Thursday, July 10, 2014

HAKI ZAKO ZA KISHERIA UNAPO KUJAKUBEBWA NA ASKARI WA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA MAKABURU WEUSI NI HIZI ZIJUWE MZANZIBARI


MAKABURU WEUSI TANGANYIKA WAKIWAPIGA NA KUWASUKUMA KWENYE GARI VIJANA WA KIZANZIBARI NDANI YA NCHI YAO.
Raia unayo haki ya:-
*Kumwomba Askari ajitambulishe kwako….
-Muulize Jina lake.
-Muulize namba yake ya Uaskari.
*Kujulishwa ni kwa nini unatiliwa mashaka au kukamatwa.
*Kuwajulisha ndugu, jamaa na marafiki ama sehemu unakofanyia kazi kwamba ama umekamatwa na Polisi au TAKUKURU.
*Kuomba na Kupewa dhamana wakati ukiwa Kituo cha Polisi ama TAKUKURU.
*Hutakiwi kutoa Fedha kama Dhamana uwapo Kituo cha Polisi ama TAKUKURU, isipokuwa maelezo utakayoyatoa na kuandikwa Kituoni hapo.
*Kuwaeleza Polisi ama Maafisa wa TAKUKURU kwamba lolote utakalolisema linaweza kutumika kama ushahidi mahakamani na usiburuzwe wakati wa kuyatoa maelezo hayo.
*Kuomba wakili wako au mtu wa karibu yako utakayemchagua ili awepo Kituo cha Polisi ama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wakati unatoa maelezo yako.
*Haki ya kuyasoma maelezo yako kabla ya kutia sahihi katika maelezo hayo.
*Kudai risiti ya Orodha ya vitu vyako/fedha zako ulizotoa ama kukabidhi Kituo cha Polisi ama TAKUKURU.
*Haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi Saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa Kituoni.
Haki za Raia Kupekuliwa
*Mtuhumiwa anayo haki ya kumpekua Polisi kabla ya yeye kupekuliwa na Polisi huyo.
*Raia kama ni Mwanamke, anayo haki ya kupekuliwa na Askari wa Kike, na iwapo Askari wa Kike hayupo, basi Mwanamke yeyote anaweza kumfanyia upekuzi, vile vile kwa Mwanaume.
*Askari hawana haki ya kuingia kwenye Gari, Nyumba au Ofisi ya Mtu wanayemtuhumu, kwa madhumuni y kufanya upekuzi bila kuwa na:
(a) Hati ya Upekuzi ambayo hutolewa Mahakamani.
(b) Mashahidi wanaotambulika rasmi Kisheria, kama vile Mwenyekiti/Mjumbe wa Serikali ya Mtaa au Kijiji husika.
(c) Jirani wa Mtu anayetuhumiwa.
Aidha, Mtuhumiwa hatakamatwa au kupekuliwa na Askari Polisi baada ya Saa 12:30 Jioni au kabla ya Saa 12:30 Alfajiri, kwa mujibu wa makosa ya Jinai (Penal Code Act).
Isipokuwa tu, kama kutakuwa na ushahidi wa kutosha kwamba kumpekua Mtuhumiwa kabla ya Saa 12:30 Alfajiri au baada ya Saa 12:30 Jioni kunaweza kuleta madhara kwa Askari Polisi, Mashahidi au Watu wengine wowote wale.
Share na marafiki zako!!!

WAKE WA WAKUBWA WA SEREKALI YA TANGANYIKA WALIWA URODA NA VIJANA WADOGO ILIWAPATE MIMBA VIJANA WASEMA WANA UWEZO HUWO KWA KUTUMIYA VUVUZELAAAA


AIBU NA FEDHEHA NCHINI TANGANYIKA WAKE WA 

VIONGOZI KATIKA SEREKALI WALIWA VITU NA 

WAGANGA WAJADI ATII KWA KUTAKA KUPATA 

MIMBAA IMEBAINIKA kuwa miongoni mwa wale wanawake 20 waliodai kufanyishwa ngono na waganga wa kienyeji ‘sangoma’ ili kupata ujauzito  baada ya kukaa  muda  mrefu  bila watoto,  wamo wake wa vigogo Bongo.

