Wednesday, July 24, 2019

KARUME NA MKONO WAKE WA CHUMA NA KUCHOSHWA NA MUUNGANO

Afbeeldingsresultaat voor karume na nyerere
Miaka 40 iliyopita, Aprili 7, 1972; Rais wa Serikali ya awamu ya kwanza ya Mapinduzi na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Abeid Amani Karume, aliuawa kwa kupigwa risasi katika mazingira na sababu za kutatanisha.
Risasi nane zilitolewa mwilini kwake mwili wake ulipofikishwa kwenye Hospitali ya V. I. Lemin, mjini Unguja kwa uchunguzi, sawa na idadi ya miaka minane ya utawala wake tangu 1964 hadi kifo chake.
Ilikuwa hivi:  Rais Karume na Makomredi wenzake wa Chama cha Afro-Shirazi (ASP) alikuwa na mazoea ya kucheza karata, damma au dhumuna kwenye ukumbi wa ofisi za makao makuu ya Chama hicho Kisiwandui, kila jioni kama sehemu ya mapumziko.  Siku hiyo alifika saa 11.00 jioni akiwa na walinzi wake, akaingia ndani nao wakabaki nje kulinda.
Ikafika zamu yake kucheza; akawa anacheza na Mzee Maalim Shaha Kombo ambaye alionekana kulemewa.  Ndipo Karume akamwita Mzee Mtoro Rehani ajitayarishe baada ya Kombo, naye akaitikia kwa kuaga kwanza aende msalani kujisaidia.
Sekunde chache baada ya hapo na kabla Mzee Mtoro Rehani hajarejea kutoka msalani, ghafla watu wawili wenye silaha walivamia chumba alimokuwa Karume na wenzake na kumimina risasi wakimlenga; na kufumba na kufumbua, akawa katika dimbwi la damu kimya, amepoteza uhai.  Hakuna mtu mwingine aliyeuawa mbali na kujeruhiwa tu, mmoja wao akiwa Katibu Mkuu wa ASP, (sasa) Hayati Thabit Kombo Jecha.
Risasi uaji (the fatal bullet), mbali ya risasi zote, iliyochukua uhai wa Karume ilitoka kwenye bunduki ya Luteni Hamoud Mohammed  Hamoud wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWT), ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa uvamizi huu na aliyefyatua risasi ya kwanza wakati Karume akicheza na wenzake.  Inasemekana, Hamoud aliuawa papo hapo na mlinzi wa Karume.
Wauaji wengine waliofuatana na Hamoud katika uvamizi huo ni Kapteni Ahmada Mohamed, Koplo mmoja wa jeshi ambaye jina lake halijafahamika hadi leo, na raia mmoja aliyekwenda kwa jina la Ali Khatibu Chwaya, ambao inaelezwa wote hao waliuawa kwenye mapambano ya silaha nje ya eneo la tukio.
Dakika chache baada ya mauaji kutokea, alifika Kanali Ali Mahfoudhi na askari mwingine, Kapteni Makame Hamis, wakauchukua mwili wa Karume na kuukimbiza hospitali.
Itakumbukwa, Kanali Mahfoudhi ni mmoja wa vijana wa Umma Party (UP) cha Abdulrahman Mohamed Babu, kilichoungana na ASP baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 na kuunda Serikali ya mseto. Ni kati ya vijana waliopelekwa Cuba kwa mafunzo ya kijeshi, na ni mmoja wa wapiganaji walioendesha mapambano ya kisayansi usiku wa Mapinduzi na kukamata uwanja wa ndege mchana Aprili, 1972.
Ni mmoja wa wanaharakati wa siasa za mrengo wa Kikomunisti ambao hawakutakiwa Zanzibar wakati wa utawala wa Karume, hivi kwamba kufuatia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Aprili 26, 1964, Karume alishinikiza kwa Nyerere wapewe kazi Tanzania Bara aweze “kupumua” ambapo Mahfoudhi alipewa cheo cha Mkurugenzi wa Operesheni katika JWT.
Wengine ambao hawakutakiwa ni pamoja na Babu mwenyewe aliyepewa Uwaziri wa Mipango ya Uchumi, na kama tulivyoona makala zilizopita, hasimu mwingine wa Karume, Othman Sharrif, ambaye alifanywa Afisa Mifugo wa Mkoa, Mtwara au Mbeya, na Balozi Salim Ahmed Salim wakati huo Balozi wa Zanzibar nchini Misri ikaridhiwa aendelee kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano nchini humo.
Tuache hayo, lakini hapa swali linazuka:  Kwa kuwa Kanali Mahfoudh hakuwa kipenzi cha utawala wa Karume tangu mwaka 1964, ilikuwaje akawa Afisa wa kwanza kuwa kwenye tukio kabla ya maafisa wengine vipenzi, kama vile Kanali Seif Bakari ambaye alikuwa pia Mkuu wa Usalama wa Taifa Zanzibar ambalo halikuwa jambo la Muungano, na wengineo?
Je, alikuwa katika ziara ya kikazi wakati mkasa huu ukitokea au alijua kilichotarajiwa kutokea? Kwa nini alikuwa mmoja wa washitakiwa zaidi ya 100 kwa tuhuma za mauaji hayo, na mmoja wa watuhumiwa 18 miongoni mwa hao walioshitakiwa wakiwa Tanzania Bara, Abdulrahman Babu akiwa mmoja wao.
Kuna dhana mbili kinzani kuhusu jinsi Karume alivyouawa na hatima ya wauaji. Dhana moja inadai kwamba, watu wanne walivamia mahali alipokuwa Karume na wenzake, wakamimina risasi mara nne au mara tano hivi, risasi ya kifo ikampata Karume shingoni akafa, huku zingine zikiendelea kumiminwa kulenga meza walipokuwa.
Inadaiwa kuwa Hamoud aliuawa kwenye eneo la tukio, ambapo wawili waliuawa baadaye na vyombo vya usalama (kwa mapambano?) na mmoja alijiua.
Dhana ya pili inadai kwamba Hamoud alikufa kwenye eneo la tukio katika mazingira ya kutatanisha, ama kwa kujipiga risasi kuepuka kukamatwa hai na kuteswa baada ya kuona asingeweza kutoroka; au alijeruhiwa vibaya na walinzi wa Karume, kisha Ahmada akampiga risasi na kumuua kumwepusha kuteswa na kutoa siri kama angekamatwa hai, kisha (Ahmada) akaweza kutoroka kwenye eneo la tukio.
Juu ya utata huu kuhusu hatima ya wauaji, ni ukweli kwamba ni Luteni Hamoud pekee aliyeuawa kwenye eneo la tukio na washiriki wengine katika mauaji waliweza kutoroka eneo la tukio na baadaye kuuawa katika mazingira yasiyofahamika.
Kufuatia mauaji hayo, watu 1,100 walikamatwa na kuhojiwa juu ya kuhusika au kutohusika kwao na mauaji, wengi wakiwa viongozi na wanachama wa zamani wa Umma Party, chama cha Babu na wanachama mashuhuri wa ASP wenye siasa za mrengo wa kikomunisti.
Inaendelea...
Yote haya yanaturejesha kwenye swali letu la awali:  je, kuuawa kwa Karume kulikuwa na lengo la kulipiza kisasi kwa chuki binafsi, kama baadhi ya watu wanavyodai, au lilikuwa jaribio la Mapinduzi lililoshindwa kwa Serikali ya Mapinduzi? Ni nani huyu Luteni Hamoud Hamoud aliyeongoza mauaji na kwa nini?
Je, lengo lilikuwa ni mauaji hayo pekee au kulikuwa na mpango mkubwa zaidi nyuma? Ukiongozwa na nani?
Kupata majibu ya maswali haya, hatuna budi kuiangalia hali ya kisiasa Zanzibar baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 na baada ya Muungano na Tanganyika, Aprili 26, 1964.
Kama nilivyoeleza katika mfululizo wa makala nne hivi karibuni katika gazeti hili kuhusu jinsi “Field Marshal” John Okello alivyoongoza Mapinduzi ya 1964, na kuundwa kwa Serikali ya Mseto kati ya vyama vya ASP na Umma, lengo kuu la Karume lilikuwa ni kuzivunja nguvu za wanaharakati wa Umma Party na za wakomunisti wa ASP walioshabihiana kimawazo na kimtazamo wa kitaifa na wana-Umma Party na kumnyima Karume usingizi.
Lakini tofauti na matarajio ya Karume, hatua hiyo iliwaleta karibu zaidi wanamapinduzi hao na kumnyima zaidi usingizi kwa hofu ya kupinduliwa, wakimtuhumu kushindwa kuongoza na kusimamia madhumuni ya Mapinduzi Visiwani.
Mungu bariki kwa Karume, ukatokea Muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika mwaka huo, akaona vyema awasambaratishe kwa kuwatafutia nafasi Tanzania Bara ambako wasingeweza kufurukuta.
Waliokumbwa na kadhia hiyo ni pamoja na Abdulrahman Babu (Umma) na aliyepewa Uwaziri wa Mipango na Uchumi kwenye Serikali ya Muungano; Kassim Hanga (ASP) aliyeteuliwa Waziri katika Ofisi ya Rais wa Jamhuri, Mambo ya Muungano; Salim Ahmed Salim (Umma) aliyeteuliwa Balozi nchini Misri.
Wengine ni Othman Sharrif (ASP) aliyeteuliwa Balozi nchini Marekani, lakini Karume akampinga Nyerere akidai hastahili, uteuzi ukafutwa; badala yake akateuliwa kuwa afisa mifugo katika moja ya mikoa ya Kusini Tanzania, Mbeya au Mtwara, na Kanali Ali Mahfoudh (Umma) aliyeteuliwa Mkurugenzi wa Operesheni katika Jeshi la Wananchi (JWT), na wengineo.
Kwa wale wenye maoni tofauti na ya kukosoa Serikali waliobaki Visiwani, hasira ya Karume aliyetawala kwa mkono wa damu iliwashukia, wengi walikamatwa na kutiwa kizuizini na pengine kupoteza au kuuwawa kikatili na katika mazingira ya kutatanisha. Mmoja ya waliouawa kikatili kizuizini ni Mzee (mwanaharakati) Mohamed Hamoud, baba yake Luteni Hamoud Mohamed muuaji wa Karume.
Tangu Mapinduzi ya Januari 12, 1964, Zanzibar haikuwa na Katiba wala Sheria; iliongozwa kwa Amri za Rais  (Presidential Decrees) kadri alivyoona inafaa.  Na kwa mujibu wa Gazeti la “The Tanganyika Standard” la March 9, 1968, Karume aliapa kutofanya uchaguzi wala kuwa na Katiba Kisiwani kwa miaka 50 tangu 1964 - 2014 Kwa madai kwamba  “chaguzi zote ni vyombo vya mabeberu kuwakandamiza wananchi”.
