa Zanzibar ulikoma April 26, 1964! Huu ni upuuuzi!  Zanzibar bado ni nchi huru, muungano, haukuondoa uhuru wa mataifa haya! Kama kanuni ya kushirikiana ni kuondoa uhuru wako basi hakuna nchi ambayo ingekubali kushirikiana na nchi nyengine!
 
Upuuzi mwengine nausoma SURA YA NNE inayo zunguzumzia HAKI ZA BINADAMU, WAJIBU WA RAIA NA MAMLAKA ZA NCHI, kwenye kipengele cha
Uhuru wa imani ya dini, kinasema:

 31.-(5) Ni marufuku kwa mtu, kikundi au taasisi ya dini kutumia uhuru wa kutangaza dini kwa kukashifu imani na dini nyingine, kujenga chuki au kuchochea vurugu na ghasia kwa madai ya kutetea imani au dini.”

Sijui hawa waloandika rasimu hii walikuwa wapo katika hali gani!! walikuwa washakunywa chibuku kwanza au tusker sijuwi. Kimsingi dini zote asili yake ni kupingana!! Mafundisho ya dini moja hayawezi kuwa sawa 100% na ya dini nyengine, kama ingekuwa hivyo kusingekuwa na dini mbali mbali! Na kwa kuwa msingi ni kutofautina (kupingana), ni wazi kabisa mafundisho ya dini mbili katika ”ishu” flani yanapotofautina huwa ni kashfa kwa kila upande  dhidi  ya mafundisho ya mwenzake.
Mathalani; Wakristo katika kutumia  katika Biblia yao wanafundishwa kwamba Yesu ni mwana wa Mungu, na wengine katika Biblia hiyo hiyo wanafudishwa  Yesu ni Mungu, LAKINI waislam katika Quraani wanafundishwa Nabii Issa  (Yesu) ni mtume tu kama alivyokuwa Ibrahim, si Mungu wala si mwana wa Mungu! Katika muktasar huu, ni wazi kwamba dini hizi mbili zina kashifiana!! na hata hao wa kristo kwa wakiristo pia wanakashifiana maana hawa wanasema mwana wa mungu na hawa wengine wanasema ni mtume Iweje Mungu wa wengine wewe useme ni mtume kama alivyokuwa Ibrahim tu, ni kashfa hii au sio kashfa..??  Vile vile upande mwengine  iweje mtume wa wengine wewe useme ni Mungu, wakati wao wanaamini Mungu ni mmoja tu, hii ni kashfa!!!

Warioba na wenzake walitakiwa watupe “maelezo ya kifungu hiki, waeleze kinaga ubaga nini maana ya neno ”kukashifu” kama lilivyotumika katika sentensi hii! Jee waislam na wakristo wakigombea kumchinjia M/Mungu (Ng’ombe) wa wahindi ni kashfa kwa wahindi au sio kashfa..?? maana wahindi Ngo;mbe kwa ni mungu na waislamu na wakiristo Ngombe ni mnyama tu je si kashfa hiyo..?? Jee dini moja inasema Yesu kasulubiwa (kwa mujibu wa vitabu vyao) na wa dini nyengine   kwa mujibu wa vitabu vyao pia wanasema Yesu hakusulubiwa… Jee hapo yupi kamkashifu yupi.?? Mmoja akisema nguruwe haramu, mwengine anasema halali, yupi anamkashifu mwenziwe.??  Warioba na wenzake wanajaribu kujenga msingi wa matatizo….wangetafuta njia nyengine ya kuu address hii ishu, lakini si katika namna hii!
Mimi naogopa kifungu hiki kuja kutumika ndivyo sivyo na dini moja dhidi ya nyengine. Kwa mfano endapo kama watawala watakaokuja watakuwa wanawapendelea waislam, basi mafundisho yoote ya wakristo yatatafsiriwa ni kashafa kwa waislam kwa mujibu wa ibara hii! Hivyo wakristo watakosa uhuru wao wa kutangaza dini yao na kuhubiri, maana watakuwa wanakiuka katiba! Vile vile, ikiwa utawala ujao utawapendelea wakristo, basi waislam itabidi quraani yao waifungia kwenye makabati maana wakisoma na kueleza mafundisho itakuwa ina wakashifu wakiristo maana kila aya inayopingana na mafundisho ya ukristo itakuwa ni kashfa…ni wazi hawatakuwa na uhuru wakutangaza wala kuendesha dini yao!!
au warioba na hao walevi wengine walio andika hili gazeti mumeona hii ndio njia ya kuhalalisha kuwa serekali yenu haina dini..?
 
Nikaendelea kusoma SURA YA SITA,  inayohusu MUUNDO WA JAMHURI YA MUUNGANO.  Sehemu hii ya Muundo wa Muungano inasema:
57.-(1) Jamhuri ya Muungano itakuwa na muundo wa shirikisho lenye serikali tatu ambazo ni:
(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
(b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na
(c) Serikali ya Tanzania Bara.”
 
Huu ni upuuzi ulovuka mipaka, maana kwenye  sura ya kwanza Warioba amekiri kwamba JMT ni muungano wa mataifa mawili huru, Tanganyika na Zanzibar! Lakini cha ajabu anapopendekeza uwepo wa serkali tatu anaogopa kuirudisha Tanganyika! Eti serkali ya Tanzania Bara!!! Jee visiwa vyengine vilivyoko kwenye bahari ya hindi kama vile mafia ambavyo si sehemu ya  Zanzibar vitakuwa viko chini ya serkali ipi katika hizi mbili! Maana serkali ni za TZ bara na ZNZ tu! Kwanini Warioba aone tabu kuitaja Tanganyika..??