mganga akifanya vitu vyake ili mwanamke huyo apate mtoto mtadanganywa mpaka lini wanawake..??
Kamanda Kiondo akielezea kuhusu uhalifu wa Sangoma walionaswa kwa kufanya ngono na wake wa vigogo.
Uchunguzi uliofanywa na waandishi wetu kwa baadhi ya wanawake  hao umebaini kuwa,  waume wao wanafanya kazi  katika nyadhifa za  juu serikalini ya Tanganyika, wengine ni wastaafu  na kwamba waume hao  hawajui kinachoendelea kuwa wake zao wanaliwa uroda na mwabwa mdogo ambao ni wa ganga.
Kwa mujibu wa mwanamke mmoja (jina kapuni), katika sakata hilo kuna wake wa maprofesa, kanali mstaafu wa JWTZ na mmoja ambaye mume wake aliwahi kuwa kamanda wa polisi wa mkoa (RPC) ambaye kwa sasa naye ni mstaafu wote washaliwa uroda alisema mwanamke huyo.
Kamanda Kiondo akizidi kuonyesha vifaa vilivyokuwa vikitumiwa na waganga hao wa kienyeji.
Mwanamke huyo alizidi kudai kuwa, ndoa moja katika hizo ilivunjika baada ya mume kubaini kuwa, mkewe alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa sangoma hao.
‘KUFULI’ ZILISHATUMIKA
Uchuguzi zaidi ulibaini kuwa zaidi ya nguo za ndani  ‘kufuli’ za  wanawake zaidi ya 20 zilizokutwa  na polisi  kwa sangoma hao maeneo ya Tandika jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika zilikuwa zimeshavaliwa hivyo hakukuwa na mpya jambo lilionesha kuwa, zilivuliwa wakati wa tukio linalodaiwa lilikuwa na kutengezea dawa.
Baadhi ya hao vijana walio kuwa wakiwala uroda wake wa wakubwa serekalini nchini Tanganyika ili wapate uja uzito.
KWA NINI WALITOA TAARIFA POLISI......??
“Sisi tuliamua kutoa taarifa polisi kwa sababu tumekuwa tukifanya ngono na wale waganga kwa muda mrefu bila kupata ujauzito na mbaya zaidi tulishatumia mamilioni ya pesa  baada ya kuuza mali zetu, zikiwemo nyumba,” alisema mwanamke huyo nje ya kituo cha polisi.
Wanawake hao ambao hawakupenda majina yao  yatajwe kwa kuhofia waume zao kujua, walisema  ni  kweli baadhi yao wamekaa katika ndoa kati ya miaka nane hadi  10 bila kupata watoto wala mimba zilizoharibika.
Kamanda Kiondo akionesha baadhi ya nguo za ndani, 'kufuli' zilizokutwa kama ushahidi kwa baadhi ya wanawake waliofanyishwa ngono na sangoma hao.
Hata hivyo, baadhi yao walirudishiwa fedha zao baada ya Kamanda Kiondo kuwabana waganga hao.
KAULI YA RPC
Wiki iliyopita Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke chini ya Kamanda, SACP Englibert Kiondo liliwatia nguvuni sangoma wawili wakiwa na matunguli na zana nyingine za kuagulia binadamu.
Kamanda Kiondo akikusanya tunguli zilizotumiwa na waganga hao wahalifu tayari kwa kuzichoma moto mbele ya wahandishi wa habari.
Vitu hivyo viliteketezwa moto kwenye Kituo cha Polisi Temeke mbele ya  waandishi wa habari.
“Ninaamini kuwa kwa vitendo  hivyo  vya kujamiiana ni hatari na huu ni ubakaji, kwani kuna uwezekano wa kuambukizana maradhi  mbalimbali ikiwemo  Ukimwi, kwa hiyo hizi zana nazichoma moto,” alisema  Kamanda Kiondo
Tunguli zikiteketezwa kwa moto.
Waliokamatwa katika zoezi hilo nikijana mwenye umri wa (32) na mwengine mwenye umri wa miaka (25) ambao wote kwa pamoja wanashikiliwa na jeshi hilo la nchi ya Tanganyika.