Na kadiri kalamu ya Karume ya wino wa damu ilipozidi kuandika historia ya ukatili, udikteta na umwagaji damu kwenye kurasa ngumu za kukwaruza ndivyo alivyojichongea na kujiongezea upinzani na uadui kwa jamii ya Kizanzibari.
Kufikia mwaka 1967 hofu ya Karume dhidi ya wenzake na kwa nafasi yake ilitia fora kiasi cha kuogopa kivuli chake mwenyewe. Na ili kuendelea kuwamaliza wenzake, mwaka huo zilitungwa tuhuma za uongo dhidi ya watu 14 makada wa ASP katika kumpindua, zikiwalenga hasa wenye fikra za kikomunisti.
Walioingizwa kwenye tuhuma hizo ni pamoja na mawaziri wa Serikali yake mabwana Abdallah Kassim Hanga, Salehe Saadallah Akida, Abdul Aziz Twala na makatibu wakuu wa wizara, Aboud Nadhif na Mdungi Ussi na baadaye Othman Sharrif.
Wote waliokuwa Visiwani walikamatwa, kisha Karume akamwomba Nyerere kuwarejesha Zanzibar kutoka Bara, Othman Sharrif na Hanga ili “wakahojiwe” lakini wote wakaishia kuuawa kikatili bila kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Mmoja wa mashahidi wa uongo walioandaliwa dhidi ya “watuhumiwa” kwa vyombo vya Karume, alikuwa Ahmada ambaye kwa uongo wake, watu wanne akiwamo Hanga, Twala, Saadallah na Othman, walinyongwa mwaka 1969.  Kwa uongo huo, Ahmada alizawadiwa cheo cha kapteni jeshini.  Ni Kapteni Ahmada huyu, aliyeshiriki kwenye mauaji ya Karume miaka mitatu baadaye.
Kwa hofu ya jamii ya Kizanzibari kufikiwa na fikra na mawazo mapya ya kimaendeleo, Karume alipiga marufuku vijana wa Kizanzibari kwenda nje kwa masomo ya juu ikiwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam; alipiga marufuku pia ujenzi wa Chuo Kikuu Visiwani.
Mbali na kutokuwapo kwa utawala wa sheria enzi za Karume, unyanyasaji wa kijinsia na ubaguzi kwa misingi ya historia na kisiasa ulitia fora. Kwa mfano, mwaka 1966, alitoa amri (decree) kuwanyima wazazi haki ya kuwakataa wanaume walioposa binti zao kama njia ya kuondoa ubaguzi wa rangi.
Kwa sababu hii, wasichana, hasa wale wa Kiarabu walilazimishwa kwa nguvu ya Serikali kuolewa kwa nguvu. Karume mwenyewe, wakati huo akiwa na umri wa miaka 65, aliwania kuoa kwa nguvu, wasichana wanne wa Kiajemi, na alipokataliwa, aliamrisha wazazi wao watiwe kizuizini na kuchapwa viboko kwa kosa la kuzuia mpango wa ndoa mchanganyiko, na baadaye kutimuliwa Zanzibar.
Chini ya mpango huo, raia wa kigeni waliotaka kuchumbia wasichana wa Kizanzibari walitakiwa kuilipa Serikali Sh. 64,000,000, bila hivyo hawakuruhusiwa kuwaoa.
Karume alikuwa ameanza kuwa mwiba kwa Mwalimu Nyerere pia juu ya Muungano. Kwa mfano, alimkatalia Nyerere kwa lugha ya dharau na kejeli juu ya Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea na Azimio la Arusha kutumika Zanzibar.
Na kuhusu akiba ya fedha za kigeni ya Zanzibar iliyofikia dola milioni 80 mwaka 1972, alimuonya asithubutu kuitolea macho, akamwambia:  “Fedha ya kichwa cha Malkia si yako na usiniulize, labda niulize juu ya hii (sh.) yenye picha ya kichwa chako”.
Na kuhusu Muungano, Karume alikuwa ameanza kuchoka nao. Siku moja alisema, “Muungano ni kama koti tu; likikubana unalivua”.
Ufa huu kati ya viongozi hao wawili juu ya Muungano, ndio uliosababisha kamati ya kupendekeza Katiba (Constitutional Committee) isiundwe na Bunge la Katiba (Constitutional assembly) lisiteuliwe ndani ya muda wa mwaka mmoja tangu Muungano, kama ilivyotakiwa chini ya Mkataba wa Muungano wa Sheria ya Muungano ya 1964.
Wadadisi wa mambo ya siasa wanakubaliana kuwa, kama Karume angeendelea kutawala miaka kadhaa baada ya 1972, Muungano ungefikia kikomo kwa njia ya kutisha na kusikitisha.
Kufikia mwaka 1972, upinzani kwa Serikali ya Karume ulikuwa umechukua harakati za uasi wa umma, chini kwa chini kwa mara ya kwanza tangu Hanga na wenzake wanyongwe mwaka 1969.
Inaendelea...
KATIKA sehemu ya kwanza ya makala haya toleo lililopita, tuliona jinsi Rais wa Serikali ya awamu ya kwanza Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Abeid Amani Karume, alivyouawa kikatili na wanajeshi wakati akicheza bao, Aprili 7, 1972 mjini Unguja.
Kwa kifupi, tuliona kwamba, kwa vigezo vyovyote vile vya utawala na uongozi, Karume alitawala kwa mkono wa chuma; alitawala kidikteta katika nyanja zote za maisha ya Wazanzibari kisiasa, kiuchumi na kijamii.   Alikuwa kero pia kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kwa Muungano.
Kwa kusema haya sina maana kwamba Karume hakutenda mema kwa Zanzibar na kwa Wazanzibari; bali najaribu kutafiti tu kuona ni mazingira na sababu zipi zilizochochea na kuharakisha kuuawa kwake; kati ya sababu hizi kuu za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kimuungano.  Kwa vyovyote vile, moja au zaidi ya mambo haya manne yalichangia.
Tunajua kwa mfano, kwa baadhi ya Wazanzibari, Karume alikuwa mtawala mkatili asiye na huruma wala hakujua kusamehe; lakini pia alikuwa na sifa za pekee nzuri kama kiongozi na binadamu; alikuwa mhimili na mtetezi wa Waafrika wa Kizanzibari na hakuyumbishwa na siasa za migogoro Visiwani.
Alikuwa mwenye fikra zenye kujitegemea, alifanya maamuzi yake bila woga wala kuhofia matokeo; alikuwa kiongozi mwenye kuthubutu na mwenye kujituma.
Mwisho tutaona jinsi mpango mzima wa mauaji ulivyoandaliwa kwa wasomaji kuona kama ilikuwa chuki binafsi au mapinduzi.  Si madhumuni ya makala haya kumwona Karume kama dikteta mwema (benevolent dictator) au dikteta katili (ruthless tyrant), maana hilo ni jambo la maoni ya kila mtu binafsi.
Alitawala kwa mkono wa chuma
Tumeona jinsi Karume alivyoitawala Zanzibar kwa mkono wa chuma, na namna alivyowaengua wote aliodhani hawakuwa upande wake, ama kwa kuwahamishia kwenye Serikali ya Muungano, ama kwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha.
Sambamba na hatua hiyo, jamii ya Kiarabu wasio Wazanzibari, iliamriwa kuondoka, na wale Waarabu raia waliobaki waliishi chini ya jicho kali la Serikali; waliweza kukamatwa, kama Wazanzibari wengine na kutiwa kizuizini bila kufunguliwa mashitaka.   Walifanyiwa jinsi serikali ilivyofikiri inafaa; mashamba na mali zao zilitaifishwa bila kufidiwa.
Wapo waliohukumiwa na “Mahakama ya wananchi” (tutaiona baadaye), kifungo na kuchapwa viboko kuonyesha kwamba Serikali ya Karume haikuwa ya mchezo; akaionya jamii ya Ki-Athnasheri wa Kiajemi kwamba kama wangeendelea kuleta “mgogoro”, wangefukuzwa wote Zanzibar licha ya kuwa raia.
Alitawala bila Sheria wala Katiba
Karume alitangaza utawala wa chama kimoja cha ASP na kuamrisha kila Mzanzibari mtu mzima, kuwa mwanachama. Kila familia ilitakiwa kutundika picha ya Karume nyumbani; kutofanya hivyo lilikuwa kosa la jinai lenye adhabu kali.
Kikosi cha Usalama wa Taifa chini ya Kanali Seif Bakari, kilichopewa jina la “Viwavi Jeshi”, na kufunzwa Ujerumani Mashariki kikaiva kwa mbinu za utesi na mauaji, kilipewa mamlaka ya kukamata, kutesa, kutia kizuizini na hata kuuwa bila mashitaka.  Yeyote aliyelalamika, hata juu ya upungufu wa chakula tu, aliitwa “adui wa Mapinduzi” na hivyo mhaini.  Enzi hizo, nduguyo akigongewa mlango usiku na kutakiwa kwa mahojiano na Serikali, usingemwona tena milele.
Wakati wa Karume hapakuwa na utawala wa Sheria wala Katiba;  amri za rais (decrees) ndizo zilizotawala nchi.  Mapema mwaka 1966, mfumo wa mahakama wa kawaida ulipigwa marufuku; na Oktoba 1966, rais alijipa madaraka ya kuteua mahakama maalumu za watu wasiozidi 14 wenye mamlaka ya kusikiliza kesi za makosa ya kisiasa kama vile uhaini, uhujumu uchumi na wizi wa mali ya umma.
Mahakama hizi hazikufungwa na kanuni zozote katika kusikiliza kesi; huduma za kisheria kwa watuhumiwa zilifutwa na mawakili kupigwa marufuku Zanzibar.  Upande wa mashitaka ndio uliokuwa pia upande wa utetezi; kwa maana kwamba, mwendesha mashtaka wa serikali alipomaliza kuwasilisha mashtaka dhidi ya mtuhumiwa aligeuka kuwa mtetezi wa mtuhumiwa.
Mahakama hizi zilipewa uwezo wa kutoa hukumu za kifo.  Mwaka huo huo (1966), Baraza la Mapinduzi lilipiga marufuku pia haki ya kukata rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa ya Afrika Mashariki [EACA] na rufaa zote zikawa kwa Rais Karume pekee.
Mwaka 1970, Karume alipitisha amri (decree) ya kuanzishwa mahakama (za kienyeji) za watu watatu.  “Mahakimu” wapya wa mahakama hizo waliteuliwa na Karume mwenyewe kutoka miongoni mwa makada wa ASP.
Moja ya sifa ya kuteuliwa ni kutokuwa msomi wa sheria, na ikiwezekana uwe hujui kusoma na kuandika.  Adhabu ya kifo ilipanuliwa kuingiza makosa kama vile utoroshaji wa karafuu, uhaini na utoaji mimba.   Matumizi ya vidonge vya uzazi wa majira lilikuwa kosa kubwa pia.