Katika ibara ya (5)  anasema Washirika wa Muungano watakuwa na hadhi na haki sawa ndani ya Jamhuri ya Muungano na watatekeleza majukumu yao kwa masuala yote yasiyo ya Muungano katika mamlaka ya Washirika wa Muungano kwa mujibu wa masharti yatakayowekwa na Katiba za Washirika wa Muungano

Lakini cha ajabu baadae anasema wabunge wa Bunge la Muungano kutoka Zanzibar wawe 20, na kutoka bara wawe 50! Sasa hiyo hadhi na haki sawa ipo wapi hapo..??? ndio nikasema ni upuuzi mtupu.
 
Zaidi ni upuuzi kujifanya unaiachia Zanzibar iendeshe uchumi wake na ichangie gharama katika kuendesha serkali ya JMT, wakati umeibana kifursa katika njia za kuendesha uchumi wake!!! Zanzibar ni visiwa, uchumi wake unategemea bahari, biashara, na utalii! Hivyo sera zake katika kuendesha uchumi wake hazihitaji zitegemee fadhila au huruma kutoka Serkali ya Muungano!!
Unapoweka mambo ya nje kuwa ni ya Muungano, ni kuinyima fursa Zanzibar kutumia nafasi za uwakilishi wa mabalozi wake kwenye kuitangaza Zanzibar katika nyanja ya utalii na uwekezaji!! Kuweka ushuru kuwa ni sehemu ya Muungano, ni kuifanya Serkali ya Mapinduzi Zanzibar ishindwe kuifanya Zanzibar kuwa bandari huru, inafanya SMZ ifuate sera za uchumi wa nchi ya Tanganyika, ambazo kamwe haziwezi kuivusha Zanzibar, kwa sababu ki jiografia, kimali ghafi na kimazingira, Zanzibar na Tanganyika ziko tofauti sana, hivyo hata sera zao kiuchumi lazima ziwe tofauti ili ziiwezeshe nchi hizo kufaidi rasilimali zao na fursa za kichumi walizonazo!!!
Zanzibar ili iendelee inahitaji Benki kuu na sarafu yake, ni upuuzi ulovuka kiwango cha uhayawani kufanya Benki kuu ni jambo la Muungano!! Zanzibar imebanwa kwa muda mrefu katika kuendesha uchumi wake, sasa inahitaji kujijenga, unapo ilazimisha Zanzibar eti vijisenti vyake iviweke kwenye mfuko wa pamoja na Tangayika ambayo kwa muda wa miaka 50 imetumia jina la Tanzania kijanja katika kujijenga na kujiimarisha kiuchumi ni uhayawani uliokubuhu!!! naikiwa hivyo ndivyo itakavyo kuwa basi hakuna haja ya kuandika rasimu wala mavi ya rasimu maana bado munaisulubu Zanzibar katika njia za kiujanjanjanja munao kama watu wa Zanzibar wamelala sio..? labda hao wahafidhina wenu ndio bado wamelala ila Wazanzibari washamka.

 
Warioba anasema hati ya Muungano ndio msingi wa serkali ya Muungano, lakini halafu anasema vyama vya siasa iwe sehemu ya Muungano!!! Huu ni upuuzi pia, maana vyama vya siasa (TANU na ASP) vimeunganishwa 1977, wakati Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulikuwa 1964! Ni wazi kwamba muungano haukuhusisha vyama vya siasa…sasa yeye Warioba kasoma hati ipi ya muungano ilosema vyama vya siasa ni sehemu ya Muungano..??

Hii SURA YA TISA, SEHEMU YA KWANZA inayuhusu KUUNDWA KWA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO ndo imeniacha mdomo wazi eti inasema:

4) Katika kila Jimbo la Uchaguzi kutakuwa na nafasi mbili za ubunge, moja kwa ajili ya mwanamke na moja kwa ajili ya mwanamme.”
 
Hivi hiki kioja Ndugu Warioba kakitoa wapi.?? Kwani ameambiwa waTanzania wanahitaji Bibi na Bwana bungeni..?? Nani alimwambia bungeni kunapigwa ”bluz”, kwa hiyo kunahitajika ”pea” (Bibi na Bwana..??) Kwani nani alimwambia Bi Halima Mdee anawakilisha wanawake wa Kawe tu  au  Mama Anna Kilango anawakilisha wanawake wa  Same tu,  au nani alimwambia Warioba kwamba Zitto Kabwe anawakilisha wanaume wa Kigoma tu..??
 
Hayo mataifa yanayoongoza kwa kupiga chapuo ya uwakilishi sawa wa kijinsia kwenye vyombo vya sheria na maamuzi basi hawajafikia hatua hii! Tumeiga kutoka wapi yaa ilahii toba!!! Khaa imeshakuwa bunge la BIBI NA BWANA…mi simo! na Wazanzibari pia hawamo ndio maana tunata nchi yetu kisha nyinyi mtabaki na Tanganyika yenu mufanya Bibi na Bwana ndani ya bunge lenu munywe chibuku na kucheza Bluzz mpaka asubuhi.
 
Kuna haja gani yakuwa na makamo wa raisi, kwanini marais wa pande zote mbili wasiwe makamo wa rais wakiwa na hadhi sawa! Yanini kuwa na bunge la watu 70 wakati hata wabunge 20 wangetosha kujadili wizara nne za muungano?

TUNA TAKA NCHI YETU YA ZANZIBAR HATUTAKI RASIMU YA WALEVI NA WAPUMBAVU WALA KATIBA YA WALEVI NA WAPUMBAVU ZANZIBAR KWANZA

No comments:

Post a Comment