Tuesday, July 8, 2014

KATIBA NI KWA WANANCHI WOTE AU NI KWA CCM..?? NCHI YA TANGANYIKA NI YA CCM AU NI YA WANANCHI..??


Mwenyekiti wa ccm na raisi wa Tanganyika
Wakubwa wapanga kuisambaratisha kwanza chadema, kisha CUF na NCCR-Mageuzi
Muinjilisti ataka maaskofu waache woga, wamuonye Kikwete kuhusu katiba
JE UKAWA yaiponza CHADEMA....???  IMEBAINIKA kwamba msukosuko unaotokea katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) unatokana na hasira za serikali kushindwa kushawishi chama hicho na vingine vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kurejea kwenye Bunge la Katiba mwezi ujao.
Habari za uhakika kutoka vyanzo vyetu ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali zinasema kuwa hata mgogoro kati ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na CHADEMA una msukumo wa serikali, ili kudhoofisha chama kikuu cha upinzani kabla ya kuendea vingine kabla ya Agosti, mwaka huu na kuwadumaza rai kuendelea kuwa masikini huku wakuu wakila manono yao.
Serikali imekuwa inashinikiza kila taasisi itoe kauli dhidi ya msimamo wa UKAWA kutorejea bungeni, lakini nguvu kubwa imeelekezwa kwa CHADEMA kwa kuwa ndicho kinaonekana kuongoza UKAWA, na kwamba hicho kikiyumba, vingine vitayumba na kuingiliwa kirahisi.
Baadhi ya makada wa CCM ambao hawakubaliani na msimamo wa chama chao kuhusu rasimu ya pili ya katiba, waliliambia muandish wetu hili kwamba hata suala la mgogoro unaoibuka kati ya CHADEMA na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, ni wa kutengenezwa ili kudhoofisha chama hicho.
Akizungumza kwa kujiamini, na akikubali kunukuliwa bila kutajwa jina, kada huyo alisema wa CCM:
“Unajua, serikali imeshindwa kushawishi wapinzani wakubaliane na msimamo wetu kuhusu rasimu. Mara kadhaa umesikia viongozi wa upinzani wakitoa matamko kwamba hawatarejea kwenye Bunge la katiba, la sharti lao ni moja, kwamba ili warejee lazima mjadala ujikite katika rasimu iliyoletwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo ndio maoni ya wananchi lakini sisi CCM hatutaki tunafanya tunavyotaka sisi.
“Sasa ukichunguza, utaona kwamba kweli wapinzani wana hoja, lakini sisi chama chetu kimeamua kufuata kauli ya mwenyekiti, kwamba serikali tatu haziwezekani, zitavunja Muungano, ingawa si wote tunakubaliana naye katika hilo.
“Lakini woga wa kumpinga mwenyekiti ndiyo umetufikisha hapo, maana hata sisi tusiokubaliana naye tunalazimika kunyamaza tu ili usipoteze tonge yako au wewe muandishi unasemaje alimuhoja muandishi wetu.
“Sasa bwana mkubwa ameona atumie viongozi wa dini na watu wenye sauti katika jamii, ili kusukuma hoja hii, na ndiyo maana unasikia baadhi ya viongozi wa dini wanasema UKAWA warejee bungeni bila masharti.
“Hata ofisi ya msajili imeshinikizwa, kwamba kwa kuwa CHADEMA ndicho kinaongoza UKAWA, kikisha tetereshwa, uongozi uka-panic kwa sababu ya presha ya migogoro, hawatakuwa na uwezo wa kusimamia UKAWA, na wakishalegea hao, itakuwa rahisi kushughulika na wenzao CUF na NCCR-Mageuzi.”
Alisema ofisi ya msajili inajua fika kwamba Katiba ya CHADEMA haina matatizo, lakini kwa kuwa wapo wanachama waliofukuzwa ambao walilivalia njuga suala hilo, na kwa kuwa chama kipo katika uchaguzi wa ndani, na kwa kujua nafasi ya viongozi wakuu wa chama katika mchakato huo, serikali iliona ijaribu hata mbinu hiyo.