Karume alichochea hasira na chuki kubwa ya Wafanyabiashara wa Kiasia mwaka 1971, pale alipowapa notisi ya mwaka mmoja kufungasha virago kwa madai ya kuonekana kudhibiti uchumi wa Zanzibar.  Hasira yao iliungana na ile ya Waarabu ugenini waliofukuzwa mwaka 1964 na kupokonywa mali na mashamba yao bila kulipwa fidia; achilia mbali wale ambao mabinti zao waliozwa kwa nguvu kwa Wazanzibari Waafrika.
Wakati huo huo, Karume aliendelea kuwaachisha kazi na kuwatimua Visiwani, watumishi wa serikali waliojulikana au ndugu zao kuwa wafuasi wa zamani wa vyama vilivyopigwa marufuku vya ZNP na ZPPP na nafasi zao kujazwa na “watiifu” kwake.  Hata hivyo, kwa huruma ya Nyerere, walipewa utumishi serikalini Tanzania Bara.
Mapema mwezi Januari 1972, Waziri mdogo, Ahmed Badawi Qualletin, na afisa mwingine wa Serikali, Alli Sultani Issa, walifukuzwa kazi.  Kisha, Februari 1972, ujumbe mzito wa watu sita ulitumwa kwa Nyerere kumwambia awarejeshe Zanzibar, Abdulrahman Babu na wenzake kadhaa wakahojiwe kwa tuhuma za kutaka kuiangusha Serikali.
Babu ambaye alikuwa bado mwenye ushawishi mkubwa wa kisiasa Zanzibar, na aliyeamua kutorejea Zanzibar ya Karume kwa kuhofia usalama wake, kivuli chake na mzimu wa wahanga wa ukatili vilimtisha na kumnyima usingizi Karume, mithili ya Macbeth kwa mzimu wa Mfalme Duncan na Banquo, aliowaua kwa upanga ili atawale.
Nyerere, kwa kuhofia yaliyompata Hanga, Twala, Othman Sharrif na wengine kutokea alipowarejesha Zanzibar mwaka 1967, safari hii alikataa kumrejesha Babu Zanzibar, ingawa alikubali shinikizo la Karume la kumwachisha uwaziri katika Serikali ya Muungano.
Karume aliwatimua pia wataalamu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) na kufunga Kituo chao cha Utafiti na Udhibiti wa malaria Visiwani kwa madai kwamba, Wazanzibari walikuwa “malaria proof”, yaani hawaguswi wala kuugua malaria.
Kwa hatua hiyo, ugonjwa wa malaria uliongezeka kwa asilimia 45.  Na ingawa Zanzibar ilikuwa na akiba kubwa ya fedha za kigeni, zaidi ya pauni za Uingereza milioni 14 kwenye Benki ya Urusi mjini London, (taarifa nyingine zinadai dola milioni 80), Karume hakuwa tayari kutumia fedha hizo kudhibiti malaria wala kuagiza chakula; badala yake akaona muhimu zaidi kuanzisha kituo cha televisheni ya rangi na ya pekee barani Afrika wakati huo.
Mwaka huo huo (1971), katikati ya mrindimo wa njaa Visiwani, Karume alipiga marufuku uagizaji wa chakula (mchele, sukari, unga wa ngano) kutoka nje, kama hatua ya kujitegemea kwa chakula. 
Hatua hii ilizua tafrani na malalamiko na kusababisha biashara ya magendo ya chakula kushamiri; hapo, “Viwavi Jeshi” na mahakama za “kangaroo” zikapata wahanga kukamatwa, kushitakiwa na kunyongwa.  Watu wengi wakaikimbia Zanzibar. Aprili 1972, ukosefu wa chakula ulikithiri. Ni wakati huo Rais Karume alipouawa ghafla. 
Kwa yote hayo, pamoja na tabia yake ya kutoamini wasomi na kuchukia wataalamu, Karume hatimaye alianza kuchukiwa pia na Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi wenye siasa za mrengo wa ki-Karl Marx.
Karume adha kwa Nyerere na Muungano
Nyerere alikuwa ameyatoa sadaka mengi ya Tanganyika kwa Zanzibar, ilimradi tu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ufikiwe. Kwa mfano, wakati Tanganyika ilipoteza hadhi ya kuwa nchi na baadaye jina lake, pale Muungano ulipobadili jina kutoka “Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar”,  kutwa “Jamhuri ya Muungano wa Tan-zan-ia”, Zanzibar ilibakia kuwa Zanzibar, na Karume akabakia Rais wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania.
Si hivyo tu, Wazanzibari watano walipewa uwaziri kamili katika Baraza la Mawaziri 14 la Muungano.  Na ingawa idadi ya Wazanzibari ilikuwa asilimia tatu tu ya Watanganyika, lakini Zanzibar iliruhusiwa kuwa na Wabunge 52 katika Bunge la Muungano, wakiwamo Wajumbe wote 32 wa Baraza la Mapinduzi.
Licha ya upendeleo huu, Nyerere hakufanikiwa kudhibiti mhimili wa kisiasa Zanzibar chini ya Karume.  Mfano, Zanzibar chini ya Karume, ilikataa kuhamishia kwenye Muungano mambo mengi yaliyopaswa kuwa chini ya Serikali ya Muungano;  kwa mfano, iliendelea kudhibiti jeshi lake la ulinzi na Idara ya Uhamiaji, Karume akiwa amiri jeshi wake Mkuu.  Ndiyo kusema, aliuawa na wanajeshi  wa jeshi lake la Zanzibar, si Wanajeshi wa JWTZ.
Karume alikataa Serikali ya Muungano kugusa akiba ya fedha za kigeni ya Zanzibar, japokuwa fedha lilikuwa jambo la Muungano.  Aidha, Karume na Baraza lake la Mapinduzi walikiuka mara nyingi mapendekezo ya kisera kutoka Bara kiasi kwamba Nyerere hakuwa na kauli tena juu ya sera za kiserikali.
Karume akakataa pia mazungumzo zaidi ya kikatiba kwa hofu ya Zanzibar kupoteza hadhi na mamlaka yake.  Karibu kila alichopendekeza Nyerere, alipata jibu la mkato kutoka kwa Karume:  “Kama hivyo ndivyo, tuvunje Muungano”.
Mitazamo hasi ya viongozi hawa wawili juu ya Muungano, ndiyo iliyosababisha mchakato wa kupata Katiba ya Muungano ndani ya mwaka mmoja kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano usifanyike, na Muungano kuongozwa kwa Katiba ya Muda kwa miaka 13 hadi 1977 na baada ya Karume kufariki.
Nyerere alipowasilisha na kupitishwa kwenye Bunge la Muungano, Mpango wa kwanza wa Maendeleo wa miaka mitano, na kutangaza nia yake kuona unatumika pia Visiwani, Karume aliupinga; akaja na mpango wake tofauti wa miaka mitatu kwa Zanzibar ulioandaliwa na mchumi kutoka Ujerumani Mashariki.
Kwa yote hayo na mengine, Nyerere alianza kuonyesha dhahiri chuki yake kwa utawala wa kimabavu wa Karume.  Naye (Karume) alipotambua hilo, alizuia mwingiliano huru wa watu kati ya Visiwani na Tanzania Bara kwa hofu na kwa sababu zinazofahamika.
Si mara moja, hofu na wasiwasi wa kimaasi vilipojionyesha Zanzibar, mamlaka za usalama zilimshauri Mwalimu kufuta ziara zake Visiwani.  Hofu hizi zilijidhihirisha zaidi pale Othman Sharrif, baada ya uteuzi wake wa Ubalozi Marekani kufutwa kwa shinikizo la Karume na kurejea Zanzibar, alipokamatwa na kutiwa kizuizini bila kosa.
Ilibidi Nyerere aingilie kati na kumwita Karume Ikulu, kuonyesha jinsi alivyochukizwa na kitendo hicho; lakini Karume alimkatalia, kuonyesha kwamba Nyerere hakuwa na mamlaka kwake. Sharriff aliachiwa baadaye kwa hiari ya Karume, na Nyerere akamteua kuwa Afisa Mifugo Tanzania Bara. 
Hata hivyo, Oktoba 1969, wakati Nyerere akiwa ziarani nchi za nje, Sharrif alikamatwa Tanzania Bara na kurejeshwa Zanzibar alikouawa.
Zipi adha nyingine kwa Nyerere?  Ni nani huyu Luteni Hamoud Hamoud?  Kwa nini aliongoza mauaji ya Karume? 
Inaendelea...
KATIKA sehemu ya pili ya makala haya wiki iliyopita, tuliona jinsi Rais Abeid Amani Karume alivyotawala kwa mkono wa chuma bila kufuata katiba wala utawala wa sheria, na hivyo kujitengenezea maadui wengi katika jamii ya Kizanzibari na kwa makada wenzake wa ASP wenye siasa za mrengo wa kushoto ambao, alianza kuwatimua kazi au kuwahamishia kwenye Serikali ya Muungano.
Tulimaliza kwa kuona kwa sehemu tu, jinsi alivyogeuka kuwa adha na kero kubwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kwa Muungano wenyewe, kiasi cha kuuweka Muungano huo kwenye hati hati ya kuvunjika.  Tuendelee na sehemu ya Tatu, kuona kilichofuata.
Karume alikuwa mwiba kwa Nyerere
Mbali ya Karume kuweka wazi kwa kusema kwamba, “Muungano ni kama koti tu; likikubana au kukuzidishia joto unalivua na kuendelea na safari yako”, pia alijipa ujasiri usio wa kawaida kwa kumkatalia Nyerere hadharani kila mara juu ya baadhi ya mambo ya Muungano akisema: “…..kama ni hivyo, sikubali, bora tuvunje Muungano”.
Ni ujasiri huu wa Karume usio wa kawaida juu ya jambo nyeti kama hili, uliofanya Nyerere atoe tamko lake maarufu juu ya hatima ya Muungano akisema:  “Kama watu wa Zanzibar, bila ya ulaghai kutoka nje, wataona ni bora kuvunja Muungano, mimi siwezi hata kidogo kuwapiga mabomu na kuwaua wananchi wa Zanzibar.  Kama waliingia katika Muungano kwa hiari yao, vivyo hivyo wanaweza pia kujitenga kwa hiari yao.  Hatukuishinda Zanzibar (kuwafanya mateka) vitani” (Soma:  William Edgett Smith, “Mwalimu Julius K. Nyerere”, tafsiri ya Kiswahili na Paul Sozigwa, uk. 154).
Wakati Mwalimu alikuwa mstari wa mbele katika kupinga ubeberu wa Marekani wakati wa vita ya Vietnam, na kwa ukombozi wa nchi za dunia ya tatu kwa ujumla, Karume alimbeza na kutangaza adhabu kali Visiwani kwa yeyote aliyelaani na kupinga ubeberu, au kuimba nyimbo za kuikashifu Marekani.