Hata hivyo, mbinu hiyo imeshindwa kuitikisa CHADEMA kwa kuwa kimeonyesha kumbukumbu za maelezo kuhusu hoja husika, na viongozi hawajishughulishi na propaganda hizo, bali wanaendelea na kazi zao.
Katika wiki moja iliyopita, vyombo vya habari vimekuwa vinaripoti habari kutokana na matamko kutoka kwa watu na taasisi kadhaa nchini yanayowataka wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kurejea bungeni bila masharti ili kuhakikisha katiba mpya inapatikana.
Waziri Mkuu alitoa kauli yenye kuonyesha kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa utategemea uwapo wa katiba mpya. Mwanasheria Mkuu wa Serikali mstaafu Jaji Mark Bomani alizugumza na vyombo vya habari akisema ni vema wajumbe wajikite kwenye masuala mengine kwanza badala ya kubishania hoja ya muungano na muundo wake.
Mara mbili ndani ya wiki moja, viongozi waandamizi wa Kanisa Katoliki wametoa kauli za kuwataka wajumbe hao warudi bungeni bila masharti.Tamko la hivi karibuni ni lile la Baraza la Maaskofu Katoliki Tanganyika (TEC), lililotolewa juzi na Rais wake, Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa.Katika tamko hilo, waliwataka wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, wawe wamoja na kufanya kazi yao kwa mtazamo usioegemea siasa za vyama.
Waliwakumbusha wajumbe hao kuwa yeyote anayedharau hitaji la katiba mpya ama anayejaribu kupuuza na kuweka kando rasimu ya pili, huyo si mwakilishi wa utashi wa watu, na kwamba mwisho wake historia itamhukumu.
“Kwa moyo wa sala na tafakari makini, tulifuatilia mlivyojadiliana katika Bunge la Katiba kuanzia Februari hadi Aprili 2014. Katika siku 67 ninyi wateule wa rais mpatao 600, mlijadiliana pasipo umoja, mkishambuliana kwa kauli kali kati yenu, mkikashifiana pasipo udhibiti wa uongozi mliojichagulia wenyewe kwa kanuni na sheria mlizojitungia,” lilisomeka tamko hilo.
Kwa mujibu wa TEC, mwenendo huo ulikuwa wa kusikitisha na kuchukiza katika mahali pale panapoheshimika. Kwamba, kanisa lilitegemea majadiliano katika kuheshimiana hoja za kizalendo na kiungwana zitokanazo na mambo ya masuala makuu yaliyopendekezwa katika rasimu ya pili ya katiba.
“Badala yake, tulijionea mabishano makali na mpasuko uliosababisha upotoshaji wa nia iliyokusudiwa. Hatimaye hila na gilba zikateka kabisa jukumu adili la Bunge la Katiba.
“Tukumbuke Rais Jakaya Kikwete kwa uthubutu na ujasiri wa kipekee, alianzisha mchakato wa kuunda katiba mpya, na kisha aliridhia kwa kuipokea kwa furaha rasimu ya pili ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba,” lilisomeka tamko hilo.
Kwamba, ni lazima kujiuliza ni nini kilitokea hadi kugeuza kabisa mwelekeo mzima wa mchakato wa katiba kwa kuikejeli na kuishutumu vikali rasimu hiyo katika wakati wa kipekee kabisa wa kihistoria wa uzinduzi wa Bunge Maalumu. Hata kusahau gharama kubwa ambayo ilibebwa na walipa kodi ambao wako katika hali ngumu ya maisha mlo moja kwa siku kisha nyinyi mnacheza na kutaka kuigeuza katiba kuwa ni ya CCM na sio ya wananchi wote.
“Na sasa hali hii inaonyesha dhahiri jambo hili limeiingiza nchi katika mgogoro mkubwa unaoashiria hatari mbeleni,” walisema mamia ya watu walio hojiwana kutuwa mawazo yao kuhusu wapi tunaeleke.
Maaskofu waonywa kuhusu UKAWA
Hata hivyo, Mwinjilisti Medard Kyabashasa wa Kanisa la Tanganyika Assemblies of God (TAG), wa Mbagala, Dar es Salaam nchini Tanganyika, amekerwa na matamko ya viongozi wa dini dhidi ya UKAWA, bila kujali sababu iliyowafanya kususia Bunge, na bila kumkemea Rais Jakaya Kikwete aliyesababisha mzozo huo.
Kwa mujibu wa Mwinjilisti huyo, msimamo wa UKAWA ni kusimamia maoni ya wananchi, wakiwemo maaskofu wenyewe. Hivyo, kilichowatoa bungeni ni kutetea maoni ya wananchi yanaachwa, ambayo watawala wanataka yapuuzwe, tume itukanwe na kuacha watu wakileta mawazo yao ya mifukoni na matumbo yao yasiyo shiba.
Kutokana na hali hiyo, Kyabashasa amewataka viongozi wa dini wawe wawazi, waache unafiki wa kupamba jambo ovu.
“Viongozi wa dini waache unafiki, kama wanadhamiria kweli kusaidia katiba ipatikane, lazima wawakemee wabunge wa CCM na mwenyekiti wao kwa kuvuruga mchakato na kung’ang’ania kujadili vitu ambavyo havimo katika rasimu ya pili na ambavyo vipo kinyume cha sheria,” alisema Kyabashasa.
Aliongeza kuwa viongozi wote wa dini wanajua wazi kuwa aliyevuruga mchakato wa katiba mpya ni Rais Jakaya Kikwete. Badala ya maaskofu na viongozi wengine wa dini kumkemea moja kwa moja, wamekuwa wakifumbafumba halafu wanalaumu UKAWA na kuanza kuwasihi warejee bungeni.
Alihoji kuwa maaskofu wanapowaomba UKAWA kurejea bungeni, kinachoenda kujadiliwa baada ya UKAWA kukubali wito wao ni nin..i? Je, ni rasimu ya pili yenye maoni ya wananchi kama ilivyoandikwa na Tume ya Jaji Warioba au kwenda kujadili msimamo wa CCM unaolazimisha maoni ambayo hayapo kwenye rasimu...??
“Tuliona UKAWA walitumia kila njia kuhakikisha maoni ya wananchi yanajadiliwa ikashindikana na baada ya hapo, wakaamua kutoka kama njia ya kuonyesha shinikizo kwa wajumbe wenzao kurejea katika mstari wa kujadili rasimu halali iliyopitishwa kisheria,” alisema.
Mwinjilisti huyo akitoa mifano kutoka katika Biblia, aliwataka maaskofu na viongozi wengine watakaotoa matamko, kuiga mfano wa Yohana Mbatizaji, alivyomwambia Herode waziwazi kuwa kuchukua mke wa ndugu yake lilikuwa kosa.
“Mungu ametupa akili na uelewa, tusifanye mambo kwa makusudi halafu tunaanza kutegemea maombi, ni kama vile tunaona mtu anatunywesha sumu kwa makusudi, halafu tunakazana kuomba Mungu sumu isituue,” alisema mwinjilisti huyo.
Aliwataka viongozi wa dini wailamu CCM wazi wazi, waeleze kosa la CCM na Kikwete waziwazi, ndipo wapate ujasiri wa kuwasihi UKAWA kurejea bungeni wakakae wajadili rasimu ya pili ya katiba.
“Viongozi wa dini wawaambie viongozi wa CCM kuwa wanavuruga nchi kwa makusudi kwa jeuri ya wingi wao bungeni, jeuri ya fedha na dola, hadi kulazimisha mambo ambayo yapo kinyume cha maoni ya wananchi,” alisema.
CCM hawakuwa na nia ya dhati ya kuleta katiba mpya, walijua mchakato ukianza ni wapi wataivuruga, hivyo wa kulaumiwa ni wao, ndio maana wanatamba kwamba mchakato ukikwama turejee kwenye katiba ya zamani.
“Viongozi wa dini tuna nafasi kubwa sana ya kuirejesha serikali kwenye mstari kama Bunge limeshindwa. Tuikemee serikali waziwazi inapokwenda kinyume, tumechoshwa na wizi, leo unasikia Escrow, leo rushwa, lakini viongozi tunapotoa matamko tunaogopa kuiambia CCM kuwa imefanya hayo, tumebaki tunaomba kusali ili amani iliyopo iendelee…, iendelee ili waendelee kuiba, kula rushwa na kufanya ujangili.....???” alihoji.
Tangu UKAWA waamue kutoka bungeni Aprili 16 mwaka huu, kumekuwa kukitolewa matamko na watu pamoja na taasisi mbalimbali za kidini, huku mengi yakiishia kuwasihi UKAWA kurejea bungeni bila kuangalia kiini kilichowafanya watoke.