Mwalimu alipokosana na Uingereza kwa nchi hiyo kuukingia kifua utawala wa kidhalimu, kibaguzi na wa mabavu (UDI) wa Ian Smith nchini Rhodesia Kusini (sasa Zimbabwe), na kwa sababu hiyo uhusiano wa Mwalimu na Balozi wa Uingereza nchini, Sir Horace Phillip kuingia mkwara, Karume alionyesha hadharani kila mara kusuhubiana na Balozi huyo kwa kicheko cha bashasha na uswahiba kwa chukizo kwa Nyerere.
Tunaweza kutua kidogo hapa kuangalia nyuma mazingira aliyokuwamo Karume, miezi michache kabla ya kifo chake; bila shaka tutabaini kuwa, kiongozi huyo alikuwa katikati ya uhasama na uadui wa kujitakia.
Kwanza alikuwa na uhasama mkubwa na jamii pana ya Kizanzibari kwa udikteta wake uliokithiri uliosababisha mauaji, watu kutiwa kizuizini au kuhamishiwa Bara.  Pili, kulikuwa na tatizo la njaa na mlipuko wa malaria; mambo ambayo hakuonekana kujali.
Tatu, kulikuwa na uhasama mkubwa wa kisiasa kati yake na makada wenzake wenye siasa za Ki-Karl Marx ndani ya ASP waliomtuhumu kushindwa kuongoza, achilia mbali jamii ya Kiarabu aliyoitimua kikatili Zanzibar na iliyoendelea kutema laana kwake ughaibuni.
Nne,  kulikuwa na Nyerere ambaye alianza kumuona kama mzigo na kero kwa Serikali ya Muungano na kwa siasa za kimataifa.  Yote haya yalikuwa baruti tosha kuweza kulipuka na kumdhuru Karume kwa namna yoyote iwayo.
Ni nani huyu Luteni Hamoud?
Luteni Hamoud Mohamed Hamoud, alikuwa mtoto wa mzee Mohamed Hamoud ambaye alikamatwa na kutiwa kizuizini na Karume miezi kadhaa baada ya Mapinduzi ya Januari 1964, na hatimaye kufariki dunia akiwa kizuizini.
Miaka kadhaa baadaye, wakati Hamoud Hamoud akichukua mafunzo ya kijeshi huko Tashkent nchi iliyokuwa katika  Shirikisho la Urusi ya zamani, alifahamishwa na mmoja wa wanafunzi wenzake juu ya kuuawa kwa baba yake.  Kwa uchungu mkubwa, aliapa sawia na baadaye, kwamba angemuua Karume kulipiza kifo cha baba yake.
Mfumo wa Usalama wa Zanzibar ulioenea kila mahali, ulijulishwa haraka na mmoja wa ma-ofisa usalama waliokuwa kwenye mafunzo pamoja na Hamoud, juu ya kusudio hilo la Hamoud.
Lakini cha kushangaza ni kwamba, Hamoud aliporejea Zanzibar baada ya mafunzo hakukamatwa wala kuwekwa kwenye uangalizi; badala yake alipandishwa cheo kuwa luteni usu, katika sherehe iliyohudhuriwa na Karume mwenyewe kama Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Zanzibar.
Ikumbukwe kuwa, suala la Usalama wa Taifa halikuwa jambo la Muungano; liliongezwa kwenye orodha mwaka 1984 kufuatia kadhia ya Aboud Jumbe ya kuchafuka kwa hewa ya kisiasa Zanzibar, likaunganishwa kusomeka kwa pamoja na jambo la Ulinzi kuwa “Ulinzi na Usalama”.
Pale risasi ya Hamoud ilipochukua uhai wa Rais Karume miezi kadhaa baadaye, Serikali ilisisitiza kwamba, mauaji hayo yalikuwa sehemu ya njama kubwa ya kuangamiza Mapinduzi ya 1964, kutokana kwamba, Hamoud na wauaji wenzake walikuwa wanachama wa zamani wa Umma Party, kilichokiunga mkono ASP huko nyuma, na kukipa [ASP] mwelekeo bora wa kiitikadi [Ukomunisti] na kuheshimika kisiasa.
Kufuatia mauaji hayo, watu 1,100 walikamatwa na kuhojiwa.  Babu alikamatwa na kutiwa kizuizini Tanzania Bara kwa tuhuma za kuongoza mpango mzima; nao maofisa wa ngazi za juu wa Kizanzibari Jeshini Bara, kama Ali Mahfoudh na wengine, nao walishukiwa na kuondolewa kwenye utumishi wa Jeshi Tanzania Bara bila kurejeshwa Zanzibar.
Mgongano dhana ya mauaji
Kuna dhana mbili zinazogongana, lakini zote zenye nguvu; juu ya sababu za kuuawa kwa Karume.  Dhana ya kwanza ni hii ya Hamoud kulipiza kisasi.
Lakini suala la kulipiza kisasi linakoma pale tunapoona watu kama Kapteni Ahmada na raia Ali Chwaya ambao hawakuwa na uhusiano wa kifamilia na marehemu Mohamed Hamoud aliyeuawa, kujiingiza katika kulipiza kisasi.
Lakini, kama tutakavyoona baadaye, Kapteni Ahmada alijiingiza kama hatua tu ya kujisafisha kwa kujutia ushahidi wa uongo aliotoa dhidi ya Hanga na wenzake 18 waliouawa mwaka 1969, na yeye kuonekana kama adui na msaliti wa umma wa Kizanzibari.  Inapofikia hapo, inakuwa dhahiri kwamba mpango huo ulibeba hasira za jamii pana ya Kizanzibari.
Dhana ya pili ambayo ndiyo msimamo wa Serikali ni kwamba, mauaji hayo yalikuwa mpango mpana wa kupindua Serikali.  Dhana hii inapata nguvu kutokana na watu wengi kuhusishwa na tuhuma hizi, lakini kama tu tuhuma dhidi yao zilikuwa za kweli; vinginevyo dhana ya kwanza inashinda.
Mipango ilivyopangwa na kupangika
Chuki binafsi?  Hapana, Hamoud hakuwa peke yake; ilikuwa ghadhabu ya umma kwenye jamii pana ya Kizanzibari, kila kundi au sehemu ya jamii na malalamiko yake.
Kwa mujibu wa taarifa za Usalama wa Taifa Zanzibar, mipango ya kupindua Serikali ya Karume ilianza kusukwa tangu 1967 – 1972 ndani ya Zanzibar na Tanzania Bara, ambako nyumba ya Abdulrahman Babu ilikuwa kituo cha mikutano ya Wazanzibari ya kupanga Mapinduzi hayo.
Kama hivi ndivyo, Karume alikuwa na sababu tosha kumtaka Nyerere kumrejesha Babu Zanzibar “kuhojiwa”, Februari 1972.
Mkutano wa mwisho ulifanyika Aprili 2, 1972, ambapo ilikubaliwa Mapinduzi yatekelezwe Aprili 7, 1972, yakihusisha makundi mawili: kundi la Wazanzibari kutoka Bara, wengi wao wakiwa wanajeshi, na kundi la Wazanzibari ndani ya Zanzibar, likihusisha raia na wanajeshi wachache.
Pamoja na uamuzi huo, kikao kilitoa majukumu mazito kwa baadhi ya washiriki, ikiwa ni pamoja na Hamoud na Ahmada kupewa jukumu la kuiba silaha kutoka kambi ya kijeshi, Bavuai.
Ilikubaliwa kuwa, Babu na wafuasi wake kutoka Bara wasafiri kwa mtumbwi kwenda Zanzibar Aprili 6 kuamkia alfajiri ya Aprili 7, na kufikia eneo lililopo kati ya mitambo mikuu ya mawasiliano [Cable and Wireless] na Klabu Starehe.  Baada ya hapo, Babu abakie amejificha kwenye nyumba ya Hamoud Hamoud, iliyotizamana na Klabu Starehe eneo la Shangani, kusubiri saa ya mapambano kuwadia.
Kwa mujibu wa taarifa, Babu aliondoka Dar es Salaam kwa mtumbwi uliofungwa redio mbili za mawasiliano, jioni ya Aprili 6, safari iliyoelezwa kuwa ya “kuvua samaki”; wakati madhumuni halisi yalikuwa ni kuwafikisha Babu na wafuasi wake Visiwani usiku wa Aprili 6, kwa maandalizi kamili ya kupindua Serikali
Jioni hiyo, Aprili 6, Uongozi wa Jeshi uligundua upotevu wa silaha nyingi Kambini Bavuai.  Na ingawa uongozi ulikuwa bado haujamhusisha mtu yeyote, lakini Hamoud, Hamada na askari wengine walianza kufuatiliwa kwa siri.
Yaelekea kufikia hapo, Babu alijulishwa na kuonywa kwa njia ya redio akiwa baharini, juu ya kugunduliwa kwa mpango mzima wa Mapinduzi; akakatiza safari na kurejea haraka Dar es Salaam hima.  Haijulikani kama wafuasi wake walikuwa wamekwishafika Zanzibar au la; au kama nao walijulishwa na kurejea Dar es Salaam. 
Lakini kuwapo Visiwani wanajeshi kama Kanali Mahfoudh  (Mkurugenzi wa Operesheni JWTZ, Dar es Salaam) na Luteni Hashil Seif (Kikosi cha Wanamaji, Ukonga, Dar es Salaam) saa ya kuuawa Karume, kunaonyesha baadhi yao tayari walikuwa Zanzibar kusubiri wenzao.
Saa 12.00 asubuhi, Aprili 7; Ali Khatibu Chwaya (raia) alikwenda kwa Ali Mshangama Issa (afisa wa tatu, meli M.V. Afrika, mkazi wa Zizi la Ng’ombe, Zanzibar), kumweleza juu ya kutowasili kwa kundi la Dar es Salaam. 
Baadaye asubuhi hiyo, Ali Mshangama, Chwaya, Miraji Mpatani  (karani wa shirika moja, Zanzibar), Mohammed Abdullah Baramia (Mtunza Bohari, Idara ya Elimu), Ahmada na Hamoud, walikutana nyumbani kwa Hamoud na kuonyesha kukerwa na kusikitishwa kwa kutowasili kwa wapanga mapinduzi kutoka Dar es Salaam, hasa wakijua pia kwamba, silaha zilizoibwa bado zilikuwa nyumbani kwa Hamoud, na hatari ya kuweza kugunduliwa.
Ilipofika saa 6.00 adhuhuri siku hiyo, Mshangama, Hashil Seif, Amar Saad Salim, maarufu kama “Kuku” (afisa usafirishaji, Idara ya Siha, Zanzibar) na Chwaya, walikutana nyumbani kwa Amar Saad ambako Mshangama, Hashil Seif na Baramia walipendekeza mpango wa kupindua Serikali uahirishwe hadi watakapopata taarifa tofauti kutoka Dar es Salaam.
Kwa hiyo, saa 9.00 mchana siku hiyo, saa mbili tu kabla ya kuuawa kwa Karume, Baramia alikwenda nyumbani kwa Hamoud eneo la Shangani kuwasilisha pendekezo hilo.  Alimkuta Miraji Mpatani nje ya nyumba na kumweleza Baramia kwamba, pamoja na kundi la Dar es Salaam kutowasili, Ahmada na Hamoud walishikilia Mapinduzi yafanyike tu siku hiyo, kwa sababu Ahmada alikuwa anatafutwa na maafisa wa Jeshi.
Je, ni kwa sababu hii Luteni Hamoud, Kapteni Ahmada na Chwaya waliamua kufanya Mapinduzi, licha ya wenzao kutaka yaahirishwe?.
Inaendelea...