Monday, July 7, 2014

DR SLAA ASEMA ELIMU IMEANGUKA,WATU WANAKULA MLO MOJA,HUDUMA ZA AFYA NI DUNI,MAJI NAYO NI TATIZO HALAFU NIMSIFU KIKWETE KWA LIPI HASA...???


Dar es Salaam nchini Tanganyika. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema hakuna jambo lolote litakalomfanya amkumbuke Rais Jakaya Kikwete wa nchi yao ya Tanganyika baada ya uongozi wake mwakani, akisema anachofanya sasa kiongozi huyo ni kuzindua miradi iliyowekwa na Serikali ya Awamu ya Tatu.
“Sina la kumkumbuka Kikwete,” alisema Dk Slaa katika mahojiano maalumu na gazeti hili yaliyofanyika makao makuu ya Chadema, kabla ya kuorodhesha mlolongo wa matatizo yaliyoibuka katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne kuelezea sababu za kutomkumbuka kiongozi huyo wa nchi.
“Kipindi anaingia madarakani alikuwa na kaulimbiu yake ya Maisha Bora kwa Kila Mtanganyika, Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya, lakini leo mmemsikia anaizungumza kauli hiyo..??? Yeye mwenyewe ameikimbia, sasa unataka nimsifu kwa lipi,” alisema Dk Slaa baada ya kuulizwa kama kuna jambo ambalo linaweza kumfanya amkumbuke Rais Kikwete katika kipindi chake kinachokaribia miaka 10 akiwa Ikulu.
Dk Slaa, aliyegombea urais wa nchi ya Tanganyika pamoja na Rais Kikwete mwaka 2010 na kushika nafasi ya pili, alifafanua kuwa tangu rais huyo aingie madarakani mwaka 2005 hajafanya kitu chochote kitakachomfanya amkumbuke, zaidi ya kuwasababishia Watanganyika maumivu kwa ugumu wa maisha na kuanzisha miradi isiyokuwa na tija. “Elimu inaanguka, tunaweka rekodi ya dunia nzima kwa watoto 5,000 kumaliza shule wakiwa hawajui kusoma na kuandika; wananchi wanakula mlo mmoja; huduma za afya bado ni duni; maji nayo ni tatizo halafu nimsifu Kikwete, kwa lipi hasa...??
“Hata barabara anazozindua ni miradi ya muda mrefu ya Serikali ambayo chama chochote kikiingia madarakani ni lazima kiitekeleze. Mimi nimekuwa bungeni kwa miaka 15, sasa nawaeleza miradi hiyo ambayo leo Kikwete anaizindua na kujisifu ni mwendelezo wa mipango aliyoiacha (Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin) Mkapa,” alisema Dk Slaa.
Wakati wa kampeni za urais za mwaka 2005, Kikwete alijinadi kwa kaulimbiu ya Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya sambamba na Maisha Bora kwa Kila Mtanganyika na kushinda kwa kishindo na baadaye aliongeza neno ‘zaidi’ kwenye kampeni za mwaka 2010 huku akiibuka na miradi kama Kilimo Kwanza na sasa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN),
“Kikwete ameanzisha miradi mingi, ikiwamo Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), lakini haina jipya linaloweza kubadili maisha ya Watanzania,” alisema Dk Slaa ambaye aliacha kugombea ubunge mwaka 2010 ili awanie urais kwa tiketi ya Chadema.

Katibu mkuu huyo alipinga kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali mstaafu, Jaji Mark Bomani aliyeshauri Bunge Maalumu la Katiba liahirishe mjadala wa muundo wa serikali hadi baadaye, akisema kutokufanya hivyo ni sawa na kujenga nyumba bila msingi.
“Nimeshangaa kidogo Jaji Bomani akisema tusijadili muundo wa Muungano. Huwezi kwenda kujadili haki za binadamu wakati haki hizo hujui zitatolewa na nani; huwezi kujadili afya, maji, elimu, matatizo ya wafugaji na wavuvi wakati hujui mambo hayo yatatolewa na nani. Ni lazima sura ya kwanza na sita zikajadiliwa kwanza.
“Wakati unajadili muundo wa serikali ambao ndiyo utatumika kutoa huduma muhimu kwa wananchi, ni lazima kwanza ukubaliane na sura hizo ndipo uanze vipengele vingine vilivyopo katika Rasimu ya Katiba,” alisema Dk Slaa.
Aliongeza: “Sisi Ukawa tuko tayari hata usiku wa manane kurudi bungeni, lakini tukihakikishiwa kwamba maoni ya wananchi yaliyomo katika rasimu hiyo yataheshimika, tofauti na hivyo hatutarudi bungeni.”
Kauli hiyo ilikuwa inajibu hoja za Jaji Bomani alizozitoa alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wiki iliyopita, alilishauri Bunge Maalumu la Katiba kuweka kando suala la muundo wa Serikali kwa kuwa ndiyo chanzo cha mgawanyiko baina ya wajumbe.
Pia aliwashauri wajumbe wa kundi la Ukawa linaloundwa na vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi kurejea bungeni ili mchakato huo uweze kuendelea.
Alisema suala la muundo wa Serikali licha ya kusababisha mgawanyiko limesababisha hoja nyingine muhimu kusahaulika.
Maandamano hayaepukiki
Alisema akiwa Katibu Mkuu wa Chadema anafurahishwa jinsi anavyoona kwamba Watanganyika sasa wamefunguka wanajua haki zao, njia ya kuzidai, pia kuzipigania.
“Kwa hali hii uhuru unakaribia kufika wakati wake, kiongozi yeyote anafurahia kuona fikra na tabia za wananchi zikiimarika. Kwa hali hii ukiona vinaelea, ujue vimeundwa.
“Hayo hayakuja hivi hivi. Ilifanyika kazi kubwa kwani watu walipigwa, walipoteza mali zao, walipigwa mabomu, wamefilisika na wengine wamepoteza maisha yao. Hivyo leo hii maandamano yamekuwa sumu kwa wabunge na viongozi wa CCM kutokana na uzito wake.
“Leo hii nawashukuru Watanganyika kwani maandamano yamefanikiwa na lengo lilikuwa kuionyesha Serikali kwamba tunaungwa mkono na wananchi, lakini wabunge wengi wa CCM hawayapendi, ndiyo maana wanayapinga kwa nguvu nyingi bungeni,” alisema Dk Slaa wakati akijibu swali aliloulizwa ni kitu gani ambacho anakifurahia katika uongozi wake wa chama hicho.

Friday, June 27, 2014

KARIBU MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

WAHIMIZENI WAUME ZENU,KAKA ZENU,WAJOMBA ZENU,BABU ZENU IKIWA WANAJIWEZA KUSWALI TARAWEHE IN SHAA ALLAH


SECOND MARRIAGE-A STORY THAT WILL MAKE YOU CRY(WACHENI WAUME ZENU WAOWE WAKE WENGINE MUSTIRI UMMAH MUSIWE MABAHILI WA WAUME ZENU)