MAREHEMU ABDULRAHMAN MOHAMMED BABU NA BARUA YAKE

20794_10200451249000010_7099013988883810320_n

                     Marehemu Abdulrahman Mohammed Babu
Ahmed Rajab
JUMAPILI, Novemba 9, 1975, siku mbili kabla ya Ureno kusalimu amri na kuipa Angola uhuru wake, Radio Tanzania, Dar es Salaam, ilinguruma ikiwapasha Watanzania habari motomoto wasizozitarajia siku hiyo ya mapumziko.

Habari hizo ziliihusu serikali yao. Rais Julius Nyerere aliibadili serikali yake kwa kuliteua Baraza jipya la Mawaziri. Majina ya mawaziri na wizara zao zilipotangazwa, ilibainika kwamba baada ya miaka mingi Nyerere aliona bora abadili mtindo na awe na waziri kamili wa sheria.

Chaguo lake la waziri wa kuiongoza wizara mpya lilikuwa Julie Manning. Manning alikwishapata umaarufu kwa kuwa mwanamke pekee katika kundi la mwanzo la wanafunzi waliohitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya kuingia chuoni humo 1963. Kadhalika, yeye ni mwanasheria wa kwanza wa kike na jaji wa kwanza wa kike nchini Tanzania.

Mara ya mwisho Nyerere alipokuwa na waziri wa sheria ilikuwa kabla ya kuundwa Tanzania alipokuwa Rais wa Jamhuri ya Tanganyika. Waziri wake wa sheria alikuwa Chifu Abdalla Said Fundikira.

Nyerere na Fundikira walitoka mbali. Wote walikuwa watoto wa machifu, waliosomea Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda. Muhimu zaidi walikuwa wapiganiaji uhuru wa Tanganyika. Juu ya yote hayo, miaka michache tu baada ya uhuru walikorofishana na mwaka 1963 Fundikira alijiuzulu uwaziri.
Nyerere hakuona haja ya kumteua waziri mwingine wa sheria hadi 1975 alipomteua Manning. Kwa muda wa miaka 12 mambo yaliyohusiana na sheria yalikuwa yakisimamiwa na waziri wa mambo ya ndani ya nchi. Watanzania walikwishaizoea hali hiyo ya ‘sheria kutokuwa na wizara mahususi.’

Kipindi hicho kilikuwa kipindi kigumu kwa sheria na kwa haki za binadamu Tanzania, hasa Zanzibar ambayo ilikuwa na mfumo wake wenyewe wa kisheria uliokuwa wa ajabu ajabu.
Huko, watu wengi walifungwa jela bila ya kushtakiwa. Kuna waliokamatwa na vyombo vya dola na ambao hadi leo hawajulikani walipo na kuna walioteswa mateso ya kila aina hadi wakafariki. Kuna waliokamatwa kwa visingizio vya kisiasa na kuna waliokamatwa kwa sababu za wivu.

Yaliyokuwa yakitendeka katika Gereza Kuu la Zanzibar yameelezewa vizuri kwenye riwaya “Haini” ya Adam Shafi, aliyewahi kuwa mfungwa wa kisiasa gerezani humo.

Nyerere alipoamua kumteua waziri kamili wa sheria, magereza ya Tanzania yalikuwa yamesaki wafungwa waliokuwa wamehukumiwa kwa kuhalifu sheria.

Walikuwako pia chungu ya watu waliokuwa wamewekwa kizuizini kwa sababu za kisiasa. Wafungwa hao walikuwa wametiwa korokoroni bila ya kufikishwa mahakamani. Huko jela walikuwa ‘wageni wa Nyerere.’

Mnamo mwaka 1962, Bunge la Tanganyika liliidhinisha Sheria maalumu iliyompa Rais haki ya kuamrisha mtu akamatwe na afungwe endapo atahisi kwamba mtu huyo ni kitisho kwa usalama wa taifa. Sheria hiyo ilitumiwa pia dhidi ya mafisadi, wahujumu uchumi na wahalifu wengine.

Iliainisha kwamba mtu anaweza kukamatwa kwa amri ya Rais na kuzuiwa gerezani kwa muda usiozidi siku 15 bila ya kushtakiwa au kufikishwa mahakamani.

Hayo ni madaraka makubwa aliyopewa Rais. Aliwaumiza wengi kwa kuyatumia kwani sheria hiyo ilikuwa kama wavu uliowakumba waliokuwamo na wasiokuwamo.

Ingawa sheria ilisema kwamba mtu anaweza kushikwa kwa muda usiozidi siku 15, hata hivyo, shirika la haki za binadamu la Amnesty International liliwahi kusema kuwa kulikuwako watu waliokuwa wamewekwa ndani kwa muda uliofikia hata miaka 10 bila ya kujuwa walituhumiwa kwa kosa gani.

Wakati hali ilikuwa mbaya hivyo katika magereza ya Tanzania Bara, hali katika magereza ya Zanzibar ilikuwa mbaya zaidi kwa sababu ilikuwa kawaida wafungwa kuteswa.

Megereza ya Tanzania yana historia ndefu. Yale ya Tanganyika yalijengwa toka nchi hiyo ilipokuwa chini ya utawala wa Wajerumani kabla ya mwaka 1914. Ya Zanzibar yalijengwa miaka mia moja iliyopita Waingereza walipojenga gereza la mwanzo la kisasa visiwani. Waingereza walipoitawala Tanganyika waliyajenga mengine na baada ya uhuru serikali ya Tanganyika ikayaongeza.

Moja kati ya magereza ya mwanzo yaliyojengwa Tanganyika baada ya uhuru ni lile la Ukonga, jijini Dar es Salaam. Ukonga ni gereza lenye sifa mbaya. Lina historia ya kuwa na idadi kubwa ya wafungwa kushinda nafasi iliyo nayo, chakula chake kibovu na huduma zake za afya pia ni duni.

Kwa sasa Tanzania ina magereza yasiyopungua 120 kwa wafungwa wasiopungua 45,000. Wafungwa hao hubanana utadhani kuku waliotiwa susuni, au katika tenga, kupelekwa mnadani.

Nimeambiwa kwamba siku hizi takriban nusu ya wafungwa hao ni washtumiwa wanaozuiliwa kusubiri kesi zao au wafungwa waliowekwa rumande.

Zaidi ya watu elfu moja walikamatwa na kuwekwa kizuizini Zanzibar baada ya kuuliwa Sheikh Abeid Karume Aprili 7, 1972 na mwaka mmoja baada ya tukio hilo, 81 miongoni mwao walishtakiwa. Kumi na saba kati yao wakiwa pamoja na Abdul Rahman Babu, waziri wa zamani katika Serikali ya Muungano, walishtakiwa ilhali wenyewe wakiwa hawapo Zanzibar.

Kama alivyoeleza karibuni Bibi Ashura Hilal, aliyekuwa mkewe Babu, katika kurasa za gazeti hili, Nyerere alikataa kuwapeleka Zanzibar ambako hamna shaka wangeliuliwa. Badala yake aliwafunga bila ya mashtaka yoyote katika magereza mbalimbali ya Bara.

Aliitumia ile sheria iliyompa nguvu za kuwaweka watu kizuizini bila ya kuwafikisha mahakamani. Akina Babu waliselelea wakisota gerezani kwa muda wa miaka sita hadi Aprili, 1978. Siku Julie Manning alipoteuliwa awe waziri wa sheria Babu na baadhi ya wenzake walikuwa wamefungwa Ukonga. Hawakuwa wakisubiri kesi wala hawakuwekwa rumande.

Siku 12 baadaye, mnamo Disemba 21, Babu alishika kalamu na kumuandikia barua Manning iliyokuwa na maneno takriban 1,300. Baada ya kumpongeza kwa kuteuliwa kushika nyadhifa hiyo muhimu, Babu alilitoa dukuduku lake na la wenzake kuhusu hali zao za gerezani akitumai kwamba hatimaye waziri atachukuwa hatua za kuwatoa Watanzania kutoka kwenye aibu hiyo.

Halafu humo humo Babu alimpa Manning darsa za kisiasa, maadili, sheria na za historia. Kwa mfano, alimnukuu Fidel Castro aliyewahi kusema kwamba hakuna kazi iliyo ngumu “kushinda kumshtaki mtu asiye na hatia.” Babu alimuelezea Castro kuwa “mpiganiaji thabiti, adhimu na shujaa wa haki za umma.”

Kadhalika, Babu alimwandikia Manning hivi: ““Tatizo la kijamii, naliwe kubwa vipi na lenye kutisha vipi, linaweza tu kutanzuliwa kwa njia za kijamii na siyo kwa ukandamizaji.” Halafu Babu akamtajia Manning Jenerali Francisco Franco, aliyekuwa dikteta wa Hispania tangu 1939 hadi alipofariki 1975. Babu aliandika: “Franco alijaribu kukandamiza, na tazama mchirizo wa damu na uvundo aliouacha.”

Barua hii inaonyesha kwamba ijapokuwa Babu alikuwa ndani gerezani akishikiliwa na vyombo vya dola asiweze kufurukuta, hata hivyo, bado alikuwa akiyajuwa vyema yaliyokuwa yakijiri nje ya kuta za gereza la Ukonga.