Second Marriage – A Story That Will Make You Cry

by Sana -June 11, 2014

The words reverberated through my brain. Why..? Am I not 
good enough..? Never! I will never accept a second wife! If 
you want a second wife you can go out and get one as long 
as you know that I will not be here when you come back..!!!
Those were my words to my husband a few years ago when 
he mentioned to me that he is intending to marry again a 
second time. It was a woman recently divorced, 4 children. 
She is having a hard time, he said, she don’t know where 
the next meal is coming from or how to provide adequately 
for her children. “Where is their father..?” I asked, “Can’t he 
take care of his own kids..? Why do you a strange man 
have 
to carry another man’s burden..? Surely there are other 
ways 
that you can help her out financially without having to 
MARRY her!
I could not imagine myself in a plural marriage. Sharing my 
husband with another woman. Sharing his love, his smiles, 
his jokes with a woman other than myself. I could not 
fathom 
him holding her close and whispering loving words in her 
ears. It was unacceptable. An outrage. After all I have been 
to him. Wife, lover, mother, doctor, housekeeper. I raised 3 
of his beautiful children. How can he insult me by marrying 
another woman as if I am not good enough. Not pretty 
enough. Not young enough or just plain not ENOUGH.!!!
NO..!!! I could not accept that and I vehemently made my 
stance clear to him. If she walks in, I walk out! Plain and 
simple. If he is willing to risk our marriage, our life, our 
children for another woman, then he must go ahead. I will 
not stand for it!
It all seems so many years ago now. When I thought that 
life 
would last forever and that nothing will ever change. But it 
did..
My husband did not get married to a second wife. After all 
my warnings and threats of leaving he abandoned the 
idea. I 
don’t know what happened to the women and children. My 
guess is that they moved on to another town.
He never mentioned a second wife again and I was happy 
with that. I managed to hang on to my husband but I didn’t 
know that our time was running out.His last words to me 
were that he had a headache and is 
going to lie down till Esha. He never read Esha namaaz that 
night, because he never woke up.
I was devastated by his sudden death. The man whom I 
have spent my life with, snatched away from me in a 
second. 
I mourned him for a long, long time.
Neglecting my children and the business. Soon all went to 
waste and we started losing everything one by one. First the 
car then the shop, then the house.
We moved in with my brother and his family. My 3 children 
and I crowded the house and my sister in law soon became 
annoyed by our presence. I needed to get out, to work and 
find a place of our own instead of living off the leftovers of 
others. But I had no skill.When my husband was alive we 
lived comfortably. I had no 
need to go out and work or or equip myself with a skill. Life 
was very difficult for me and my children and I wasn’t young 
anymore. I missed him everyday with every beat of my 
heart. 
How could ones condition change so drastically..?
One day my brother told me that someone he knew is 
looking for a wife. He was a good person, good akhlaq 
(manners) and very pious. Perfect for me, but he wants me 
to be his second wife.
It’s the second time in my life that the word second wife was 
mentioned to me. But how different the circumstances.
He came to my brothers house to see me. There was an 
immediate connection between us. I liked him and I liked 
everything about him. He told me that his first wife knows 
that he is intending to marry again but that she is obviously 
not supportive of the idea and that he doesn’t know what 
her 
reaction will be when he tells her that he had found 
someone. His answer he said, will be dependent on her 
acceptance of Polygamy.
I started reading Istikhara that night. I so desperately 
wanted 
it to work out. I remembered so many years ago when the 
life of another woman depended on my decision and what 
my decision was. I felt contrite, I felt that because I did not 

give another woman a chance, a space in my life, that Allah 
will punish me this time around. I repented, not once in my 
life did I think my action worthy of repentance because I had 
done nothing wrong. I only protected what was mine.
Now that I am on the receiving end, I realized how wrong I 
was in denying another woman this PRIVILEGE of a 
husband.
I prayed that she will accept me.
He phoned me a few days later telling me that his wife is 
having a hard time accepting it but that she is willing to 
meet 
me.
I was nervous the day of the meeting. I prayed a lot the day 
before and asked Allah to help me. When I met her, she 
was 
a person, a woman like me . A woman who loves her 
husband and fears losing him.
She took my hand and with tears in her eyes said: ” This is 
very hard for me, but I hope that we can be sisters”..
Her words broke my heart. All I needed in these dark days 
was a hand reaching out to me and embracing me, giving 
me hope and the will to carry on.
His wife was to me, the woman that I could not be and I will 
be forever grateful for that. I thought that no one could love 
her husband the way I loved mine, but she taught me the 
true meaning of unconditional love.