Alimueleza Manning, kwa mfano, kuhusu jinsi wafuasi wake waliokuwa wameshtakiwa kwenye kesi ya uhange huko Zanzibar walivyokuwa wakiteswa ili wakubali kwamba kulikuwa na mpango wa kuipindua serikali ya Afro-Shirazi Party.

“Inajulikana kwamba watu wanne wamekufa kwa kuteswa. Wawili walipigwa risasi ili wenzao watishike na wakiri [kwamba kulikuwa mpango wa kupindua].”

Aliwataja watu hao kuwa ni Luteni Mikidadi Abdulla Ali, maarufu kwa jina la ‘Meki’ na Luteni Ali Othman. Aliongeza kwamba wengine wawili, aliowataja kuwa ni Abbas Muhammadiya na Muhammed Saghir, walifariki baadaye baada ya kuteswa na kunyimwa huduma za afya.

Kwa hivyo, watawala na vyombo vyao vya dola vilishindwa kumzuia Babu aliyekuwa gerezani asiwe na mawasiliano na walio nje na kuyajuwa yanayotendeka mitaani hadi serikalini.
Na hayo yasingeliwezekana lau pasingekuwako ushirikiano kati ya baadhi ya askari jela wakizalendo na wafungwa wao.
Walikuwepo bila ya shaka ‘mabwana jela’ waliowasaidia wafungwa kwa kuhongwa lakini walikuwako wengine waliouweka uzalendo mbele na wakawasaidia wafungwa kama kina Babu kwa sababu wakiziamini fikra zao.

Halafu kuna mianya hata katika udhibiti wa dola ambayo humwezesha anayethubutu akaweza kuipenya. Bila ya kueleza mengi niseme tu kwamba binafsi niliweza kuipenya mianya hiyo mara mbili nikaingia Ukonga kwa njia ya ‘halali isiyo halali.’ Mara moja kumtembelea Babu na mara ya pili kumtembelea jamaa yangu, Badru Said, aliyekuwa amefungwa naye.

Mara ya mwanzo ‘bwana gereza’ aliniruhusu nizungumze naye Babu kwa muda mrefu sana kuliko uliokuwa ukiruhusiwa kisheria. Ulikuwa mrefu mno hata aliyenishindikiza gerezani aliingiwa na wasiwasi nje ya jela akidhania kwamba labda na mimi pia nimeshikwa. Hakuna mwingine ila mkewe Babu, Ashura.
Kwa hakika, bibi huyu katika mahojiano yake yaliyopita na Raia Mwema hajaeleza hata chembe ya mchango wake katika juhudi za kuwapigania akina Babu na wafungwa wenzake wa kisiasa.

Pengine Watanzania watashangaa kusikia kwamba watu watatu waliokuwa muhimu katika kampeni ya kuwapigania wafungwa hao walikuwa wanawake: yeye mwenyewe Ashura pamoja na Shirin Hassanali aliyewahi kuwa katibu muhtasi wa Babu na bibi mwengine ambaye kwa sasa sitotaka kumtaja kwa vile sikupata bado ridhaa yake.

Wao, kwa njia zao wazijuwazo wenyewe, ndio walioanzisha mawasiliano na wafungwa na kuwezesha barua zao zitoke nje. Si barua tu bali hata muswada wa kitabu cha Babu cha “African Socialism or Socialist Africa?” na miswada miwili mifupi ya Kanali Ali Mahfoudh. Mmoja ulihusu mapambano ya ukombozi wa Angola na mwengine ulimhusu Sheikh Abeid Amani Karume.

Ule wa Babu waliniletea London na nikaupatia mchapishaji na ile ya Mahfoudh niliondoka nayo mwenyewe baada ya kuizuru London.

Katika barua yake kwa Manning, Babu alisikitika kwamba sumu ya mateso ya Zanzibar ilikuwa inanyemelea Tanzania Bara. Aliandika hivyo kwa sababu Tahariri ya gazeti la Daily News la Novemba 18, 1975 ilitaka “maharamia’ wateswe ili wakiri makosa yao.

Babu alimwandikia hivi Manning: “Mwandishi wa tahariri haelewi kwamba ikiwa leo tutakubali maharamia wateswe, kesho itakuwa ni zamu ya wahariri kuteswa…”

Baada kushukuru kwamba Nyerere “mwenye kukirihishwa na umwagaji wa damu” ndiye aliyekuwa Rais wa Tanzania Babu alitahadharisha kwamba “Nyerere ni binadamu na akija akarithiwa na mtu mwenye maadili ya paka shume, basi maadili yote ya kisiasa na ya kijamii yatakuwa ya kipaka shume, ikiwa atarithi taasisi zilizopotoka kimaadili.”

Babu aliihitimisha hivi barua yake: “Tunatumai kwa dhati kwamba kwa vile sasa sheria imepata Waziri, haki itatendeka. Hatudai zaidi ya haki yetu ya kutendewa kwa mujibu wa sheria za nchi, na tufunguliwe kutoka maisha haya ya usumbufu, kwa mujibu wa sheria. Usiifanye historia ikaja kusema (kutuhusu) kwamba: “Waligonga kwa nguvu mara kwa mara kwenye kwenye lango la haki lenye nuru, lakini hawakujibiwa.”

Barua ambayo mahabusi Babu alimwandikia waziri Manning ni yenye kusisimua na ni muhimu kwa historia. Kwa hakika, sikuitendea haki kwa kuidokoadokoa hapa na pale. La kushangaza ni kwamba ina mengi ya kimsingi kuhusu dhana nzima ya haki ambayo bado yanaikabili Tanzania.

Juu ya muda wote uliopita tangu iandikwe na mageuzi yaliyotokea nchini, mengi anayoyalalamikia Babu humo bado tungali nayo. Sio katika magereza tu bali katika jamii nzima ya Tanzania kwa jumla.

Wafaransa wana usemi wao unaoielezea vizuri hali kama hiyo. Wao husema: “plus ça change, plus c’est la même chose.” Yaani, kila mambo yanavyozidi kubadilika, ndipo yanavyozidi kubaki yalivyo.

Imekuwa kama watawala wetu hawajajifunza chochote kutoka historia.

Wanasahau kwamba ni muhimu kujifunza kutokana na yaliyopita. Wasipofanya hivyo watazidi kutuhasiri na kutuumiza kwani watarejelea kufanya makosa yale kwa yale na dhunubu hizo kwa hizo, mara baada ya mara.

TUKAE MKAO WA KULA KWA KAMPENI ZIJAZO NA AKILI ZETU VISIWANI

Afbeeldingsresultaat voor zanzibar
KAMPENI ZA KWETU NA USHUKU WA AKILI ZETU VISIWANI
Na: Mwandishi Maalum
Kuna watu hadi leo bado wanashangaa kwa nini Zanzibar imeshindwa kujikwamua na makucha ya ukoloni mpya uliojengwa kwa misingi ya hadaa iitwayo Muungano. Kwa lugha nyepesi Zanzibar haijapata kuwa huru, tusidanganyane. Lakini hali hii pamoja na kuwa inachangiwa na mataifa makubwa ya magharibi, mchango wetu sisi wananchi wa Zanzibar kama Zanzibar ni mkubwa mno katika kujihakikishia kuwa tunabakia kuwa watumwa wa ukoloni usiokwisha wa Mkoloni Mweusi Tanganyika.
Nina kila aina ya ushahidi kuwa Wazanzibari wenyewe wanapenda kutawaliwa dumu daima. Kwa mfano, Zanzibar ilitawaliwa na Mwarabu kwa miaka karibu mia mbili. Hakukuwa na lolote la maendeleo tulilofanyiwa zaidi ya lile la kuchanganya damu baadhi yetu na kisha kuishi katika dhambi ya kubaguana kwa makabila. Dhambi ambayo bado ipo baina ya Wazanzibari wenyewe, ilhali wote au tuseme asilimia 99 tukiwa Waislamu. Na juu ya madhila yote tuliyofanyiwa, najua wengine watapinga lakini hakuna mkoloni mwema ingawa kuna watu wengi Zanzibar wanaojitanibu na Uarabu na hata wanatamani bado nchi hii ingekuwa chini ya Utawala wa OMAN. Hili moja tu.
Ushahidi wa pili kuwa sisi ni watumwa wa akili zetu, ni pale mwenyezi Mungu anaposema kuwa hatabadilisha katika watu jambo mpaka wao watakapotaka libadilike. Sasa hapa utaona, kwa vile hadi leo tunasifia na kuutamani ukoloni wa Mwarabu, wenzetu wenye nguvu ya mataifa yenye nguvu zaidi ya Waarabu, wakaitumia fursa hiyo kututawala. Wametutawala sio kwa lazima, bali kwa akili na mapenzi yetu. Hapa namaanisha kuwa akili ya Mzanzibari haijawahi kuwa huru na kwa maana hiyo, akili isiyo kuwa huru haina haja ya kupewa uhuru. Itabakia kuwa akili ya kiutumwa tu!
Sababu kubwa ya kuwa tunabakia kifungoni kama nilivyotangulia kusema, ni akili zetu. Ni uhakika kuwa wengi wetu tumenyimwa elimu ya kujitambua lakini pia hata baada ya zama za ukweli na uwazi kufika, bado inakuwa vigumu sana kwa Mzanzibari kujikwamua na makucha ama ya ukoloni mweusi na ule ukoloni wa Viongozi ambao hawana la kuwapa wananchi zaidi ya lugha chafu kila ifikapo siku za kampeni za uchaguzi na kuwadanganya tutafanya hivi na vile na hakuna moja walilo fanya zaidi ya nusu karne sasa.
Mfano mwingine ulio hai, ukitaka kujua kwa kiasi gani akili zetu na zile za viongozi wetu zimefilisika, sikiliza kampeni zetu za siasa hasa majira au tuseme msimu kama huu wa uchaguzi. Nijuavyo, na uzoefu wangu unaonyesha kuwa, watu huenda kampeni kusikiliza mipango ya wagombea juu ya murua wao na wa nchi yao. Kwa kuwa muwazi na fasaha zaidi, watu huenda kwenye kampeni kusikiliza ni kiongozi au chama gani kina sera na ilani nzuri ya maendeleo kwao ili wapate waamue nani wamchague. Hivi ndivyo kampeni za watu wenye akili timamu zinavyofanywa. Kwetu sisi hali haiko hivyo!
Ukitaka kuthibitisha fuatilia mikutano yote ya vyama vya siasa inayofanyika hapa kwetu. Tena hasa hasa mikutano ya chama fulani hivi. Utakutia mkutano wa kampeni wa masaa matatu mazima unahutubiwa na viongozi wasiopungua kumi, na hakuna hata mmoja anayezungumza la maana zaidi ya matusi. Tena matusi ambayo wale wanaoyazungumza, hawathubutu hata kuyazungumza majumbani mwao lakini ktk jukwa la kampeni wanatukana kama hawana akili vizuri hiyo ndio barabara,viwanda,hospitali,umeme,maji,skuli,elimu wanao wahidi wananchi matusi.
Kinachoshangaza sana ni kuwa, ikiwa huwezi kutumia matusi ya namna ile nyumbani kwenu au kwako, kuna haja gani uyaseme hadharani kwenye uwanja uliojaa watu – wazee, watu wenye heshima zao na hata viongozi wa dini, achilia mbali mastuhu zako na mastuhu wa wenzako?
Kampeni za kwetu visiwani, tangu kuanza kwa vyama vingi, imekuwa matusi ndio ilani ya vyama na sera zao. Na cha kushangaza wananchi, wengi wao wakiwa watu wazima waliojistiri vizuri, husafiri masafa marefu kufuatilia kampeni kama hizi kusikiliza matusi ya nguoni tu nakuchekelea!
Hili kwa kweli linanifanya nizihakiki upya akili za watu wetu hapa visiwani. Pia hali hii inanipa bishara kuwa kwa akili zetu zilivyo, maendeleo yatabakia kuwa ndoto kwani hakuna maendeleo kwa watu waliotawaliwa na wakoloni. Hakuna maendeleo pia kwa watu ambao ni watumwa wa akili zao mbovu. Na kwa maana hii, tutabakia kuwa hivi milele iwapo hatukubadilika.
Kampeni za vyama vya siasa za visiwani siku hizi ni zaidi ya kashfa. Tena kashfa ambazo hazina sitaha wala hazijali nani yupo na nani hayupo. Nani namstahi na nani simstahi. Awepo mkubwa awepo mdogo, matusi ndiyo ilani na sera ya vyama vyetu vya siasa. Kampeni zetu badala ya kutuambia kuhusu sera za kilimo, uvuvi, na maendeleo kwa ujumla zinatumia historia ya watu waliopata vyeo kwa kupiga ama kucheza Sunsumia.
Badala ya kampeni zetu kutuambia vipi ilani zao zitaboresha elimu ambayo kwa hakika inakufa kibudu kila uchao, tunaambiwa habari za vipi kiongozi fulani alipatikana ndani ya ndoa ya mama yake na baba yake. Kwa mfano, Kiongozi wa siasa anayetaka chama chake tukipigie kura, anathubutu kumsema mtu mzima mwenzake kuwa mama yake asingemzaa kama hakutoka nje ya ndoa ya baba yake. Maneno kama haya na mengine, tumeyazoea kuyasikia katika kampeni za kwetu na cha aibu zaidi, waliopo wote wanafurahia kusikia hivyo.
Nilitarajia kuwa kampeni zetu zitazungumzia namna gani zitaboresha huduma za afya kwa wananchi. Hilo sijalisikia kamwe kwa kweli. Badala yake, nasikia kuwa kiongozi fulani anataja msururu wa viongozi anaodai ni mashoga na wengine waliouza kaburi za baba zao. Haya kweli tuseme yametendeka, lakini yanatuhusu nini sisi kama wananchi ambao tunataka maendeleo yetu na ya nchi yetu?
Itatusaidia nini sisi kujua kuwa kiongozi fulani ni shoga au alikuwa mwanachama wa Sunsumia? Hii ina mshabaha gani na maendeleo yetu? Inatusaidia nini Wazanzibari kujua eti fulani mama yake kaolewa kwa mahari ya shilingi 500 alizogaiwa na kiongozi fulani na kisha akauza kaburi la baba au mama yake?
Ukweli, yote haya hayatusaidii kitu na wala si maneno ambayo watu wenye akili timamu wanaweza kuyajadili hadharani. Pia si maneno ambayo watu wenye akili timamu wanaweza kuyafuatilia kwenye kila mikutano tena kwa kusafiri masafa kuyapigia ngoma na kofi kwa kuyafurahia, ilhali huko makwao hakuna waliloacha kutokana na nchi yao kufilisika kimaendeleo. Inashangaza sana kwa kweli kuona watu wetu bado wanashabikia vyama ambavyo vimekuwa vikipata kura kwa umahiri wao wa kutukana na sio sera za maendeleo ya kweli.
Kwa hali hivi iendavyo, sasa natilia mashaka kwa kuhoji iwapo akili zetu Wazanzibari ziko sawa ama kwa lugha nyepesi naweza kusema inaonyesha hatujatulia. Na kwa hali hii hatuwezi kupata maendeleo wala kufika popote! Tutabakia kwenda katika kampeni kufurahia matusi ya viongozi ambao wapo kwa ajili ya neema zao tu na hawana cha kutupa sisi wanyonge isipokuwa lugha ya matusi iliyotokana na kufilisika kwao kisiasa. Kufilisika ambako kunazifilisi akili zetu pia na kutufanya tuamini kuwa viongozi wajuzi wa kutukana tu ndio wanaoweza kutuletea maendeleo katika visiwa vyetu. Tubadilike wananchi.

PIC ZA HISTORIA YA NCHI YA TANGANYIKA JAPO HAMUITAKI NCHI YENU YA TANGANYIKA


Hii Picha Ilipigwa Siku ya Nyerere Alipoweka Jiwe la Msingi Chuo Kikuu Cha Waislam, Chang'mbe 1968 Nyerere Anapeana Mkono na Mufti Sheikh Hassan bin Amir ...

Hii Picha Ilipigwa Siku ya Nyerere Alipoweka Jiwe la Msingi Chuo Kikuu Cha Waislam, Chang'mbe 1968 Nyerere Anapeana Mkono na Mufti Sheikh Hassan bin Amir ...

Uongozi wa East African Muslim Welfare Society katika ni Solomon Eliufoo (Waziri wa Elimu) na Tewa Said Tewa (Territorial President EAMWS) kulia kabisa aliyevaa kanzu na kilemba ni Mufti Sheikh Hassan bin Amir

uhuru day,people go berserk-kwa mbali naona ki bajaj kumbe hizi bajaj ni za siku nyingi

L - R: Sheikh Suleiman Takadir aka Makarios, John Rupia, Julius Nyerere na Bantu Group 1955

Kutoka Kushoto:Iddi Faiz Mafongo(Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na TANU),Sheikh Mohamed Ramia(Khalifa wa Qadiriyya),Julius Nyerere,Saadani Abdu KandoronaHaruna Taratibu. Picha imepigwa Dodoma

Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Al Habib Omar bin Ahmed bin Abubakar bin Sumeit Nyuma Yake ni Ali Mwinyi Tambwe, Abbas Sykes na Chini ni Sheikh Kassim bin Juma



ofisi ya taa kamba ya kuwa ofisi ya tanu

bara za wazee walio anzisha cha cha taa na kuwa tanu ndio hili


Aliyekaa Katikati ni Ilunga Hassan Kapungu na Kushoto Kwake ni Ali Salum Mkangwa na Aliyesimama Nyuma ni Mwandishi

Aliyesimama wa kwanza kulia ni Mzee Ali Msham mwenyekiti wa tawi la TANU Magomeni Mapipa wakati TANU inawaunganisha wananchi kupigania uhuru wa Tanganyika.
Bibi Titi Mohamed, Nyerere na John Rupia Mkutano wa TANU Jangwani, Dar es Salaam 1950s

Bi titi Mohamed akiwahubiri watanganyika kugombania uhuru wa nchi yao ya tanganyika



mkutano wa tanu

Urambo House, Tabora, mwaka 1951. siku hizi mnaita saloon nchini tanganyika

Kushoto Mohamed Jumbe Tambaza na Kulia ni Mshume Kiyate mashuja wa uhuru wa nchi ya tanganyika walio sahauliwa

Tawi hili la TANU Magomeni Mapipa lilikuwa na nguvu na viongozi mashuhuri wa TANU walifika mara nyingi kuzungumza na wanachama na viongozi wao.

gari la tanu nchini tanganyika


Ali Msham aliyekaa katikati katika moja ya mikutano ya ndani ya TANU aliyokuwa akifanya uani nyumbani kwake Mtaa wa Jaribu, Magomeni Mapipa

Bibi Titi Mohamed (1926 - 2000) Shujaa wa Uhuru wa Tanganyika

Waliosimama wa pili kushoto ni Ali Msham (Mwenyekiti wa Tawi la Magomeni Mapipa) na wa nne ni Bi. Khadija biti Jaffar wa tano Bi. Mtendwa biti Iddi Sudi,

Ofisi ya TANU Mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa kama ilivyokuwa ikionekana katika miaka ya 1950 ikiwa imezungikwa na wanachama wake.


.............?????????????????????????????.....................NDANI YA GININGI DODOMA NCHINI TANGANYIKA


GININGI DODOMA NCHINI TANGANYIKA

HII WALIPO KUTANA JIJINI DAR ES SALAAM IKULU YA NCHI YA TANGANYIKA
MBONA HUJA APISHWA NA 2020 HIYOOO INAKUJA WAPE UKWELI WAZANZIBARI MAALIM.

SIMULIZI YA MZEE THABIT KOMBO JECHA KUHUSU MAPINDUZI

Afbeeldingsresultaat voor sheikh thabit jecha
Asimulia walivyoihadaa serikali ya wakati huo kwa kuandaa ngoma wanamapinduzi waingie Unguja
Yeye, Aboud Jumbe nusura wamshawishi Sheikhh Karume kuyasitisha saa chache kabla ya kuyatekeleza
THABIT Kombo ‘Jecha’ ni majina ambayo ukiyataja, wakereketwa wa historia ya Zanzibar lazima watapatwa na kigugumizi kwa namna mzee huyu alivyojitolea nusu ya maisha yake kupigania haki za Wazanzibari walio na tamaa ya madaraka na nusu nyingine kuulinda Muungano feki wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na hadhi ya Mapinduzi ‘Matukufu’ ya mwaka 1964
Kila Januari 12, 2014, Zanzibar inaadhimisha miaka zaidu ya nusu karne tangu Mapinduzi hayo yaliyouondoa utawala wa kisultani visiwani humo yafanyike, ambapo wakwezi na wakulima waliungana na kusema; “uonevu sasa basi wengi wa wakwezi hao na wakulima walikuwa ni wageni tu sio Wazanzibari. Tunataka visiwa vyetu vilivyotawaliwa kwa miaka mingi bila ridhaa yetu vilejee mikononi mwetu ati wanajinadi.”
Katika kitabu kiitwacho ‘Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha,’ maneno au simulizi za mwanamapinduzi huyo zilizokusanywa na mwandishi, Luteni Minael-Hosanna O. Mdundo, kinaelezea kwa kina namna mzee huyo alivyokuwa na mchango mkubwa katika historia ya visiwa hivyo kukiangamiza mpaka leo tumaji.
Kama vile kukitia nakshi kitabu hicho kilichosheheni nyaraka mbalimbali muhimu za kihistoria, utangulizi wake uliandokwa kwa ustadi mkubwa na Baba wa Taifa ambaye ndiye Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere.
Mara nyingi Raia wa Kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Karume alipokwama katika masuala mbalimbali, mshauri wake mkubwa alikuwa Sheikh Thabit Kombo na hata Mwalimu Nyerere wakati akiwa Rais na baada ya kustaafu, alimtumia mzee huyu katika mambo mengi ya kisiasa na ushauri.
Kwa maneno yake mwenyewe Mwalimu kwenye utangulizi wa kitabu hicho, anasema: “Sheikh Thabit Kombo ndiye aliyependekeza Karume awe kiongozi wa chama kipya (Afro Shirazi Party – ASP). Karume, naamini kwa moyo na nia safi kabisa, hakutaka kuwa kiongozi wa chama kipya hicho!
“Bila busara, hekima na ujasiri wa Sheikh Thabit, pengine vyama hivyo (African Association na Shirazi Association) visingeungana au kama vingeungana, baadaye ungetokea mzozo kuhusu uongozi.
“Sheikh Thabit alikuwa kiongozi mpendwa, mwenye sifa njema, aliyependwa na watu wa kila rika kwa ushauri… Alikuwa radhi wakati wote kuwasikiliza wanyonge na wakati mwingine hata kuwavumilia wajinga na wakorofi kwa kiwango cha kushangaza.
“Nyumbani kwake na ofisini palikuwa mahali pa watu wa kila aina kuchota busara, wakiingia na kutoka mchana na usiku.”
Sheikh Thabit Kombo aliyezaliwa Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja mwaka 1904, hakubahatika kusoma sana elimu ya darasani (anasema aliishia chumba cha nne tu), lakini Mwenyezi Mungu alimjalia kipaji kikubwa cha kujifunza na kuzungumza kwa ufasaha hata kuweza kuwashawishi watu wenye mioyo migumu kuungana na vyama vya ukombozi wa Zanzibar na vya Afrika.

Anasemaje kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar?

Kuna mambo mengi ya kumzungumzia Sheikh Thabit Kombo, hata tukajaza gazeti zima hatuwezi kuyamaliza, lakini kwa kuwa leo ni siku ya kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar, hatuna budi kumtaja kwa muktadha huo.
Kila mmoja wetu hadi leo hadithi ya Mapinduzi ya Zanzibar inamshangaza, hakuna anayeamini kama wakulima na wakwezi ndio walioyaratibu bila msaada kutoka nje!
Lakini Sheikh Thabit Kombo anasema sababu kubwa ya ufanyika mapinduzi hayo ni madhila ya Waarabu waliyowafanyia wakazi wa Zanzibar, ambayo mengine hayasimuliki kwa namna yalivyokuwa mabaya!  
Katika mazungumzo yake na Luteni Minael-Hosanna kuhusu Mapinduzi ya Januari 1964, Sheikh Thabit Kombo anasema: “Usiniulize vijana wetu walioendesha Mapinduzi walipata wapi mafunzo au nani hasa alivamia mahala gani. Mimi sijui.
“Nasikia hadithi tu kila mmoja akijinasibu baada ya kushinda, mengine ya kweli na mengine ya uwongo mtupu.
“Ninachojua mimi ni kwamba Kamati Kuu ya ASP (wakati huo yeye akiwa ni Katibu Mkuu wa ASP) ilikaa ikasononeka sana baada ya mkutano wa pili wa London (uliojadili uhuru wa Zanzibar na kuendelea kumpa Sultani mamlaka).
“Tumesononeka kwa sababu matumaini yetu yote ya kuupata uhuru wa nchi yetu kwa njia ya vote (kura) yalikuwa yamefutika; iliyobaki sasa nchi kutawaliwa maisha yetu yote na vijitu vichache ambavyo vinafurahia sana dhuluma dhidi ya Mwafrika kama ilivyo sasa vijitu vii chache vya CCM wanafurahia maisha wengi wa Wazanzibari wako ktk hali ngumu sana.
“Hatimaye tukazaa shauri kwamba baada ya uhuru huo bandia (Desemba 10, 1963), ‘British Resident’ (Kiongozi Mkazi Mwingereza) akitoka tu, basi tushike mapanga tumng’oe Sultani. Uamuzi huo najua tena wote tulikuwa na kauli moja katika siri yetu kubwa na Mwenyezi Mungu akatubarikia katika dua letu.”
Hata hivyo, Mapinduzi hayakuwa rahisi bali kuliingia fitina nyingi ambazo kwa namna moja au nyingine zilianza kuwakatisha tamaa wanamapinduzi hao, Sheikh Thabit Kombo, anaelezea kisa kimoja usiku wa kuamkia siku ya Mapinduzi.
“Saa tano asubuhi Januari 11, 1964, ulikuwa ndio wakati wa kukamilisha mipango yote na kufanya marekebisho ya mwisho kama hapana budi. Tukakutana Sheikh Karume, Aboud Jumbe na mimi, viroho vinatudunda.
“Mimi nilikuwa nimepata fununu kuwa huenda mipango yetu imegundulika. Basi baada ya mkutano wetu, nikamshauri Sheikh Karume kwa hii habari yetu ya Mapinduzi inaonekana imeenea katika mji mzima, watu wanaizungumza, Aboud Jumbe naye akathibitisha kuwa na yeye kaisikia Miembeni. Basi tukaulizana tufanyeje,” anaeleza Sheikh Thabit.
Katika maelezo yake anasema walikubaliana kumuita Ofisa wa Polisi Unguja wamweleze kuwa kuna watu wanataka kufanya vurugu mjini, hivyo polisi waimarishe ulinzi. Lengo la kufanya hivyo ni kuwa ili machafuko yakitokea basi wao wawe katika mikono salama.
“Kumbe fikira ile ya kumwita Superintendent (Ofisa wa Polisi) ilikuwa mbinu ya kufaa sana, maana askari waliokuwako Bomani walipunguzwa nguvu na vikosi vya Mapinduzi vikaweza kuingia Bomani kwa urahisi na kuchukua silaha,” Sheikh Thabit Kombo (UK.134).
Kwa maelezo ya Sheikh Thabit Kombo, vikosi vya Mapinduzi viliingia maeneo ya mjini ambako siku hiyo kulikuwa na sherehe ya ‘Fete’ kuanzia saa 10 jioni, sherehe ilifanyika na watu wa kila rangi walikusanyika kwa furaha bila hofu.
Sherehe hiyo iliandaliwa na ASP ili kuwawezesha wakulima na wakwezi waliokuwa wakiishi mashambani, kuingia Unguja mjini bila vikwazo au vizuizi kutoka serikalini kama ilivyokuwa kawaida hasa nyakati za jioni kipindi hicho.
Kama walivyoagizwa na utawala wa Kisultani kuwa sherehe ilipaswa kuisha saa sita usiku, ulipotimu muda huo, ngoma zikazimwa na hapo ndipo ikawa mwanzo wa utekelezaji wa mipango ya Mapinduzi.
“Kwa mawe, marungu na mapanga, vijana hawa wakawa na ujasiri wa kushambulia makao makuu ya Jeshi la Polisi na kuyateka haraka haraka. Halafu wakakamata Ziwani. Hapo walipata silaha nyingi na walikuwapo waliokuwa wanajua kuzitumia, hivyo hivyo wakateka kituo cha Mtoni.
“Kivumbi kikawa Malindi, kule kulitokea mapambano makali, lakini moyo wa vijana wa ASP ambao sasa walikuwa wanatumia silaha (za moto) walizokuwa wamejinyakulia Ziwani na Mtoni, ukawasukuma hadi wakashinda. Haukupita muda wakawa wameikamata Malindi pia.
“Rahaleo ndiko kulikokuwa Makao Makuu ya Mapinduzi na Sheikh Karume alikuwa kule tokea usiku hadi alfajiri wakati sehemu zote muhimu zimekwisha kushikwa na vijana wetu wote wanazo silaha. Sasa mapinduzi yakatangazwa katika Sauti ya Zanzibar,” anasimulia Sheikh Thabit Kombo (UK.134)
Awali Sheikh Thabit Kombo, alimtaja John Okello, Abdallah Natepe na Yusuf Himid kama miongoni mwa vijana waliokuwa mstari wa mbele katika kutekeleza Mapinduzi, lakini akikiri kutomfahamu vyema Okello.

Sultani otoroka
Kuhusu Sultani kuikimbia Zanzibar wakati wa Mapinduzi, Sheikh Thabit Kombo anasimulia: “Sultani hakukamatwa. Wakati vijana wanashughulikia vile vituo muhimu, yeye akapata nafasi ya kupuruchuka na kukimbilia melini na meli yake ikaeleaelea karibu na Unguja kwa muda mrefu.
“Kwa bahati nzuri sana Mwalimu Nyerere akaombwa na Serikali ya Uingereza amhifadhi Sultani hadi hapo mipango ya kumsafirisha itakapokamilika.
“Na Mwenyezi Mungu akampa Mwalimu Nyerere busara kubwa ya kulikubali ombi hilo haraka haraka. Kutahamaki, Sultani keshafika Dar es Salaam, mgeni wa Mwalimu Nyerere.
“Hata sisi (viongozi wa ASP) tulikuwa na hofu juu ya Sultani aliyepuruchuka, kama angepata akili kwenda Pemba na halafu kutoka kule akaomba msaada wa majeshi kutoka nchi za nje, hali yetu ingekuwa ngumu sana.”
SEMA HAKUWA NA AKILI HIZO MAANA HAKUJUWA CHOCHOTE KATUACHA KATIKA MASHAKA NA DHIKI MPAKA LEO HII 2019 TUNAELEKEA 2020 TUMO TABUNI YEYE SALAMA SALMINI NA FAMILIA YAKE UINGEREZA.

NANI MUOGO ZAIDI BABU ALI AU MAALIM SEIF NITAPISHWA KABLA 2020 BABU ALI NITAIFANYA ZANZIBAR KUWA DUBAI


HAYA 2020 HIYOOO BABU ALI USHAKWISHA NA DHULMA YAKO MAALIM NA WEWE ULIYE JIDAI TUTADAI HAKI YETU KWA UPOLE KABLA YA 2020 TUTAIPATA HAKI YETU IKO WAPI....???